Nani mtunzi wa Voyage Mboso?

June 5, 2012

Kuna nyimbo ambazo kwa mashabiki wa Wenge Musica kwa ujumla wanazikumbuka sana wimbo huu wa Voyage Mboso, Wengi walijua huu Wimbo ni Wimbo wa JB Mpiana lakini ukweli ni kuwa huu ulikuwa ni Wimbo wa Adolph Dominguez na ndio maana walipoparanganyika Werasson alikuwa akiupiga sana wakati bado yuko na Dominguez na walipoanchana Werasson aliacha kuupiga na Dominguez aliendelea kuupiga. Angalia hapo chini utaona Voyage Mboso ya Werason pia.

Kwenye Original Version utamsikia vizuri Ekokota Machine Roberto Wunda,kwenye vyombo ni Patient Kusangira, Didie Masela Vando Mass, Mbonda na wengineo.


Happy Birthday JB Mpiana Babaa Daida

June 5, 2012

JB Mpianaaa

Leo June 2 ni siku ya kuzaliwa Papaa Sherii Salvatory De La Patria JB MPIANA, kama wapenzi wa muziki wa Lingala tunaungana nae katika kusherehekea siku yake hii  ya kuzaliwa ambapo anatimiza miaka 45. JB alizaliwa 1967 na mzee Mpiana Lusambo na mama Agnes katika eneo liitwalo Kananga ndani ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya watu wa Congo akiitwa jina lake halisi Jean Bedel Mpiana wa Tshituka.

Tangu aanze kujihusisha na muziki Jb amejipatia sifa nyingi za utunzi na uimbaji bora ikiwemo kuwa mwanamuziki wa kwanza katika kizazi chake(cha nne) cha muziki wa Congo kujipatia tuzo ya GOLDEN DISC,Mtunzi wa wimbo bora wa mwaka 1988-Mulolo ambao uliipandisha sana Wenge MUSICA 4×4 tout terrain na kuifanya ijulikane Africa nzima,pia Jb aliweka rekodi nyingine pale 1999 alipokuwa mwanamuziki wa kwanza kwa kizazi cha nne cha wanamuziki wa Congo kupiga kupata nafasi ya kupiga katika kumb maarufu duniani zilizopo Paris ufaransa ziitwazo Zenith, Olympia, Bercy pamoja na Stade des Martyrs ambapo show yake ndani ya Olympia ikaja kuwa voted kama best show of the 20th Century kwa wanamuziki wa Congo.

Pichani JB Mpiana akiwa amembeba kipenzi mwanaye anayeitwa Daida kama utasikia anamtaja sana kwenye nyimbo zake. 

Happy Birthday Papaa na Daida Jb Mpiana, tunakutakia maisha marefu na mafanikio katika kazi yako


%d bloggers like this: