Tabou Fatu Top Model Mamaa na Compressoo

October 6, 2011

 

image

Ingawa ni ya Kusikiliza lakini sikiliza umsikie JB alivyomlilia mamaa Tabou Fatou

Anaitwa Tabou Fatu Top Model a.k.a. Mamaa na Compressoo,huyu ni mwanadada mrembo mcongoman mfanyabiashara anaeishi Bruxells Ubelgiji, anamiliki maduka makubwa ya nguo (Boutique) huko ubelgiji na ufaransa, ni mrembo kweli na anajua kujipigilia pamba, hapa katopa simple tu lakini kapendeza,JB aliwahi kumtungia wimbo mzima acha kumtaja mara kadhaa kwenye nyimbo zake, pia fallly ipupa ana wimbo aliutunga kwa heshima ya mwanamama mjasiriamalia huyu wa kiafrika, Nadhani nimejibu swali lako mdau wangu Peter, Merci Mingi Papaa Hadj Le Jbnique kwa Compilation hii.

Sikiliza huu Wimbo then Sikiliza Baada ya Werrason jinsi Aimelia Lyase Doming’ong’o alivyompokea, Jamaa wamepokezani uzuri sana humu ndani.


Steve Jobs Dies: Apple Chief Created Personal Computer, iPad, iPod, iPhone

October 6, 2011

image

Steve Jobs, the mastermind behind Apple‘s iPhone, iPad, iPod, iMac and iTunes, has died, Apple said. Jobs was 56.

“We are deeply saddened to announce that Steve Jobs passed away today,” read a statement by Apple’s board of directors. “Steve’s brilliance, passion and energy were the source of countless innovations that enrich and improve all of our lives. The world is immeasurably better because of Steve. His greatest love was for his wife, Laurene, and his family. Our hearts go out to them and to all who were touched by his extraordinary gifts.”

The homepage of Apple’s website this evening switched to a full-page image of Jobs with the text, “Steve Jobs 1955-2011.”

Read the rest of this entry »


Kwa Wapenzi wa iPhone tu

October 5, 2011

Introducing iPhone 4S.

image

iPhone 4S

Dual-core A5 chip. All-new 8MP camera and optics. iOS 5 and iCloud. And introducing Siri. It's the most amazing iPhone yet.

Pre-order from 7 October. Available on 14 October.


UFUNGUZI WA SWAHILI FASHION WEEK KUZINDULIWA ARUSHA

October 4, 2011

The Fashion Coordinator Washington Benbella describing to the Press concerning the Awards Catergory during the Press Conference at Southern Sun Hotel on 4th-Oct-2011

Marketing Manager of Swahili Fashion Week,Hamis K.Omary answering questions from the media people concerning the Awards Catergory of Swahili Fashion Week

The Project Manager of Swahili Fashion Week Gillian Rugumamu explaining to the press concerning the Launch in Arusha and Swahili Fashion Week Awards,next is the Fashion Coordinator Washington Benbella.

Read the rest of this entry »


Cindy Olomide alipomwaga chozi jukwaani

October 4, 2011


Wimbo unaitwa Lily Kanik uliimbwa na Koffi Olomide. Wimbo huu ndio uliompa Cindy maks alipoitwa kwenye interview ili awe mmoja wa waimbaji wa Koffi, Lily Kaniki ni mama yake na Claudia Sasou Ngueso mke wa Denis Sassou Ngueso.


Cindy alipokuwa akiimba wimbo huu alitoa machozi utaona anashindwa kuimba kabisa na Koffi anamwambia aendelee kuimba, kisa cha kutokwa na machozi ni fikra akikumbuka alikotoka na anasema wimbo huu kila akiuimba anakumbuka safari ya ndoto yake ya kuja kuwa mwanamuziki, kwa Sasa Cindy si tu mwanamuziki ndani ya Quartier Latini bali ni mpenzi wa Koffi Olomide ambaye wameshibana kwelikweli.
Katikati ya mwaka huu Koffi alimnunulia gari ainaya Jaguar kama zawdi kwa kumzalia “kindu chedi”.
Ndani ya video hii utamuona kwa mbali Zakarie Bababaswe ambaye alikuwa mshereheshaji kwenye Concert hii iliyofanyika Inter Continental Hotel huko Kinshasa. Kiukweli hii ni Cencert ya kuitazama jumapili ukiwa umepumzika na Glass ya wine pembeni.

Merci mingi Papaa Julie We Ston kwa kuniletee DVD hii direct from Congo Merci Papaa Cisco ndani ya Kwetu Saloon weeeee!! kitokoooo.


Blog Mpya ya Michezo na Burudani

October 4, 2011

image


Shaggy Live in Nairobi

October 3, 2011

Djojo Ngonda ya "MAITRE" FICARE MWAMBA

October 3, 2011

“MAITRE” FICARE MWAMBA,huyu jamaa ni mpiga solo na rythm anaeheshimika sana na members karibu wote wa wenge kuanzia makaba,werrason,jb mwenyewe na wengine,heshima yake imetokana na misimamo yake ya kumwambia ukweli yeyote hata kama anamuheshimu kiasi gani na pia hakua mpenda makundi na mpaka sasa amekuwa hivyo,kiukweli jb bila huyu bcbg ingekuwa imeshamshinda,jb ni mtu wa kupokea maneno bila kupima hasa akiletewa na mtu anaemuamini, lakini mara kadhaa ficare ameweza kumkosoa jb katika maamuzi yatokanayo na maneno ya kuletewa na thanx God jb anamsikiliza huyu bwana other vijana wengi mnaowaona leo wasingekuwepo bcbg kama ilivotokea kwa tutu caludji ambae aliondoka ama aliondolewa bcbg kwa maneno ya kupikwa na majungu ya mpiga drums kipenzi kwa jb SEGUIN MIGNON wakati wa maandalizi ya ANTI TERRO huko South Africa.

Mbali na uwezo wake mkubwa mkubwa wa kupiga gitaa pia alikuwa mtunzi, kibao hiki kiliimbwa kwa kiasi kikubwa na Werasson pamoja na Adolph Dominguez akishirikiana na machampion wengine ni utunzi mahiri wa kijana Fi Carre Mwamba. Wakati huo list ilikuwa imekamilika kila idara.

Albamu hii ni moja ya albamu zenye mafanikio makubwa kwa kundi la Wenge kama Wenge ambapo kila mmoja alipata nafasi ya kumamua na vijana walikamu vilivyo, hebu sikiliza kisha uniambie wewe unakumbuka nini ukisikia nyimbo hizi, Mi namkumbuka Jema Mandari huyu jamaa alikuwa akiupenda sana huu wimbo, pamoja na wana BCBG woote bila kuwasahau Werassonique.

Kitu kingine ambacho FICARE anaeheshimika sana na jb ni udhibiti wa matumizi ya fedha ambapo ficare mwamba ndio mkurugenzi wa mambo ya fedha hapo bcbg cheo alichokikalia toka bcbg ya mpiana ianzishwe mpaka leo,kwa wasiomfahamu jb ni mkali sana kwenye matumizi mabovu ya fedha,sasa kama ficare kakaa hapo kipindi chote hicho ujue jb amekubali service yake,kumbuka moja ya sababu za mwanzo kuwakosanisha jb na werra wenge original ni jb kukerwa na udhiti mbovu wa werra kwenye mambo ya fedha werra akiwa mkurugenzi wa fedha.

Kiufupi Ficare mwamba ndani ya bcbg ni kama grisi kwenye chuma,yani chuma kikipata moto grisi ndio husaidia kisizidi kusuguana.


Fitness Master

October 2, 2011

FM--karibu-fm-A3-poster

Welcome Fitness Master (Tanzania) Gym & Health Center @ Ada Estate/ aside Leader Club – Kinondoni.


Werrason alipowachezesha mchaka mchaka Stade De France

October 2, 2011

Werrason ni bingwa wa kuvumbua vipaji ingawa mara zote tumeona anaongoza kwa kupoteza vichwa hasa akimtengeneza mtu mwishowe huishia kukimbiwa na sababu kubwa ni mkwanja, Show kama hii huwa zinampatia donge nono ikija kwenye mgao mara zote kwa Wazaire huwa ni issue na hii inatokana na mikataba mibovu, alipokuwa akihojiwa na CFI JB Mpiana alisema kuwa kwa sasa huwa anaingia mikataba na wanamuziki wake kila wakipata kazi kubwa ya kufanya.


JB Mpiana aendelea kutamba Kin

October 2, 2011

image

Kijana NONO Fudji ambaye ana vituko ananikosha sana kwa style yake ya uchezaji awapo jukwaani, huyu anakuja juu sana na kufanikiwa kutunga wimbo huu wa Mombamba ambao unawika sana kwa sasa.

Leo tunawaletea kwa uchache kinachoendelea ndani ya jiji la Kinshasa na Congo kiujumla kuzihusu bendi mbili pinzani kutoka kizazi cha wenge, bendi hizo ni wenge bcbg ya kwake Salvatory De La Patria  Jb Mpiana na wenge musica maison mere ya kwake Le Roi De La Forret Werrason.Hii ni baada ya kuziweka hadharani album zao mbili yani Sayons Serieux ya Bcbg na Malewa suite fin a.k.a.malewa no.2 ya Wmmm.

Kwa upande wa bcbg,sayons serieux imeendelea kufanya vizuri na kuzidi kupata mafanikio ukilinganisha na album mbili zilizopita za bendi hiyo. Bcbg wanaonekana kuimarika zaidi kwenye album hii huku nyimbo kama MOMBAMBA,ETOILE DU BERGER a.k.a.Claudia Sassou Nguesso, BOLONIA na CODE MORAL ya Abraham Mignon zikiendelea kuwashika zaidi bana ba Congo kwa kuombwa zirudiwe mara kadhaa na wapenzi wa muziki kwenye local live concerts jijini humo.Kati ya hizi MOMBAMBA imekua juu zaidi  kiasi cha wapenzi kulazimisha irudiwe mara tatu kwenye tamasha maarufu la kila mwaka lijukanalo kama FIKIN. Pia  rap ama animation mpya ya atalaku/rapper no.1 wa bcbg kwa sasa Genta Lisimo “antibiotique” iitwayo “ROTA ROTA” ikizidi kupata umaarufu. Naye repa/atalaku mwingine wa Bcbg aitwaye Police anaonekana kujiimarisha zaidi katika kuipata nafasi ya kuwa atalaku no.2 wa Bcbg.


Shaggy totally rocks Nairobi!

October 2, 2011

image

image

image

image

image

image

image

Picha zote na EABL, Kiukweli jamaa aliwaacha watu hoi kwa mujibu wa comments za wadau si unajua jamaa yuko down to earth haringi kabisa tofauti na ma super stars wengine.

image

Wakurugenzi wa Prime Time Promotion Joe na Mkewe Johayna Kulia kabisa, Gody Kusaga Tshirt Nyeusi na wadau wengine wakihakikisha kila kitu kinakwenda sawa, ikumbukwe Prime Time ndio walioratibu Tamasha hili kubwa na kudhaminiwa na EABL kupitia kinywaji chake cha Tusker.

image

Pichani Mwanamuziki Jaguar ambaye anatamba na wimbo wake wa Kigeugeu akikamua kabla jamaa wenyewe wa Tusker All Stars hawajakamua na wanamuziki toka nje, Tamasha lilifana vilivyo.


Anayesema Makaba hana kitu hebu angalia hii

October 2, 2011

Mara nyingi huwa napenda kusikiliza muziki huku nikisikiliza kitu kimoja kimoja, Napenda sana wapiga vyombo bana, binafsi namkubali sana Allain Prince Makaba, na kipindi cha BCBG ilee nilikuwa nawakubali sana wapiga vyombo wa kipindi kile Kama Allain Makaba, Patient Kusangira, Burkina Faso Kasongo Mboka Liya, nilifedheheshwa nikaona kuna mdau anasema Makaba si kitu daha jamani hivi huyu mtu kaanza jana kuupenda muziki wa Congo ama? Hebu msikilize Makaba hapo kuanzia 5:40 utaniambia kisha toa maoni yako.


Eve and Cabo Snoop on Stage Together!

October 1, 2011

 

image

image

image

image

image

image

Mambo yenda yakiongezwa kwenye viwanja vya Carnival huko Nairobi muda huu na sasa ni zamu ya Eve E na Cabo Snoop wakilishambilia jukwaa, usilale tunakupa vitu LIVE updates hapa hapa jukwaani, Shukrani kwa EABL kwa Picha hizi.


Cabo Snoop …Mambo ya Windek

October 1, 2011

image

image

image

image

image

Tunaendelea kuwaletea mambo yanavyokwenda huko Nairobi kwenye Tusker All Stars ambapo wasanii mbali mbali wanatumbuiza na sasa ni zamu yake Cabo Snoop toka Angola ambaye anatamba na Windek na Prakata tumba…. Stay tuned many more to come hapa hapa (Picha zote na EABL Tusker Fun Page).


Alpha on Stage at Tusker All Stars Concert!

October 1, 2011

image

image

image


Msechu akifanya vitu vyake jukwaani

October 1, 2011

image

image

image

image

image

Concert ya Tusker All Stars inaendelea jijini Nairobi hivi sasa huku Msechu akiwa jukwaani nikiwa naandika habari hii bado Shaggy, Cabo Snoop na EVE E wakisubiriwa kwa hamu na mashabiki lukuki waliohudhuria kipute hicho, Picha zote kwa hisani ya EABL.


Mambo yanapamba moto huko Nairobi Kenya

October 1, 2011

image

Mashabiki wakipanga foleni kuingia kwenye Tusker All Stars Concert ambapo wanamuziki washiriki wa Tusket All Stars wakishirikiana na Wanamuziki wengine kama Shaggy, EVE E na Cado Snoop ambaye anatamba na wimbo wake wa Windeck na Prakata Tumba.


Nairobi hapatoshi weekend hii

October 1, 2011

4_003

Eve E akiwa amepozi kiaina. Ujio wa wanamuziki hawa akiwemo Shaggy na Cabo Snoopy umefanikishwa na Prime Time Promotion ya jijini Dar Es Salaam na kudhaminiwa na kampuni ya Bia ya EABL kupitia kinywaji chake cha Tusker. (Picha zote na Blog ya Jiachie)

 

9

Mwanamuziki kutoka nchini Jamaica,anaefanya kazi zake za kimuziki nchini Marekani,Orville Richard Burrell a.k.a Shaggy akiwa amepozi mara baada ya kutia saini bango lenye tangazo la kampeni mpya ya East African Breweries Ltd, iliozinduliwa hivi karibuni kwa ajili ya kuielimisha jamii kuhusiana na suala la ulevi wa kupindukia ijulikanayo kama “Unywaji pombe kistaarabu” ama ” RESPONSIBLE DRINKING CAMPAIGN”

 

8_002

Msanii mmojawapo wa Tusker All Stars 2011 akitia saini kwenye bango lenye tangazo la kampeni mpya ya East African Breweries Ltd,iitwayo “Unywaji pombe kistaarabu” ama ” RESPONSIBLE DRINKING CAMPAIGN”

 

 

3_003

Baadhi ya wanamuziki waliojitokeza kuunga mkono kampeni mpya ya EABL-Kenya ( RESPONSIBLE DRINKING CAMPAIGN),wakiwa wamepozi picha pamoja kwenye baadhi ya Tax zenye kuhamasisha kampeni hiyo jijini Nairobi,kulia ni Davies,Eve E,Peter Msechu,Cabo Snoop pamoja na Shaggy.

 

10_002

Mmoja wa Wakurugenzi wa Clouds Entertainment,Ruge Mutahaba pichani kulia akizungumza jambo na Shaggy leo mchana nje ya hoteli ya Kimataifa,Serena,jijini Nairobi.

 

1_002

Pichani kulia ni Mkurugenzi wa Masoko wa EABL-Kenya,Caroline Ndungu sambamba na baadhi ya wafanyakazi wa kampuni hiyo wakiwa na wanamuziki watakaotumbuiza kesho kwenye tamasha la Tusker All Stars 2011,wakitoka nje ya hoteli ya Serena,iliopo katikati ya jiji la Nairobi,Kenya mapema leo mchana kwa ajili ya kuunga mkono kampeni mpya ya Unywaji pombe kistaarabu ” RESPONSIBLE DRINKING CAMPAIGN”,ambayo nchini Tanzania ilizinduliwa hivi karibuni (kwa picha ya tukio hilo bofya hapa).


Maalum kwa FACEBOOKERS ONLY

October 1, 2011

xsx