JB Mpiana aendelea kutamba Kin

image

Kijana NONO Fudji ambaye ana vituko ananikosha sana kwa style yake ya uchezaji awapo jukwaani, huyu anakuja juu sana na kufanikiwa kutunga wimbo huu wa Mombamba ambao unawika sana kwa sasa.

Leo tunawaletea kwa uchache kinachoendelea ndani ya jiji la Kinshasa na Congo kiujumla kuzihusu bendi mbili pinzani kutoka kizazi cha wenge, bendi hizo ni wenge bcbg ya kwake Salvatory De La Patria  Jb Mpiana na wenge musica maison mere ya kwake Le Roi De La Forret Werrason.Hii ni baada ya kuziweka hadharani album zao mbili yani Sayons Serieux ya Bcbg na Malewa suite fin a.k.a.malewa no.2 ya Wmmm.

Kwa upande wa bcbg,sayons serieux imeendelea kufanya vizuri na kuzidi kupata mafanikio ukilinganisha na album mbili zilizopita za bendi hiyo. Bcbg wanaonekana kuimarika zaidi kwenye album hii huku nyimbo kama MOMBAMBA,ETOILE DU BERGER a.k.a.Claudia Sassou Nguesso, BOLONIA na CODE MORAL ya Abraham Mignon zikiendelea kuwashika zaidi bana ba Congo kwa kuombwa zirudiwe mara kadhaa na wapenzi wa muziki kwenye local live concerts jijini humo.Kati ya hizi MOMBAMBA imekua juu zaidi  kiasi cha wapenzi kulazimisha irudiwe mara tatu kwenye tamasha maarufu la kila mwaka lijukanalo kama FIKIN. Pia  rap ama animation mpya ya atalaku/rapper no.1 wa bcbg kwa sasa Genta Lisimo “antibiotique” iitwayo “ROTA ROTA” ikizidi kupata umaarufu. Naye repa/atalaku mwingine wa Bcbg aitwaye Police anaonekana kujiimarisha zaidi katika kuipata nafasi ya kuwa atalaku no.2 wa Bcbg.

Advertisements

3 Responses to JB Mpiana aendelea kutamba Kin

  1. chembera says:

    hii blog ni nzuri sana,hasa kwa sisi washabiki wa miziki ya congo…ila kinachoonekana sasa ni waandishi na mnaofahamu historia za muziki huo kutuvuruga washabiki…kwani nanyi mmeingia kwenye mtego wa kushabikia kati ya JB na WERRA,,kila mwandishi kutoa sifa kwa ampendae na kumponda asiyempenda,mnatuchanganya mashabiki…tupeni taarifa na mtuache sisi tununue CD na tutoe uamuzi wa nani zaidi.

  2. Anonymous says:

    mbona albuma ya malewa 2 hamuiongelewi wakati tayari mlituambia imetoka inaweza onekana kweli mnapendelea

  3. As soon as I considered about issues like: why such information is for free here? If you write a book then not less than on selling a guide you receive a percentage, mainly because. Thank you and excellent luck on informing persons a lot more about this.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: