Anayesema Makaba hana kitu hebu angalia hii

Mara nyingi huwa napenda kusikiliza muziki huku nikisikiliza kitu kimoja kimoja, Napenda sana wapiga vyombo bana, binafsi namkubali sana Allain Prince Makaba, na kipindi cha BCBG ilee nilikuwa nawakubali sana wapiga vyombo wa kipindi kile Kama Allain Makaba, Patient Kusangira, Burkina Faso Kasongo Mboka Liya, nilifedheheshwa nikaona kuna mdau anasema Makaba si kitu daha jamani hivi huyu mtu kaanza jana kuupenda muziki wa Congo ama? Hebu msikilize Makaba hapo kuanzia 5:40 utaniambia kisha toa maoni yako.

13 Responses to Anayesema Makaba hana kitu hebu angalia hii

 1. Issa Mahmoud says:

  Watu wanaropokaga tuu
  Mi mwenyewe nikliona si unajua tena kaka watu wameanza kupenda muziki huu majuzi ndio maana vinginevyo Makaba ni moto na kila mpenda muziki si Congo tu anajua hilo.

  Nakubaliana na wewe Makaba anatisha ana heshima yake.

  Merci Mingi Papaa Pius Bamalaaa.

 2. Farid wa Muscat says:

  Nakubaliana na wapenzi wengi wa muziki wa Africa ya kua Makaba ni mtu alijijengea sifa na heshima kubwa katika muziki kwa upigaji wake mahiri wa Solo guitar .

 3. peter says:

  Leo tunawaletea kwa uchache kinachoendelea ndani ya jiji la Kinshasa na Congo kiujumla kuzihusu bendi mbili pinzani kutoka kizazi cha wenge, bendi hizo ni wenge bcbg ya kwake Salvatory De La Patria Jb Mpiana na wenge musica maison mere ya kwake Le Roi De La Forret Werrason.Hii ni baada ya kuziweka hadharani album zao mbili yani Sayons Serieux ya Bcbg na Malewa suite fin a.k.a.malewa no.2 ya Wmmm.

  Kwa upande wa bcbg,sayons serieux imeendelea kufanya vizuri na kuzidi kupata mafanikio ukilinganisha na album mbili zilizopita za bendi hiyo. Bcbg wanaonekana kuimarika zaidi kwenye album hii huku nyimbo kama MOMBAMBA,ETOILE DU BERGER a.k.a.Claudia Sassou Nguesso, BOLONIA na CODE MORAL ya Abraham Mignon zikiendelea kuwashika zaidi bana ba Congo kwa kuombwa zirudiwe mara kadhaa na wapenzi wa muziki kwenye local live concerts jijini humo.Kati ya hizi MOMBAMBA imekua juu zaidi kiasi cha wapenzi kulazimisha irudiwe mara tatu kwenye tamasha maarufu la kila mwaka lijukanalo kama FIKIN. Pia rap ama animation mpya ya atalaku/rapper no.1 wa bcbg kwa sasa Genta Lisimo “antibiotique” iitwayo “ROTA ROTA” ikizidi kupata umaarufu. Naye repa/atalaku mwingine wa Bcbg aitwaye Police anaonekana kujiimarisha zaidi katika kuipata nafasi ya kuwa atalaku no.2 wa Bcbg

  ANGALIA HIYO POST THEN TAZAMA HISTORIA YA WENGE MUSICA THEN WACHAMBUE WAPIGAJI ndani ya bcbg album ya ,sayons serieux then rudi nyuma…

 4. peter says:

  …..Kama Makaba alitaka kumzibia GENTALISIMO…….pengo la KALUJI nani angeziba Hata Bukinafaso aliondoka na Solo….Bado BCBG ipo ..tuache ushabiki Mbona Mwamba alimudu kupiga solo Zenith!! Nawashukuru wadau kwa kutuma post nzuri ila tatizo huwa hamzisomi na kuchambua na kulinganisha na historia………

  HII NI KWA WADAU WA WENGE BCBG:SOMA HIVYO VIPANDE KUTOKA MTANDAO BORA KUSINI MWA SAHARA SPORTSTAREHE KISHA CHAMBUA KWA MAKINI then nitakuuliza swali………

  Bendi ikasafiri bila Blaize Bula mpaka Paris.Lakini wakiwa katika maandalizi kuelekea siku ambayo watapiga zenith ambako ndio walipangiwa kupiga kwanza kabla ya olympia,ulizuko mgogoro kati ya JB na Makaba,mgogoro ambao chanzo chake kilikua ni makaba kutokubaliana kabisa uamuzi uliochukukuliwa na bendi huko Kinshasa ku-recruit wanamuziki wapya ambao makaba aliona kama hawakuwa na uwezo wa kutosha kuwa wanamuziki wa wenge BCBG mpya,hapa tukumbuke kwamba katika mtiririko wa vyeo walivyopeana makaba alikua ndio artistic director hivyo hakuwakubali wasanii wapya yani Jules Kibens, Rio, Chai Ngenge na Genta.

  Mgogoro huo ulidumu mpaka siku ya show yenyewe ndani ya zenith dakika chache kabla ya kupanda stejini kuanza show kulitokea majibizano ya maneno baina ya marafiki hao yaliyopelekea mpaka JB Mpiana kulia machozi baada ya Alain Makaba kutumia maneno makali sana yaliyofanana na matusi dhidi yake, JB aliumia sana moyoni kwani kazi ya ku recruit aliifanya Blaize Bula, Jb akasusa kupanda jukwaani hali iliyopelekea showa rasmi ichelewe kuanza huku kina Alain mpela na Aimelia wakiwa wanaendelea kuimba nyimbo za utangulizi stejini, ikabidi mkewe Jb, mama Amida Shatur pamoja na rafiki yake JB waliekuwa pamoja maisha ya utotoni JDL ambae wakati huo alikua ni mpiga keyboard wa Wenge El Paris waingilie kati kumsihi JB apande stejini kwani wapenzi hawatawaelewa kabisa hasa ikizingatiwa Blaize Bula nae hayupo (JDL kwa sasa yuko na bcbg kama muimbaji).
  Sehemu ya Show ya Zenith ilivyokuwa
  Baadae Jb akakubali na kupanda stejini akiwa amevaa crown ya mfalme kichwani na koti refu lenye rangi ya dhahabu akisindikizwa na Tutu Kaludji ukumbi mzima ukizizima kwa kushangilia na moja kwa moja akashika mic na kuanza kuimba wimbo wake COURAGE kwa hisia kali na masikitiko makubwa, huku akiwataja wakongwe Papa Wemba, Pepe Kalle, Adui yake wakati huo Koffi Olomide (japo alipomtaja watu walizomea) huku akisema kwamba yeye ni mdogo kwa hao wote, unaweza kutazama hapo chini jinsi alivyokua akiimba kwa hisia kali wimbo huo siku hiyo,ambapo baada ya huu akaamba mulolo, Parie Bouge (Kin e Bouger) na n.k. mnaweza kuitafuta video hii kamili kwa ambao hamjaiona, mimi huwa hainichoshi kuitazama, ni nzuri sana,imeandikwa JB Mpiana & WENGE bcbg Zenith 1999!
  vIDEO:

  Wenge alikomelea kwenye kutunga zaidi na vijana walipewa nafasi vijana zaidi, Wimbo huu unaitwa Serge Palmi ukiwa ni utunzi wa kinaja Burkina Faso Mboka Liya aka Burkifaso Kasongo mmoja wa vijana wakongwe kwenye BCBG.
  Katika show hii kwa upande wa makaba nae alisusa kabisa kupiga solo, akakaa back stage, mpaka mwishoni kabisa alipobembelezwa sana na wadau wa bcbg ndio akapanda stejini akapiga solo kwenye wimbo omba ambao hupendwa sana na wamama wa congo, tena hakua yule makaba tunaemjua, mcheshi, mchangamfu na mbwembwe nyingi stejini,bali alikua amenuna, mwenye hasira akipiga solo lake huku akiwa amewapa mgongo mashabiki!!mimi mwenyewe nilipoiona hii video enzi hizo 2000 kabla ya kujua kilichotokea nilimshangaa
  sana makaba kwa style ile ya upigaji gitaa huku amewapa
  mgongo mashabiki, niliona kama ilikua ni dharau!tafuta video ya live concert hii bora kabisa uangalie vituko hivyo vya prince makaba.

  NAWASILISHA

 5. peter says:

  mbona MASHABIKI hawakuondoka JB Mpiana & WENGE bcbg Zenith 1999! Ninani alipiga solo…..mafanikio ya Zenith 1999 yalibebwa na na nani…….wadau tuwe kama msumeno….hata Baba Daida anamwaminia Mwamba zaidi ya mashabiki…

 6. Hadj Le Jbnique says:

  hapo unapotaja mwamba nadhani unamaanisha “MAITRE” FICARE MWAMBA,huyu jamaa ni mpiga solo na rythm anaeheshimika sana na members karibu wote wa wenge kuanzia makaba,werrason,jb mwenyewe na wengine,heshima yake imetokana na misimamo yake ya kumwambia ukweli yeyote hata kama anamuheshimu kiasi gani na pia hakua mpenda makundi na mpaka sasa amekuwa hivyo,kiukweli jb bila huyu bcbg ingekuwa imeshamshinda,jb ni mtu wa kupokea maneno bila kupima hasa akiletewa na mtu anaemuamini,lakini mara kadhaa ficare ameweza kumkosoa jb katika maamuzi yatokanayo na maneno ya kuletewa na thanx god jb anamsikiliza huyu bwana other vijana wengi mnaowaona leo wasingekuwepo bcbg kama ilivotokea kwa tutu caludji ambae aliondoka ama aliondolewa bcbg kwa maneno ya kupikwa na majungu ya mpiga drums kipenzi kwa jb SEGUIN MIGNON wakati wa maandalizi ya ANTI TERRO huko South Africa.Ipo stori yake ngoja niishie hapa.
  Kitu kingine ambacho FICARE anaeheshimika sana na jb ni udhibiti wa matumizi ya fedha ambapo ficare mwamba ndio mkurugenzi wa mambo ya fedha hapo bcbg cheo alichokikalia toka bcbg ya mpiana ianzishwe mpaka leo,kwa wasiomfahamu jb ni mkali sana kwenye matumizi mabovu ya fedha,sasa kama ficare kakaa hapo kipindi chote hicho ujue jb amekubali service yake,kumbuka moja ya sababu za mwanzo kuwakosanisha jb na werra wenge original ni jb kukerwa na udhiti mbovu wa werra kwenye mambo ya fedha werra akiwa mkurugenzi wa fedha.

  Kiufupi Ficare mwamba ndani ya bcbg ni kama grisi kwenye chuma,yani chuma kikipata moto grisi ndio husaidia kisizidi kusuguana.

 7. peter says:

  asante kaka Hadj Le Jbnique kwa mchango wako kama msumeno

  Kiufupi Ficare mwamba ndani ya bcbg ni kama grisi kwenye chuma,yani chuma kikipata moto grisi ndio husaidia kisizidi kusuguana….mkuu nakuaminia nilimwona Mwamba alivyokuwa grisi katika..Zenith 1999 …umechambua vizuri sana ….bila ushabiki….

 8. Hadj Le Jbnique says:

  Ficare mwamba pia ni mtunzi mahiri sana,mfano wa kazi zake za kutukuka ni hii hapa chini,kiukweli i love this song kuanzia mpangilio wake mpaka message,mtazame hapo mwanzo wa video anavyoanza na gitaa lake….huu wimbo sijawahi kuusikiliza ama kuutazama bila kuu rewind,unaitwa le spoir de chicago utunzi wake ficare mwamba le grand maitre,vocals zimetiwa na jb mpiana a.k.a.papa na daida mwenyewe,Bogus Bompema anaeingia baada ya jb kumaliza hapo,Richard mukena(anaeingia na sauti flani nzito akiwa na miwani mieusi na kumtajana papa wa roma na pia papa na daida),jdl mtu mrefu mwenye miwani kaimba vizuri sana humu na kumtaja mke wa mpiana meree Amida na mwisho anamalizia shai ngenge then linamwaga sebene la kistarabu,ficare anafanya vurugu zake,hii ni album ya internet,zawadi yako hii bwana peter,isikilize na kuitazama vizuri mwanzo mwisho.merci mingi

 9. Odran chaula says:

  nimefurahi saaana kupata habari hizi najiuliza nilikua wapi kuiijua blog hii inayo chambua muziki wa DR congo vilivyo,ki ukweli muziki wa dR congo uko juu sana babari kwamba bongofleva iko juu ni ndoto za mchana nampenda saaana jb mpiana hasa anapo shika mic sibanduki luningani pia ferre golla ameanza kuuteka moyo wote hao ni mahiri wa kuimba na wa heshimu werrason.Koffi fall ipupa

  • Jesse Grillo says:

   I am always amazed that you’re somehow capable to create such top level content almost every day. About how many articles does your team usually create in any given year? I just wanted to say that this post is awesome. When I started my lap top your website was already running. If you have the time, shoot me an Email and we will chat because I have an idea you will love.

 10. Anonymous says:

  pichazao

 11. Songs says:

  I’ve learn several just right stuff here. Definitely value bookmarking for revisiting.
  I surprise how much effort you set to make one of these wonderful informative web
  site.

 12. Yplan says:

  Spot on with this. awesome blog and thought|Thanks for expressing your own post I�d constantly stick to|Thank you almost all for the details. Well written! This site was running when I turned on my lap top. I am shocked at how fast your page loaded on my cell phone.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: