Cindy Olomide alipomwaga chozi jukwaani


Wimbo unaitwa Lily Kanik uliimbwa na Koffi Olomide. Wimbo huu ndio uliompa Cindy maks alipoitwa kwenye interview ili awe mmoja wa waimbaji wa Koffi, Lily Kaniki ni mama yake na Claudia Sasou Ngueso mke wa Denis Sassou Ngueso.


Cindy alipokuwa akiimba wimbo huu alitoa machozi utaona anashindwa kuimba kabisa na Koffi anamwambia aendelee kuimba, kisa cha kutokwa na machozi ni fikra akikumbuka alikotoka na anasema wimbo huu kila akiuimba anakumbuka safari ya ndoto yake ya kuja kuwa mwanamuziki, kwa Sasa Cindy si tu mwanamuziki ndani ya Quartier Latini bali ni mpenzi wa Koffi Olomide ambaye wameshibana kwelikweli.
Katikati ya mwaka huu Koffi alimnunulia gari ainaya Jaguar kama zawdi kwa kumzalia “kindu chedi”.
Ndani ya video hii utamuona kwa mbali Zakarie Bababaswe ambaye alikuwa mshereheshaji kwenye Concert hii iliyofanyika Inter Continental Hotel huko Kinshasa. Kiukweli hii ni Cencert ya kuitazama jumapili ukiwa umepumzika na Glass ya wine pembeni.

Merci mingi Papaa Julie We Ston kwa kuniletee DVD hii direct from Congo Merci Papaa Cisco ndani ya Kwetu Saloon weeeee!! kitokoooo.

4 Responses to Cindy Olomide alipomwaga chozi jukwaani

 1. Hadj Le Jbnique says:

  Nice stuff!

 2. Fatuma Mtanga says:

  Hivi kuna uhisiano gani kati ya familia ya rais Dennis Sassou Nguesso wa congo brazaville na wanamuziki wa congo kinshasa?inaonesha familia hiyo inaguswa zaidi na wanamuziki wa nje kuliko wa nyumbani kwao,maana kwao kuna extra musica na naamini zipo nyingine pia iweje wanashobokea zaidi wanamuziki wa nje na kuacha kuwapa sapoti wa nyumbani

 3. peter says:

  Hata mimi nimetokea kuupenda mziki wa Kongo kuliko huu wa hapa nyumbani hii ni kutokana kwa ukame wa mipini live kama enzi zile za Ndala Kasheba…Kassim Mapili ..V..King Nguza….ilipendeza sana

 4. Hadj Le Jbnique says:

  Usemavyo fatuma mtanga ni sawa familia hiyo kweli imekua na uhusiano wa karibu zaidi na wanamuziki wa congo ya kabila kuliko wa nyumbani brazaa,japo pia hajaitelekeza moja kwa moja extra musica ambayo imesadia na inaendelea japo si kiviiile kuitangaza congo brazavile katika ulimwengu wa muziki duniani,mfano mzuri ni hapa roga roga alipomuimbia mtoto wa kiume na anaetajwa kuwa mrithi wa kiti cha urais wa mzee dennis sassou nguesso,huyu si mwingine bali ni yule anaefahamika kama KIKI DENNIS SASSSOU NGUESSO au KIKI NGUESSO kwa ufupi,msikilize roga roga akimlilia KIKII,Hamna video ila mtaona taswira mbalimbali kwa maana ya picha za mnato za familia ya mzee nguesso,kiki mwenyewe,mkewe na shughuli mbalimbali zinazoihusu first family ya congo brazaville.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: