Djojo Ngonda ya "MAITRE" FICARE MWAMBA

“MAITRE” FICARE MWAMBA,huyu jamaa ni mpiga solo na rythm anaeheshimika sana na members karibu wote wa wenge kuanzia makaba,werrason,jb mwenyewe na wengine,heshima yake imetokana na misimamo yake ya kumwambia ukweli yeyote hata kama anamuheshimu kiasi gani na pia hakua mpenda makundi na mpaka sasa amekuwa hivyo,kiukweli jb bila huyu bcbg ingekuwa imeshamshinda,jb ni mtu wa kupokea maneno bila kupima hasa akiletewa na mtu anaemuamini, lakini mara kadhaa ficare ameweza kumkosoa jb katika maamuzi yatokanayo na maneno ya kuletewa na thanx God jb anamsikiliza huyu bwana other vijana wengi mnaowaona leo wasingekuwepo bcbg kama ilivotokea kwa tutu caludji ambae aliondoka ama aliondolewa bcbg kwa maneno ya kupikwa na majungu ya mpiga drums kipenzi kwa jb SEGUIN MIGNON wakati wa maandalizi ya ANTI TERRO huko South Africa.

Mbali na uwezo wake mkubwa mkubwa wa kupiga gitaa pia alikuwa mtunzi, kibao hiki kiliimbwa kwa kiasi kikubwa na Werasson pamoja na Adolph Dominguez akishirikiana na machampion wengine ni utunzi mahiri wa kijana Fi Carre Mwamba. Wakati huo list ilikuwa imekamilika kila idara.

Albamu hii ni moja ya albamu zenye mafanikio makubwa kwa kundi la Wenge kama Wenge ambapo kila mmoja alipata nafasi ya kumamua na vijana walikamu vilivyo, hebu sikiliza kisha uniambie wewe unakumbuka nini ukisikia nyimbo hizi, Mi namkumbuka Jema Mandari huyu jamaa alikuwa akiupenda sana huu wimbo, pamoja na wana BCBG woote bila kuwasahau Werassonique.

Kitu kingine ambacho FICARE anaeheshimika sana na jb ni udhibiti wa matumizi ya fedha ambapo ficare mwamba ndio mkurugenzi wa mambo ya fedha hapo bcbg cheo alichokikalia toka bcbg ya mpiana ianzishwe mpaka leo,kwa wasiomfahamu jb ni mkali sana kwenye matumizi mabovu ya fedha,sasa kama ficare kakaa hapo kipindi chote hicho ujue jb amekubali service yake,kumbuka moja ya sababu za mwanzo kuwakosanisha jb na werra wenge original ni jb kukerwa na udhiti mbovu wa werra kwenye mambo ya fedha werra akiwa mkurugenzi wa fedha.

Kiufupi Ficare mwamba ndani ya bcbg ni kama grisi kwenye chuma,yani chuma kikipata moto grisi ndio husaidia kisizidi kusuguana.

17 Responses to Djojo Ngonda ya "MAITRE" FICARE MWAMBA

 1. Farid wa Muscat says:

  Ficare Mwamba ni mmoja wa wanamuziki wenye mfano wa kuigwa mimi binafsi nampenda sana, hasa katika ule mwimbo wa voyage mboso ndio hua unanifanya nimkumbuke sana

 2. Hadj Le Jbnique says:

  kweli kabisa mdau ficarre amekua akikaa kimya na kuibuka na vitu vikali toka enzi za wenge musica original,miongoni mwa kazi zake za kutukuka ni hiyo djo djo ngonda ambayo imekua ikitumiwa na karibu wenge zote zilizopo sasa kwenye majukwaa yao,pia kuna kitu kingine kinaitwa decision nacho kikali pia,halafu kuna le spoir dE chicago kwenye album internet ya bcgb,na sasa kwenye hii album mpya ya bcbg sayons serieux amekuja na kitu HOMME D’AFFAIRE ambamo vocalas zimetiwa na jb mwenyewe,shai ngenge,didi kalombo n.k. nimeitafuta video yake sijaipata lakini angalau tuyasikilize hayo mambo yake ya ndani(homme d’affaire)

 3. peter says:

  ….bana Wenge …juzi nilikuwa Karatu kwenye pub moja nikaweka live ya Baba Daida Oyo Eza Oeuvre LIVE FIKIN …wakuu hapakutosha……kuna staili mpya ya kucheza Soyonsy kaka balaa!! huko utamkuta zambrotta(mama malkia), virginie (napenda midomo yake anavyo ichezesha akiwa anadansi), tantine, yetsi, ,brinette(muana nsuka) na kuna moja anaitwa maarufu kama Electrikee (namaanisha umeme) balaa!! Kwa wapenzi wa instrumental live hii itawaburudisha sana…..mesiii Farid wa Muscat,Hadj Le Jbnique papa PIUS na Bana Wenge asanteni kunikumbusha djo djo ngonda kwa sasa napata PETANGON!!

 4. Hadj Le Jbnique says:

  watu wako hawa hapa bwana peter,wapate hapo mmoja mmoja,anaanza mwana nsuka a.k.a shakira

  inaendelea hapa bcbg walitembelewa na Le Fondeteur(mwanzilishi wa wenge)Didier masela na kukakibidhiwa na jb mpini wake ule wa bass akaukung’uta kisawasawa na kuwachezesha wa bebe cherie(wacheza show wa bcbg ya papa cherie)

 5. peter says:

  … mesiiii Kaka Hadj Le Jbnique nimeiona na nimeikubali nakumbuka Mwana nsuka alikuwa mtoto mdogo full kipaji…..Namkubali JB KUKUZA VIPAJI….pia kuna dogo anaitwa OBAMA….Hatari….balaa!!

  Bana wenge tunaomba mwenye post kuhusa madancer haswa hawa kike walioko kwa Baba Daida mtupe kidogo…mimi huwa nazimika sana na huyu dada Virginie Bukasa…….lakini kuna mwingine anaitwa Mbiliadema(umeme)….

  nawashukuru sana Bana Wenge mnaotupa habarisha….inapendeza sana…

 6. Hadj Le Jbnique says:

  Dogo Barack Obama ndio huyu hapo chini,actually huyu dogo yuko kikosi chapili cha bcbg kinachoitwa PPU yani presidential protection unit,hiki ni kikosi maalum cha ulinzi wa rais mpiana kiko tayari tayari wakati wowote kunapotokea maafa ya usaliti ndani ya bendi kubwa kumlinda rais asiadhirike wakati anatafakari cha kufanya kuziba nafasi ya msaliti yeyote alie ondoka kundini

 7. Hadj Le Jbnique says:

  official dancers wa bcbg ni zambrotta, virginie, tantine, yetsi, nina, ananancy, sandralima,chermaine,brinette(muana nsuka) na beverly,blanche Pia yupo mkongwe Monica Seles lakini yeye kwa huwezi kumuona majukwaani ila ndio Choreographer(mwalimu na pia ndie anaewafanyia usaili madancer wanaotaka kujiunga bcbg),na hii hata bendi za huko nyumbani zinaweza kujifunza,maana nasikia kuna wacheza show ambao walikuwapo tangu enzi za diamond sound ikibinda nkoe pale silent inn mwenge (sijui kama bado ipo)mpaka leo bado wananengua tu majukwaani,wenzao umri ukuenda huwa wanakuwa walimu kwenye bendi zao na kuwapisha damu changa kama hawa wakin muana nsuka.

 8. ALLy says:

  Samahani papaa, hivi Tabu fatu ni nani manake Jb, werasoon na hata Koffi huwa wanamtaja sana

 9. peter says:

  Merci ..Hadj Le Jbnique ……nimefurahishwa sana na ufafanuzi wako Kaka nafikri bendi zetu za hapa na hata timu zetu wangeiga huu mfano…Jb huwa anawaleta jukwaani hawa madongo halafu watatema cheche kisha anawarudisha kwenye ngome na mashabiki wanabaki midomo wazi….inapendeza sana nimefurahishwa na hii tafsiri ya …PPU yani presidential protection unit,hiki ni kikosi maalum cha ulinzi wa rais mpiana kiko tayari tayari wakati wowote kunapotokea maafa ya usaliti ndani ya bendi kubwa kumlinda rais asiadhirike wakati anatafakari cha kufanya kuziba nafasi ya msaliti yeyote alie ondoka kundini

 10. peter says:

  Merci ..Hadj Le Jbnique ……nimefurahishwa sana na ufafanuzi wako Kaka nafikri bendi zetu za hapa na hata timu zetu wangeiga huu mfano…Jb huwa anawaleta jukwaani hawa YOUNG SINGERS halafu watatema cheche kisha anawarudisha kwenye ngome na mashabiki wanabaki midomo wazi….inapendeza sana nimefurahishwa na hii tafsiri ya …PPU yani presidential protection unit,hiki ni kikosi maalum cha ulinzi wa rais mpiana kiko tayari tayari wakati wowote kunapotokea maafa ya usaliti ndani ya bendi kubwa kumlinda rais asiadhirike wakati anatafakari cha kufanya kuziba nafasi ya msaliti yeyote alie ondoka kundini

 11. Hadj Le Jbnique says:

  Tabou Fatu Top Model a.k.a.mamaa na compressoo,huyu ni mwanadada mrembo mcongoman mfanyabiashara anaeishi Bruxells Ubelgiji,anamiliki maduka makubwa ya nguo(Boutique)huko ubelgiji na ufaransa,ni mrembo kweli na anajua kujipigilia pamba,hapa katopa simple tu lakini kapendeza,JB aliwahi kumtungia wimbo mzima acha kumtaja mara kadhaa kwenye nyimbo zake,pia fallly ipupa ana wimbo aliutunga kwa heshima ya mwanamama mjasiriamalia huyu wa kiafrika

  http://parmislesmomis.skyrock.com/photo.html?rev=5

 12. Anonymous says:

  Ahsante sana Mukubwa!!!!

 13. Admiring the dedication you put into your blog and detailed information you provide. It’s good to come across a blog every once in a while that isn’t the same unwanted rehashed information. Wonderful read! I’ve bookmarked your site and I’m including your RSS feeds to my Google account.

 14. We stumbled over here coming from a different web page and thought I might as well check things out. I like what I see so now i am following you. Look forward to looking over your web page for a second time.

 15. Its my excellent pleasure to go to your blog site and to enjoy your fantastic posts right here. I like it a good deal. I can come to feel that you paid significantly focus for those articles, as all of them make sense and are really valuable.

 16. Thanks for your post. What I want to say is that when you are evaluating a good on the net electronics go shopping, look for a site with entire information on key elements such as the security statement, safety details, any payment options, and other terms in addition to policies. Generally take time to read the help as well as FAQ pieces to get a superior idea of how the shop is effective, what they can perform for you, and in what way you can make use of the features.

 17. Admiring the commitment you put into your blog and detailed information you provide. It’s great to come across a blog every once in a while that isn’t the same outdated rehashed information. Great read! I’ve saved your site and I’m adding your RSS feeds to my Google account.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: