SABABU RASMI ZA MGAWANYIKO WA WENGE MUSICA BCBG 4X4 TOUT TERRAIN NA MIAKA MITATU YA MWANZO YA BCBG NA MAISON MERRE (Sehemu ya II)

Majuzi tuliona jinsi Wenge kuanzia Mwanzo ilivyoaanza mpaka ilipofikia kumeguka kwa JB Mpiana na Werason (Kama uliikosa bofya hapa), Leo hii tunaanza kuiangalai Wenge BCBG ya JB Mpiana. Endelea…

Shukrani za kipekee kwa Hadji Le Jbnique kwa kukokotoa na kutohoa habari hii mpaka leo unaisoma wewe, Respect Grand Rapids nakati ya USA.

image

Adolph Dominguez, Blaise Bulla, Werrason, Didie Masela na Allain Makaba

walikuja kushtuka na kugundua Kina werra hawako nao tena wenge ilipopata contract kwa jitihada za SIPE kwenda kutumbuiza Ulaya Katika ukumbi wa BATACLAN,Paris na wakati huo huo kuitumia nafasi hiyo kwenye kufanya album ya TITANIC huko huko Paris

Wenge BCBG ilizaliwa JB Mpiana akiwa kiongozi wa bendi,Blaize Bula akiwa Chef d’orchestre,Alain “Prince” Makaba akiwa artistic Director na SIMON SIPE akiwa producer. Waimbaji wakiwa JB mwenyewe, Alain Mpela, Aimelia Lyase Demingongo na Blaize Bula, wapiga guitar Alain Makaba,Burkinafaso Mbokalia na Japonais(solo & rhythm),Patient Kusangila(rhythm & Bass), Titina(Drums), Ali Mbonda, Seguin Mignon(Tumba), Theo Bidens (keyboard), na Powerful AtalakUs toka kwao Roberto Ekokota “Le Grand Chibuta na Tutu Caluggi.

image

Kundi la Wenge Musica BCBG 1987, Kwenye Mic ni Werrason na JB Mpiana, Picha na Wikipedia

Mwanzoni wanamuziki wengi wa kawaida kundini humo akiwemo Alain Mpela ambae amekiri walikua hawajui kinachoendelea walikua wakidhani bado ni wenge musica ileile moja kwa kuwa mpaka nyimbo za album ya TITANIC walizifanyia mazoezi pamoja (nadhani ndio maana hata tukisikiliza kwa makini TITANIC na FORCE INTERVENTION RAPIDE zinavyoanza ni kama zinafanana)na kwa wenge walivyokuwa wanafanya kazi,ilikua ni kawaida kwao wakati mwingine kupiga show hasa local wakiwa hawajakamilika wote,sometimes wanaweza kuwepo wote akamiss labda makaba na blaize bula au hao wakawepo akamiss werrason, au wote wakawepo akamiss JB,

Hivyo basi kitendo cha werra,adolphe na didier masela hakikuwashangaza na kuwafanya wahisi labda kuna mgawanyiko wa bendi tayari,wakajua ni utamaduni wa wenge wa kawaida si unajua mastaa wakiwa kundi moja tena,japo walikua wanajua mitafaruku imekuwa ikiendelea mara kwa mara katika maisha ya wenge lakini si yakufikia kuzigawa bendi.

Lakini walikuja kushtuka na kugundua Kina werra hawako nao tena wenge ilipopata contract kwa jitihada za SIPE kwenda kutumbuiza Ulaya Katika ukumbi wa BATACLAN,Paris na wakati huo huo kuitumia nafasi hiyo kwenye kufanya album ya TITANIC huko huko Paris.,ndipo katika hali isiyo ya kawaida wakiwa na katika maandalizi ya ziara hiyo ambayo hupewa kipaumbele sana na wanamuziki wa congo wakawa wanashangaa mbona jamaa hawaonekani hata mazoezini wakati kuna safari nzito kama hiyo!na ilikua ni katika kipandi hicho hicho pia ambapo Ali Mbonda akaingia kwenye historia ya kuwa mwanamuziki wa kwanza kuitosa bendi mpya ya WENGE BCBG kwenda kwa kina WERRASON baada ya jina lake kutokuwemo kwenye trip nyeti kama hiyo huku jina la msaidizi wake chipukizi wakati huo katika kupiga mbonda (tumba) Seguin Mignon likichukua nafasi yake(Seguin sasa hivi ndio mpiga drums namba moja wa BCBG).

Kwa hiyo hiyo ndio ikawa safari yao ya kwanza ulaya bila kina werrason,wakapiga show hiyo hapo chini kama wanavyoonekana huku wakihitajika kutoa maelezo ya kina kwa mashabiki kuwaeleza kilichotokea huko nyumbani Kinshasa na kupelekea kujiweka pembeni na wenzao(werra,adolphe na masela),Ekokota yupo kundini hapo anaonekana akifanya kazi na Tutu Caludji “no.1”.

na

Baada ya Ali Mbonda kujiondoa kundini baada ya kukerwa na kutojumuishwa kwenye safari ya ulaya jambo ambalo limekua la kawaida mno kwa Ali na wanamuziki wengi offcourse wa congo wanapokosa kuwemo kwenye tour za Ulaya,Mtu wa pili kujiondoa BCBG akawa ROBERTO EKOKOTA mara baada ya concert hiyo ya BATACLAN hapo juu aliamua kupumzika kutokana na matatizo ya kiafya hali iliyomfanya ashindwe hata kuweka Atalaku zake kwenye album ya TITANIC na kumuacha Tutu Caludji amalize kila kitu mwenyewe,ndio vile tunaisikia TITANIC mpaka leo,pale ni bila le Grand Chibuta Ekokota,angeshiriki sijui ingekuwaje,mi sijui tuwaachie wenyewe!.

Baada ya kumaliza recording ya TITANIC walirejea nyumbani congo wakimuacha Alain Makaba huko ulaya kwake ambako alishakua amehamia. Walipofika Congo wakawakuta kina werrason ndio wameshaitengeneza bendi yao wanajiandaa Force Intervention Rapide(Lakini walikua bado hawajaipa hilo jina, maana nalo lina hadithi yake halikuja tu kama mvua),Baada ya mapumziko mafupi ya safari ya ulaya kazi ikaanza kwa Chef d’Orchestre Blaize Bulla Kuanza kutafuta vijana wa kuwa recruit. Hapa walihitaji mpiga bass yani pure bassist atakaeziba pengo la Didier Masela badala ya kumtegemea Patien Kusangila ambae kiasili alikua ni mtu wa rhythm guitar,pia walihitaji atalaku ataeziba pengo la Ekokota,kwa upande wa bass Blaize Bulla akaanza kumchokonoa Koffi kwa kuvamia ngome yake na kufanikiwa kumshawishi Sunda Bass ambae hata hivyo hakua na nafasi huko Quartier latin, alikua ni under ground bassist nyuma ya Fally Tyson na mwingine pia.

image

Engineer Blaise Bula, Alishiriki kwa Kiasi kikubwa kuiunda Wenge BCBG ya sasa.

Hivyo Sunda Bass akawa mtu wa kwanza kuwa recruited,baada ya hapo chini wenge bcbg chini ya Blaize Bulla ambae alipania kuisuka bendi upya ikawaita ma-atalaku wa tatu kuwafanyia majaribio ili wampate mmoja atakaemsaidia Tutu Caludji,miongoni mwa walioitwa ni Bidjana ambae baadae alienda zaiko huyu Genta Lisimo “Anti biotique” ambae wakati huo alikua akitokea Anti Choc kwa mzee Bozi Boziana,Tutu Caludji akamkubali zaidi Genta ambae nafasi yake kule kwa Bozi ikazibwa na Theo Mbala toka Big Stars ya Defao.

Engeneer Blaize Bula hakuishia hapo katika harakati zake za kuijenga BCBG, akaona kuna haja pia ya kuimarisha safu ya uimbaji kwa kuongeza waimbaji wachache,ndipo akawasiliana na rafiki yake na muandishi wa nyimbo zake wa siku nyingi toka enzi za wenge musica original ambae pia alikua muandishi wa nyimbo wa CHOC STARS na si mwingine bali ni JULES KIBENGA MAKIESE a.k.a. Jules Kibens(najua wengi mtashangaa lakini ndio ukweli),pia akamtafuta RIO KAZADI “rIO de janeiro” ambae alikua Chef D’ Orchestre katika bendi iitwayo JOLINO akiwa na akina KABOSE, CHAI NGENGE na baadae BILL CLINTON Pia alikua chini yake hapo JOLINO.

image

Hata Rais Kabila pichani amejaribu kwa uwezo wake kuwapatanisha wanamuziki wa Congo, kama ilivyo kwa picha hii.

Rio nae akamwambia Blaize Bulla kwamba kama anamtaka yeye basi pia amchukue na rafiki yake Chai Ngenge,Blaize akakubali hivyo wote wakajiunga BCBG,Pia kutokana na kutomuamini Burkinafaso kutokana na tabia yake ya kuhamahama Bulla aliamua pia kumchukua ALBA ACCOMPA aje asaidiane nae na kwa kuwa wote kundini walimjua ALBA kutokana na kwamba alishajaribiwa kundini wenge oariginal na kuonekana anafaa lakini akawa amechelewa wakati anajiandaa kujiunga na bendi ndio ikawa inavunjika.Baada ya hapo ikawa ni mazoezi tu na show za ndani,then wakapata contract nyingine kubwa ya kupiga kusafiri kwenda ulaya kupiga ZENITH na OLYMPIA,Safari ambayo ilizua mtafaruku mkubwa ulioitingisha sana BCBG Katika historia ya maisha yake,mtafaruku uliosababisha JB awe kama alivyo hivi tunavyomuona sasa na BCBG yake.

Je nini kilitokea….twende pamoja siku ya Ijumaa tutakapo kuwa tunakamilisha makala hii ya Historia ya kuvunjika kwa Wenge Musica na miaka mitatu ya mwanzo ya JB Mpiana na Werrason.

Kama una maoni usisite kuniandikia kwa piusmicky@yahoo.co.uk au SMS ONLY 0713 666616.

25 Responses to SABABU RASMI ZA MGAWANYIKO WA WENGE MUSICA BCBG 4X4 TOUT TERRAIN NA MIAKA MITATU YA MWANZO YA BCBG NA MAISON MERRE (Sehemu ya II)

  1. Anonymous says:

    MUNAKOSEAGA MUKISEMANGA JB HAKUFANZA KINDU, MI NILIIPENDANGA WENGE KWA SHABABU YEA JB MUPIANA, HAPA BURUNDI WATU BANAPENDAGA JB MUPIANA SHANA, KWA SABABU JB MUPIANA ANAPIGA MUZIK YA BATU BASTARAB SI KAMA WERA ANAPIGA MUZIKI YA BAHUNI GAHUNI,
    NAWAPENDA BATANZANIE NA HII BLOG NAIPENDAGA SASA

    BANDIA BANDA – BUJUMBURA

  2. Anonymous says:

    Mi sikatai JB Mzuri lakini Weraason ni mzuri kwenye Stage, na JB mzuri kwa kuimba pia

  3. Ntilya J says:

    Kaka Asante sana kwa Hii nimeipenda sana hii Story natamani uiweke yoote nisome leo kaka fanya hivo basi

    MDAU UK

  4. MAMA TABU FATOU LA TANZANIANE says:

    Ali Mbona nae bwana…yani kukosa safari ya ulaya ndio akanuna na kwenda kusemelea kwa werrason….ila jamani tuache utani namkumbuka sasa Roberto Ekokota kumbe nae alishiriki kuiandaa TITANIC japo hakurokodi kutokana na kuumwa,yuko wapi siku hizi kimaisha?Halafu hapo uliposema nyimbo titanic ya bcbg na force intervention rapid ya maison merre zinavyoanza zinafanana ni kweli kabisa,nimejaribu kuzikiliza vizuri nimekubali

  5. Anonymous says:

    kumbe engineer blaize bulla ndio aliwasajili jules kibens na chai ngenge ndani ya bcbg?kwanini tutu kaludji aliachana na bcbg,nilikua nampendaga sana

    • Hadj Le Jbnique says:

      chanzo cha tutu kaludji kuondoka wenge bcbg kina stori yake ndefu tu nikipewa nafasi huko mbele nitakimwaga hapa,lakini kiufupi sababu kubwa za wanamuziki wengi kukimbia bcbg miaka ya hivi karibuni baada ya kurelease anti terro ni mpiga drums na mwanamuziki ambae jb anampenda na kumsikiliza sana kama mdogo wake wa tumbo moja Seguin Mignon,huyu jamaa ukikosana nae lazima uondoke bcbg,je alisababisha nani na nani waondoke wenge na kivipi,stori inakuja stay tuned papa hapa tena mambo mengine seguin mignon aliyaanzishia hapo hapo bongo darisalama akayamalizia johanesburg south africa na kuwaondoa wana kadhaa kundini bcbg kwa support ya jb

  6. chembera says:

    habari waungwana….pamoja hatujafika mwisho wa makala hii…mi niseme tu NOEL ngiama wellason yuko juu…kwani ana-recruit vijana yeye hachukui wa zamani…angalia timu aliyonayo hivi sasa..ni hatari kama huamini tafuta ile live show ya ZENITH iliyotolewa na DIEGO ”MUZICA”.

  7. Mamaa President says:

    Ni kweli kabisa werra vijana wake wanampiga tafu sana anajua sana kuvumbua vipaji

  8. Ubeleji says:

    ur very right about olympia concert,i was there,watu wengi tulishindwa kwenda coz tuliogopa kamatakamata ya wahamiaji haramu.

    Mdau Brussels,

  9. Fatuma Mtanga says:

    Kumbe makaba na mpiana ndio ugomvi wao ulivokua,lakini mimi ningekua na uwezo wa kuwakutanisha ili warudi pamoja kupiga ningefanya hivo kwa kweli,walikua wanaelewana sana kimuziki,hebu angalia hapa chini jb anavyomrusha makaba mpaka anapandisha mashetani ya kicongo blaize bula anamtuliza kwa kumshika sikio,ilikua safi sana.

  10. mkemimi,Kigoma ujiji says:

    Mimi huwa najiuliza hivi kina makaba,jb,werrason na blaize bula huwa wanajisikiaje wakiitazama video kama hii

  11. […] muendelezo wa Sehemu ya Kwanza ambayo tuliona vile Wenge Musica BCBG ilivyo vunjika, na Sehemu ya Pili ttukaona Jinsi Wenge BCBG ilivyoundwa na sasa tuko Sehemu ya […]

  12. voice of tabora says:

    Blaize Bulla jembe….nalikubali kinoma papaa,bora jb angemrudisha waje waipaishe bcbg pamoja

  13. […] ya Sehemu ya Kwanza, ya Pili na ya tatu kuitazama wenge Bcbg ya Jb Mpiana, Alain Makaba na Blaize Bula ilivyoianza miaka mitatu […]

  14. […] ya Sehemu ya Kwanza, ya Pili na ya tatu  na majuzi ya nne kuitazama wenge Bcbg ya Jb Mpiana, Alain Makaba na Blaize Bula […]

  15. […] ya Sehemu ya Kwanza, ya Pili na ya tatu  na majuzi ya nne kuitazama wenge Bcbg ya Jb Mpiana, Alain Makaba na Blaize Bula […]

  16. […] hajaamua kutoka kivyake, Kama ulipitwa Aimelia aliondokaje Wenge BCBG gonga hapa. Sehemu ya Kwanza, ya Pili na ya tatu  na majuzi ya nne LD_AddCustomAttr("AdOpt", "1"); LD_AddCustomAttr("Origin", […]

  17. […] kundi la Maison Merre la Werrason na matatizo yake, Kama uliikosa angalia Sehemu ya Kwanza hapa, ya Pili  ya tatu  na  ya nne kuitazama wenge Bcbg ya Jb Mpiana, Alain Makaba na Blaize Bula […]

  18. […] ya Sehemu ya Kwanza, ya Pili na ya tatu kuitazama wenge Bcbg ya Jb Mpiana, Alain Makaba na Blaize Bula ilivyoianza miaka mitatu […]

  19. Faustine Kaguti says:

    Nakubaliana kabisa na mawazo yako,kwamba wenge music bcbg ilikua ni band nzuri hasa katika kizazi cha nne,je wenge el paris wako wapi kwa sasa kimuziki?

  20. Faustine Kaguti says:

    Nani alikua mtunzi wa wimbo wa top model wa wenge music bcbg?

  21. Frank says:

    Ukimaliza tupe na historia ya mgawanyiko wa Extra Musica na nimakundi mangapi yametokea kutokana na mgawanyiko huo

  22. SHIMITA KUCHA says:

    Dah iyo stor inanivutia sn nataka niwe najua mambo meng ya wenqe bcbg kwn huo ni mzuka wangu WASHKAJ wote wanajua bcbg ni zaid ya vpaj mpooo?

  23. sadjadi says:

    napenda nijuwe namna gani hili bendi la wenge lili anza mpaka wa kafika kufanikisha bendi kuendelea mbele na mpaka hapo jb mpiana aliku na umri wa miaka mingapi na werra nayeye alikuwa na mwiaka mingapi na hao wengine wana muziki walikuwa na zidiana miaka mingapi

Leave a comment