Awali ni awali na hakuna awali mbovu

September 8, 2011

289245_10150368921001495_762011494_9893583_969178972_o

330026_10150368923766495_762011494_9893609_677086014_o

Pichani ni Prof. Jay akiwa na Bi Kidude wakiburudika kwa “gahawa”, Inapendeza vijana wakichota hekima kwa wakongwe.


SABABU RASMI ZA MGAWANYIKO WA WENGE MUSICA BCBG 4X4 TOUT TERRAIN NA MIAKA MITATU YA MWANZO YA BCBG NA MAISON MERRE (Sehemu ya II)

August 31, 2011

Majuzi tuliona jinsi Wenge kuanzia Mwanzo ilivyoaanza mpaka ilipofikia kumeguka kwa JB Mpiana na Werason (Kama uliikosa bofya hapa), Leo hii tunaanza kuiangalai Wenge BCBG ya JB Mpiana. Endelea…

Shukrani za kipekee kwa Hadji Le Jbnique kwa kukokotoa na kutohoa habari hii mpaka leo unaisoma wewe, Respect Grand Rapids nakati ya USA.

image

Adolph Dominguez, Blaise Bulla, Werrason, Didie Masela na Allain Makaba

walikuja kushtuka na kugundua Kina werra hawako nao tena wenge ilipopata contract kwa jitihada za SIPE kwenda kutumbuiza Ulaya Katika ukumbi wa BATACLAN,Paris na wakati huo huo kuitumia nafasi hiyo kwenye kufanya album ya TITANIC huko huko Paris

Wenge BCBG ilizaliwa JB Mpiana akiwa kiongozi wa bendi,Blaize Bula akiwa Chef d’orchestre,Alain “Prince” Makaba akiwa artistic Director na SIMON SIPE akiwa producer. Waimbaji wakiwa JB mwenyewe, Alain Mpela, Aimelia Lyase Demingongo na Blaize Bula, wapiga guitar Alain Makaba,Burkinafaso Mbokalia na Japonais(solo & rhythm),Patient Kusangila(rhythm & Bass), Titina(Drums), Ali Mbonda, Seguin Mignon(Tumba), Theo Bidens (keyboard), na Powerful AtalakUs toka kwao Roberto Ekokota “Le Grand Chibuta na Tutu Caluggi.

image

Kundi la Wenge Musica BCBG 1987, Kwenye Mic ni Werrason na JB Mpiana, Picha na Wikipedia

Mwanzoni wanamuziki wengi wa kawaida kundini humo akiwemo Alain Mpela ambae amekiri walikua hawajui kinachoendelea walikua wakidhani bado ni wenge musica ileile moja kwa kuwa mpaka nyimbo za album ya TITANIC walizifanyia mazoezi pamoja (nadhani ndio maana hata tukisikiliza kwa makini TITANIC na FORCE INTERVENTION RAPIDE zinavyoanza ni kama zinafanana)na kwa wenge walivyokuwa wanafanya kazi,ilikua ni kawaida kwao wakati mwingine kupiga show hasa local wakiwa hawajakamilika wote,sometimes wanaweza kuwepo wote akamiss labda makaba na blaize bula au hao wakawepo akamiss werrason, au wote wakawepo akamiss JB,

Hivyo basi kitendo cha werra,adolphe na didier masela hakikuwashangaza na kuwafanya wahisi labda kuna mgawanyiko wa bendi tayari,wakajua ni utamaduni wa wenge wa kawaida si unajua mastaa wakiwa kundi moja tena,japo walikua wanajua mitafaruku imekuwa ikiendelea mara kwa mara katika maisha ya wenge lakini si yakufikia kuzigawa bendi.

Lakini walikuja kushtuka na kugundua Kina werra hawako nao tena wenge ilipopata contract kwa jitihada za SIPE kwenda kutumbuiza Ulaya Katika ukumbi wa BATACLAN,Paris na wakati huo huo kuitumia nafasi hiyo kwenye kufanya album ya TITANIC huko huko Paris.,ndipo katika hali isiyo ya kawaida wakiwa na katika maandalizi ya ziara hiyo ambayo hupewa kipaumbele sana na wanamuziki wa congo wakawa wanashangaa mbona jamaa hawaonekani hata mazoezini wakati kuna safari nzito kama hiyo!na ilikua ni katika kipandi hicho hicho pia ambapo Ali Mbonda akaingia kwenye historia ya kuwa mwanamuziki wa kwanza kuitosa bendi mpya ya WENGE BCBG kwenda kwa kina WERRASON baada ya jina lake kutokuwemo kwenye trip nyeti kama hiyo huku jina la msaidizi wake chipukizi wakati huo katika kupiga mbonda (tumba) Seguin Mignon likichukua nafasi yake(Seguin sasa hivi ndio mpiga drums namba moja wa BCBG).

Kwa hiyo hiyo ndio ikawa safari yao ya kwanza ulaya bila kina werrason,wakapiga show hiyo hapo chini kama wanavyoonekana huku wakihitajika kutoa maelezo ya kina kwa mashabiki kuwaeleza kilichotokea huko nyumbani Kinshasa na kupelekea kujiweka pembeni na wenzao(werra,adolphe na masela),Ekokota yupo kundini hapo anaonekana akifanya kazi na Tutu Caludji “no.1”.

na

Baada ya Ali Mbonda kujiondoa kundini baada ya kukerwa na kutojumuishwa kwenye safari ya ulaya jambo ambalo limekua la kawaida mno kwa Ali na wanamuziki wengi offcourse wa congo wanapokosa kuwemo kwenye tour za Ulaya,Mtu wa pili kujiondoa BCBG akawa ROBERTO EKOKOTA mara baada ya concert hiyo ya BATACLAN hapo juu aliamua kupumzika kutokana na matatizo ya kiafya hali iliyomfanya ashindwe hata kuweka Atalaku zake kwenye album ya TITANIC na kumuacha Tutu Caludji amalize kila kitu mwenyewe,ndio vile tunaisikia TITANIC mpaka leo,pale ni bila le Grand Chibuta Ekokota,angeshiriki sijui ingekuwaje,mi sijui tuwaachie wenyewe!.

Baada ya kumaliza recording ya TITANIC walirejea nyumbani congo wakimuacha Alain Makaba huko ulaya kwake ambako alishakua amehamia. Walipofika Congo wakawakuta kina werrason ndio wameshaitengeneza bendi yao wanajiandaa Force Intervention Rapide(Lakini walikua bado hawajaipa hilo jina, maana nalo lina hadithi yake halikuja tu kama mvua),Baada ya mapumziko mafupi ya safari ya ulaya kazi ikaanza kwa Chef d’Orchestre Blaize Bulla Kuanza kutafuta vijana wa kuwa recruit. Hapa walihitaji mpiga bass yani pure bassist atakaeziba pengo la Didier Masela badala ya kumtegemea Patien Kusangila ambae kiasili alikua ni mtu wa rhythm guitar,pia walihitaji atalaku ataeziba pengo la Ekokota,kwa upande wa bass Blaize Bulla akaanza kumchokonoa Koffi kwa kuvamia ngome yake na kufanikiwa kumshawishi Sunda Bass ambae hata hivyo hakua na nafasi huko Quartier latin, alikua ni under ground bassist nyuma ya Fally Tyson na mwingine pia.

image

Engineer Blaise Bula, Alishiriki kwa Kiasi kikubwa kuiunda Wenge BCBG ya sasa.

Hivyo Sunda Bass akawa mtu wa kwanza kuwa recruited,baada ya hapo chini wenge bcbg chini ya Blaize Bulla ambae alipania kuisuka bendi upya ikawaita ma-atalaku wa tatu kuwafanyia majaribio ili wampate mmoja atakaemsaidia Tutu Caludji,miongoni mwa walioitwa ni Bidjana ambae baadae alienda zaiko huyu Genta Lisimo “Anti biotique” ambae wakati huo alikua akitokea Anti Choc kwa mzee Bozi Boziana,Tutu Caludji akamkubali zaidi Genta ambae nafasi yake kule kwa Bozi ikazibwa na Theo Mbala toka Big Stars ya Defao.

Engeneer Blaize Bula hakuishia hapo katika harakati zake za kuijenga BCBG, akaona kuna haja pia ya kuimarisha safu ya uimbaji kwa kuongeza waimbaji wachache,ndipo akawasiliana na rafiki yake na muandishi wa nyimbo zake wa siku nyingi toka enzi za wenge musica original ambae pia alikua muandishi wa nyimbo wa CHOC STARS na si mwingine bali ni JULES KIBENGA MAKIESE a.k.a. Jules Kibens(najua wengi mtashangaa lakini ndio ukweli),pia akamtafuta RIO KAZADI “rIO de janeiro” ambae alikua Chef D’ Orchestre katika bendi iitwayo JOLINO akiwa na akina KABOSE, CHAI NGENGE na baadae BILL CLINTON Pia alikua chini yake hapo JOLINO.

image

Hata Rais Kabila pichani amejaribu kwa uwezo wake kuwapatanisha wanamuziki wa Congo, kama ilivyo kwa picha hii.

Rio nae akamwambia Blaize Bulla kwamba kama anamtaka yeye basi pia amchukue na rafiki yake Chai Ngenge,Blaize akakubali hivyo wote wakajiunga BCBG,Pia kutokana na kutomuamini Burkinafaso kutokana na tabia yake ya kuhamahama Bulla aliamua pia kumchukua ALBA ACCOMPA aje asaidiane nae na kwa kuwa wote kundini walimjua ALBA kutokana na kwamba alishajaribiwa kundini wenge oariginal na kuonekana anafaa lakini akawa amechelewa wakati anajiandaa kujiunga na bendi ndio ikawa inavunjika.Baada ya hapo ikawa ni mazoezi tu na show za ndani,then wakapata contract nyingine kubwa ya kupiga kusafiri kwenda ulaya kupiga ZENITH na OLYMPIA,Safari ambayo ilizua mtafaruku mkubwa ulioitingisha sana BCBG Katika historia ya maisha yake,mtafaruku uliosababisha JB awe kama alivyo hivi tunavyomuona sasa na BCBG yake.

Je nini kilitokea….twende pamoja siku ya Ijumaa tutakapo kuwa tunakamilisha makala hii ya Historia ya kuvunjika kwa Wenge Musica na miaka mitatu ya mwanzo ya JB Mpiana na Werrason.

Kama una maoni usisite kuniandikia kwa piusmicky@yahoo.co.uk au SMS ONLY 0713 666616.


Justin Timberlake na Lupe Fiasco kupanda Mlima Kilimanjaro

April 30, 2009

 JustinTimberlake460 Mwanamuziki Justin Timberlake na Rapper Fiasco Lupe wataungana na muimbaji Kenna katika kampeni ya Maji safi kwa kupanda Mlima Kilimanjaro.

Nia ya kupanda mlima kilimanjaro ni kuchangia mradi ambao ulianzishwa na Kenna ambaye ni mzaliwa wa Ethipia, ikumbukwe kuwa nyingi ya nchi za Africa bado suala la Maji safi ni kitendawili.

Justin amesema kuwa anakuwa akifanya mazoezi mara mbili kwa wiki ili kuzoeza mapafu yake kwa ajili ya kubeba hewa ya Oksijeni ya kutosha ambayo inahitajika sana wakati wa kupanda mlima huo wenye urefu wa M 5800.

Tutapanda kwa wiki nzima huku tukiwa na mzigo wa paundi karibu 30 mgongoni, kazi ni kubwa mbele yetu alisema Timberlake akiongea na GQ.

Naye Kenna alisema ”Baba yangu nusura afariki kwa ajili ya tatizo la maji miaka hiyo…” nina marafiki wengi sana ambao wako tayari kusaidia kampeni hii hivyo ni lazima tuifanikishe alisema Kenna.

Kwa mujibu wa mtandao wa gazeti la Guardian wastani wa wapandaji 10 hufariki kila mwaka katika harakati za kuupanda mlima huo mrefu kuliko yote Barani Afrika.

Waandaaji wamepanga upandaji ufanyike kipindi hiki cha majira ya kipupwe.

Nakuacha na kibao Whats Goes Around Comes Around toka kwake Justin Timberlake!!


Ni Grand Finale ya Maisha Plus

April 22, 2009
Washindaniao Million 10

Washindaniao Million 10

Shindano la Maisha Plus linafikia tamati Jumapili, ambapo mshindi ataondoka na kitita cha shilingi milioni 10 papo hapo baada kudumu kwa siku 56.

Shindano hilo lililoanza Machi 1,2009 linafikia tamati ikiwa ni sehemu ya kwanza na ya pekee katika historia ya mashindano ya uhalisia( Reality Shows) nchini Tanzania.

Mratibu wa shindano hilo, David Sevuri anasema shindano hilo linamalizika huku malengo yakiwa yamefikiwa kwa kiasi kikubwa.

“Tulilenga kuwawezesha vijana kujitambua,Kuwapa ujuzi kwa kuwafundisha vitu mbalimbali, Kuendeleza vipaji vyao,kuwapa mtazamo chanya wa maisha watazamaji na washiriki,kubadilishana utamaduni na kuburudisha watazamaji, tunajivunia kusema kuwa tumeweza kufanikisha yote haya” alisema.

‘Eviction’ ya aina yake kufanyika Jumapili

Shindano limebakiwa na washiriki 10 ambao mmoja kati yao ndiye atakayechukua zawadi hiyo kubwa hapo kesho.

Mtoano utaanza kuonyeshwa kupitia TBC1 Jumapili saa tatu asubuhi ambapo kwa kuanza saa nne kamili asubuhi washiriki wawili wataaga na baadae washiriki wengine wataaga saa saba kamili mchana.

Mtoano wa mwisho utafanyika saa mbili na nusu usiku ambapo shindano litakuwa limebakiwa na washiriki watatu tu.

Mpigie kura mshiriki umtakaye ashinde

Miloni kumi imetengengwa kwa mshindi lakini uamuzi wa kumpa mshindi upo kwa mashabiki ambao ndio waamuzi katika shindano hili.

Maulid 33, Hamis 15, Moshy 19, Abdul 32, Charles 11, Steve 14, Upendo 18, Boniface 20, Teddy 36 na Modesta 37.

Unaweza kupiga kura kwenye mtandao ambao ni maishaplus.g5click.com au kwa njia ya simu kwenda 15522.

Maisha Plus kurudi tena

Ni miezi miwili imepita tangu shindano hilo lianze, kutokana na uhalisia wa shindano hilo kureflect maisha ya Watanzania wengi wameomba liendelee kuwepo,kwa mujibu wa waandaaji shindano hilo litarejea baada ya mapumziko ya muda mfupi.

Mraribu wa shindano hilo David Sevuri ameliambia Starehe kuwa kutokana na maoni ya watu wengi shindano hilo litakuwa tena TBC1 baada ya timu ya shindano hilo kijipanga upya.

“Tutarudi tena tukiwa tumeliboresha zaidi shindano hili, lakini watazamaji bado watakuwa na vitu vingi vya kutazama kwa wakati wote ambao hatutakuwepo kijijini kwa kuwa tuna vitu vingi havijaonyeshwa” alisema.

Sevuri alisema kipindi cha Maisha Plus cha Jumapili kitaendelea kama kawaida kwa muda wote wakati ‘season’ II ikisubiriwa.

Thank you all
Regards
Julieth Kulangwa


Maisha Plus wiki hii

April 10, 2009

Charles na Steve Kikaangoni tena


Washiriki wawili kutoka Arusha ambao mwishoni mwa wiki hii waitolewa na kwenda kula bata katika hotel ya Grand Villa wamepigiwa kura tena na kurudi kikaangoni na sasa watapigiwa kura tena Jumapili hii.

Jumanne ya wiki hii washiriki hao walirudi kijijini baada kupigiwa kura za kwenda kula bata lakini wiki hii wawili watakaotolewa watarudi makwao moja kwa moja.
Wiki hii washiriki hao wamewekwa kikaangoni na washiriki wengine wawili kutoka Zanzibar na Mbeya, Asha na Nassib.
Wiki hii washiriki wawili watafunga pazia la kuondoka na shindano hilo litabakiwa na washiriki 10 wa mwisho.

Nani kuaga wiki hii, unaweza kumuokoa mshiriki wako kwa kumpigia kura kwenda namba Chaz 11, Steve 14, Asha 31 na Nassib 23.

Kukesha Masaa 48, Steve awa wa kwanza kulala

Baada ya washiriki wawili kurejea kijijini washiriki wakapewa task ya kushindania shilingi milioni moja kwa kutolala kwa masaa 48 kuanzia saa sita usiku Jumanne wiki hii.
Mshiriki kutoka Arusha pamoja na kulala kwa siku mbili mfululizo alijikuta akiwa wa kwanza kuanza kulala masaa matano tu tangu kuanza kwa shindano hilo.
Steve alilala saa 12.30 asubuhi ya siku ya kwanza na kufuatiwa na  Abdul na Maulid ambao kwa pamoja walilala saa tano asubuhi siku ya kwanza ya shindano hilo.


Waliomuua Lucky Dube walamba Mvua Maisha Jela!!

April 3, 2009

lucky_dube

Jaji wa Afrika Kusini amewahukumu watu watatu kifungo cha maisha jela baada ya kuwatia hatiani kwa kumuua mwanamuziki maarufu wa reggae Lucky Dube mwaka 2007.

Lucky Dube aliyekuwa na umri wa miaka 43, alipigwa risasi na watu hao watatu katika jaribio la kumuibia gari lake katika kitongoji kimoja cha mjini Johannesburg, tukio lililoleta hofu kwa taifa hilo.

Jamaa wa Lucky Dube walitokwa machozi na baadae wakashangilia baada ya kutolewa hukumu hiyo.

Mwandishi wa BBC Mpho Lakaje akiwa nje ya mahakama kuu ya South Gauteng anasema wanamuziki pamoja na mashabiki walikusanyika nje ya mahakama hiyo kuonesha mshikamano wao.

Mahakama hiyo ilielezwa kuwa washtakiwa hao watatu, walifikiria mtu waliyekuwa wakimpora gari alikuwa raia wa Nigeria na kamwe hawakufahamu waliyemuua alikuwa Lucky Dube hadi waliposoma magazetini siku iliyofuatatu hao watatu.

Moja ya mabango nje ya mahakama hiyo kwa mujibu wa mwandishi wa BBC lilikuwa likisomeka "Lucky Dube hafanani na Mnigeria; bali yeye ni Mwafrika."

Mahakama hiyo pia imewahukumu Sifiso Mhlanga, Julius Gxowa, na Mbuti Mabe kifungo cha miaka 15 kila mmoja kwa kufanya jaribio la kupora gari la Lucky Dube.

Source: BBC


Solo thang kaua kwenye Traveller!!

April 2, 2009

msafiri Kondo

Muziki wa Bongo Flava una historia yake toka ulipotoka na mpaka sasa na historia yake inafanana na mchezo wa Tv (Soap Opera) kwani walioanza wana ishia njiani ama kwa akufa au kupotea kimchezo na wengine kubakia mpaka mwisho wa Mchezo.

Kwa wanamuziki wa Bongo Flava naweza kusema historia yao inafanana kabisa na mchezo wa Televisheni kwenye mchezo huu kwani kuna walioanza nao waliishia njiani ama kufa kisanii au kutodumu game na mpaka sasa waliobaki wanahesabika.

Msafiri Kondo aka Solo Thang aka  Maulamaa aka Traveller anasema Traveller iko tayari kwa kusikilizwa.

Akizungumza nami punde Travellah kama anavyojiita mwenewe sasa anasema kwamba Albam itakuwa tayari mwisho wa mwaka hii ni kutokana na shughuli za Studio kuingiliana na Shughuli za kimaisha “…Album itakuwa na nyimbo 12..mwisho wa mwaka huu itakuwa tayari…yani kuanza sasa mpaka itakapo kuwa tayari ni takuwa narelease hits za kufa mtu alisema Solo thang.

Kuisikiliza Traveller Gonga Hapa!

Pia tuliwahi kufanya mahojiano ya kina ambapo aliongelea mambo mengi ikiwemo Mustakabali wa Muziki huu wa Kizazi Kipya Gonga hapa upate kujikumbusha na kusoma aliongelea nini.


Kaujumbe kwa Mamiss!!

April 1, 2009

Mamiss na mguso wa jamii

Mamiss na mguso wa jamii

Washiriki wa Miss Tanzania 2008 wakizungumza na mtoto aliyejitambulisha kwa jina moja la Josephine, aliyekuwa anatoka kuokota kuni katika vichaka vya Mjimwema Kigamboni Dar es Salaam. Hii ilikuwa mwaka jana wakati mamiss hao walipokuwa kwenye mchakato wa awali wa mashindano yao ya Umalkia wa Tanzania.

Mkuu Edwin Ndaki alitoa maoni ambayo napenda kuyaweka hapa ikawa ni ujumbe kwa mamiss. Nanukuu

“… Ninacho shindwa kuelewa ni kitu kimoja. Asilimia kubwa ya warembo wanajishughulisha na mambo ya jamii kama yatima wakichukulia kama ni moja ya ‘kigezo’ cha kupata tupoint na sio kama wanajitoa kweli.

Nasema hivyo,kwani asilimia kubwa wakisha twaa taji wataenda mara mbili tatu na TV,magazeti kuuza sura eti wanasaidia watoto baada ya hapo ni full mapedshee kwa kwenda mbele watoto wanatupwa.

Wakimaliza muda wao ndio kabisaa ..watakalia tu kunyang’anyana wanaume na skendo za ngono.

Ila pongezi kwa wale wanaoendeleza libeneke hata baada ya mashindano..Mfano Faraja Kota na wengineo..

pamoja mkuu siku njema”

Mwisho wa kunukuu nadhani message derivered!!


Kwenye Maisha Plus wiki hii!!

March 31, 2009

Kissa out!!

Mwanamke pekee aliyekuwa akiuwakilisha mkoa wa Mbeya, Kissa Kiposa ameaga mashindano haya Jumapili ya wiki hii.
Kisa ambaye alikuwa kikaangoni na washiriki kutoka Mwanza na Dar es Salaam, Maulidi Wadi na Upendo Peneza aliaaga baada ya kukosa kura nyingi za kumwezesha kuendelea kubaki ndani ya shindano hilo.
Kissa alilazimika kurejea nyumbani akiwa peke yake tofauti na ilivyozoeleka baada ya mshiriki mmoja kuondoka wiki iliyopita, Juma Madaraka.

Machalii wa Arusha kikaangoni

Machalii wawili wanaowakilisha pande za A Town, Charles Ngaja na Steve Sandhu wamewekwa kikaangoni lakini kama watapa kura nyingi hawatarudi makwao na badala yake watapelekwa kula bata katika hoteli ya Grand Villa iliyopo maeneo ya Kijitonyama.
Kama kawaida washiriki hao hawajui kama wamependekezwa na pia siku ya Jumapili kama wakitolewa hawata aambiwa kama kutolewa kwao ni FAKE.
Wasichana wawili kutoka Dar na Zanzibar, Asha na Modesta nao wanaiwania nafasi hiyo ya kwenda kula bata kwa siku mbili.
Washiriki watakao tolewa watakaa kwa siku mbili katika hoteli hiyo bila kuambiwa kinachoendelea na usiku wa siku ya Jumanne watarudishwa kijijini ambako pia wanakijiji wenzao watakuwa hawaufahamu mpango mzima.

King Kong atimba kijijini

Chidi Benzino akiwa na chama zima la Familia aliibukia kijijini usiku wa ‘Live’ ya mtoano na kufanya shoo ya ‘Surprise’ kwa washiriki wa shindano hilo.
Pamoja na kuburudisha Chid pia alizungumza na washiriki huku akipigwa maswali ya hapa na pale ambayo yalimlazimu pia kukanusha tuhuma za kuwa na Bif na Profesa Jay.
Washiriki walimuuliza kama kweli ana ugomvi na msanii huyo  naye kwa kifupi alikanusha kwa kusema kuwa hana bifu na msanii yeyote Bongo.

Namba za kupigiwa kura za washirki walioko kikaangoni

Charles 11,  Steve 14, Asha 31 na Modesta 36

Unaandika MP then namba ya mshiriki na unatuma kwenda 155222


Mnyalu kuendeleza mpambano wa Inspector na Mwana FA

March 30, 2009

 

Mnyalu kuendeleza mpambano wa Inspector na Mwana FA
Msanii Mike Mwakatundu a.k.a Mike T au Mnyalu ambaye hivi karibuni aliachana na ukapera kwa kufunga ndoa na mchumba wake wa siku nyingi ameibuka na kuendeleza malumbano yaliyoanzishwa na Inspector Haroun aliyejibu wimbo wa Mwana FA, ‘Bado nipo nipo’.
Mike T alisema kwamba, wimbo wake mpya wenye jina la ‘Wala wasielewe’ aliomshirikisha Mwana FA aliyeimba wimbo wa ‘Bado nipo nipo’ unawazungumzia wana ndoa ambao huzisaliti ndoa zao na kutafuta wapenzi wengine wa pembeni.
“Kwa kifupi nataka kuleta changamoto kwa wasanii wengine waliowahi kufanya nyimbo za aina hiyo wakiwemo Mwana FA na Inspector Haroun, sipendi watu wanifikirie vibaya kwa kuwa yote ni sanaa tu na si vinginevyo,” alisema Mnyalu.

Habari hii na Abdallah Mrisho (Gonga hapo umtembelee kujua mengi zaidi)


Maisha Plus Updates: Grace na Levina out!!

March 24, 2009

Mshiriki pekee aliyekuwa akiuwakilisha mkoa wa Tanga, Levina Abdon ameyaaga mashindano haya baada ya kutopigiwa kura nyingi ambazo zingemuwezesha kubakia katika shindano hilo .
Levina ambaye ameweka rekodi ya kuwa mshriki pekee aliyekuwa na ujasiri alikuwa akiwaukilisha mkoa wa Tnaga baada ya washiriki wawili kuodnolewa katika hatua za awali za shindano hili mapema mwezi huu.
Washriki waliokuwa wakiuwakilisha mkoa wa Tanga ni Ramadhani Runza na Athanas Milanzi ambao waliodnolewa katika  hatua za mwisho za shindano hilo lililofanyika Machi 1 mwaka huu.
Naye Grace Samuel amekuwa mshiriki wa kwanza kuondoka anayeuwakilisha mkoa wa Mwanza.
Zanzibar na Mwanza ndiyo mikoa pekee iliyokuwa ikiwakilishwa na washiriki wote watatu.mkoa huo sasa unawakilishwa na Asha Alfan na Abdulkhalim Hafidhi.

Grace, Modesta na Teddy wazimia

Toka Kushoto; Modesta, Teddy na Grace


‘Eviction’ ya wiki hii ilitawaliwa na vilio baada ya washiriki watatu kuzimia baada ya kupokea matokeo.
Washriki hao walizimia kila mtu akiwa na ‘emotion’ yake, Teddy alizimia baada ya kuambiwa anabaki kijijini wakati Grace alizimia baada ya kuambiwa kuwa anarejea nyumbani.
Katika hali ya kushangaza mshiriki mwingine ambaye hakuwepo hata kwenye ‘nomination’ alizimia kizimbani wakati akimwondoa Teddy aliyeanguka na kuzimia kizimbani.

Maulid Kikaangoni tena

Baada ya kumalizika kwa mchakato wa kuwatoa washiriki wawili Jumapili hii, washiriki wengine watatu walipendekezwa kuingia katika kikaango cha kupigiwa kura.
Washiriki waliopendekezwa wiki hii ni Maulid kutoka Dar es Salaam , Kissa kutoka Mbeya na Upendo kutoka mwanza.
Hii ni mara ya pili kwa Maulid kupendekezwa, wiki ya kwanza alipenya baada ya kuwa amependekezwa sambamba na Efrancia

Mangii na Putir Peter.

Mshiriki wa Dodoma atolewa kwa ugonjwa
Mshiriki  pekee aliyekuwa akiuwakilisha mkoa wa Dodoma , Juma Madaraka amelazimika kuyaaga mashindano haya baada ya kuugua Typhoid na Malaria kali kwa muda wa siku tatu.
Mshiriki huyo alilazwa hospitalini kwa siku tatu katika hospitali hospitali moja iliyo karibu na kijiji cha Maisha Plus.

TID aka Prison Voice atua kijijni

Khalid Mohamed, maarufu kama TID a.k.a Prison Voice alitumbuiza katika shoo ya Surprise iliyoandaliwa kwaajili ya washiriki hao dakika chache kabla ya kufanyika kwa ‘eviction’.
Washiriki walilipuka kwa shangwe ya aina yake kwa kuwa ilikuwa ni mara yao ya kwanza kumuona msanii huyo tangu alipomaliza kutumikia kifungo chake mwishoni mwa mwaka jana.
TID ambaye alimbatana na Inspector Felly aliyewahi kuwa mshiriki wa shindano la Tusker Project Fame mwaka jana.


Wimbo Mpya wa AY – Leo

March 19, 2009

Mwanamuziki ambaye kwa kiasi kikubwa amepata mafanikio makubwa katika Sekta ya Muziki wa kizazi kipya AY hivi karibuni aliachia nyimbo yake mpya Leo.

Nyimbo ambayo imeshika chat kwenye radio show mbalimbali akiongea nami asubui hii AY ambaye anarejea Kesho nyumbani Tanzania akitokea ziara yake ya USA amesema kuwa Video ya nyimbo hiyo ambayo imetengenezwa na Ogopa Djs wa Kenya na imefanyiwa jijini Dar es Salaam, pia AY aliongeza “…video ni noma sana nimezidi kuinvest zaidi ili ziweze kuchezwa kwenye stations kubwa zaidi na kubadilisha soko lilipo kwa sasa kama unavyoona kazi ilivyo”.

Gonga Hapa ukapate kuisikia nyimbo hii

KWa hiyo wapenzi wa muziki kaeni mkao wa kula video iko njiani,

Kwa wanaopenda Lyrics ya wimbo huo gonga hapochini

Read the rest of this entry »


Mahojiano ya Nakaaya na CNN-Inside Africa

March 18, 2009

Mwanamuziki Nakaaya Sumari jana alionekana kwenye kipindi cha CNN Inside Africa, si kitu kigeni lakini kwa wanamuziki tena muziki wa Kizazi kipya ambao ulianza kwa kutokukubalika haya ni mafanikio makubwa sana kisanaa na kisanii pia.

Aliongea nini aliulizwa nini bonyeza kitufe upate kuona mwenyewe


Pamoja na kutolewa Maisha Plus Putir alamba ajira TBC

March 18, 2009

 putirWakati shindano la MAisha Plus likiendelea na watu wawili kutolewa hivi karibuni, Mshiriki aliyetolewa bwana Putir amelamba ajira baada ya Mkurugenzi wa TBC Tido Mhando kumtangazia kibarua pale TBC FM baada ya kuvutiwa na kipaji cha sauti kwa kijana huyu.

Bado shindano hili linaendelea na kwa sasa washiriki watatu wako kikaangani ambapo majina bado hayajatajwa hadi siku ya Jumapili ndio yatatangazwa rasmi.

Maisha Plus ni shindano liliasisiwa na wajasiriamali wabunifu wa kitanzania wakiongozwa na Masud Kipanya baada ya Kuachana na kituo cha utangazaji cha Clouds Fm. Ama kweli njaa kipimo cha akili Kipanya nakukubali sana kwa idea ambazo ni endelevu. Kila la heri kaka.


Nakaay ndani ya CNN – Inside Africa kesho!!

March 16, 2009

Wadau wa mziki wa kizazi kipya watupie jicho katika kipindi maalumu cha INSIDE AFRICA kitakacho onyeshwa siku ya Jumanne 17-03-2009,Msanii wa mziki wa kizazi kipya Mwanadada NAKAYA na mahojiano yake na CNN kuhusu mziki huo,mwelekeo wake! na maana yake.

Pamoja na mambo mengine pia watamulikia suala la mkutano wa IMF na wadau uliofanyika DAr Es Salaam, Wataongelea maisha ya uvuvi ndani ya Pwani ya Dar Es Salaam na mambo mengine kadha wa kadhaa.

Katika intro ya Topic ya Nakaaya iko kama ifuatavyo "… "Bongo Flava" is a Tanzanian form of hip-hop music with a distinctive Swahili flare. The genre got its start in Dar es Salaam, and has become enormously popular around east Africa. Now, it may be about to reach a wider audience.

Sony Music recently signed "bongo flava" artist Nakaaya Sumari. David McKenzie caught up with the rising star while she visited her local stomping grounds and shared some of her experiences.

Kila la Heri


Efrancia na Putir out ndani ya Maisha Plus!

March 16, 2009

Kama tulivyoahidi awali kuwaleteeni updates za shindano la Maisha Plus,

Washiriki wawili waliokuwa wakiwakilisha kanda ya kati, Efrancia Mangii (kulia) na Peter Putir (Shoto) wameliaga shindano la Maisha Plus hilo huku Maulid Wadi akirejea baada ya kupata kura nyingi.

Washiriki hao wamefungua dimba la kuaga katika shindano hilo lililoanza wiki mbili zilizopita. Shindano hilo linabakiwa na mshiriki mmoja anayewakilisha kanda hiyo, Juma Madaraka.

Wakati huohuo Putir ameapta shavu la kutangaza katika kituo cha redio cha TBC Fm mara baada ya utolewa katia shindano hilo.

Mkurugenzi wa TBC, Tido Mhando aliitangaza ofa hiyo wa Putir baada ya uvutiwa na sauti nzuri ya mshiriki huyo.

Watatu kikaangoni tena

Washiriki watatu kati ya 16 waliobakia wametupwa tena kwenye ukanda wa hatari ya utolewa huu mchakato huo ukiendeshwa kwa namna ya pekee.

Mara baada ya kumalizika kwa shoo ya moja kwa moja ya kuwatoa washiriki wawili washiriki 16 waliobakia walitiwa kupendekeza majina ya watu wanaowakwamisha katika kazi zao wanazopewa kila siku.

Washiriki wawili kutoka Zanzibar, Abdulhalim Hafidhi na Grace Samuel walipendekezwa katika mchakato huku mshiriki pekee kutoka Tanga, Levina Abdon naye akianguka katika kikaango hicho.

Katika mchakato wa wiki hii majina ya washiriki yaliyo Katika kikaango hayakutajwa mbele ya washiriki na badala yake yatadhihirishwa jumapili wakati watakapotakiwa kutoka na kila kitu chao tayari kwa safari.

Hakuna jina la mshiriki litakalotajwa mpaka siku ya jumapili ambapo wote watakuwa na mizigo yao tayari kwa safari kwa watakaotajwa.

Imetayarishwa na Julieth Kulangwa


Mr Paul bado ang’ara ughaibuni!!

March 12, 2009

Mwanamuziki mahiri wa mtindo wa Zouk Mr Paul aliyeko nchini Austrlia atakuwa mingoni mwa wanamuziki wahamiaji wanaoishi nchini humo ambao kwa pamoja watatengeneza Albamu ambayo itapatikana sokoni mwaka huu.

Akiongea nami Mr Paul amesema kuwa Kwa sasa anaingia studio kumalizia ngwe yake na Albamu hii inatengenezwa na kampuni inayoitwa Multicultural art ambapo yeye ataingiza nyimbo mbili zinazojulikana kama NATAMANI na ASANTE SANA. Nilimuuliza Mr Paul je nyimbo hizi ameongelea nini naye akanijibu “Nitarecord nyimbo mbili  nyimbo zitapatikana World wide through eMusic, Amazon MP3 amd Nokia Music store worldwide, Si unajua music wa Zouk ni wa mapenzi, nyimbo hizo nazo zinamguso wa kimapenzi zaidi,

Pia Mr Paul aliongeza “Hii CD itatoka katikati ya mwaka huu. nadhani utakuwa ndio mwanzo wa safari yangu ya kimuziki hapa ughaibuni kwani tayari wanamuziki wengine wameanza kuonyesha interest ya kujiunga nami kuanzisha band. nitaendele kukupa info as things are proceeding.

Mr PAul ni mmoja wa wanamuziki ambao wamefanikiwa kimaisha kupitia Muziki ambapo alijisomesha na kwa sasa ameajiriwa na kufanya kazi nchini Australia akiwa anasimamia mradi wa kuelimisha rika wa Snake Condom. Tuliwahi kufanya naye mahojiano gonga hapa usome.Gamboot dance; Muziki ulioasisiwa na watumwa migodini!!

March 11, 2009

Unapozungumzia muziki wa Afrika utaongelea Muziki wa Kongo ambao kwa kiasi kikubwa umefanikiwa kutoka nje ya bara hili lakini ukiwauliza wenyewe hasa watakwambia Muziki wa Kusini mwa Afrika ndio hasa unawakilisha bara la Afrika kutokana kuenzi utamaduni wa muafrika.

Leo tutaangalia Gamboot Dance toka kusini mwa Afrika.

Gumboot dance ni aina ya muziki ambayo ni maarufu sana kusini mwa Africa, ikiwa imejizolea umaarufu huku Afrika ya Kusini, Botswana na hata Zimbabwe.

Gumboot ilianzia Africa ta kusini kwenye machimbo ya Dhahabu miaka hiyo kukiwa na utumwa ambapo waafrika walilundikwa kwenda kufanya kazi machimboni, Kutokana na hali ya machimboni walikuwa walivaa Boot miguuni ili kujikinga na matope, inasemekana walikuwa wakipewa muda mchache sana wa kupumzika na katika muda huu ambao walikuwa wakiutumia kupata chochote watumwa hao wa migodini walitumia kujisahaulisha machungu ya kazi ngumu kwa kucheza na kuimba na walicheza huku wakiwa wamevaa boot zao miguuni, katika kucheza huku boot zile zilitoa mlio wa aina yake na kufanya huo kuwa mrindimo wa Muziki ule.

Wapo wanaosema kuwa katika Machimbo yale watumwa hawa hawakurugusiwa kuongea na hivyo kuwa wakiwasiliana kwa kutumia ishara kwa kupiga boot zao na hiyo kuwa chanzo cha aina hii ya dance.

Wapo wanamuziki wengi ambao walishafanya hata maonyesho Ulaya akiwamo Culture and Spears toka Botswana. Ambapo yeye ameongeza vionjo kama kinanda na ala nyinginezo na kuunogesha zaidi muziki huu.

Pamoja na ukweli kuwa aina hii ya muziki imenogeshwa na vyombo vya kisasa bado uchezaji wake unafuata misingi ya gamboot hata kama wachezaji hawajavaa boot na utamaduni ndio huzingatiwa ikiwa ni kuvaa kitamaduni na nyimbo zake huwa zinakusudiwa kufundisha zaidi kwani zina story fupi fupi. Upangaji wa sauti na uchezaji wa kiustadi ndio vinavutia katika kuangalia video hizi ambapo mipigi yake imepoa na kutoa nafasi kwa sauti kutawala zaidi, aina hii ya Gumboot dance imekuwa maarufu zaidi huko Botswana ambako ni maarufu kama Tseswana Dance ambapo wao wamechukua zaidi uchezaji na kuongeza ala za muziki na kuimba zaidi, Wabotswana wanajulikana kwa mauombo yao mazuri (maumbo ya kiafrika) na hivyo kunogesha zaidi uchezaji wao (angalia video ya pili) ilihali kwa Wazuru wa Afrika ya kusini wao bado ni rhythim ya boot inatawala zaidi.

Pata kionjo hapa hii nakwenda pia kwa mwanangu kipenzi Baby Glory anawapenda sana hawa.

 

NA hii hapa


Wallah Original Komedi wamepinda….!! Wizi mtupu!!

March 8, 2009

Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete, Mama Salma, Jana(6.3.2009) alizindua sherehe za maadhimisho ya Sikukuu ya Wanawake Duniani, ambayo hapa nchini yalifanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam. Katika sherehe hizo, kundi la vichekesho la Orijino Komedi lilizua balaa bada ya kuibukia uwanjani hapo na kusababisha watu kukanyagana katika kutaka kuwaona.

Pichani Msanii wa Orijino Komedi, Isaya Mwakirasa ‘Wakuvwanga’ akapanda jukwaani kumuiga kwa kurudia akiyozungumza na sauti yake. Baada ya Mama Salma, kumaliza hotuba.

Pichani chini ni wasanii wa kundi la Albino wakicheza ngoma ya Sindimba.

Picha zote kwa hisani ya GPL.


Msafiri Solo thang yu njiani aja…!

March 3, 2009

.

Solo Thang AKA Traveller

“…Dawa ya Ush***zi Tema Mate…anaekuzidi nguvu kama Tyson mng’ate,kila unachotaka sio lazima ukipate,Juma bhalo wa Mombasa mpaka leo anasaka Pete….”

Huu ni moja ya mistari ndanyi ya mawe kwenye Albamu inayokuja ya mtu mzima Solo thang inayokwenda kwa jina la Msafirikatika safari kama msafiri ukikaa sehemu mmoja kwa muda mrefu lazima utajifunza tamaduni flani za eneo husika kituu ambacho jamaa mwenye style, vokal na vina vya kweli wa long time kitambo solo thang amejifunza katika safari zake nje ya bongoland… vitu hivi na vingi vinginevyo utavifeel kwenye album yake mpya kwa jina la traveler ambayo ndio yuko busy katika hatua za kuikamilisha kama ulikuwa hujui mzigo huu ambao atahusisha maproduza kibao wa hapa tz na mamtoni, utapigwa katika lugha mbili kiingereza aka ng’eng’e aka yai na kiswahili aka jazia mwenyewe….. nimepata kuskiliza radio single kutoka album hii, single ambayo imebeba jina la album hili kwa jina la travela na mchizi hajaloose step ya vina, mdunda, ujumbe na mikogo aka swagger ziko pale pale….. mimi ndio emcee mwenyewe nisie suka nywele/ sina hereni wala upara lakini kichwani nina vina tele/ mkono ni wa duke tachez wa tongwe records na kama vipi utaratibu wa mtu mzima solo ni kwamba produza wa bongo anamtumia beati na mchizi analace vokalz na kusend back kazi for mixiing…

Habari hii ni kwa mujibu wa Deejay Fetty, Bofya hapa umtembelee.

Tuliwahi kufanya mahojiano na Solo Thang bofya hapa usome

Ngoja nikurudishe nyuma nikukumbushe kwa Wimbo huu


%d bloggers like this: