Je wajua ni nini Kilichelewesha Albamu ya Anti Tero ya JB Mpiana Sokoni?

Na Hadj Le Jbnique, Boston, Massachusetts, Usa.

Wimbo Anti Terro

Mwaka jana tulichapisha makala za kuhusu kuparanganyika kwa kundi zima la Wenge BCBG na hatimaye kujitenga kwa Werasson na wengineo, Baada ya kuangalia kuanzishwa kwa kundi la Maison Merre la Werrason na matatizo yake, Kama uliikosa angalia Sehemu ya Kwanza hapa, ya Pili  ya tatu  na  ya nne kuitazama wenge Bcbg ya Jb Mpiana, Alain Makaba na Blaize Bula ilivyoianza miaka mitatu ya mwanzo kwa misukomisuko, kisha tukaitazama kuzaliwa kwa Wenge Maison Mere ya Werrason, Didier Masela na Adolphe vile ilivyoanza pia. Tuliona jinsi bcbg ilivyoondoka na lundo la wanamuziki wa iliyokuwa wenge musica original na kuwaacha Werrason, Masela na Adolphe wakibaki peke yao labda na jina wenge musica, kazi ya kujipanga upya na kurudi kwa kishindo ikawa ngumu kwelikweli, Pia tuliona jinsi WMMM alivyojipanga na ku recruit wanamuziki wapya kama Bill Clinton Kalunji, Celeo Scam na Flam Kapayaniliahidi kuwaletea ni kwa sababu gani Albamu ya Anti Terro ya Wenge BCBG alichelewa sokoni… Endelea sasa.

Kulikua na mambo mengi ya nje ya bendi na ya ndani ya bendi yaliyochangia album ANTI-TERRO ya BCBG kuchukua muda mrefu kutoka sokoni.Miongoni mwa mambo ya nje ya bendi lilikua ni suala la ugumu wa kupata visa za kuingia ufaransa na  ubelgiji kwa wanamuziki toka Congo, na kama inavyofahamika wanamuziki wa Congo walikua wakizitegemea studio zilizoko kwenye nchi hizo kwa ajili ya kazi ya kurekodi nyimbo zao.

Na tukija kwenye mambo ya ndani ya bendi,awali Jb alipanga album hiyo iwe na nyimbo nyingi za Alain Mpela ambae alikua ni kiongozi wa bendi (Chef De Orchestre) pamoja na nyimbo bendi ya vijana wadogo ya BCBG inayofahamika kama PPU (Presidential Protection Unit) ambayo Alain mpela aliipromote sana na mbili tatu za Jb Mpiana mwenyewe huku member wengine wakitakiwa kuweka tu vocals zao kwenye nyimbo za album hiyo bila wao kuwa na nyimbo hata moja,Alain Mpela alipewa chance ya kuweka nyimbo zake sita (6).

Lakini wakiwa kwenye maandalizi ya album hiyo huku wakisikilizia suala la visa na kuumizwa kichwa ni wapi watakwenda kuirekodi ama kuifanyia mixing album hiyo kama visa itaendelea kusumbua kukatokea sintofahamu kati ya Jb na Alain Mpela, rafiki yake mtiifu ambae alimchukulia kama mdogo wake (ikumbukwe Alain Mpela na mdogo wake Bouro Mpela kuna wakati walikua wanaishi nyumbani kwa Jb kama Herritier watanabe alivyowahi kuishi nyumbani kwa Werrason baada ya Jb kumwambia akasome kwanza shule apate degree ndio arudi BCBG).

Kilichosababisha sintofahamu hiyo ya Jb na Afande Mpela ni simu ambayo ilipigwa na Koffi kwa lengo la kumshawishi Alain Mpela ajiunge na Quartier Latin yake na badala yake simu hiyo ikapokelewa na Jb huku koffi akidhani ni Alain mwenyewe ndie aliepokea simu hiyo hivyo kuendeleza mazungumzo yao yalipokuwa yameishia.

Baada ya simu hiyo Jb alikasirika sana na kumuona Alain Mpela kama bonge la msaliti kwa kuwa licha ya ukaribu wao na yeye kumchukulia kama mdogo wake aki share nae mambo mengi hakuwahi kumtonya chochote juu ya mazungumzo yake na Koffi ambae alikua adui mkubwa wa Jb wakati huo, na Jb ana kitu kimoja mpaka leo, hakuna kitu asichokipenda kama usaliti. Hivyo basi kuanzia siku hiyo Jb na Mpela hawakua brothers tena, na ule mpango wa kumpa nafasi Mpela aweke nyimbo zake 6 kwenye ANTI-TERRO Jb akaufutilia mbali na badala yake akamuachia nafasi ya kuweka nyimbo zisizozidi tatu huku kukiwa na mipango ya kumvua u chef d’orchestre.

Kuona hivyo Alain Mpela akasusia kushiriki shows na mazoezi ya BCBG kwa wiki mbili na hatimae akatangaza kujiondoa kundini huku akitoka na single maalum kwa ajili ya kumuimbia na kumsifia adui namba moja wa Jb bilionea Didi Kinuani. Mpaka hapo Jb na kundi wakawa na kazi ya kuziaondoa nyimbo za Mpela ambazo walikua tayari wameshazifanyia sana mazoezi na walikua wakizipiga kwenye shows zao za kila weekend ndani ya Kinshasa na kuanza upya kuandaa nyimbo nyingine na kujipanga upya huku wakiwa hawana mfadhili wala mdhamini kama ilivyo sasa kwa makampuni ya bia ya Congo kutoa sponsorship,wakati huo walikua wakiwategemea matajiri wakubwa wapenzi wa muziki kama huyo Didi Kinuani ambae Jb alikua tayari ameshagombana nae baada ya Dikin kumuiba mke wa Jb mamaa Amida Shatur na kumfanya mkewe.

Alain Mpela “afande” alipoondoka kundini BCBG nafasi yake kama Chef D’Orchestre kwenye bendi ilizibwa na Tutu Caludji ambae awali alikua mkuu wa mambo ya nidhamu kundini ambapo nafasi hiyo na yeye alimuachia mpiga drums Seguin Mignon ambae De La Patria JB amekua akimpenda na kumsikiliza sana akimchukulia kama mdogo wake pia,vilevile Seguin ni mtu wa karibu sana na De La Forret WERRASON na ndio amekua kiungo kati ya JB na WERRA. Hali hiyo ya kuwa na ukaribu na JB ikamfanya Seguin awe na sauti kubwa kiasi cha kwamba ukigombana nae au kama hakutaki lazima uondoke BCBG.

Je unataka kujua nini kiliendelea? Soma hapa kesho…..

[cryptex]piusmicky@yahoo.co.uk [/cryptex]

12 Responses to Je wajua ni nini Kilichelewesha Albamu ya Anti Tero ya JB Mpiana Sokoni?

 1. Maghambo Philipo says:

  Papaa Pius Bamalaa, Nakuaminia sana Mukulu wangu unanifurahisha sana na hizi story naamini kweli wee ni kiboko na ni Presidaa Bana BCBG na Darisalama, ila Afande yuko wapi? hapa naona utakuwa umemfuta machozi mpiganaji mwenzetu Hadji ambaye anakufa kuitetea Wenge.

  Merci Mingi Papaa

 2. didistone says:

  Nasubiri kwa hamu muendelezo wa stori hii tamu,hakunaga kama sports na starehe

 3. paul samara says:

  sasa nimeelewa kwa nini ANTI TERRO haikua na mvuto,nyimbo nyingi hazivutii,ni albam iliyoingia sokoni na kuondoka bila watu kuifaham,nimeelewa.

  • mkemimi,kigoma,ujiji says:

   uko sahihi,hakuna kitu muhimu kama umoja(team work)mahali popote pa kazi unapokosekana upendo ni ngumu ku practice team work,ndicho kilichowatokea bcbg wakati huo nadhani

   • Stivin says:

    Kipindi hicho akapeleka show Bercy akatumbuiza ukumbi tupu akatoka analia kuwa Koffi alinunua ticketi zote ili asipate watu.

   • Best Cbd says:

    I’m kind of impressed with your writing skills. This is a highly descriptive and well written post. I am left breathless as a result of your smart insights on this article. Thank you a lot for giving your thoughts. There’s basic… but then there’s you. I have truly enjoyed looking at your website posts.

 4. Stivin says:

  Wakati huo JB alikuwa anaota ndoto kuwa yeye ndio mpinzani wa Koffi, Mopao alipotoa Monde Arabe (Dunia ya Waarabu) JB akaamua kuja na Anti terorism kutokana na vuguvugu la ugaidi lililougubika ulimwengu wa kiarabu., akaishia kuangukia pua!

 5. Anonymous says:

  jb hakua sawasawa kipindi iko jamani,ukiacha hizo vurugu za wanamuziki kundini kwake pia ikumbukwe yeye mwenyewe alikua na matatizo makubwa ya kifamilia kwani ni kipindi hicho mkewe amida Shatur alikua amemkimbia na kuolewa na rafiki yake,na ndio mana ukifuatilia utaona hata nyimbo nyingi kuanzia internet mpaka Anti terro alizozitunga yeye zilikua ni nyimbo flani za masikitiko zilizojaa mafumbo na hisia kali za kimapenzi japo alikua hamtaji Hamida kwa jina alikua akitumia majina tofauti,sikiliza nyimbo Jeannette huu hapa hata kama huelewi lugha tizama video utaelewa,pia kuna wimbo mungine Gay mbula humo ndo kalia sana kimapenzi mzee mzima,watu hawakuelewa mashairi yake ya kina ya mafumbo kwamba alikua akimlilia Amida shatur wake

  • Stivin says:

   Visingizio, baada ya kina Blaise Bula, Makaba, na Afande kukimbia JB aliishiwa kimuziki

   • Hadj Le Jbnique says:

    Huu kwako haukua muziki kaka?maana huu ndio muziki wenu mawerasonique huu wa kelele nyingi si ndio mnaoupendaga?

   • Stivin says:

    Kama ni kelele kwa nini zinapendwa? Hadji kila siku nakwambia nyimbo za Werra you tube zina hits zaidi ya milioni moja, nionyeshe hizo za Pettie Frere Mpiana unazoziita nyimbo zina hits ngapi?

 6. Hadj le jbnique says:

  Iko sio kigezo kwani wa2 wangapi wana access ya internet kaka?kuhusu issue ya bercy na kutumbuiza ‘viti’ sijui hata kama kuna ukweli,mi ninavyofahamu ni kwamba show pekee ambayo jb alipiga paris na haikupata mahudhurio makubwa ni ile aliyopiga a week after 9 11 ambapo marekani ilishambuliwa na wanaodaiwa kuwa magaidi walioziteka ndege,na kila m2 anaeishi ulaya au america kama alikuwepo miaka hiyo huko muulize ule mshikemshike wa kamata kamata ya waafrica ulivyokua,na kama unavyojua wengi wa africa wanaishi ughaibuni kinyume cha sheria,wengi hawana makaratasi so unategemea nani angetia pua yake kwenye show ya jb then arudishwe africa,na askari sehemu kama izo ndio wanapenda kuvizia cuz wanajua lazima watawapata wengi,hivyo utaona kwamba wachache wale waliohudhuria walikua ok kimakaratasi ya kuishi ulaya,lkn pia lazima ujue jb hakujipeleka bercy,kuna wajasiriamali waliamua kuinvest kwake kutokana na demand ya public kuonyesha yeye ndio alikua deal wakati huo,hakuna mjasiriamali anaeinvest bila kuwa na uhakika kwamba atapata faida baada ya kutoa gharama,bahati mbaya hutokea,ndio kilichotokea,muwekezaji hakujua kama 9 11 atakuja kumuharibia,jb kama jb hakua na hasara,alikua kishalipwa na yeye si kazi yake kupromote show bali kupiga muziki,hivyo ukimlipa then ukaacha kupromote show wa2 wasipokuja atatimiza wajibu kwa kutumbuiza viti..!

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: