SABABU RASMI ZA MGAWANYIKO WA WENGE MUSICA BCBG 4X4 TOUT TERRAIN NA MIAKA MITATU YA MWANZO YA BCBG NA MAISON MERRE – VII

Le marquis de maison mere cont…

Huu ni muendelezo wa ile story yetu ya Kuparanganyika kwa Wenge Musica BCBG na miaka mitatu ya JB Mpiana na Werasson pamoja na vijana wao, Kuingia na kutoka kwa vijana ndani ya hawa magwiji wawili.

Baadimage

a ya Sehemu ya Kwanza, ya Pili na ya tatu  na majuzi ya nne kuitazama wenge Bcbg ya Jb Mpiana, Alain Makaba na Blaize Bula ilivyoianza miaka mitatu ya mwanzo kwa misukomisuko, kisha tukaitazama kuzaliwa kwa Wenge Maison Mere ya Werrason, Didier Masela na Adolphe vile ilivyoanza pia. Tuliona jinsi bcbg ilivyoondoka na lundo la wanamuziki wa iliyokuwa wenge musica original na kuwaacha Werrason, Masela na Adolphe wakibaki peke yao labda na jina wenge musica, kazi ya kujipanga upya na kurudi kwa kishindo ikawa ngumu kwelikweli, Pia tuliona jinsi WMMM alivyojipanga na ku recruit wanamuziki wapya kama Bill Clinton Kalunji, Celeo Scam na Flam Kapaya

Shukrani za kipekee kwa Hadji Le Jbnique kwa kukokotoa na kutohoa habari hii mpaka leo unaisoma wewe, Respect Grand Rapids nakati ya USA.

 

Katika kikao hicho wote wakakubaliana bendi ianzishwe; wakaanza mara moja kazi ya kutafuta wanamuziki wengine wa kuwajumuisha kwenda bendi yao hiyo mpya wakiwa huko huko Paris. Wakati huo huo SIMON SIPE akawa amepata taarifa zao za kuanzisha hiyo bendi, hivyo kama mfanyabiashara akaona kuna opportunity ya kutengeneza pesa kwa kufanya nao kazi vijana hao wenye vipaji na majina pia, SIPE akawafuata na kuwashawishi wawe chini yake, baada kukubaliana terms wakasaini mkataba wa miaka kumi kufanya kazi chini yake. Baada ya kusaini contract SIMON SIPE mara moja akaanza jitihada za kumtafutia BABY NDOMBE visa ya kuingia Ufaransa ili na yeye aje kujumuika na wenzake kutimiza ndoto yao ya muda mrefu ya kuanzisha bendi, jitihada za SIPE kumleta BABY Paris aungane na wenzake zilikwamishwa na watu wawili wa maison mere (Elliot na Monib) ambao mipango ilipokuwa inaelekea kukamilika BABY alipoenda makao makuu ya Maison Mere pale Zamba Playa kudai Passport yake jamaa wakaizuia,hivyo mipango ya SIPE kumpeleka BABY Paris ikawa imekwama ama tuseme imekwamishwa.

Wakati huo huko Paris mambo yalikua yakiendelea kusonga mbele, bendi ikaanza na waimbaji JDT, FERRE, MABIALA, CELEZINO waliemchukua kutoka WENGE EL PARIS, BIVA RAY kutoka CUTTURAL PAYS VIE, DJOLOKIS kutoka PPU ya Jb Mpiana ambae alienda Paris na PPU, GEMOROSE kutoka PONDERATION 8. Wapiga  maguitar walikua JAPONAIS, PICASE, MIMICHE na drammer boy alitoka ACADEMIA ile iliyoasi kutoka kwa KOFFI. Kwa upande wa atalaku akawa mwenyewe BILL CLINTON.

imageWakaandaa Posters zikatawanywa Paris nzima  kwa ajili ya kutangaza concert yao ya kwanza hukohuko Paris. Kwenye suala la jina SIMON SIPE akasisitiza lazima  wajiite LES MARQUIS DE MAISON MERE na sio LE MARQUIS tu kama walivyokuwa wakitaka wao, SIPE alitaka kila mtu ajue hao ni waasi wa WENGE MAISON MERE kitu ambacho aliamini kingesaidia kibiashara na pia kingerahisisha kazi ya kuwatangaza. Wakatengeneza album yao ya kwanza wakaiita MIRACLES ambalo lilikua liwe jina la Solo album ya pili ya WERRASON, kuona hivyo WERRASON ikalazimika kubadilisha jina la album yake hiyo na kuiita TEMOIGNAGE.

BILL CLINTON akaendeleza tena uasi dhidi ya WERRA kwa kuziingiza animation au atalaku zake alizozitunga kwa ajili WENGE MAISON MERE kama ile “Kimbongila” na “Sukali sukali elengi” ambazo kama mtakumbuka CELEO pia alizifanya kwenye ALERTE GENERALE ya WMMM kwa sababu alidai walizitunga pamoja na BILL hivyo wote wana haki ya kuzitumia. Kiufupi ni kwamba vijana walianza vizuri na kila mtu Paris na Kinshasa aliwapenda, tatizo wakaanza kugombea madaraka, kila mtu kati ya FERRE, BILL na JDT alitaka atambulike kama kiongozi mkuu, kuona hivyo FERRE akajitoa na kuanzisha Le Marquis des Beaux Garcons,baadae BILL nae akaanzisha ya kwake akiita Le Samourals Des Marquis na JDT akabaki na jina lake LE MARQUIS,akiondoa DE MAISON MERE kuukwepa mkataba wa miaka 10 wa SIMON SIPE na LE MARQUIS DE MAISON MERE, Hivyo watoto wa Bongo wanasema SIPE ikawa imekula kwake safari hii. 

Msikilize JDT hapa akiwa na WMMM

Tutatazama kuondoka kwa Alain Mpela,Burkinafaso na Baade Tutu Kaludji ndani ya bcbg na pia tutatazama kwanini anti terro ilichelewa sana kutoka licha ya kukamilika mapema.

2 Responses to SABABU RASMI ZA MGAWANYIKO WA WENGE MUSICA BCBG 4X4 TOUT TERRAIN NA MIAKA MITATU YA MWANZO YA BCBG NA MAISON MERRE – VII

  1. paul samara says:

    sehemu ya saba ndio sehemu ya mwisho kwa historia ya wenge au kna sehemu ya nane na kuendelea?

  2. […] kwa kundi zima la Wenge BCBG na hatimaye kujitenga kwa Werasson na wengineo, Baada ya kuangalia kuanzishwa kwa kundi la Maison Merre la Werrason na matatizo yake niliahidi kuwaletea ni kwa sababu gani Albamu ya Anti Terro ya Wenge […]

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: