Techno Malewa 2 kuzinduliwa December

.

Mwanamuziki Werasson Ngiama Makanda amesema kuwa Albamu yake mpya ya Techno MAlewa II itazinduliwa mnamo Dec bila kutaja tarehe rasmi.

Akifafanua Werasson amesema kuwa Album hiyo itatoka katika CD mbili kila moja ikiwa na nyimbo saba (7). Pia werasson amewataja walishiriki kutunga kwenye albam hiyo kuwa ni pamoja na Kakol (2), Miel, Héritier, Capuccino, Ali Mbonda, Elliot Mondobe, “Eboa Lottin”, Café Rhum, na  Werrason (4).

Werasson aliyasema hayo hivi karibuni baada ya kumaliza ziara ya mafanikio kwa show kubwa za aina yake huko Bukavu na Goma.

Haya ni maeneo yenye watu wengi sana na pia kiusalama bado si shwari Gavana alipata wakati mgumu kuimarisha ulinzi kipindi chote Werasson alipokuwa akifanya show hizi. Madhumuni ya show hizi ni kutangaza amani kwani Werason ni balozi wa amani “L’Ambassadeur de la paix”.

“Watu walisahau adha ya vita na hali duni ya usalama na kuanza kucheza MAlewa na Lelelele” ilisema sehemu ya ripoti ya José Mpaka wa Digital Congo.

Katika ziara hiyo pia Werasson aliwatembelea wanawake ambao ni wahanga wa vita waliobakwa pamoja na watoto Yatima na kuwatumbuiza na Nyimbo zake huku akitoa misaada kwao.

Werasson alirejea Kinshasa siku ya jumanne na kuwaahidi wapenzi na mashabiki wake kuwa hiyo ndio itakuwa zawadi yake kwao ya Christmass.

 

2 Responses to Techno Malewa 2 kuzinduliwa December

  1. Randy Boyer says:

    giggidy 🙂

    here’s some very cool techno music if you’re bored 🙂

  2. My spouse and I stumbled over here coming from a different web address and thought I may as well check things out. I like what I see so now i am following you. Look forward to finding out about your web page repeatedly.

Leave a comment