Mnigeria agunduliwa kutumia dawa

October 11, 2010

M

shindi wa mbio za medali ya dhahabu baada ya kushinda mbio za mita 100 Damola Osayemi ameonekana kutumia dawa ya kuongeza nguvu mwilini.

Rais wa shirikisho la michezo ya Jumuia ya Madola Mike Fennel amewaambia wandishi wa habari Delhi kuwa Osayemi ameomba afanyiwe majaribio mengine ili kuthibitisha matokeo ya awali.

Ombi lake limekubalika na matokeo yake ni baada ya kikao kitakachosikiliza kesi hiyo.

Damola Osayemi

Osayemi, mwenye umri wa miaka 24 kutoka Nigeria alitangazwa kuwa bingwa baada ya bodi inayotawala mashindano kumnyang’anya Sally Pearson wa Australia ushindi katika hali ya utata.

Sababu zilizotolewa na bodi hiyo ni kwamba Sally alianza kukimbia kabla ya mlio wa bastola kulia.

Hii ni mara ya kwanza kwa mwanariadha kupatikana kutumia dawa za kuongezea nguvu mwilini kwenye mashindano haya mjini Delhi.

Osayemi alionekana kuwa na chembe chembe za dawa iliyopigwa marufuku ijulikanayo kama methylhexaneamine, ambayo ni hivi karibuni tu ambapo shirika la kupambana na utumiaji wa dawa za kuongezea nguvu mwilini kuipiga marufuku kwenye orodha yake.

Endapo vipimo vya pili vitathibitisha kuwa Osayemi alitumia dawa ya kuongezea nguvu basi Katherine Endacott, aliyemaliza wa nne nyuma ya Pearson na Osayemi atapandishwsa na kupokea medali ya fedha.

Hadi sasa hakuna maamuzi yaliyofikiwa kuhusu hatma ya medali, hadi jopo la wataalamu wa afya wathibitishe au wakose dawa za kuongzea nguvu katika vipimo vinavyofanywa kwa Osayemi.


Flava Nite na UTAKE

October 11, 2010
Habari nDo HiYO

ISSUE YA WIMBO WA TAIFA YAPAMBA MOTO, KAIJAGE APIGWA STOP NA TFF

October 11, 2010

Afisa habari wa TFF aliyesimamishwa kazi
Florian Rweyemamu Kaijage

Shirikisho La Mpira wa Miguu nchini (TFF) limemsimamisha kazi afisa habari wake, Florian Kaijage (pichani) kutokana na fedheha ya kushindwa kutimiza itifaki muhimu ya kupiga nyimbo za taifa wakati wa mechi ya Taifa Stars na Morocco jumamosi jijini.

Rais wa TFF Sir Leodegar Chilla Tenga amewaambia waandishi wa habari jijini Dar leo kuwa tukio hilo ni la aibu mbele ya Rais Jakaya Kikwete, mashabiki na wageni wengine na mbaya zaidi kwa vile mchezo huo ulionyeshwa katika luninga ndani na nje ya nchi, hivyo aibu hiyo imeshuhudiwa na wapenzi wa soka kote duniani.

Amesema TFF imemua kumwajibisha Kaijage kwa kuwa ndiye aliyekuwa amepewa jukumu la kusimamia jambo hilo. Aidha alisema wakati amesimamishwa kaijage ataisaidia timu itakayoundwa kuchunguza jambo hilo na kuongeza kuwa hatua zitachukuliwa kwa yeyote Yule atakayebainika kuhusika kwa tukio hilo.

Amesema jambo hilo halikustahili kutokea kwa kuwa liliishawahi kutokea wakati wa mchezo na Brazil ambapo safari hii wahusika walipewa jukumu la kuhakikisha kuwa wanazijaribu nyimbo zote siku mbili kabla ya mchezo na kuhakikisha kuwa hakuna hitilafu yoyote na wahusika walimuhakikishia kuwa hakutatokea dosari yoyote.

“Kushindwa upigaji nyimbo za taifa ni upungufu mkubwa kiutendaji na kama nilivyosema hapo awali ni aibu kwa taifa letu, napenda kwa niaba ya tff kuomba radhi kwa Mheshiwa Rais, wapenzi waliofurika uwanjani, Watanzania kwa jumla na wageni wetu kutoka Morocco” alisema tenga.

Alisema kuanzia sasa, hata kama mitambo ya uwanjani ni mizima, patakuwepo bendi za police/jeshi ama mitambo ya tahadhari kwa ajili ya nyimbo za taifa na matangazo mengine muhimu.

Aidha, wadau wengi wa soka, ikiwemo waandishi wa habari za michezo, wamefurahishwa na hatua hiyo, na wengi wameipongeza TFF kwa kuchukua hatua hiyo kwa kile walichodai kwamba hilo ni fundisho kwa waliopo na wataokuwepo baadae.
Hii si mara ya kwanza kwa Kaijage ‘kukanyaga nyanya’ ikikukmbukwa kuwa siku Brazil walipocheza na Taifa Stars uwanja huo huo wa Taifa, na mbele ya JK, kwenye luninga la uwanjani kulioneshwa picha za mafaili ya kazi badala ya kinachoendelea uwanjani. Pia nyimbo za Taifa za nchi hizo zilipatwa na kwikwi na badala yake zikasikikika ngoma za sindimba.
Kabla ya mechi na Morocco waandishi wa habari za michezo kupitia chama chao TASWA nusura wasusie kuandika habari za TFF kutokana na utata wa kuingia uwanjani, kinara kwa upande wa TFF akiwa Kaijage ambaye pia amekuwa akilaumiwa kufanya kazi zisizomhusu kana kwamba yeye ni Katibu mkuu na sio afisa habari.

Shindano la wabunifu wa mavazi wanaochipukia lafikia ukingoni.

October 11, 2010

The 8 Finalists for the Swahili Fashion Week Emerging Designers 2010 competiton with event Organizer Mustafa Hassanali

The Judges who selected the finalists for the Emerging Designers Competition from (Right) Jamila Swai (Middle ) and Michelangela Adams from Italian Embassy(Left)

Nane waingia fainal, wapata fursa ya kuonyesha kazi zao jukwaa la Swahili Fashion Week 2010.

“Contemporary Swahili” ni kauli mbiu ya shindano 2010

 

Hatimae majina ya wabunifu 8 wenye vipaji  ambao wameingia fainali na kushindania zawadi ya mwaka katika  onyesho kubwa la wiki la mavazi  Swahili Fashion Week 2010 wapatikana.

 

Uchaguzi wa wabunifu wa mavazi wanaochipukia umefanyika Septemba 10 katika hotel ya Southern Sun jijini Dar es salaam, ambapo majina 8 yalichaguliwa na jopo la majaji  wanne  ambao ni Jamila Swai ambae ni mbunifu wa mavazi hapa nchini, Mkurugenzi wa Sanaa Nsao Shalua kutoka Baraza la Sanaa la Taifa (National arts Council), Michelangelo Adam kutoka ubalozo wa  Italia hapa ncini na Mustafa Hassanali.

 

 

Wabunifu hao 8 waliongia fainali watashindana  katika kuonyesha kazi zao katika onyesho kubwa la wiki la mavazi Swahili Fashion Week litakayofanyika mwezi wa Novemba mwaka huu.

 

Mratibu wa Swahili Fashion Week, Ndugu Washington Benbella amesema kuwa “  Wabunifu wote 16 walikuwa wazuri  na wameonyesha vipaji vya hali ya juu, na  kuonyesha kuaTanzania ina vipaji vikubwa katika sanaa ya ubunifu wa mavazi”.

Wabunifu wa mavazi wanaochipukia waliofanikiwa kuingia fainali ni pamoja na Pooja Narendrakumar Jeshang, Abduel Urassa, Shaban Mfaume, Kelvin Boniface, Subira Rahma Wahure, Angelina Muna and Grace Kijo.

Majaji walikuwa na kazi ya ziada, kwani walikuwa makini katika kuangalia mambo mbalimbali ili kuweza  kupitisha majina 8 ya wabunifu wa mavazi wanaochipukia, kwani walilazimika  kuangalia uwezo katika ubunifu na kuchora, kwa kiasi gani mchoro unavitia, rangi iliyotumika katika mchoro na mambo mbalimbali yanayohusiana na ubunifu kwa ujumla.

Sahili Fashion Week ni jukwaa pekee linalowaleta pamoja wabunifu wa mavazi  na watengenezaji wa bidhaa za mapambo kutoka nchi zote zinazozungumza lugha ya Kiswahili, ili kuonyesha ubunifu wao, kuuza bidhaa wanazozalisha, kubuni ajira, sambamba na kutengeneza mtandao kwa wabunifu kutoka maoneo hayo wanayoongea lugha ya Kiswahili, sambamba  na kuhimiza dhana nzima ya kuthamini bidhaa zinazotengenezwa Afrika Mshariki.

Msisitizo zaidi umewekwa katika kuhakikisha kwamba sekta ya ubunifu inakuwa kikanda. Swahili Fashion Week inalenga kukuza sanaa ya ubunifu na kuwa jukwaa bora la kibiashara kimataifa kwa nchi za Afrika Mahariki.

Kwa mara ya tatu sasa Swahili Fashion Week imekuwa ikifanyika, ambapo kwa mwaka huu itafanyika November 2010, Dar Es Salaam , Tanzania .

Shindano hili linafanyika kwa mwaka wa tatu sasa, halina kikwazo cha umri, na linatoa fursa kwa watu wote wanaoamini kwamba wana kipaji cha ubunifu, na wanataka kuwa wabunifu. “Swahili Fashion Week ni jukwaa bora kwa wabunifu kuonyesha uwezo wao wa ubunifu na kuibua sindano la wabunifu wapya, ni jukwaa linalowawezesha watu kufikia malengo yao ”, aliongeza Mustafa Hassanali muandaaji wa Swahili Fashion Week.

 

Imetolewa na

Saphia Ngalapi
Media & PR Manager


White Shadow: Kengele nyingine dhidi ya haki za Albino Tanzania

October 11, 2010

Liron Sharoni ni mzaliwa wa Israel na mpiga picha wa kujitegemea ambaye anafanya kazi na “Cordon Press” ya huko Spain Barcelona ambako ndio maisha yake yalipo kwa sasa. Tulikutana kwenye facebook akiwa ni mmoja wa wadau waliojitokeza kutia saini petition ambayo lengo lake lilikuwa kukusanya saini ambazo zingekabidhiwa kwa Rais kwa ajili ya kuishinikiza serikali kuchukua hatua kutokana na mauaji ya Albino hapa Tanzania, Jitihada ambazo leo tumeona matunda kwanu ndipo taasisi kama Under the Same Sun waliamua kulivalia njuga na mafanikio makubwa yameshapatikana.

Shimon alikuja TAnzania mwanzoni mwa mwaka huu na alipiga picha nyingi ambazo hivi karibuni zitaonyeshwa kwenye jumba la makumbusho onyesho ambalo limepewa jina la White Shadows.