Tusker Project Fame Jumapili ya leo

October 10, 2010
Kuwa tayari kwa kuangalia kipindi cha Project Fame leo usiku kwenye kituo cha televisheni cha TBC, ni shindano la kusisimua linaloonyesha uwezo wa washiriki katika vipaji vya kuimba na kutawala jukwaa kaa tayari kwa shindano hilo linalokujia kwa hisani ya kinywaji cha TUSKER kinachotengenezwa na kampuni ya bia ya SBL.

Tchasho Mbala

October 10, 2010

Kwa wale wapenzi wa Muziki wa Kikongo watakuwa wanamjua au kumsikia Richard Tshasho Mbala aka Kashogi (Pichani na mkewe),ukisikiliza nyimbo nyingi za Congo utasikia jina hili, yeye ndiyo mdhamini mkuu wa Album ya Fall Ipupa (Droit chemin’) amemuoa Elvira Mujinga Mukuna,katika harusi ya kifahari ilifanyika huko Orléans (France), Inasemekana watu maarufu katika Congo na wanamuziki wakubwa wa Congo walialikwa ikiwa ni pamoja na wengine kupatiwa Ticket za Ndege kushuhudia harusi hiyo.
Shukrani kwa Big Producer Maghambo