Feux De L’Amour (Moto wa Mapenzi) Wimbo wenye ujumbe murua wa Mapenzi kwa kizazi cha sasa.

JB Mpiana ni mwanamuziki ambaye anasifika sana kwa Rhumba za uhakika na zenye mguso hasa,

Leo nitakuchezea kibao chake kinaitwa Feux De L’Amour akimaanisha mioto ya mapenzi.

Kwa wasiojua lugha iliyotumika humu JB Mpiana alikuwa akiongelea mapenzi ya sasa akiwalalamikia akinadada akisema kuwa yapo wapi mapenzi ya ukweli ya enzi za mababu zetu ambapo watu walikuwa wakipendana kiukweli tofauti na siku hizi ambapo akinadada wamekuwa wakichagua wanaume kila mtu anataka mwanaume aliyesoma, mwanaume alina kazi nzuri, mwenye pesa, inakuwaje kwa wale ambao hawajasoma? Inakuwaje kwa wale ambao hawana kazi nzuri na hawana pesa?

kiujumla ameongelea mtaguso wa mapenzi wa sasa ambapo nadharia nzima ya mapenzi ni unanini? wewe ni nani? na dhana hii ndio inayojenga mapenzi kwenye ulimwengu wa sasa.

Hii si tafsiri sahihi ni majumuisho ili kukupa nini hasa kimeongelewa kwenye wimbo huu, naungana na Bw. Shaibu Thabit ambaye amenitumia tafsiri ya Wimbo huu kama ifuatavyo:-

L’amour est-ce aimer ou etre aimer? Bien que L’amour soit Le symbole d’un sentiment partage, etre aimer n’est jamais le signe d’un bonheur parfait = Je mapenzi ni kupenda au kupendwa? ingawa mapenzi ni ishara ya kubadilishana hisia, kupendwa kamwe si maana ya faraja iliyokamilika.

Bolingo eza maladie mabe dokotolo nango motema symptoma nango souci, kasi kisi nayango se presence ya motooyo ozali kolula, Lokola nalula masiya ye nde kisi nangai= Mapenzi ni ugonjwa mbaya, Dalili yake ni mawazo lakini dawa yake ni kuwepo kwa umpendaye,kama navyompenda Masiya(Yesu) ndio dawa yangu.

Bolingo lokola maladie contagieux tuna na bamoureux decus tuna na B’aveugles d’amour surtout na badivorces, Bakopesa yo temoignage na bango okoyoka mawa, okoyoka ngolo, okotikala stupefart, se kokamwa kamwa mama, se koimbaimba mama, se kotuna tina nzambe akela L’amour = Mapenzi kama ugonjwa wa kuambukiza lazima uwaulize waliokosa kupendwa, waulize vipofu wa mapenzi, waulize walioachika watakupa ushuhuda wao, utawaonea huruma,utakarahishwa, utastaajabika, Utakuwa unashangaashangaa mama, na kuimbaimba na kujiuliza kwa nini Mungu aliumba mapenzi.

Yango na po na nga Amida, hata na pasi tokovanda, hata bikebi tokoliya hata thomson tokotonda. Yesu kutu mwana ya nzambe babota ye na nandako ya mpata, Kasi mokili oyo ya tata naye, Likolo nase ya bango, kamweve o makamwisi mama = Kwa hiyo nimemchagua Amida katika mashaka tutaishi, hata samaki(thomson) tutakula tutashiba, Yesu ambaye ni mwana wa Mungu alizaliwa katika zizi la wanyama. Lakini dunia hii ni ya Babaye, mbingu na ardhi ni vya kwao Usishangae maajabu.

Na Kin Liboso ya kolinga moto bakoma kotuna ofandaka wapi, A biso tovandina mwalekwa nani akolinga biso mingi baboya bango na bango, Mosika eleki, bangungi baleki Taxi kutu eboya bango = Kinshasa kabla ya kumpenda mtu wamekuwa akiuliza unakoishi, Ah sisi tunaoshi Malekwa (Manzese,Uswahilini) nani atakaetupenda. Wengi wamekataliwa eti ni mbali mno mbu wamezidi huko hata Taxi haziendi huko.

Basusu liboso ya koloba Oui” bakoma kotuna otangaka wapi, Ah biso tubuka Bic mwa kala nani akolinga biso, Tika tokosa hata kokosa, Nga nazali graduet, Nga nazali licencie, Nga nazali enginieur, mpo balinga nga mama = Wengine kabla ya kusema ndio” huuliza ulikosoma wapi Ha sisi tuliovunja kalamu (Bic)yaani (kuacha shule) toka siku nyingi nani atatupenda, Wacha tudanganye mimi nina degree, mimi nina shahada ya juu, mimi mkandarasi ili tupendwe.

Basusu liboso ya kolinga moto bakoma kotuna de quele famille es-tu? Ah biso famille ezanga riche nani akolinga biso nzambe ya mpungu bandela mokili oyo otunaka mokomoko soki nani akolinga kobotama lisusu na famille ya pauvre. = Wengine kabla ya kumpenda mtu huuliza umetokea katika familia ya namna gani? Ha sisi familia fukara nani atakayetupenda,Baba Mungu rdia maumbile halafu muulize kila mtu kama yupo atayekubali kuzaliwa tena katika familia ya kimaskini.

Passe na nga eleki mabe yango naeffacer basouvernir nyoso ya mabe na bango nanga, memoir nanga eyebi kaka kombo ya Amida Chaty naye nde pelerinage edainayo petola nga mama sukolangamama, salisa nga nabika. = Maisha yangu yaliyopita ni mabaya ndio maana napenda kufufa zote mbaya kwenye ubongo wangu. Kumbukumbu yangu yajua tu jina la Amida Chaty Nimekuja kwako kama mpitaji,nitakase,nisugue nisaidie nipone.

Nalinga mindele,Bayindo,mikuse, milayi nalinga mike mpe minene, kasi chancelier wapi alatisanga palata ata bronzo hatanatolo, soit disant nga se amoureux,ancien de saio asala kala, roi de guere O mosala mpunda mama = nimependa weupe na weusi warefu na wafupi wembamba na wanene yupo wapi afisa zawadi hata medali ya chuma kifuani ieleweke kuwa mimi ni mpenzi mkongwe wa Saio( aliyepigana vita vya Saio mfalme wa vita Kazi isiyo na Mshahara……

Mtohoo huo ni mchango wa msomaji wangu maarufu Shaibu Thabit Mwambungu ambaye alikuwa nao kwenye maktaba yake.

Respect kwa wasomaji wangu wote, Mamaa Sophia Kessy, Pendejee Maghambo Philipo popote ulipo tuko pamoja, Julie ellyston Suvereign, Batty My Brother pamoja, Mukubwa Edgar Kiiza muzee ya Malaysia, Ally Tandika diwani muzee ya Azam, Mukubwa Six Mzee wa Matombo, Tom Baba Maya aka Chiluba, Mukubwa Gerald Kitima Baba Kara, Dulla Asumani muzee ya Tigo, Hadj le Jbnique, Patrol de Patrol Shaibu Thabit, Farid, bila kumsahau Swahiba Alhaj Tameem Mngoya Juma Ahmed Lukuta wa Kibanda Kicheba kwa Semkopi pamoja na Werasonique wooote, . Pamoja sana.

Nakutakieni Weekend njema.

Alamsiki.

Advertisements

10 Responses to Feux De L’Amour (Moto wa Mapenzi) Wimbo wenye ujumbe murua wa Mapenzi kwa kizazi cha sasa.

 1. Hadj le Jbnique says:

  MERCI MINGI PAPAA CHERIE LA TANZANIANE PIUS.

 2. Teddy says:

  Yaani umenisahau mimi wee kaka mbaya wewe . pamoja na kumwomba kaka Mwambungu atuwekee mambao hadharani. Safi saana haya ndiyo mambo tunayoyapenda na kutakiana amani sisi wana ukoo wa Wenge. Siyo kila siku kuvimbiana pua nani zaidi nani zaidi.

  Peace and Love

 3. piusmickys says:

  Teddy usijali nitakuwekea yako pekeyako wiki ijayo naweka Tour Eifel usijali sana, ila tuko pamoja na asante kwa support.

 4. farid from muscat says:

  oooooooooooooh merci mimngi papaa Pius zawadi yako nimeipata na nimefurahi sana otiki ngai nazua libomaa ya bana wenge

 5. Hadj le Jbnique says:

  Baada ya TOUR EIFEL ya kwake TITINA ALCAPONE enzi hizo akiwa na BCBG ndani ya TITANIC,unaweza kufikiria pia OMBA ya kwake mwenyewe Mpiana Tshituka pia iko na message nzuri ni Rhumba tunacheza taratibu as usual.Sasa inabidi tujiliwaze na nyimbo za zamani tu,maana SAYONS SERIEUX tuliyoisubiri for three years ndio hivyo tena ilivyotoka,kwa wapenzi wa sebene na ambao hawaelewi lingala japo kidogo itawaboa zaidi maana nyimbo nyingi including 4 za JB mwenyewe ziko katika style ya CONGO RHUMBA,no sebene/generique at all.Binafsi nimeipenda rhumba DJIKI DJIKI ya kwake mpiana mwenyewe.Album ina nyimbo 19 i.e. CD 1 & 2,But I insist for those who loves Rhumba Music & understand Lingala,album hii kidogo wanaweza ku enjoy but for foreigners ambao always wanajudge according to generique & sebene itawaboa sana,maana album yote CD 1 & 2 kuna generique 3 na sebene 2 ikiwamo TELECOMMANDE(Generique)na EZALA ZALA wimbo wa GENTA LISIMO unaoisha na sebene la nguvu but with a mute solo Guitar,Mikono ya PATOU SOLO haikupewa nafasi ya kutosha kufanya kazi yake.

  Kitu ninachikiona katika congo misic nowdays,hasa baada ya kuzisikiliza album za hawa Big Three in KIN,yaani JB MUKUBWA,DE LA FORRET WERRASON na PAPA FOLOLOO Le Shake spear du Congoo KOFFI yaani MALEWA(Werra)this SAYONS SERIUX(JB)na ABRACADABRA ya KOFFI ni kwamba miziki wa congo unaonekana kushuka(ninavyoona mimi si lazima mungine aone as me),kwani sizioni dalili zozote za hizi album tatu za hawa wakubwa kama zinaweza kudumu na kusikilizwa kwa angalau miaka 10 toka sasa kama tunavyoendelea ku enjoy kusikiliza FEUX DE L’AMOUR,TITANIC,LOI ya koffi au Hata angalau KIBUISA MPIPA ya WERRA.

  BUT NARUDIA HIVI NI JINSI NINAVYOONA MIMI NA HII NI TATHMINI YANGU MIMI BINAFSI.MERCI BEACOUP.

 6. Teddy says:

  Ohoo Papa Hadj thanks a lot for your expert opinion. Mimi nafikiri kadri umri unavyozidi kwenda na nguvu nayo huwa inapungua. Na nafikiri sasa ndiyo kipindi muafaka wa Kizazi cha Ferre Gola na Fally Ipupa kuja kuwashika.Ila jamani nitajifunza wapi Kilingala niweze faidi hii miziki ya zamani ya wenge.Maana enzi zile tulikuwa tunacheza tu pale Silent In. Hivi wewe kaka nawe tofauti ya Sebene na Generique ni nini?

 7. king says:

  mukubwa pius,tafsiri ya ‘omba’ndo kitu pekee nahitaji kupata kaka,tafadhali.sielewi maana yake lakini sijawahi kuchoka kusikiliza.

 8. Hadj le Jbnique says:

  Lingala mbona sio ngumu,kwa kuanzia hapa pitia hapa http://www.brighthub.com/aducation/languages/articles/46371,pia fuatilia tafsiri(sahihi)za nyimbo kwenye media-news papers na hasa TV na Redio.

  Sebene is the final part of congolese music,mwanzoni watu wanaimba kutoa message then mwisho wanaachia wapiga instruments wafanye kazi za mikono yao kwa kushirikiana na animateur na kelele zake.That is sebene,in short we can say it is the totality of all instruments plus vocals especially atalakus.

  Generique is just a show case of the sebene,haina tofauti sana na sebene but in generique hakuna kuimba,ni kufanya fujo mwanzo mpaka mwisho kupiga kelele za instruments and vocals,kutaja majina ya wapenzi na sponsors plus animation offcourse,inaonekana kama kitu kimoja lakini ukifuatlia kwa makini utaona vina tofautiana japo kidogo,katika muziki wa congo vinatofautishwa.

  Mimi bado naendelea kuiskiliza vizuri sayons serieux,kwa wapenzi wa rhumba sikilizeni “MBUA” ,”MOMBAMBA” ,”LONIATARA”,”ETOILE DU BERGER”,wapenzi wa sebene/generique sikilizeni “TELECOMMANDE” na “EZALA ZALA” i’m sure u’ll enjoy a lot.Kwenye TELECOMMANDEE mtamskia JB a.k.a. MUSWAHILI akiongea kiswahili akimsalimia rafiki yake Mukubwa Shabani HABARI GANI?

 9. Thanks on your marvelous posting! I truly enjoyed reading it, you may be a great author.I will ensure that I bookmark your blog and will eventually come back in the foreseeable future. I want to encourage one to continue your great work, have a nice afternoon!

 10. I want you to thank for your time of this fantastic study!

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: