Mwanamuziki wa FM Academia Afariki China kwa Unga, Wa Akudo akamatwa nao.

Marehemu Aristote Shungu Papa Tee enzi za uhai wake

Rapa wa Bendi ya Akudo Impact ‘Wazee wa Masauti’, Kanal Top Ambaye amekamatwa na Unga (pichani).

Habari zilizotufikia zinasema kuwa Mwanamuziki mahiri wa bendi ya FM Academia Alistoti Shungu amefariki dunia nchini china. Kwa mujibu wa mpashaji habari wetu anasema kuwa Marehemu Shungu ambaye wimbo wake ulitazamiwa kupigwa kuanzia leo kwa ajili ya kuitambulisha albamu mpya alifariki wiki iliyopita huko China alipokuwa amekwenda kibiashara.

250509

Marehemu Shungu enzi za Uhai wake akiwa na Presidaa Nyoshi.

Kwa mujibu wa habari inasemekana Aristoti Shungu ambaye alikuwa muimbaji na mtungaji amefariki baada ya Madawa aliyokuwa amebeba kupasuka tumboni. Shungu ambaye ni mzaliwa wa Congo alitokea hapa nchini na hivyo kuendeleza wimbi la watanzania na wapitio Tanzania kukamatwa na madawa ya Kulevya nchini China. Spoti Starehe imetumiwa picha za unaosemekana ni Mwili wa Shungu ukiwa Mochuary baada ya kufariki, kwa sababu ya maadili hatuwezi kuzitumia hapa.

Wakati huo huo habari zilizotufikia zinasema mwanamuziki mwingine raper wa kundi la Akudo Sound Kanal Top amekamatwa na unga hukohuko china.

Meneja wa Bendi ya Akudo Impact, Ramadhan Pesambili, Novemba 14, mwaka huu alisema kwamba wamepata taarifa za kushikiliwa kwa Kanal Top nchini China kwa tuhuma hizo.
“Taarifa hizo tumezisikia, tunazifuatialia kwa umakini mkubwa na kuweza kujua kama ni kweli ama la, maana zinachanganya sana,” alisema Pesambili. Aidha,  meneja huyo ameonesha kusikitishwa na habari hizo na kudai kwamba zinaichafua bendi yao kutokana na watu mbalimbali kumpigia simu kumuulizia juu ya taarifa hizo na wengine  kumfafanulia zaidi jinsi Kanal Top alivyonaswa.
“Kama meneja wa Akudo nasikitishwa na taarifa hizo, kwa kuwa Kanal Top hatuko naye zaidi ya miezi minne sasa, mwanzo aliaga anakwenda Kongo kuoa na  aliporudi aliomba ruhusa ya kwenda Dubai kufanya shoo ya wimbo wake wa Mama Vanesa nasi tukamruhusu kwa moyo wote.
“Wiki tatu zilizopita tulisikia habari za uvumi huo na tulipofuatilia tukagundua si kweli,” alisema meneja huyo.
Pesambili alisema kuwa hata Mzee  Kapuya (Juma, mmiliki wa Akudo) alisikia uvumi huo na akasema kama kweli Kanal Top anajihusisha na biashara hiyo basi asirudi kwenye bendi yake na ikiwezekana akamatwe kabla hajachafua hali ya hewa.
“Lakini  kabla hatujachukua hatua zozote ndiyo juzi tukasikia tena kuwa amekamatwa nchini China.
“Viongozi wa Akudo tumesikitishwa sana na taarifa hizo ingawa bado tunaendelea kuzifuatilia ili tuweze kujua zaidi, maana tunasikia amekamatwa akiwa na wanamuziki wa FM Academia, wengine wanasema alikuwa na mkewe,” alisema Pesambili huku akikiri simu ya China ya Kanal Top haipatikani.

Kwa sheria za nchini China mtu akikamatwa na madawa ya Kulevya anaweza Kunyongwa, kwani bado China haina mpango wa kubadilishana wafungwa na nchi ya Kongo DRC.

6 Responses to Mwanamuziki wa FM Academia Afariki China kwa Unga, Wa Akudo akamatwa nao.

 1. tungwe says:

  huyo marehemu wa fm Academia alishiriki nyimbo zipi

 2. Jabir Ahmad says:

  LOO!! POLENI SANA BEND YA AKUDO HAYA YOTE NI MAJARIBU TU.LAKINI MADAWA NI HATARI SANA KATIKA DUNIA HII.

 3. ramadhani kitana says:

  kitana apa ah sinameng ila faida ya shotcat ndoiyo

  • ramadhani kitana says:

   tena roo ina niuma kwasababu jina lanchiyetu linaharibiwa na watu wachache bas watz wote tunaonekana iyo ndotabiayetu,

 4. Anonymous says:

  nauliza kanal top nasikendo yasembe kaachiwa na yuko wapi , umajua nilizidi kupenda akudo kwajili yake rapar msofe mtoto yakipare

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: