Wenger; Nimeaibishwa na Man U

August 30, 2011

Arsene Wenger aumizwa kwa mabao 8-2

Arsene Wenger amesema ameaibishwa kwa kuzabwa mabao 8-2 dhidi ya mahasimu wao wakubwa Manchester United katika mchezo wa Ligi Kuu ya England.

image

Arsene Wenger

Wayne Rooney alifunga mabao matatu katika mechi hiyo ikiwa ni mara yake ya sita kupachika mabao matatu katika mechi moja kwenye uwanja wa Old Trafford huku Manchester United kwa ushindi huo wakikamata usukani wa Ligi hiyo na kumuacha Wenger akiendelea kukabiliwa na mzozo unaokuwa katika klabu ya Arsenal.

“Bila shaka unajihisi kuabishwa unapofungwa mabao manane,” alisema meneja huyo wa Arsenal. “Ilikuwa siku mbaya sana.”

Wenger amesisitiza ni mapema mno kusema kama sera yake ya uhamisho imeingia dosari kufuatia kuondoka kwa Cesc Fabregas na Samir Nasri na kukosa kiungo wa kuchukua nafasi zao.

Lakini hivi sasa anakabiliwa na kibarua cha kusajili wachezaji kabla ya dirisha la usajili halijafungwa siku ya Jumatano saa tano usiku.

Wenger, ambaye amesisitiza hatang’atuka, anatarajiwa kukamilisha usajili wa mshambuliaji wa Monaco, ambaye pia ni nahodha wa timu ya taifa ya Korea Kusini Park Chu-Young kabla muda wa usajili haujamalizika.

Pia anataka kusajili mlinzi wa kati na kiungo na Arsenal huenda ikarejea tena mbio za kumsajili mlinzi wa kati wa Bolton, Gary Cahill. Maombi yao mara ya kwanza yalitupwa.

Wenger, ambaye alianza kuwa meneja wa Arsenal mwezi wa Oktoba mwaka 1996, ameongeza kusema: “Hatuna budi kutafuta wachezaji wanaofaa na iwapo tutawapata tutawasajili. Pesa tunazo na iwapo tutawapata watakaoimarisha kikosi chetu tutafanya hivyo. Iwapo hatutafanya hivyo, basi itakuwa hatujawapata wachezaji hao wanaotufaa.

Baada ya Arsenal kufungwa vibaya mabao 8-0 mwaka 1896 ugenini na timu ya Loughborough Town katika ligi ya daraja la pili, Wenger ameongeza: “nahisi kufungwa huku kumetokana na hali maalum.

“Wachezaji wetu wengi hawachezi na tumecheza mechi tano tu. Tulichoka mwishoni lakini wachezaji wetu wanane muhimu hawakucheza.”

Meneja wa Manchester United Ferguson alitoa maneno ya kufariji akisema: “Tunaishi katika dunia iliyojaa kubeuana na vyombo vya habari vya habari vipo katika mashindano ya kutojali na kuwa tayari kumalizana.

“Ni vigumu kuelewa kwa wakati huu, lakini kazi iliyofanyika miaka 15 iliyopita sasa inaonekana ni ya ajabu sana.

“Alianzisha aina ya soka ya kipekee na mtindo wa usakataji soka wa aina yake na akachukua wachezaji wanaovutia kiuchezaji na pia amefanikiwa kuuza vizuri wachezaji. Hilo naliheshimu.”

Nahodha wa Arsenal Robin van Persie, ambaye alikosa kufunga mkwaju wa penalti uliookolewa na mlinda mlango wa United wakati Gunners walipokuwa nyuma kwa bao 1-0, amekiri timu yake haina budi kuimarika kabla ya mchezo ujao wa ligi utakaofanyika Emirates dhidi ya Swansea tarehe 10 mwezi wa Septemba.

“Hatuna budi kurudi katika mstari,” alisema mshambuliaji huyo. “Tutakabiliana na Swansea katika wiki mbili zijazo, ambao ni wapinzani wazuri na nausubiri kwa hamu mpambano huo.

“Sidhani kama tunaweza kujificha nyuma ya kivuli cha majeruhi ama kusimamishwa wachezaji. Hakuna kisingizio. Na wao wanao majeruhi pia, hii ni soka.”

Mlinzi wa zamani wa Arsenal Lee Dixon amesema Gunners tayari hawakupewa nafasi ya kutwaa ubingwa, lakini akasisitiza Wenger bado ni mtu anayefaa kwa kazi hiyo.


Eid Njema wadau

August 30, 2011

image


SABABU RASMI ZA MGAWANYIKO WA WENGE MUSICA BCBG 4X4 TOUT TERRAIN NA MIAKA MITATU YA MWANZO YA BCBG NA MAISON MERRE – (Sehemu ya I)

August 29, 2011

image

SURA MPYA YA BLOG NA MAMBO MAPYA!!!

Mengi yamesemwa sana kuhusiana na kuparanganyika kwa kundi hili na hatimaye kutokea Wenge zaidi ya sita huku mbili kubwa ya JB Mpiana na ya Werason zikionyesha upinzani wa hali ya juu.

Kuanzia wiki hii nitakuwa nikiwalete Makala ya Historia Ndefu ya WENGE MUSICA BCBG 4X4 TOUT TERRAIN NA MIAKA MITATU YA MWANZO YA BCBG NA MAISON MERRE. Ilikujua nini Hasa kilitokea baada ya kupata mwanya wa mmoja wetu kuongea na mtunzi wa kitabu cha Historia hiyo. Makal hizi zitakuwa zikikujia Kuanzia leo Jumatatu, Jumatano na Ijumaa ikiwa ni muendelezo, hivyo usikose kupita hapa Jumatatu, Jumatano na Ijumaa, kujua kwa undani nini kilitokea na kusababisha bendi hii ya kizazi cha nne cha Musiki wa Congo kuparanganyika, ungana nasi kwenye masimulizi haya ya kusisimua EXCLUSIVE. Shukrani za kipekee kwa Hadji Le Jbnique kwa kukokotoa na kutohoa habari hii mpaka leo unaisoma wewe, Respect Grand Rapids nakati ya USA.

imageNilibahatika kukutana na mdau mmoja mwana familia mwenzetu wa wenge ambae yeye amekwenda mbali kidogo,ameamua kuandaa kitabu maalum kwa ajili ya Clan ya wenge “THE STORY OF CLAN WENGE”,Kitabu ambacho mimi kwa mtazamo wangu nadhani kitatusaidia sana wana wenge family dunia nzima tujue nini hasa kilitokea mpaka wenge musica bcbg 4×4 Tout Terrain original kutokuwepo tena ulimwenguni na kuifunga kabisa ama kuipunguza mijadala ya malumbano baina ya wana familia wa iliyokuwa wenge musica ya ukweli.

Kitabu kitakua katika lugha mbili,kitakua mkifaransa na mkilingala lakini nimejaribu kumshawishi akiweke pia mkingereza ili watu wa afrika mashariki pia waweze kukisoma na kukielewa kwani nimemueleza kwamba pia sehemu hizo na zambia,malawi,zimbambwe ambako wanaongea zaidi english wapo wanafamilia wengi sana wenge,ameniahidi kulifanyia kazi hilo,hivyo likifanikiwa nadhani itakua ni fursa nzuri hata kwa wasiojua french au lingala kufahamu kilichojiri hasa kwa kuwa mwandishi amejitahidi sana kuzungumza na wahusika wakuu wa iliyokuwa wenge musica original kuanzia wanamuziki viongozi mpaka wanamuziki wa kawaida,mapromota mpaka maproducer na wadau wa karibu sana.

So stay tuned,kama kawaida yetu hapa,habari zote za muziki na wanamuziki wa congo na kinachoendelea katika muziki wa congo kila wakati sisi tutakua wa kwanza kuzipata zikiwemo hizi za kitabu hiki.

Lakini kwa kuwa nilifanya nae mazungumzo ya kina muhisika wa kitabu hiki,leo nitadodosa kidogo yaliyomo ndani ya kitabu hicho kwa kuwa nimefanikiwa kuzipata dondoo zake,ila naomba kudiclare interest kabla ya kuanza kwamba mimi ni mnazi mkubwa wa JB japo simchukii WERRA pia,ila kwa kuwa leo nimeruhusiwa kukaa kwenye jukwaa hili la heshima hapa juu joho langu la ushabiki naliweka kando ili niweze kuwa fair,hivyo mtaona sehemu ambazo jb atakua alichemsha nitamgonga bila kujali,sehemu ambazo werra alikua right nitampa credit zake bila hiyana.Twende pamoja sasa:

imageArticle hii ni sehemu tu ya kitabu husika ambayo inaelezea zaidi miaka mitatu ya mwanzo ya kila kundi yaani wengee BCBG kwa upande mmoja na wengee MAISON MERRE kwa upande wa pili,itatusaidia kujua nani alifanya nini na jinsi gani baadhi walijitoa tena kwenye hizo wenge mpya mbili baada ya muda mfupi.Lakini kwanza lazima tufahamu nini hasa kilikua chanzo cha wenge musica bcbg 4×4 kuvunjika.

WENGE iligawanyika na kusambaratika vipande viwili mwaka 1997 December kufuatia sintofahamu kati ya JB MPIANA na WERRASON, Huo ndio ukweli japo unauma. Yapo mambo mengi yalizungumzwa na yanaendelea kuzungumzwa kufuatia hiyo sintofahamu iliyopelekea mtafaruku huo wa mafahali hao wawili,wengine wakidai chanzo alikua ni mwanamke,wengine wakidai JB MPIANA alikua akikerwa na udhaifu wa WERRASON Katika udhibiti wa mapato ya bendi (werrason alikua ndio mtunza fedha wa bendi ikumbukwe) lakini pia kuna wengine wamekua wakidai chanzi ilikua ni chokochoko za Mzee Papa Wemba na Koffi Olomide ambao inasemekana walikua wakiionea wivu wenge kutokana na kuwa iliundwa na vijana wadogo wakati lakini ikawa haikamatiki kwa mafanikio.

Yote yanaweza kuwa majibu lakini sababu hasa iliyopelekea sintofahamu hiyo na hatimaye wenge kusambaratika kwa mujibu wa wahusika wenyewe ilikua ni mambo mawili,kwanza kabisa mafahali hao wawili iligundulika kwamba ni vigumu kwao kufikia malengo na matarajio yao ya hali ya juu waliyokua wameshayaingiza vichwani mwao wakiwa pamoja,kila mmoja alitaka kumpanda mwenzie kichwani awe mkubwa yeye,na jambo la pili alikua ni producer wao SIMON SIPE,yeye aliona anapata hasara ku deal na lundo la viongozi 6!(JB,WERRA,MAKABA,MASELA,DOMINGUEZ,BLAIZE BULA) ambao ukifanya nao kazi wote walikua wakihitaji treatment sawa, sasa ili kubana matumizi akaona ni bora kwa upande wake awepo kiongozi mmoja ambae atakua anadeal nae kwa ajili ya kushughulikia mambo mbalimbali yahusuyo production,na mapato yatokanayo na concerts na mauzo ya cd ambayo pia yalikua yakisimamiwa na SIPE,Hapa ikjitokeza kitu inaitwa Less Leaders Mo Money…!

image

Kwa hiyo mwanzoni mwa 1998,WENGE BCBG ikazaliwa ikijulikana mwanzoni kama WENGE MUSICA BCBG Lakini baadae wakaondoa neno MUSICA kutokana na kwamba Didier Masela ambae ndio muanzilishi wa hilo jina hakuwamo kundini humo,yeye alibaki na Adolphe na Werra,wakaamua kumuachia MUSICA yake.Sasa mpaka hapa tunaona BCBG ndio ilikua bendi ya kwanza ku exist,

Hivyo ili kutochanganya mambo nitaizungumzia kwanza miaka mitatu ya mwanzo ya BCBG then MAISON MERRE nitamaliza nayo.

Usikose Jumatano kwa kujua kwa undani kuhusu miaka mitatu ya Wenge BCBG ya JB Mpiana na kuondoka kwa watu kama Dominguez, Aimelia, Ali Mbonda na wengineo. Kama una lolote tuandikie piusmicky@yahoo.co.uk au tuma sms 0713 666616.

Hapa nitakuacha na kibao cha Promesse bouboule ikiwa ni utunzi wake shujaa Allain Mpela, hiki ni moja ya vibao vilivyowatambulisha kwenye jukwaa la muziki kitaifa na kimataifa. Salamu zangu za dhati kwako Big Producer Maghambo, Hadji Le Bcbgeeque, Jema Mandali nakati ya USA, Papaa Julie We Eston Ndenge nini Papaa, Mamaa Salma Jaruf nakati ya London, na funs wote wa Blog yangu nawatakia Eid El Fitr Njema. .


KUMRADHI

August 29, 2011

NDUGU WAPENDWA WASOMAJI, NIMELAZIMIKA KURUDISHA MUONEKANO WA ZAMANI HASA BAADA YA KUPATA MAONI YENU WADAU. TUNATHAMINI MCHANGO WENGU NA ASANTE KWA EMAIL ZENU TUTAREKEBISHA KADRI SIKU ZINAVYOKWENDA.
ASANTE
PIUS


Arsenal ina wenyewe bwana.

August 29, 2011

image


Man United, Man City zafanya mauaji EPL.

August 29, 2011

image

Kiukweli mashabiki wa Arsenal hawataisahau mechi ya jana na itabaki ni moja ya kumbukumbu za uchungu kwa miaka ya karibuni.

Wayne Rooney amepachika mabao matatu peke yake wakati Manchester United ikiinyuka Arsenal kwa mabao 8-2.

Young

Young na Rooney

Danny Welbeck ndiye alifungua karamu ya magoli baada ya kuunganisha pasi ya Anderson.

David De Gea aliokoa penati iliyopigwa na Robin Van Persi, na baadaye kidogo Ashely Young kufunga bao la pili.

Rooney aliandika bao la tatu na la nne kwa mikwaju miwili ya adhabu, kabla ya kufunga bao moja kwa mkwaju wa penati.

Nani na Park Ji Sung walifunga nao na Ashley Young kuongeza jingine.

Mabao ya Arsenal yalifungwa na Theo Walcott na Robin Van Persie.

Awali Manchester City waliizaba Tottenham Hotspur kwa mabao 5-1.

Edin Dzeko alifunga mabao manne, na Sergio Aguero akifunga moja. Bao pekee la Spurs lilifungwa na Younis Kaboul.

Kwingineko Newcastle United imeibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Fulham. Leon Best akifunga mabao yote ya Newcastle na goli la Fulham kufungwa na Clint Dempsey.

West Brom walishindwa kuutumia vyema uwanja wao wa nyumbani baada ya kuchapwa bao 1-0 na Stoke City. Goli hilo pekee lilifungwa na beki Ryan Shotton katika dakika ya 89.

Dondoo za Mchezo

image

image

 

image


Koffi Olomide na Quatier Latin ya enzi hizo.

August 28, 2011

Kipindi hiki mimi ndio naamini koffi alikuwa na wacheza show waliokamilika kila idara,akina mamaa Zina Bilao, Nonoo Diamaa (Nono Diamond) ambae baadae alitimkia BCBG na kukawa na taarifa za Jb kuwa na uhusiano nae kimapenzi at the same time Aimelia nae akijihusisha nae, hali inayoelezwa kupelekea Aimelia kukosana na Jb na kuwa ndio sababu ya Aimelia kutimkia kwa Werra, mambo haya yapo kwani hata kisa cha Patient kusangila kutopatana na werra inaelezwa ni sababu ya mcheza show pekee wakike aliekuwa wenge original Nana Sukari ambae werra alikua akimdate na kusangila pia, ndio maana hata kusangila alipojiunga na maison mere hakudumu, werra alikua anamfanyia visa ikiwemo kumuacha katika tour ya ulaya ndipo kusangila akatimka zake na kuhamia Paris.

Nikirudi kwenye kikosi hicho cha koffi enzi hizo katika wacheza show pia alikuwamo mrembo Miley kunde a.k.a. George Weah,Claudine AC Milan,pia kulikua na powerful atalakus toka kwa Mboshi Bola na mwenzie Parabolique wakipokezana hapo,kwenye bass alikuwepo Fally Tyson,drums Estetique,vocals za kufa mtu mtu zikiongozwa na mzee mzima mokonzi mwenyewe papaa na Didistone Koffi, Bouro mpela, suzukii 4×4 na wengine, hapo Fally Ipupa atii mguu naona labda alikua shule ya msingi

Mama Grace Artoi na Germany (Grace Diplomasia) hii yako mamaa, Mukulu Japhate wa Dallas Inn heshima kwako, Big Prodyuza Maghambo, Julie Weston BABA B kitokooooo!!


Tshobo; Fally Ipupa akimshirikisha Meje 30

August 27, 2011

Ametamba sana na kibao chake Delestage na hapa Spoti Starehe niliwahi kuandika kuhusu Mwanadada The New African Diva Meje 30 kama hukusoma gonga hapa.

Binafsi nilibahatika kumuona Live alipofanya Show ya Pamoja na Tshala Muana pamoja na JB Mpiana hapa Dar Es Salaam pale Ubungo Plaza. Ilikuwa show bab Kubwa.

Mwanadada huyu amepikwa na Tshala Muana anasemwa kuwa ndiye anayetegemewa kuibeba ngao ya wanamuziki wa Kike wa Congo akishirikiana na akina Cindy Olomide.

Mwanadada huyu anasifika kwa jinsi anavyoweza kutunga na kuimba msikilize jinsi walivyonata na beat akishirikiana na Bingwa wa Shindano la Miaka 50 ya Congo kwa kundi la wanamuziki walioimba Kifaransa Fally Ipupa kipenzi cha akina dada.

Ni wimbo ambao kila mmoja angependa kuusikiliza kwa jinsi walivyoimba vizuri. Nisiongee sana nikuache upate uhondo.


AY Anahitaji kura yako

August 27, 2011

image

Bofya hapa kupiga Kura yako


Re Union ya Zain Wenge

August 27, 2011

Hii ilikuwa Mwaka jana ambapo AirTel walifanikisha kuwaunganisha baadhi ya wanamuziki wa iliyokuwa Wenge BCBG.

Kuanzia jumatatu nitakuwa nawaletea story ndefu ya kilichoiua Wenge BCBG. Usikose makala hii EXCLUSIVE hapa Spoti na Starehe.

Image

Allain Makaba Sololist na kulia mwenye miwani myeusi ni Werason Ngiama Makanda.

 

Image
On the Stage.

Image
Far Left – Aimelia liasse, White Coat – Adolph Tata, 3rd Right -Werrason, 2nd Right – Blaise Bula, Far Right – Alain Mpela

Image

Image
Far Left – Aimelia liasse Domingongo , 2nd Left on Guitar -Didier Masela, White Coat – Adolph Tata, 3rd Right -Werrason, 2nd Right – Blaise Bula, Far Right – Alain Mpela

Image

Image
Far Right – Alain Mpela, 2nd Right – Blaise Bula, 2nd Laft – Adolph Tata, Far Left – Aimelia Liasse

 

Image

Image
Far Left – Blaise Bula, Right on Microphone – Alain Mpela

Image
Far Right – The Prince Alain Makaba, 2nd Right – Alain Mpela, 3rd Right – Blaise Bula


Chelsea yaishinda Norwich 3-1

August 27, 2011

Juan Mata

Aifungia Chelsea bao katika mechi yake ya kwanza Stamford Bridge

Juan Mata katika mechi yake ya kwanza katika uwanja wa Chelsea wa Stamford Bridge, aliweza kufunga bao lake la kwanza akiichezea timu yake mpya, na kuiwezesha kusonga hadi kuongoza ligi kuu ya Premier, angalau kwa muda mfupi, baada ya kuifunga Norwich magoli 3-1.

Liverpool baadaye ilijipenyeza hadi nafasi ya kwanza, kwa kupata ushindi kama huohuo, ilipocheza katika uwanja wa nyumbani wa Anfield dhidi ya Bolton na kuizaba magoli 3-1.

Hata hivyo, licha ya kupata ushindi, mashabiki wengi wanafikiria kwamba Chelsea haikucheza kama ilivyotazamiwa.

Chelsea walikuwa wa kwanza kupata bao, kupitia mchezaji Jose Bosingwa, lakini Norwich wakasawazisha kupitia mchezaji Grant Holt.

Frank Lampard alitia wavuni mkwaju wa penalti na kuongeza mabao hadi 2-1, baada ya kipa John Ruddy kumwangusha Ramires, akihisi mchezaji huyo wa Chelsea alikuwa anajiandaa kufunga.

Mata aliiandikishia Chelsea ushindi, lakini raha ya ushindi huo kugubikwa na kutojua hali ya Didier Drogba ni vipi, baada ya kujeruhiwa kichwa.

Kipa Ruddy alikuwa anajaribu kuondosha mpira alipompiga ngumi ya uso Drogba.

Katika mechi nyingine, Aston Villa na Wolves walishindwa kufungana, na mechi kwisha 0-0.

Matokeo yalikuwa ni kama hayo pia katika mechi kati ya Swansea na Sunderland.

Everton iliwafunga Blackburn goli 1-0.

Wigan nayo iliwafunga QPR magoli 2-0.

Kuhusiana na Liverpool kuishinda Bolton na kuwa kileleni, meneja Kenny Dalglish ameisifu timu yake ya Liverpool, akisema walionyesha wazi kwamba waling’ara katika uwanja wa Anfield.

Kenny Dalglish

Meneja wa Liverpool amewasifu wachezaji wake kwa kuwa kileleni katika ligi kuu ya Premier

“Ilikuwa ni burudani kutazama walivyocheza,” alielezea baadaye, kufuatia mabao kutoka kwa Jordan Henderson, Charlie Adam na Martin Skrtel.

Meneja wa Bolton Owen Coyle alikiri kwamba Liverpool walistahili ushindi wao wa magoli 3-1 lakini akaongezea: “Tulijiharibia wenyewe mwanzo wa kipindi cha pili kwa kuwaruhusu kutufunga magoli mawili zaidi.”

Bao la Ivan Klasnic ambalo lilipatikana katika dakika za mwishomwisho katika mechi halikuwapa faraja yoyote Bolton.

Kumbuka pambano kali zaidi Jumapili ni mechi kati ya Manchester United na Arsenal, saa kumi na mbili za Afrika Mashariki.

Pambano hili litatangazwa moja kwa moja katika Ulimwengu wa Soka, matangazo ambayo yataanza saa kumi na moja unusu.

Ungana naye Charles Hilary na Salim Kikeke.


James Dangu alifariki 27 Agost

August 27, 2011

Cool James, Mtoto wa Dandu au CJ Massive zilikuwa aka za James Dandu. Mwanamuziki aliyezaliwa 1970 katika jiji la Mwanza.

Alianza shughuli za muziki mwaka 1983, lakini album yake ya kwanza aliitoa 1986. Akajiunga na mwanamuziki kutoka Kenya Andrew Muturi na kuanzisha kundi la Swahili Nation. Na wakaweza kutoa single iliyoitwa Mapenzi.

Mwaka 1990 alijitoa kundi hilo na kuanzisha kampuni yake Dandu Planet Mwaka 1993 akiwa na Black Teacher alitoa album iliyokuwa na vibao kama Dr Feelgood, iliyoweza kushinda tuzo la Best Scandinavian Dance Track 1994, pia kulikuwa na nyimbo kama Godfather na The rhythm of the track.

Alianzisha kampuni nyingine Dandu Entertainment na kufanya kazi kadhaa kupitia wanamuziki wa Afrika Mashariki. Dandu hatasahaulika kwa wale wanaofahamu chanzo cha tuzo za kila mwaka za muziki za Kilimanjaro Music Awards ambazo zilianza kwa jina la Tanzania Music Awards (TAMA). Alifariki katika ajali ya gari tarehe 27 Agosti 2002 akiwa na umri mdogo wa miaka 32.

Mungu amlaze pema peponi.


JB Mpiana na Fally huko Grand Hotel Kinshasa.

August 26, 2011

Hiii ilikuwa Show ya JB Mpiana huko Grand Hotel Kinshasa na mara alipanda Fally Ipupa angalia na kusikiliza jinsi jamaa walivyopiga kolabo la kufa mtu, then angalia Pendejee anavyomwaga Dorari uwanjani. Kisha mtamuona Ja Pipina Nyangalakata na Dolary jukwaani ambaye amekuwa akiimbwa sana na JB Mpiana.


Tujikumbushe JB MPIANA CONCERT DE L OLYMPIA 1999 LIVE

August 26, 2011

Kuna Shabiki wangu mmoja anaitwa Papaa Mawata Salum ni shabiki mkubwa sana wa Wenge BCBG kuna baadhi ya DVD anauliza kama mtu anaweza kuwa nazo, sina hakika kwenye Library yangu nitaziangalia ila kama kuna mtu ana DVD hizi naomba tuwasiliane ili nami nipate Copy.

1. JB Mpiana 3 Concert De L Olympia 1999 Live/DJOMEGABP – DVD hii naiona kwenye mtandao lakini madukani hapa Bongo bado haijawahi kuuzwa je unaweza kunipatia copy hii na itagharimu shs? za kibongo?
2. JB Mpiana et Wenge BCBG – Live A Paris Titanic Volume 1 and 2
3. Wenge Musica 4 x 4 Live in Abidjan
4. Papa Wemba et Wenge Musica Concert in Paris On same stage with Wenge Musica of Mpiana et Werrason et Adolphe

Video ya leo ni kwako Mkuu Mawata, Papaa Maghambo Le Fimitive, Mukubwa Ling’ande mna nini bwana kama mbwayi mbwayi bwana. na Mashabiki wote wa Blog yangu, mi nasema hivi bado Wenge ni Baba ya Muziki hata kama hawataki.


Mh. Rage atembelewa na wageni wake mjengoni

August 26, 2011

Picha zote kwa hisani ya Muhidini Michuzi Blog

image

Wageni wa Mh. Rage wakiwa mjengoni walikoenda kumtembelea, wakifatialia mijadala Bungeni, wakiwa na “Ubao” wao.

 

image

Wageni wa Mh. Rage wakitoka Bungeni.

 

image

Wageni wa Mheshimiwa Rage wakiwa na Wabunge baada ya kupeleka “Ngao” Yao Bungeni.

Viongozi na Wachezaji wa Simba majuzi walitua Bungeni walikoenda kuonyesha Ngao yao baada ya kuifunga yanga kwenye mechi ya Ngao Ya Jamii iliyokusudiwa kwa ajili ya ufunguzi wa Ligi ya Vodacom.

Mashabiki wa klabu hizi mbili hasimu ambao ni watani wa jadi  (Nikiwemo mimi wa Yanga) walilumbana juu ya hatua ya Klabu ya Simba nayo kupeleka Ubao wao (Ngao) Bungeni huku mashabiki wa Yanga wakisema kuwa walikuwa na haki zaidi kupeleka Kombe lao kwa vile ule ni ushindi mzito  kulinganisha na huu wa Simba.

Angalizo:

Mashabiki wa Simba msikasirike ni katika kuendeleza utani wa Simba na Yanga.


Fally alipowachezesha Etoo, Drogba, Sagna na Akon

August 25, 2011

Ukiangalia kwenye Video hii utawaona Drogba, Etoo, Sagna na Akon wakicheza pamoja na Fally Ipupa. Hii ilikuwa huko Abdijan.


Ferguson amaliza ‘mzozo’ wake na BBC

August 25, 2011

Na BBC

Meneja wa Manchester United Sir Alex Ferguson amekubali kuanza kuzungumza na BBC.

Alex

Alex Ferguson

Ferguson alianza kususia kuzungumza na BBC mwaka 2004 baada ya kituo hicho kutoa tuhuma dhidi ya mwanae, Jason, katika kipindi kimoja cha televisheni.

Taarifa iliyotolewa imesema: “Sir Alex na BBC wameweka kando tofauti zao ambazo zilisababisha Sir Alex kutojisikia kuzungumza na BBC na vipindi vyake.”

Manchester United inacheza na Arsenal siku ya Jumapili kwenye uwanja wa Old Trafford.

Taarifa ya pamoja iliyotolewa siku ya Alhamisi, inafuatia mazungumzo kati ya Sir Alex na mkurugenzi mkuu wa BBC, Mark Thompson, na mkurugenzi wa BBC kanda ya kaskazini Peter Salmon.

Taarifa hiyo imeongeza: “Suala hilo limefikia muafaka na pande zote mbili kuridhia.

“Sir Alex sasa atakuwa akiweza kuzungumza katika kipindi cha BBC Match of The Day, Radio 5 live na vyombo vingine vya BBC kama ilivyokubaliwa.

“Hakuna maelezo zaidi yatatolewa na pande mbili hizo kuhusiana na suala hilo.” imemaliza taarifa hiyo.


TAARIFA RASMI KUHUSU HUSSEIN MACHOZI KUREJEA TETEMESHA

August 24, 2011

c-sir, hussein & sagna

 

Hii ni taarifa rasmi kwa media na wadau wote kuhusiana na HUSSEIN MACHOZI kurejea katika familia ya TETEMESHA RECORDZ, iliyomtengeneza na kumkuza kimuziki mpaka hapo alipo toka mwaka 2007.

Kumekuwa na taarifa nyingi hapo katikati lakini hii ndio taarifa rasmi na ya kweli kuwa yalitokea matatizo kidogo mwaka jana (2010) mwanzoni, yaliyotokana na Hussein kukiuka baadhi ya masharti ya mkataba wake na Tetemesha, yaliyopelekea uongozi kuamua kusitisha kwa muda mkataba wake ili kumpa nafasi ya kupewa nguvu msanii mwingine aliyekuwa ndio anaaza kutambuulishwa mwaka jana anayefahamika kama SAGNA. Baada ya kumtambulisha vizuri Sagna, mwaka huu pia Tetemesha tumeweza kumtambulisha msanii mwingine wa tatu aitwaye C-SIR MADINI.

Sasa tumeona ni wakati muafaka wa kumrudisha Hussein Machozi rasmi ndani ya Tetemesha baada ya kukaa nae chini na kufanya makubaliano mapya na kusaini mkataba mwingine toka katikati ya mwaka huu, isipokuwa tumechelewa kuwapa taarifa kwasababu tulikuwa tunaweka kwanza mambo kadhaa sawa.

NEW SONG:

Hussein Machozi akiwa chini ya Tetemesha Entertainment ameshaanza kurekodi baadhi ya nyimbo mpya zitakazotoka mwaka ujao 2012, lakini kwa sasa tunautambulisha wimbo wake ambao ni REMIX ya wimbo alioutoa mwaka jana unaitwa “UNANIFAA”.

Katika version ya mwanzo ya wimbo huo aliimba peke yake, lakini katika remix hii amewashirikisha wasanii wenzake wa Tetemesha ambao ni C-sir Madini na Sagna.

Unanifaa remix imeandikwa na Hussein mwenyewe verse yake na chorus, na verse za Sagna na C-sir zimeandikwa na mwandishi rasmi wa Tetemesha anaitwa JOSEFLY kwa kushirikiana na Kid Bwoy.

Version ya mwanzo ya wimbo huo ilifanyika Akhenato Records chini ya Lil Ghetto. Remix beat imefanywa na Amba, na vilivyosalia vyote vimefanyika Tetemesha Recordz.

CREDITS:

Artists: HUSSEIN MACHOZI FT. C-SIR MADINI & SAGNA

Song title: UNANIFAA (REMIX)

Written by: Verse-1: JOSEFLY, Verse-2 & Chorus: HUSSEIN MACHOZI, Verse-3: JOSEFLY & KID BWOY

Produced by: AMBA for TETEMESHA RECORDZ 2011

Vocals Recorded by: KID BWOY

Mixed by: KID BWOY

Studio: TETEMESHA RECORDZ (Mwanza)

CONTACTS:

Hussein Machozi 0718 877728

Kid Bwoy 0713 131073

Thanx for the support.

Sandu George. (Kid Bwoy)

C.E.O Tetemesha Entertainment.


Messi Kiboko, Dakika 15 Afunga mabao matatu

August 23, 2011

Leone Messi ameonyesha kuwa yeye ni kiboko pale alipoingia badala ya Fabregas na kupachika mabao matatu ndani ya dakika 15. Katika mchezo ambao mwanasoka Cesc Fabregas kwa mara ya kwanza amefunga bao lake la kwanza tangu arejee klabu yake ya zamani ya Barcelona katika mechi ya kirafiki dhuidi ya Napoli pale Barca waliposhinda 5-0. Fabregad aliwafurahisha mashabiki waliokuwa na hamu ya kumuona ikiwa ni mara ya pili anaingia uwanjani tangu ajiunge na klabu hiyo pale alipopachika goli safi dakika ya 25 ya mchezo ambao uliisha kwa karamu ya magoli.

Hata hivyo alikuwa Seydou Keita aliyeipatia timu yake bao la pili na baadaye Lionel Messi aliingia badala ya Fabregas na kufanya mauaji alipofunga mabao matatu peke yake ndani ya dakika 15.


Villas-Boas ampongeza Mata wa Valencia

August 23, 2011

Na BBC

Meneja wa Chelsea Andre Villas-Boas amempongeza kiungo wa Valencia Juan Mata, huku kukiwa na taarifa yu-karibu kusajili na klabu ya Chelsea.

Juan Mata

Juan Mata

Taarifa kutoka vyombo vya habari vya Hispania zimesema mchezaji huyo wa Valencia mwenye umri wa miaka 23, anajiandaa kujiunga Stamford Bridge kwa kitita cha paundi milioni 23.5.

Baada ya ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya West Brom siku ya Jumamosi, Villas-Boas ana uhakika wa kumsajili Mata.

Amesema: “Ni mchezaji anayefunga mabao na kusaidia kutengeneza mabao kwa wengine na anaweza kucheza katika kikosi chochote duniani.”

Villas-Boas ameongeza: “Si mchezaji wetu kwa sasa lakini anavutia…….ni mchezaji mzuri sana.”

Mata amekuwa katika kikosi cha Valencia tangu mwaka 2007 na ameisaidia timu ya taifa ya Hispania chini ya umri wa miaka 21 kuweza kushinda Ubingwa wa Ulaya mwaka huo.

Villas-Boas awali alizungumzia umuhimu wa kusajili wachezaji wa kiungo na klabu hiyo pia bado inamuwinda kiungo wa Tottenham Luka Modric.