Werrason kwa Sebene bana namkubali

Huwa nikiongea na ma werasonike nasemaga kabisa bila kuficha katika vitu ambavyo Werasson amefanikiwa ni Sebene lake, huwa napenda sana nyimbo za Werrason zinazoanza na moto tangu mwanzo tofauti na JB ambaye nyimbo zenye sehemu mbili huwa anazipatia sana yaani zinaanza na kupokezana kwa Verse kisha zinachanganya, anyway huuu ni mtazamo wangu na jinsi nilivyojipanga ili kuwatendea haki wote wawili na niwe na sababu ya kununua albamu za wote wawili, Werrason anaenda akibadilika na katika wimbo huu bado nahisi Animateur alikuwa na kazi ya ziada ya kutuletea ladha ile yaki Maison Merre. Nawatakia Weekend njema msikose uwanjani kwani wiki ijayo tutaendelea na makala zetu za Wenge na habari nyingine kemu kemu hapa hapa jamvini.

Kama kawaidauwanja uko wazi kama vitu tuma message kwa 0713 666616 sio usiku wa manane au tuma email kwa piusmicky@yahoo.co.uk

Weekend njema.

Advertisements

13 Responses to Werrason kwa Sebene bana namkubali

 1. Richard MALEWA says:

  Merci Miiiiingi Papa Pius! La Grand Congolese Music Bloglist du Tanzanie! Weeeeh! Ndenge Nzaliiiiiii!

 2. PDG Tony says:

  Igwe le roi de la foret champion!!!!

 3. voice of zamba playa says:

  nimeziangalia na kuzisikiliza video zote mbili,ya pili siwezi kuiongolea sana kwa sababu ni generique,kelele zinahusika sana tu,zaidi nimeiangalia video ya kwanza kwa kuirudia rudia mo than 3 timez,sijaona,thats not the werrason i knew,tukiacha ushabiki katika video hiyo sana sana ni wadada tu ndio wamependeza kimavazi ya kisasa lakini muziki hakuna hapo wala tusidanganyane,maana mpaka muziki umeisha hata sijaelewa ni muziki wa aina gani hasa…hauonekani kama ni muziki wa congo hasa,labda ndio kwa ajili ya soko la nje,mi sijui,hata sijui unaucheza vipi let say club muziki kama huo,otherwise werrason has to do something better than that jamani,najua wengi tunampenda na tungependa atuletee mambo kama aliyoyafanya huko nyuma,but it seems as amelewa sifa kwa kuwa anajua we going to support him kwa lolote,but inaweza isiwe ivo kila wakati.

  WERRA BROTHER WE SUPPORT YOU DON’T LET US DOWN.

 4. sankara de nkuta le tanzaniane says:

  namlilia flam kapaya,ameondoka na solo lake na arrangements zake kiujumla.

 5. Predator says:

  Ni ukuweli ndugu ya kwamba Kapaya Flam ameenda na ni uchungu maanake jinsi alikuwa akichangia ladha ya miziki za Werra hailinganishwi na wengine WMMM. Mtaniwia radhi lakini nikisema kwamba Werra ni msanii hodari sana ndio maana jina ‘Le Grand Formateur’ halitamilikiwa na msanii yeyote mwingine Congo. Namlinganisha na Arsene Wenger kwa ushupavu wa kukuuza talanta changa na kulea ujuzi wa wanamuziki wanaoinuka. Wengine hata wanasema the “Werra-Wenga Magic’ yaani kila wakati mwanamuziki wa WMMM akitoroka Werra hasiti kupata atakayejaza nafasi yake aliyetoka. kuna huyu guitarist chupikizi (simkumbuki jina) alikuwa anafanya backstreet practice freestyle na Alain Mpela, alitokea mara ya kwanza WMMM kwa wimbo Mayi ya Sika (Album Temps Present) ameweza kuujaza nafasi yake Kapaya upesi wa kushangaza. Ujue pia Polystar na Thierry Mogratana wameushikilia upande wa gitaa kikamilivu sana kiasi mpaka huwezi kugundua virahisi pengo lililoachwa na Kapaya. Werra anajulikania kujaza bendi na talata yajayo mpaka hata mmoja akitoka hawezi kupambana na kutafuta msanii badala. Sasa hivi tukiongea, Merlin Buiton na Deplik wanang’ang’ania kujaza nafasi yake Heritier Watanabe, kumaanisha hamna upungufu wa talanta kwa nyumba ya mama. Maoni yangu hayo

 6. Predator says:

  Eee ni mimi bado hapa kwenye hii mada niliyochangia dakika tano zilizopita juu ya Werra-Wenger Magic. Kijana yule niliyemsahau jina, nishakumbuka aitwa Karibu Variete, mcheza gita promising sana

 7. Anonymous says:

  ndio yule wmmm wanaemwita new makaba au arc en ciel(rainbow)ambae aliingizwa kundini baada ta petit poussin kuondoka kundini kurudi shule ufaransa baada ya kuona werra anazingua upande wa malipo na muziki haulipi tena au

 8. Predator says:

  Nakuambia ndugu yangu huyo kijana anafurahisha sana namna alivyoibuka kutoka streets hadi WMMM tu mara moja. Ukiangalia alivyocharaza gita kwenye ‘mayi ya sika temps present’ basi sina budi kukubaliana nawe kwamba ndiye alain makaba mpya. Anyway, najua wakiwa pamoja na talanta mya mwingine anaitwa Kimbangu, basi WMMM bado haitafikiwa na wengi kwenye upande wa gitaa. Ndiye huyu hapa Kimbangu akifanya mambo kwenye kionjo ya Malewa concert 2010: http://www.youtube.com/watch?v=XoaESVlNcrI

 9. PAPA NELSON,Makambako town,Iringa says:

  mdau hapo juu mbona hatukuelewi unamzungumzia kimbangu huyu hapa au baada ya kimbangu yupo mwingine,kuwa wazi,maana ni kama unamuongelea m2 mmoja ukidhani ni wawili

  • Predator says:

   Papa Nelson video hii umeweka hapa ndio ile ile niliyopeana kwenye ile link nimeattach kwenye maoni yangu unless unajirudia, maanake unaniuliza kama namaanisha Kimbangu mwingine yet ni the same guy umeonyesha hapa

 10. Anonymous says:

  Nyie kuwalinganisha hawa watoto na flamme ni matusi…flamme anaimba,ana arrange music anapiga gitaa ana rap,anapiga key board anapiga drums,anacompose nyimbo…yule ni mwanamuziki kamili.hembu muoneni hapa kazi anazozifanya kwa steji

 11. Fatuma Mtanga says:

  kweli kabisa mdau nakuunga mkono flamme yuko juu sana

 12. Jesse Grillo says:

  Any team would be lucky to have you on it. I love leafly but I’ve always been a supporter of weed edibles. Your creative potential seems limitless.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: