Tujikumbushe JB MPIANA CONCERT DE L OLYMPIA 1999 LIVE

Kuna Shabiki wangu mmoja anaitwa Papaa Mawata Salum ni shabiki mkubwa sana wa Wenge BCBG kuna baadhi ya DVD anauliza kama mtu anaweza kuwa nazo, sina hakika kwenye Library yangu nitaziangalia ila kama kuna mtu ana DVD hizi naomba tuwasiliane ili nami nipate Copy.

1. JB Mpiana 3 Concert De L Olympia 1999 Live/DJOMEGABP – DVD hii naiona kwenye mtandao lakini madukani hapa Bongo bado haijawahi kuuzwa je unaweza kunipatia copy hii na itagharimu shs? za kibongo?
2. JB Mpiana et Wenge BCBG – Live A Paris Titanic Volume 1 and 2
3. Wenge Musica 4 x 4 Live in Abidjan
4. Papa Wemba et Wenge Musica Concert in Paris On same stage with Wenge Musica of Mpiana et Werrason et Adolphe

Video ya leo ni kwako Mkuu Mawata, Papaa Maghambo Le Fimitive, Mukubwa Ling’ande mna nini bwana kama mbwayi mbwayi bwana. na Mashabiki wote wa Blog yangu, mi nasema hivi bado Wenge ni Baba ya Muziki hata kama hawataki.

5 Responses to Tujikumbushe JB MPIANA CONCERT DE L OLYMPIA 1999 LIVE

 1. Farid wa Muscat says:

  hata mimi nazitafuta sana video hizo na hasa hio ya 4 kuna show si ya kawaida kabisa na hapo ndio enzi za Tutu Calludji alipokua akishika mike watu wote ni lazima wasimame watake wasitake,
  TAFADHALINI JAMANI ATAKAEZIPATA BASI ANIJULISHE NA MIMI TUWASILIANE

 2. Anonymous says:

  Hata Franco Luambo Lwazo Makiadi alikuwa Baba wa Muziki Kongo Miaka ya 70

 3. Hadj Le Jbnique says:

  Ya kwanza pia mimi ninayo matangazo yake pia yanaptikana kwenye video clip ya TITANIC ALBUM jb akiwa amevaa kama mkuu wa majeshi,ya pili sijaelewa mnamaanisha live ipi ya TITANIC na ilipigwa wapi,namba tatu na nne pia niko nazo kwenye mikanda mikubwa ile ya video nafanya jitihada niihamishie kwenye cd,ninazo video nyingi live za wenge ikiwemo pia ya wenge musica na zaiko langa langa on one stage ambapo Le Grand ChibutA Roberto Ekokota alimfunika mbaya Atalaku wa Zaiko alietaka kupambana nae jukwaani,JB na Mzee Nyoka Longo wakawapisha wapambane…..ilikua safi sana hiyo,anaetaka nimpatie awasiliane na mimi kwa namba hii 616-635-9725.Lakini na mimi pia naitafuta sana live moja ya wenge musica na Le Anti choc ya mzee Bozi Boziana akiwa na warembo wake mamaa mokonzi Scola Miel na Betty,niliwahi kuiona video hiyo miaka ya tisini,ni kali sana,ilikua ni kama mashindano ya kucheza mmoja mmoja kutoka kila upande anapita mbele then wanashindana,Jb nakumbuka walishindana sana na mama Scola Miel,Koffi Alibaba akiwa kwa bozi enzi hizo alipambana sana Big tata Adolphe ….nani naijua hii video?tupeane taarifa.

  otherwise nilikua sijaja siku nyingi humu leo nimekuta big change kidogo nipotee

 4. Hadj Le Jbnique says:

  Ahaaaa!hiyo ya pili vol 1 na 2 pia ninazo kwenye mikanda mikubwa VHS,Kweli hiyo ilikua ni paris ziara ya kwanza ya wenge bila kina WERRA ndani ya paris,ilikua kabla hawaja release album ya TITANIC lakini ilikua tayari imeshatungwa na ziara hiyo pamoja na kupiga hiyo show pia waliitumia kurekodi hiyo album ambayo ilikuwa imeshapikwa na ilikua irekodiwe kwa pamoja na kina werra ambao nao walishiriki kuiandaa lakini ugomvi ulipotokea ikabidi waondoe nyimbo zao na vocals zao,ndio maana kama mtafuatlia na kuchunguza sawasawa mtaona album ya kwanza ya kina na album ya titanic zinafanana,hasa nyimbo za zilizobeba majina ya album hizo,isikilize vizuri nyimbo ya TITANIC vile inaanza then isikilize nyimbo FORCE INTERVENTION RAPIDE pia inavoanza ndio utanielewa ninachosema,

 5. Anonymous says:

  jamani kwa kweli nimezitafuta sana hizo dvd sijazipata kwa atayepata kwa kweli naomba tujulishane wadau….

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: