Werasson awakana wanamuziki wa Congo nchini

June 30, 2008
[image]

MWANAMUZIKI mkongwe wa Jamhuri wa Kidemokrasia ya Kongo, Werasson amesema hamjui mwanamuziki hata mmoja kutoka Kongo anafanya muziki hapa Tanzania.

Hivi karibuni wanamuziki wengi kutoka Kongo waliokuja hapa nchini walijitangaza kuwa wengine ni ndugu wa Werrason huku wengine wakisema kuwa wenyewe ni watoto wa mkongwe wa Muziki nchini humo Pepe Kalle, na katika tukio la karibuni ni pale mwanamuziki ally Choki alipoonekana amepiga picha na Werason alipokwenda kutafuta wanamuziki huko na kusema kuwa Werasson alimsaidia kutafuta vijana.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam juzi Werasson alisema ’simfahamu mwanamuziki hata mmoja wa Tanzania wala mkongo ambaye anaimba muziki hapa huyo anayejiita mtoto wa Pepe Kalle pia hamfahamu.

“Mimi nipo na mtoto mmoja wa Pepe Kalle ambaye namfundisha muziki pale Kongo, lakini huyu wa Tanzania mimi simfahamu kwakuwa watoto wake wote nawajua na hivyo labda awe mwingine zaidi,” alisema Werassons.

Werrason alisema kwa kuwa hawajui wanamuziki wa Kongo walipo hapa nchini lakini yuko tayari kukutanao na kufanya mazungumzo ya kuendelea muziki Tanzania.
(Picha na Mpoki Bukuku)


Monday, June 30, 2008

June 30, 2008

Karibuni nyumbani mwayego….!

A German supporter waits on a traffic light for the arrival of the German football team with thousands of supporters who gathered at Berlin's Brandenburg Gate on June 30, 2008 to greet their team upon their return from Vienna, where they lost by 0-1 to Spain in the final of the Euro 2008 Football Championships June 29. AFP PHOTO JOHN MACDOUGALL (Photo credit should read JOHN MACDOUGALL/AFP/Getty Images)
Shabiki wa Timu ya Ujerumani akiwa amesimama juu ya Taa za kuongozea magari wakati wachezaji na makocha wa Timu ya Taifa ya Ujerumani wakiwasili huko Ujerumani jana, Hebu pata picha hawa jaa wangeshinda mtiti ungekuwaje? Germany's striker Lukas Podolski sings to supporters of the German football team at the "Fanmeile" (fan zone) next to Berlin's Brandenburg Gate on June 30, 2008, the day after the Euro 2008 final Germany vs Spain in Vienna, Austria. Spain won their first trophy in 44 years as they beat three-time champions Germany 1-0 in the Euro 2008 final.  AFP PHOTO DDP/POOL/ GERO BRELOER  (Photo credit should read GERO BRELOER/AFP/Getty Images)
Mchezaji wa Ujerumani Lukas Podolski (Juu na chini pichani) akiimba mbele ya mashabiki waliokusanyika kuwapokea mashujaa wao.
Germany's striker Lukas Podolski appears on a giant screen as thousands of fans cheer the German national football team at the "Fanmeile" (fan zone) in front of Berlin's Brandenburg Gate on June 30, 2008, one day after the Euro 2008 final Germany vs Spain, held at Ernst-Happel stadium in Vienna, Austria. Spain ended their 44-year wait for a major international title with a 1-0 victory over Germany at the Euro 2008 final.      AFP PHOTO  DDP/ MICHAEL GOTTSCHALK (Photo credit should read MICHAEL GOTTSCHALK/AFP/Getty Images)
Germany's head coach Joachim Loew (L) signs his name in the city's Golden Book next to Berlin's Mayor Klaus Wowereit as supporters of the German football team gather at the "Fanmeile" (fan zone) next to Berlin's Brandenburg Gate on June 30, 2008, the day after the Euro 2008 final Germany vs Spain in Vienna, Austria. Spain won their first trophy in 44 years as they beat three-time champions Germany 1-0 in the Euro 2008 final.  AFP PHOTO DDP/POOL/ GERO BRELOER  (Photo credit should read GERO BRELOER/AFP/Getty Images)
Kocha wa Ujerumani Joachim Loew (L) akitia mkono kwenye kitabu cha city’s Golden Book kulia kwake anayemkazia jicho ni Meya wa Berlin Klaus Wowereit pale mamia kwa maelfu ya washabiki wa Ujerumani walipokusanyika “Fanmeile” (fan zone) huko Berlin
Hii ni baada ya mchezo wao wa jana na Hispania kwenye fainali za Euro 2008 na Spain kushinda kwa 1-0. Picha zote na AFP

Serena na Venus hatarini kucheza Fainali wao kwa wao

Venus Williams
Venus na Serena, Ndugu wote wawili wameshinda mechi zao leo Jumatatu huko Wimbledon, Kama mambo yakienda hivi basi kuna hati hati ya Wawili hao ambao ni mtu na dada yake kucheza Fainali wao kwa wao. (Picha na AP)

Kili Music Award yafana

Wasanii mbali mbali wamefanikiwa kunyakua Tuzo mbali mbali kwenye tamasha la Kili Music Award usiku wa kuamkia leo, Kwa habari na picha zaidi bofya hapa kwa Haki Ngowi (Picha na Haki Ngowi)

Mchezaji Taifa Stars adaiwa “Jezi” baada ya kubadilishana na Eto’o wa Cameroon

Kipanya wa Leo na habari ndio hiyo hapo chini…

Na Phillip Nkini wa Mwananchi

UMILIKI wa jezi za timu ya Taifa Stars umezua balaa kwa baadhi ya wachezaji wa timu hiyo kujikuta wakikatwa fedha zao za posho kwa madai ya kufidia jezi ambazo ama walibadilishana na wenzao wa Cameroon au kupoteza.

Kwa upande wake, Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) linasema: ”Jezi si mali ya wachezaji.”

Kampuni ya Bia ya Serengeti Breweries na Benki ya NMB, wadhamini wa Stars wamekuwa wakitoa vifaa kwa wachezaji wa timu hiyo kuanzia vile vya mazoezi hadi vya mechi mbalimbali ambazo timu hiyo imekuwa ikicheza.

Lakini, pamoja na hali hiyo kumezuka tatizo kwa baadhi yao (wachezaji) na uongozi wa timu hiyo kukosana baada ya baadhi yao kubadilishana jezi majuzi na wachezaji wa Cameroon, Indomitable Lions, jambo ambalo limewazulia mambo.

Mchezaji mmoja kinda wa timu hiyo (jina tunalo) alishindwa kumpa Geremi Njitap wa Cameroon jezi yake kwenye mchezo kati ya Stars na Cameroon mjini Yaounde baada ya mchezaji huyo kutaka wabadilishane.

Kinda huyo aliiambia Mwananchi kuwa alihofia kuja kurejea nchini na kudaiwa jezi.

Lakini, beki wa timu hiyo alibadilishana jezi na mshambuliaji wa Cameroon, Samuel Eto’o Fils baada ya Mcameroon huyo kumfuata mwenyewe na kumtaka afanye hivyo.

Hata hivyo, pamoja na wachezaji hao kudaiwa jezi hizo Ofisa Habari wa TFF, Florian Kaijage aliithibithishia Mwananchi kuwa jezi si mali ya wachezaji, bali ni mali ya shirikisho hilo na mchezaji atakapoipoteza, basi utaratibu wa malipo utafanywa.

”Jezi sio mali ya wachezaji ni mali ya Shirikisho la Soka, kila mchezaji anapewa jezi kwa kufuata utaratibu maalum ukipewa lazima urudishe usiporudisha unaandaliwa utaratibu wa kulipia.”

“Sisi bado tupo nyuma sana hatujafika huko walipo hao akina Senegal au Cameroon kuwa na wadhamini wakubwa, kiasi kwamba mchezaji mmoja kuwa na jezi zaidi ya kumi. Hapa kwetu, tunaweza kutumia jezi moja kwenye mechi mbili wenzetu kila mechi na jezi yake.

”Ukiangalia mchezaji kama Eto’o anandaliwa jezi zaidi ya 50 na Kampuni ya Puma ni tofauti sana na sisi, ingawa kubadilishana moja mbili siyo vibaya, lakini isiwe watu kumi na kuendelea,” alisema Kaijage.

Uchunguzi wa Mwananchi umeonyesha kuwa wachezaji hao wa Stars wamekuwa hata wakati mwingine wakipigiwa simu wakiwa majumbani kwao ili warudishe jezi ambazo wamekuwa wakiondoka nazo kwa bahati mbaya au ambazo zimekuwa zikipotea.

Ukweli ni kuwa kila mchezaji wa Stars anapopoteza jezi moja hukatwa posho yake kuanzia Sh20,000 na kuendelea.

Hali hiyo ndiyo inayosemekana kuwa itamkumba beki na nahodha msaidizi, Nadir Haroub Cannavaro aliyeamua kubadilisha jezi na Eto’o.

Eto’o, ambaye yuko katika ziara ya nchi kadhaa za Afrika, alionekana jijini Kampala, Uganda akiwa na jezi yenye nembo ya NMB huku akitoa mafunzo ya soka kwa watoto.

Werasson awakana wanamuziki wa Congo nchini

[image]

MWANAMUZIKI mkongwe wa Jamhuri wa Kidemokrasia ya Kongo, Werasson amesema hamjui mwanamuziki hata mmoja kutoka Kongo anafanya muziki hapa Tanzania.

Hivi karibuni wanamuziki wengi kutoka Kongo waliokuja hapa nchini walijitangaza kuwa wengine ni ndugu wa Werrason huku wengine wakisema kuwa wenyewe ni watoto wa mkongwe wa Muziki nchini humo Pepe Kalle, na katika tukio la karibuni ni pale mwanamuziki ally Choki alipoonekana amepiga picha na Werason alipokwenda kutafuta wanamuziki huko na kusema kuwa Werasson alimsaidia kutafuta vijana.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam juzi Werasson alisema ’simfahamu mwanamuziki hata mmoja wa Tanzania wala mkongo ambaye anaimba muziki hapa huyo anayejiita mtoto wa Pepe Kalle pia hamfahamu.

“Mimi nipo na mtoto mmoja wa Pepe Kalle ambaye namfundisha muziki pale Kongo, lakini huyu wa Tanzania mimi simfahamu kwakuwa watoto wake wote nawajua na hivyo labda awe mwingine zaidi,” alisema Werassons.

Werrason alisema kwa kuwa hawajui wanamuziki wa Kongo walipo hapa nchini lakini yuko tayari kukutanao na kufanya mazungumzo ya kuendelea muziki Tanzania.
(Picha na Mpoki Bukuku)

Wajerumani “Mbendembende” kwa Waspaniola

Germany 0-1 Spain
Spain's Iker Casillas celebrates with the trophy after the Euro 2008 final between Germany and Spain in the Ernst-Happel stadium in Vienna, Austria, Sunday, June 29, 2008, the last day of the European Soccer Championships in Austria and Switzerland. Spain defeated Germany 1-0.
Wachezaji wa Spain wakisheherekea baada ya kukabidhiwa “mwali ” wao
In this handout picture distributed by Spain's soccer Federation, Spain's King Juan Carlos, right, holds the Euro 2008 European Soccer Championship trophy with Spain's Prime Minister Jose Luis Rodriguez Zapatero, left, standing beside him.  Spain's soccer team won the trophy by beating Germany 0-1 in the final of Euro 2008 championship played Sunday in Vienna, Austria.
Pichani ni Mfalme wa Spain Juan Carlos, aliyeshika kombe walilokabidhiwa Spain jana na kushoto kwake ni Waziri Mkuu wa Spain Jose Luis Rodriguez Zapatero usiku wa kuamkia leo.
Some German supporters sit on the ground on a huge German flag in the Munich fan zone at the Olympic stadium after the Euro 2008 championships final football match Germany vs. Spain on June 29, 2008 at Ernst-Happel stadium in Vienna, Austria. Spain won their first trophy in 44 years as they beat three-time champions Germany 1-0 in the Euro 2008 final.  AFP PHOTO   DDP / TIMM SCHAMBERGER   (Photo credit should read TIMM SCHAMBERGER/AFP/Getty Images)
Mashabiki wa Ujerumani wakiwa hawaamini kilichotokea wamebaki uwanjani hata baada ya mpira kumalizika.
Germany's Micheal Ballack reacts at the end of the Euro 2008 final between Germany and Spain in the Ernst-Happel stadium in Vienna, Austria, Sunday, June 29, 2008, the last day of the European Soccer Championships in Austria and Switzerland. Spain defeated Germany 1-0.
Kepteni wa Ujerumani Micheal Ballack akiwa haamini kama dakika 90 zimekwisha na wameshindwa kuchomoa goli moja la Spain katika mchezo uliofanyika Ernst-Happel stadium huko Vienna, Austria,
(Picha zote na AP)

Fernando Torres ndiye shujaa wa Spain baada ya kupachika bao dakika yaa 33 bao lililodumu hadi kipyenga cha mwisho na kuwafanya Spain kutawazwa kuwa mabingwa wapya wa Mtanange wa Euro 2008 baada ya kuisaka nafasi hiyo kwa miaka 44.

Torres alipachika bao hilo swafi dakika ya 33 ya mchezo kipindi cha kwanza licha ya juhudi za Kapteni wa Ujerumani Ballack waspaniola walikaza na kulinda goli lao huku wakifanya mashambulizi ya hapa na pale.

Huku akisherehekea miaka 70 ya kuzaliwa , Kocha Luis Aragones alitanabaisha atang’atuka kuifunza timu ya Spain na inasemekana Kocha mwingine Vicente del Bosque ndiye anaweza kuchukua timu hiyo ambayo kwa bahati atarithi vijana wenye vipaji wadogo na wenye hari na mtazamo kwenye kombe la Dunia.
Mpaka dakika 90 bao likabaki 1-0, ama kwa hakika kanauma, kamonga tuu!!