Kidiamfuka; Utunzi wa El dorado uliombeba Fally Ipupa

April 9, 2014

Kwa wapenzi wa Fally Ipupa wimbo huu Kidiamfuka ni mmoja wa nyimbo zilizompa nafasi na chat mwanamuziki huyo. Kiukweli Wimbo huu wengi wetu tulidhani ni utunzi wake Fally Ipupa ilihali wimbo huu mtunzi halisi ni El Dorado ambaye pia ametunga wimbo 100 kilos wake FERRE GOLA na Detresse ambao awali ulidhaniwa ni wa Mimiche Bass, sikiliza wimbo huu kisha nipe maoni yako.


Papito Remix Utunzi wa “Teja” Zulema wa Wenge

April 9, 2014

Ingawa wimbo huu maarufu toka kwa Wenge ya JB Mpiana unajulikana kama utunzi wake JB Mpiana kiukweli kabisa Wimbo huu ni utunzi wake kijana machachari Zulema ambaye ni bonge la kipaji ambacho kiukweli kwangu naona kinapotea.

Zulema ni muimbaji mzuri ambaye kwa kipidi kirefu amekuwa akisumbuliwa na uteja kwa utumiaji wa madawa ya kulevya. JB Mpiana aliamua kumsaidia Zulema kama mdogo wake na kuna kipindi alipelekwa kwa wataalamu na kupatiwa ushauri nasaha ana alitangazwa kuacha matumizi ya madawa hayo.

Mwanamuziki Zulema wa wenge bcbg ni kijana mwenye kipaji cha hali ya juu ambacho kilivumbuliwa JPS PRODUCTIONS ambao walimpeleka wmmm ya werrason ambako alifanyiwa interview na mtaalam wa vocal wa WMMM wakati huo FERRE GOLA na kufuzu vizuri interview hiyo ila tatizo likawa alikuja kugundulika kwamba licha ya kipaji cha sauti alichonacho anakabiliwa na tatizo la utumiaji wa madawa ya kulevya hali iliyowafanya wmmm wasite kumuingiza moja kwa moja kwenye kikosi cha kwanza na kuamua kumpeleka kwenye bendi yao ya pili iitwayo OPERATION DRAGON, Ndipo Jules kibens wa bcbg ambae waliwahi kupiga pamoja zamani Folk Stars alipokwenda kumshawishi JB Mpiana wamnyakue ZULEMA kwa kuwa ana kipaji.

Nakutakieni siku njema, Post hii imerudiwa kwa heshima ya Ndekwa Mwana Bebg nakati ya Dare salaam hesmima mingi kwako Mukulu wa Bakulu, Gilbert wa Mikumi Pamoja sana, Mamaa Gladys, Papaa James Maselle, heshima kwako, Mwambungu nakati ya Tunduma, Steve BCBG pamoja mzazi, Frank Le Jeebeenique, Mukulu Hadji Le Jeebeenique miss u brother.


President de Taut le Chegee; Jukwaa moja na Shaggy

April 9, 2014

Kuna mahali panafika mashabiki wanapenda ladha tofauti na ndio maana wanamuziki wengi wa Congo kwa sasa wamekuwa wakichanganya na kushirikisha vionjo tofauti ili kuleta ladha tofauti na kutanua wigo wa mashabiki wao.

Werrason ambaye anapendwa sana hasa na vijana amekuwa akijaza sana kwenye show zake huko Congo, huku ngome yake kuu ikiwa kitongoji cha Bandal (hii ni mahala kama Kinondoni) huko watoto wote wa mujini wanapatikana mwenyewe anajiita President de Taut le Chegee – Rais wa Machokoraa na wenyewe wanampenda sana, kiufupi ni mtu wa watu wote matajiri mpaka masikini. Angalia hapa Tamasha lililoandaliwa na Vodacom huko DRC akiwa jukwaa moja na Shaggy.


Koffi vs Youssou Ndour: Mabingwa wa sauti jukwaa moja.

April 9, 2014

Koffi ametangaza kuachana na muziki baada ya kutoka kwa Albamu yake ya 20 ambayo itatoka siku yoyote. Amefanya kazi hii kwa mafanikio akifanikiwa kuinua bendi hata pale ambapo wanamuziki wote karibia waliondoka na kutangaza kikosi kipya, akiwa amefanya Kolable na wanamuziki wengi wa ndani na nje ya Congo DRC.

Hebu sikiliza hiki kipande tu alipopanda jukwaani huko Grand Hotel na mwanamuziki Youssoun Ndour wa Afrika ya Magharibi.


“Mayi ya Pembe” Beach maarufu yenye historia kwa wanamuziki wa Congo

April 9, 2014

Huwa nawatania marafiki zangu wa Congo laiti kama wangekuwa na Beach kama tu za kwetu sijui ingekuwaje maana hiyo Planet Sono Beach (Mayi ya Pembe) ni sehemu tu maji yametuama pembezoni mwa mto, ni eneo liko nje kidogo ya mji wa Kinshasa kama unaelekea Airport kwa wanaoijua Kinshasa, Ukiangalia haina chochote cha kuvutia ila vurugu zake ni balaa kila mwanamuziki mkubwa ameshapiga huko na sio mara moja. mara nyingi show zao huanza mchana watu wakila na kunywa na kuendelea mpaka lyamba.

Hii ni show ya JB Mpiana akiwa na Wenge BCBG huko Planet Sono Beach Mayi ya Pembe. matamasha mengi ya wanamuziki wa Congo hufanywa hapa yakiandaliwa na kudhaminiwa na makampuni makubwa ya vinywaji kama Primus ambao ni wadhamini wa JB Mpiana, Skol ambao ni wadhamini wa muda mrefu wa Koffi, Tigo na wengineo.

Ni show ambazo zinatia raha kuangalia kwani kuna kuwa na kila aina ya shamrashamra na watu wanajiachia sana kwani hakuna kiatu kirefu (mchuchumio) wala kuogopa kutoka jasho, wengi wa washabiki huwa wamevaa beach wear au smart casual tuu kwani wako beach.


TAFSIRI YA WIMBO " RENDEZ VOUS MANQUÉ " UTUNZI WA WERRASON NGIAMA

March 19, 2014

Uwezo wa Werasson unaonekana sana kwenye nyimbo kama hizi ambapo huwa anazipatia sana kutokana na sauti yake. Kwangu mimi albamu ya Kibuisa Mpipa ama Solola Bien ni Albamu ambazo kiukweli nazikubali sana na nazisikiliza kila uchao sijajua ni kwa nini inawezekana zina touch fulani ya Ki BCBG, najua hili litawaudhi baadhi lakini kiukweli hpa namkubali sana Werasson.

Uchambuzi huu umeletwa na mwanajamvi Lubonji wa Lubonji wa Music na Lubonji Page, Shukrani kwako kamarade na maujuzi haya.

A l’heure des adieux / WAKATI TUKIAGANA

En partant loin de toi / NIENDAKO NI MBALI SANA NAWE

Mes yeux ce sont vidé tout d’un coup de lumière et je suis resté en jungle à force de pleurer / PUNDE, NURU YA MACHO YANGU IKAWA IMETOWEKA,MACHOZI YAENDELEA KUNIDONDOKA,NIKAAMUA KWENDA KUJIFICHA MUSITUNI

Nayaki ko tala yo jeudi na pokwa oh / NILIPITIA NYUMBANI KWAKO ALHAMISI JIONI ILI KUKUJULIA HALI

Nakuti lopango bakangi / GETI NIMELIKUTA LIMEFUNGWA

Na beti sonnette, na frapper na porte / WALA SIJABONYEZA KENGELE ILIOKO GETINI, NILIAMUA KUUGONGA MLANGO

Oboyaki nayo kondima / HUJAJA KUNIFUNGULIA

Nzok’ozalaki nakati ya chambre / KUMBE ULIKUA ZAKO CHUMBANI

Ozalaki kotanga photo roman na mbanda / UKITIZAMA PICHA NA MWANAUME MWENGINE

Otikaki consigne na sentinel, soki amoni ngaï a loba ozali té / UKAMPA AMRI MLINZI ASIFUNGUE MLANGO ATAKAPO NIONA,ASEME TUU HAUPO

Oko niokolo nga pourquoi tina / KWANINI WANINYANYASA KIASI HICHO!!

Oko sambwisa ngaï nzoto ah mama ah / WAFANYA MWILI WANGU UMEKONDA AH MAMA AH

Soki na zui mosusu, yo moto ya liboso y’oko benga nga ndoumba / NIKIAMUA KUCHUKUA MKE MWENGINE UTAKUA WA KWANZA KUNIPAKAZIA ETI MIMI MALAYA

WANAIMBA KWA PAMOJA :

Soki MILENE oboyi nga / KAMA KWELI HUNITAKI TENA MILENE

Lobela nga na yeba mama aah / NIAMBIE KIUWAZI NTAKUELEWA

Yak’okangela nga motema / KUKAA KWAKO NA MANENO MOYONI

Nako koka te GUY GUY na JOSÉ KONGOLO / KWAKWELI NASHINDWA GUY GUY NA JOSE KONGOLO

Soki MILENE oboyi nga / KAMA HUNIPENDI TENA MILENE

Lobela JACKIE WATUNDA bébé DEDASSE / JARIBU KUONGEA NA DADA JACKIE WATUNDA PAMOJA NA BÉBÉ DEDASSE

Yak’okangela nga motema / KUKAA KWAKO NA MAMBO MOYONI

Nako koka te MARRAINE MANDIBULE / KWAKWELI SINTOWEZA TENA MARRAINE MANDIBULE

WERASON :

Malheur ou bonheur / SHIDA AU RAHA!!!

Bato ya mokili bo ponela nga / NAWAOMBENI JAMANI NISAIDIENI KWA KUNICHAGULIYA MWENGINE

Mpo pasi nazali ko yoka eleki oyo ya moto ya volcan / SHIDA NILIONAYO INAMOTO KUZIDI WA VOLCANO

Oyo ba pompiers bakoka nanu ko boma te eh eeh hein / MOTO AMBAO HATA ASKARI ZIMAMOTO HAWAWEZI KUPAMBANA NAO

WANAIMBA KWA PAMOJA

Soki MILENE oboyi nga / KAMA KWELI HUNITAKI TENA MILENE

Lobela JACKIE WATUNDA bébé DEDASSE / JARIBU KUONGEA NA DADA JACKIE WATUNDA PAMOJA NA BÉBÉ DEDASSE

Yak’okangela nga motema / KUKAA KWAKO NA MANENO MOYONI

Nako koka te MARRAINE MANDIBULE / KWAKWELI SINTOWEZA TENA MARRAINE MANDIBULE

WERASON :

Miso na nga emona nde makambo / NILIO YAONA NILIYASHUHUDIA MWENYEWE NA MACHO YANGU

Ebongaka ko yoka lisolo epayi ya moto / SIO YA KWAMBA NILIAMBIWA NA MTU

Oyo ya nga miso nde témoin, na banzaki illusion nzoka nde réalité / MACHO YANGU YENYEWE SHAHIDI, NILIHISI NI UONGO KUMBE UKWELI MTUPU

Pasi oyo nazali komona, photocopie ya souffrance ya YESUS na purusé / MAUMIVU NILIO NAYO KWA LEO, NAYALINGANISHA NA YALE ALIYO YAPATA BWANA YESU AKIWA MSALABANI

Chemin de la croix / NJIA YA MSALABA

Bolingo ezanga juge / PENZI LANIHUKUMU PASIPOKUA NA HAKIMU

Ezanga n’ango pe punissable epayi ya mbulamatari yeh / KADHALIKA PIA SEREKALI YANIHUKUMU

Nako funda ya ngo wapi / NANI YULE ATAKAE NITETEA?

WANAIMBA KWA PAMOJA

Soki MILENE oboyi nga / KAMA KWELI HUNITAKI TENA MILENE

Lobela nga na yeba mama aah / NIAMBIE KIUWAZI NTAKUELEWA

Yak’okangela nga motema / KUKAA KWAKO NA MANENO MOYONI

Nako koka te GUY GUY na JOSÉ KONGOLO / KWAKWELI NASHINDWA GUY GUY NA JOSE KONGOLO

Soki MILENE oboyi nga / KAMA HUNIPENDI TENA MILENE

Lobela JACKIE WATUNDA bébé DEDASSE / JARIBU KUONGEA NA DADA JACKIE WATUNDA PAMOJA NA BÉBÉ DEDASSE

Yak’okangela nga motema / KUKAA KWAKO NA MAMBO MOYONI

Nako koka te MARRAINE MANDIBULE / KWAKWELI SINTOWEZA TENA MARRAINE MANDIBULE

WERASON :

Natindi LUVELELA HUGUES na nga ah / NIMEKUTUMIA MJUMBE WANGU LUVELELA HUGUES AJEAKUONE

Nasengi PATCHO PUANDA a bondela ah / PIA NAMUOMBA PATCHO PANDA AJE KUNIOMBEA MSAMAHA

Natindi MOVADI FREDY a bondela eh / NIKAMTUMA PIA MOVADI FREDY AJE KUKUBEMBELEZA

Okangi motema oboyi ko futa eh pona nini / WAKATAA KATU KUWASIKILIZA KWA NINI ?

ADJANI SESELE :

Loin des yeux, près du cœur CLAUDE PEMBA mah / INGAWA UPO MBALI NAMI , LAKINI PENZI LAKO LANIJAA MOYONI CLAUDE PEMBA

Eric OKANGÉ okomisi nga kilawu lawu na bolingo nayo eh / PENZI LAKO LANITIA WAZIMU ERIC OKANGE

Y’olobaki na ngaï yo keyi LONDRES y’oko zonga ah / WANIAGA WAENDA LONDON KWA MDA MCHACHE UTARUDI

Na kanga se motema DOMINIENGI ako yah / HUKU WASISIWASI UNIJAA, NAJIPA MOYO YA KWAMBA KWELI UTARUDI
… Dédicaces

BABY NDOMBE :

Marie oy’abota nga amonela nga pasi aza lokola yoh / MAMA YANGU MZAZI MARIE HUA KANIONEA HURUMA KAMA WEWE!!!

Le vieux nkoyi a respectaka yo SIDEZI MAMPATA / KAMA VILE WERRASON ANAVYO MUHESHIMU MKEWE SIDEJI MAMPATA

Y’a WERASON po abika se avanda na lilita / KWA WERASSON KUPONA YAMBIDI AKAJIHIFADHI MAKABURINI

HAMED MBALA, ELYSÉE BIJOU MBUMA bako lela yoh nga BABY eh / HAMED MBALA,NA ELYSÉE BIJOU MBUMA WATAINGIA KWENYE KILIO

WERASON :

Bolingo ezali mbeli té po y’ozokisa moninga / USICHUKUE MAPENZI KAMA KISU UTAKACHO MDHURU MWENZIO

Ezali pe boloko té oyo nga na kangami / WALA MAPENZI SI JELA NINAYO FUNGIWA NDANIEMO

Nako luka na mi kebisa kasi nzoto mokomi kolenga / INGAWA MWILI WANGU WAONYESHA DALILI ZA WOGA,NTAJITAHIDI ILI NIBAKI IMARA

FERRE :

MILENE ko kumisa oyo na kumisaka yo o ti nga wapi ? Yeah yeah yeah / MAZURI NILIKUA NIKIYAKUTENDEA ILIKUA KUKUPENDA,KUKUENZI NA KUKUJALI, LEO HII WANITIA WAPI MILENE ?

Obosani oyo nioso nasala pona yo, po lelo nakoma mpiaka Yeah yeah yeah / MEMA YOTE NILIOKUFANYIA WAYASAHU KWAKUA LEO NAISHIWA NA HELA

Yeba awa na mibomi ozali responsable ya kufa na nga MILENE Yeah yeah yeah / KAA UKIJUA LEO HII NAJIUA NA MTUHUMIWA WA KWANZA NI WEWE

JUS D’ÉTÉ MULOPWE :

Likambo eko sala ngaï pasi CHARLES NKONDÉ na lekisa tango na zueli yango lifuta te oh, weah / KINACHO NIUMIZA NIKUONA NIMEPITISHA MDA WANGU BUREE,PASIPOKUA NAFAIDA YEYOTE

Nga na lelaka MAMIE BAKIMBE a boyi nga hum / NALIA ZANGU MIE !!! MAMIE BAKIMBE KANIKATAA!!!

ASANTENI


FUJO HAZIKUZUIA SHOW YA FERRE GOLLA AFRIKA YA KUSINI

March 19, 2014

Mwanamuziki Ferre Golla akitumbuiza huko Afrika ya Kusini kwenye show ambayo fununu zilienea kuwa ingekatizwa na vurugu za Combattants.

Fujo zilizozuka majira ya saa mbili usiku wa onyesho la Ferre Gola huko Afrika ya KUsini hazikuzuia show hiyo kufanyika, kwa mujibu wa shuhuda Johnbas ambaye alikuwemo kwenye show hiyo akisema awali fununu zilizagaa kuwa “Combattans” wangevamia show hiyo majira ya saa tatu za usiku wakipinga kufanyika kwake lakini waliojitokeza ama walikuwa vibaka ama wahuni alisema shuhuda wetu.

“tulikuwa tumekaa Lobby majira ya saa mbili tukisubiri show ianze, ndipo likafika kundi la vijana wapatao 20 wakiwa na silaha za jadi pamoja na fimbo za kuchezea Golf ndipo walipoanza kuanya fujo nje ya ukumbi ila hali ilidhibitiwa na Mabaunsa na walipoongezeka walidhibitiwa na kutawanyika kila mtu kivyake” alisema shud=huda huyo.

Hawakuwa Combattants wale ni vibaka tuu ambao walitaka kupora watu kwani hata polisi walipoitwa walipofika walikuwa wametanwanyika kila mtu kivyake. alisema shuhuda huyo. Awali wapo waliosema kuwa vijana hawa waliletwa maalumu kwa ajili ya kupambana na Combattants habari ambazo hazijathibitishwa na yeyote wakiwemo waandaaji.

Katika vurugu hizo Baunsa mmoja aliumia kwa kukatwa na kitu kikali kichwani na kuvuja damu, aliwaishwa hospitaly na kupatiwa matibabu.

takribani muda sasa jumuiya ya vijana wa Congo wanaoishi Ufaransa, Ubelgiji na Afrika ya Kusini wamekuwa wakishinikiza mageuzi nchini DRC na kupinga siasa za huko na kuonyesha ghadhabu zao kwa wanamuziki wa DRC hasa waoonyesha kusupport utawala wa Kabila, hili limedhihirika wazi hasa baada ya maonyesho kadhaa ya wanamuziki wa DRC kuhairishwa kwa kuogopa fujo za vijana hawa awanaojulikana kama Combattants.

Show ya Ferre iliendelea na ilifana sana.


Follow

Get every new post delivered to your Inbox.

Join 93 other followers

%d bloggers like this: