Serge Kasanda (Serkas) Tajiri anayeimbwa sana Congo

image_thumb[3]

Serkas akiwa na Rais Kabila, Mapema mwaka huu.

Ukisikiliza Nyimbo za Congo zenye umaarufu wa Mabanga utasikia jina moja maarufu sana la Serkas au Serge Kasanda.

Anaitwa Serge Kasanda au Serkas kama unasikiliza nyimbo za Bolingo huyu jamaa anatajwa sana hasa na akina JB Mpiana. Serkas kama anavyofahamika mwenyewe ni mfanyabiashara mkubwa wa madini ya Almasi si kama wengine wapigaji Serkas yeye ni mfanyabiashara halali na anajulikana hata na viongozi wakubwa wa Congo.

JB Mpiana anamuita FMI (fond monetair international) kama vile Central Bank yaani ndio pesa zote zinatunza na kuhifadhiwa hapo kwani jamaa inasemekana ana cheda ya ajabu na kikubwa jamaa haringi kwani anatoa misaada sana huko kwao.

Serkas ana mali na amewekeza sana kwenye biashara akiwa anamiliki kampuni kadhaa zikiwemo IMMO SERKAS SPRL, SERKAS et SONS SPRL, GRUPO SERGIO e FILHOS LTD ikiwa inafanya biashara halali za ndani na nje ya Congo.

Jamaa ni mkasai ambalo ni kabila kubwa na ndio kwenye Almasi nyingi ya Congo akina Zadio Congolo wanatoka huko pia.

Kwenye Valentine ya mwaka huu Serkas alimzawadia mkewe Gari zuri la kifarari aina ya Marcedes Benzi yenye rangi nyekundu ndani kote. Serkas ni maarufu kwani gari zake zote huwa zinajina lake badala ya namba za kawaida.

Hivi karibuni alifungua apartments zake kwenye barabara maarufu ya June 30 au maarufu kama Boulevard du 30 Juin, hii ni barabara ya uhuru na June 30 ndio tarehe yenyewe, eneo hili ni maarufu kwani kumechangamka na makazi ni aghali ukilinganisha na eneo jingine.

image

Serkas akiwa ofisini kwake akikagua mawe – almasi

image

Mke wa Serkas akiwa ndani ya gari yake siku ya wapendanao – Valentine ya mwaka huu 2011

image

image

Serkas akiwa na Rais Kabila, Mapema mwaka huu.

 

image

Sehemu ya Apartment zinazomilikiwa na Serkas.

image

image

Sehemu ya magari yake

image

Cha mutu cha mutu cha zambe cha zambe, acheni Mungu aitwe mungu kuna watu wamebarikiwa na nafasi wanazitumia, komaa babu tutafika tuu.

Advertisements

4 Responses to Serge Kasanda (Serkas) Tajiri anayeimbwa sana Congo

 1. Anonymous says:

  papa puis le grand leadeur nime kukubali hiyo kali

 2. Ndekwa'Kwise says:

  Salute…… Sasa Kardozo Mwamba wanamuita “Le Bilgate bana Congolee” kumbe kuna wababe wake?

 3. Kyekuu A Town says:

  Naipenda Spoti Starehe kwa kuwa napata vitu vipya ambavyo nimevisikia sana ila sikuvijua, hii chiboko Papaa Serge Kadanda anatisha dah

 4. Silas says:

  Sasa huyu na Moize Katumbi nani ni tajiri zaidi ya mwingine?

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: