Albamu mpya ya Ferre Gola akimshirikisha Celine Deon na Rick Ross kutoka Desemba.

November 2, 2012

ferre

Niliwahi kuandika jinsi kizazi cha nne kilivyoamua kuupeleka muziki wa Congo international, Mwanamuziki Ferre Gola baada ya Fally kuimba na Olivia yeyey ametoka na Mwanamuziki Mcanada mwenye asili ya Ufaransa Celine Dion na bingwa mwingine ambaye majuzi aliwakonga nyoyo mashabiki wa Tanzania kwenye tamasha la Fiesta Rick Ross.

Ferre ameipa albamu yake hiyo mpya jina la BoƮte Noire ama Black Box itakuwa sokoni December ambapo amesema itakuwa ni zawadi ya Christmass kwa mashabiki wake, hayo yalithibitishwa na Meneja wa Mauzo na Masoko wa kampuni ya Jet Set bwana Vasco Mabiala, Bwana Mabiala pia alisema kuwa albamu hiyo imepewa jina hili kwa vile Black Box ni kisanduku ambacho kinatoa wingu la ni nini kimetokea hasa kwenye ndege zikipata ajali, anaeleza kuwa kwenye box la albamu hiyo yeye ndio atafungua milango endelevu kwenye sokola Ulaya na America kwa kuwashirikisha miamba hao wawili ambao wanakubalika na wana mashabiki sio Marekani tu bali duniani kote.

Ferre amesema kuwa Nyimbo zote ziko tayari, zimeshafanyiwa uchanganyaji na Video ziko kwenye hatua za umaliziaji ili zitoke kwa pamoja. 


SABABU RASMI ZA MGAWANYIKO WA WENGE MUSICA BCBG 4X4 TOUT TERRAIN NA MIAKA MITATU YA MWANZO YA BCBG NA MAISON MERRE – V

September 7, 2011

image

Baada ya Sehemu ya Kwanza, ya Pili na ya tatu  na majuzi ya nne kuitazama wenge Bcbg ya Jb Mpiana, Alain Makaba na Blaize Bula ilivyoianza miaka mitatu ya mwanzo kwa misukomisuko, kisha tukaitazama kuzaliwa kwa Wenge Maison Mere ya Werrason, Didier Masela na Adolphe vile ilivyoanza pia. Tuliona jinsi bcbg ilivyoondoka na lundo la wanamuziki wa iliyokuwa wenge musica original na kuwaacha Werrason, Masela na Adolphe wakibaki peke yao labda na jina wenge musica, kazi ya kujipanga upya na kurudi kwa kishindo ikawa ngumu kwelikweli, Pia tuliona jinsi WMMM alivyojipanga na ku recruit wanamuziki wapya kama Bill Clinton Kalunji, Celeo Scam na Flam Kapaya

 

Mpaka hapo bendi ikawa imekamilika na kuanza mazoezi. Ikafanya official show yake ikiendelea kutumia jina la WENGE MUSICA BCBG 4X4, Lakini baadae wakaachana na neno BCBG kwa kuwa lililetwa na kuwa introduced hapo WENGE MUSICA original enzi hizi na Jb Mpiana, Badala yake wakaweka la kwao “MAISON MERE” hivyo ikawa sasa wao ni WENGE MUSICA lakini MAISON MERE sio tena BCBG. Wenge Maison Mere maana yake wakimaanisha Wenge yao ndio Wenge Mama au Wenge Makao makuu ikiwa na makao yake makuu ZAMBA PLAYA ndani ya Kinshasa.

Je hilo jina MAISON MERE lilibuniwa na nani? alikua ni Werrason? jibu hapana, alikua ni Didier Masela? jibu hapana, je alikua Tata Mobitch Adolphe Dominguez? jibu pia hapana. Ukweli ni kwamba jina Maison Mere lilibuniwa na kupendekezwa na Baby Ndombe! Hilo ndio jibu sahihi.

Tukiacha hilo la jina bendi ilianza Rais akiwa Adolphe Dominguez huku Werra de la Forre akiwa makamu wa rais na artistic director pia, Didier Masela akiwa Chef d’orchestre. Baadae  ya muda kidogo ikaonekana Werra ndio awe rais kutokana nadhani na mvuto wake kwa mashabiki ambao tayari walikwishaanza kumshindanisha na Jb Mpiana wa Bcbg. Wakati huo huo JAPONAIS ambae alijiunga akitokea kwa Jb mpiana akapewa cheo cha artistic director alichokuwa nacho Werra akiwa pia makamu wa rais wa bendi.Na maandalizi ya album yao ya kwanza ile FORCE INTERVENTION RAPIDE yakawa yamekamilika, wakairelease hiyo album huku dogo FERRE GOLA akipewa aimbe vocals za Jb Mpiana.

Hapa muhimu kukumbuka kwamba album ya TITANIC ya BCBG Kiukweli ilikua imetayarishwa kwa pamoja na iliyokuwa wenge musica original kwa maana ya kwamba pia kina werrason walishiriki maandalizi ya album hiyo na walishaifanyia mazoezi na pia kupiga show. Kama utatazama nakusikiliza vizuri video hiyo hapo chini ambayo ni moja kati ya live concert za mwisho mwisho za wenge musica original ikiwa pamoja utaweza kusikia mipigo iliyokuja kusikika kwenye titanic baadae, hapa ilichezwa na kina werrason ndani ya wenge original, ukisikiliza vizuri mwishoni mwishoni mwa hii video utausikia mpini ambao baadae ulikuja kusikika kwenye wimbo wa borkinafaso uitwao Serge Palmi unaopatikana kwenye album ya Titanic, hapa Burkinafaso alikuwa anawachezesha kina Werrason huo mpini wake wa solo ambao baadae waliucheza kina Jb kwenye titanic.

 

Kuibuka kwa Bill Clinton

Kwa hiyo kiufupi ni kwamba album ya titanic ilikua iwe album ya wenge musica original ikiifuatia pentagone ambayo ndio album ya mwisho ya wenge musica original kama kundi. Tukiachana na hayo, mwaka 1999 mwimbaji kijana Heritier Bondongo akajiunga na maison mere then wakafanya album yao ya pili wakiita SOLO LA BIEN ambayo kiukweli ilipata mafanikio makubwa sana sokoni huku ikimuibua pia BILL CLINTON na kumfanya awe kipenzi cha mashabiki katika ulimwengu wa wapenzi wa muziki wa Congo kutokana na kazi yake nzuri na style yake ya kipekee ya atalaku aliyokuja nayo ambayo naweza kusema ndio iliyomtoa Tutu Kaludji sokoni na style yake iliyokuwa imekamata sana kabla ya ujio wa BILL CLINTON na pia baada ya kung’atuka Roberto Ekokota kwenye muziki.

Album hiyo pia ikafungua milango kwa maison mere kuanza kupata mikataba minono ya kwenda kupiga shows ulaya ambako walifanikiwa kumrecruit mpiga guitar kiraka PATIENT KUSANGILA ambae kina werra walikua nae wenge musica original lakini alibaki kwa Jb baada ya mgawanyiko lakini baada ya muda mfupi akamtosa Jb baada ya concert ya bcbg kule zenith 1999 baada ya kupewa nafasi finyu ya kupiga guitar kwenye show hiyo kama tulivyoona huko nyuma katika mfululizo wa makala haya. Baada ya kuachana na JB kusangila alibaki Paris akiishi huko ndipo kina werra walipoenda na maison mere wakamkuta na kumshawishi ajiunge nao.

 

Mimiche amrithi Masela kwenye Bass Guitar

imageMambo yakaendelea, wakiendelea kupata kazi nyingi ndani na nje ya africa, badae wakiwa katika tour nyingine Canada CHRISTIAN MABANGA ambae alikua amerithi nafasi ya  DIDIER MASELA (aliyekua amejiondoa kundini baada ya tour ya ulaya) kama Chef d’orchestre akaugua ghafla ikabidi abaki Canada kwa matibabu zaidi, ndipo Ferre Gola akapewa nafasi hiyo, akawa Chef d’Orchestre na wakarelease album ya TERRAIN EZA MINE ikiwa ni album ya tatu ya kundi kabla ya album binafsi ya werrason, ile KIBUISA MPIPA. Baada ya Masela kuondoka kundini ikabidi waanze mpango wa kumsaka mrithi wake katika bass guitar, ndipo wakampata MIMICHE kutoka kwenye bendi ya PEPE KALLE 

 

Patient Kusangira ajitoa WMMM 

Then wakapata deal nyingine ya kusafiri kwenda kupiga paris, lakini kabla ya kuelekea paris walitakiwa kupitia  Congo Brazaville kwanza, wakiwa katika pilikapilika za maandalizi ya safari hiyo, ndipo KUSANGILA akaachana na Maison Mere kutokana na jina lake kuondolewa katika kikosi kitakachosafiri kuelekea Brazzaville na baadae Paris, kitendo ambacho kilionekana na wengi akiwemo Kusangila mwenyewe kama ni adhabu ya kisasi toka kwa werrason kutokana na ugomvi wao wa siku nyingi toka Wenge Musica original uliosababishwa na mwanamama mchezo show pekee wa wenge musica original kipindi hicho NANA SUKALI.

image

Ikumbukwe kuwa Werre alishawahi kufanya jaribio la kumfukuza Kusangila wenge original lakini Jb na viongozi wengine kundini hawakukubaliana na adhabu hiyo kali dhidi ya Kusangila kwa kuwa walikuwa wakifahamu kinachoendelea kati ya watatu hao kundini yani Werra, Kusangila na Nana Sukali, hivyo ikaonekana ni wivu wa kimapenzi tu na badala yake wakapendekeza asimamishwe tu na si kufukuzwa kabisa, hivyo kitendo hiki cha kuachwa katika safari ya ulaya bila ya sababu za msingi kikatafsiriwa na wanaojua historia ya wawili hawa werra na kusangila kama ni muendelezo tu wa ugomvi wao wa siku nyingi sababu ya mwana mama Nana sukali. Pia werra aliwahi kufanya jaribio la kumtimua Tutu Kaludji kwa kutomuheshimu yeye Werra kama kiongozi na badala yake kumheshimu zaidi Jb na Viongozi wengine kundini.

 

WMMM yafanya Show ya Bercy na Aimelia Lyase atambulishwa rasmi kwa mashabiki.

Baada ya kujiondoa Maison Mere Kusangila kwa msaada wa marafiki zake Sam Tshintu na Modogo akarudi zake Paris. Kwa upande wa bendi ya Maison Mere baada ya kumaliza kazi Brazaville wakachukua zao flight kuelekea Paris, na kupiga ndani ya BERCY Show yenye mafanikio makubwa sana na isiyosahaulika miongoni mwa wapenzi wa maison mere, watu walijaa kupita kiasi na ndipo Werra alipopachikwa jina la Le PHENOMENA na Pia ndio siku werra alipomtambulisha Aimelia Lyase Demingongo kama mwanamuziki mpya wa Maison Mere akitokea kwa mahasimu wao wakuu wenge bcbg.

 

Dominguez ajitoa WMMM

image

Pichani ni Dominguez alipiokuja nchini, hapa akibadilishana namba na Steven Kanumba wa Bongo Movie

Baadae mwaka 2001 “Big Tata” Adolphe Dominguez nae akajitoa, bendi sasa ikawa ya Werrason peke yake.Kwa upande mwingine   mwanamuziki “mtata” na mzee wa kuhamahama Ali Mbonda akatimka Maison Mere na kurudi bcbg na baadae mwishoni mwa 2001 akarudi tena Maison Mere, JAPONAIS nae akaondolewa kwenye nafasi kama Artistic Director, nafasi yake ikachukuliwa na fundi, mtaalam wa solo guitar na music arrangement kiujumla Flam Kapaya.

Next kuzaliwa kwa Le Marqius de Maison Mere, nini chanzo cha vijana kufanya uasi huo na kwa nini hawakufanikiwa licha ya kuanza kwa kishindo?, tutajua zaidi.

Natuma salamu kwa Bana Werason wote Mukulu Timothy Banda shukrani sana kwako kwa mchango wako kwenye blog hii, La Suvereign Maghambo, Mukubwa Chizenga, Muddy Saloon, Choki na Nelly nakati ya Kinondoni, Japhet Malya muzee wa Koffi na WMMM, Abdul Tall na wapenzi wote wa Werason.