Arsenal kusajili watatu wapya

Meneja wa Arsenal Arsene Wenger amesema ataimarisha kikosi chake kwa kusajili wachezaji wapya "wawili au watatu" kwa ajili ya msimu ujao.

Wenger

Kusaka mwelekeo: Arsene Wenger kuimarisha kikosi msimu ujao

Wenger atatangaza kusajili mchezaji mmoja kabla ya Kombe la Dunia. Mchezaji huyo anatazamiwa kuwa mshambuliaji wa Bordeaux Marouane Chamakh.

Huku mikataba ya walinzi wa kati William Gallas, Sol Campbell na Mikael Silvestre ikiisha mwezi Juni, upande wa ulinzi pia huenda ukahitaji kuimarishwa.

Ninakiamini kikosi nilichonacho, lakini kama naweza kuongeza wawili au watatu, nitafanya hivyo

Arsene Wenger

"Ninakiamini kikosi nilichonacho, lakini kama naweza kuongeza wawili au watatu, nitafanya hivyo" amesema Wenger.

"Inategemea na nani ataondoka. Je tutaweza kumsajili tena Gallas? tutajaribu kukiimarisha kikosi ingawa bado hatujazumgumza na yeyote" ameongeza Arsene Wenger.

Amesema ana imani na kikosi chake kuwa imara zaidi msimu ujao kwa sababu wachezaji wana nafasi ya kurekebisha ubora wao.

Wenger amekiri kuwa alisikitishwa na matamshi ya Andre Arshavin, akisema anaipenda Barcelona.

Arshavin aliyetokea Zenir St Petersburg mwezi Januari mwaka 2009, ana uguza jeraha, na huenda asicheze dhidi ya Blackburn siku ya JUmatatu.

One Response to Arsenal kusajili watatu wapya

  1. Isaq Kifaluka says:

    Binafsi sifurahishwi na mfumo anaoutumia Wenger kwa kuweka chipukizi wengi katika timu,tunataka kuona pia wakongwe wanapata nafasi ya kuonyesha uwezo wao na kutoa changamoto kwa chipukizi ili timu iwe imara zaidi na zaidi

Leave a comment