Franck Ribery kutocheza fainali

May 18, 2010

Rufaa ya mpachika mabao mashuhuri wa Bayern Munich Franck Ribery kutaka adhabu yake ya kutocheza mechi tatu baada ya kuoneshwa kadi nyekundu, imetupwa na mahakama maalum inayosuluhisha masuala ya michezo na hataweza kucheza katika fainali ya Jumamosi ya Ubingwa wa Ulaya dhidi ya Inter Milan.

Ribery akioneshwa kadi nyekunduSiku Ribery alipooneshwa kadi nyekundu

Ribery alikata rufaa kwa mahakama hiyo baada ya kupewa adhabu ya kutocheza michezo mitatu na UEFA baada ya kutolewa kwa kadi nyekundu katika mchezo wa nusu fainali mzunguko wa kwanza dhidi ya Olympique Lyon.
Mchezaji huyo raia wa Ufaransa, alifahamu hatma yake kupitia taarifa iliyosema: “Mahakama hiyo imetupilia mbali rufaa na imethibitisha adhabu ya kufungiwa michezo mitatu iliyotolewa na UEFA.

“Kwa kadri itakavyokuwa, mchezaji huyo hataweza kucheza katika mchezo wa fainali ya Ubingwa wa Ulaya kwa mwaka 2010. Sababu iliyotolewa kuhusiana na uamuzi huo itachapishwa na mahakama hiyo katika siku chache zijazo.”
Ribery, ambaye tayari amekwishatumikia adhabu hiyo kwa kukosa mechi moja, alipewa kadi nyekundu baada ya kumkanyaga Lisandro Lopez.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Bayern Munich Karl-Heinz Rummenigge akizungumza na waandishi wa habari: “Kwa yeye kukosa fainali ya Ubingwa wa Ulaya kwa kosa la kucheza rafu ni adhabu kali sana.”
Ni jambo lisilo la kawaida kwa kosa kama la kufungiwa mchezaji kupelekwa mbele ya mahakama hiyo ambayo zaidi inashughulikia masuala yenye utata zaidi na yaliyo nje ya uwanja.


%d bloggers like this: