Hellen Dausen, muwakilishi wa Tanzania kwenye shindano la dunia Miss Universe 2010.

May 17, 2010

image

image

image

Anaitwa Hellen Dausen akiwa ni Miss Universe 2010 na ndiye muwakilishi wa Miss Universe World.

kipaji hiki kiliibuliwa toka Arusha na yeye ni Model na ni muwakilishi wa nne wa Miss Universe


Harusi za Kimalay, Sehemu ya Pili.

May 17, 2010

n618528368_1348020_2812

Nimeirudia hii baada ya kupata ombi toka kwa Bi. Harusi mtarajiwa Dada Mayasa, sijui labda anataka kuiga vindu humu.

Mara ya mwisho niliandika kuhusu harusi za kimalay (gonga hapa) na huu ni muendelezo wa mfululizo ma tukio zima la siku hiyo ambayo kila mmoja huwa anaiwazia maishani.

Wamalay tumefanana nao kwa Mila na Desturi kwa kiasi fulani, ama kwa hakika ukibahatika kuhudhuria harusi za kimalay utafurahi mbwembwe na shamrashamra za harusi. Kwa kawaida wao hawachangishani kama tunavyofanya sisi, ni jukumu la familia kufanikisha shughuli hii, na kwa taarifa yako sherehe ya kawaida ya mtu wa kawaida hugharimu kuanzia Ringit 100,000 hadi laki tatu kutegemeana na familia. Ringit 100,000 ni sawa na Tsh 30,000,000/- , Milioni 30.

Gonga hapo chini upate kuona mtirirko wa matukio kwenye harusi hii ya rafiki yangu Nazmi ambaye alimuoa bibiye Aimi.

Read the rest of this entry »


“Amani” Wimbo wa Kichina ulioitangaza Tanzania nje, ila…

May 17, 2010

kundi hili ni maarufu sana Asia huku kiongozi wake Hayati Wong Ka kui akiwa bado anachukua Tuzo mpaka miaka ya karibuni. Ingawa walijiunga tena mwaka 2005 lakini bado kundi la mwanzoni albam zao ziko sokoni mpaka wa leo.

Wong Ka Kui alifariki dunia June 30 1993 pale jukwaa lilidondoka wakati wakifanya shooting kwenye moja ya maonyesho huko Japan, Wong pamoja na wanaband wake wengine watatu walifariki dunia ambapo Wong alifariki dunia baadaye akiwa hospital.

Ukiongelea mafanikio kila albamu yao kati ya 10 walizopata kutoa kila moja iliuza zaidi ya kopi million 5 kwa asia pekee.

Mwaka 1991 Beyond walitoa wimbo unaoitwa Amani kutoka kwenye albamu yao iliyojulikana kama Deliberate, Wimbo wa amani uliandikwa na Wong mwenyewe baada ya kufanya ziara hapa Tanzania. Wong alipenda sana kujua kuhusu Africa baada ya kutoa wimbo uliolaani ubaguzi wa rangi na kutaka Mandela aachiwe, wimbo huu ulijulikana kama Glorious Age na uliwafungua macho Asia kuhusu Africa na ndipo alipoamua kuja kutembelea africa.

Wimbo huu uliitangaza sana Tanzania hasa kwa Asia ingawa si kwa mazuri kama njaa na picha zilizomo ila ukisema Tanzania Mchina yeyote mpenzi wa muziki watakuuliza kama unawajua Beyond, kiukweli ni wachache wanajua kuhusu kundi hili.

Alipoulizwa alisema kuwa ameamua kutunga wimbo wa Amani kwanza kutokana na hali ilivyokuwa kwenye nchi nyingi za Afrika ambazo zilipigana vita za ukombozi wenyewe kwa wenyewe, pia alisema alivutiwa na mandhari nzuri aliyoiona lakini akasema sehemu za vijijini kuna shida na watoto hawana chakula, jambo lililopelekea yeye kufanya Concert maalum kwa ajili ya kuchangia watoto wenye uhitaji, sina hakika kama ziliwafikia lakini inasemekana pesa zilichangwa toka Hongkong, China, Malaysia, Singapore na Japan alipewa nani siwezi kujua.

Mwaka jana Bendi ya Kilimanjaro Connection ilikuwa ziarani Asia na wakapiga kambi Malaysia jijini Kuala Lumpur, moja ya nyimbo zilizowafanya wawe maarufu na kupendwa na nipale walipopiga kwa ufasaha nyimbo za kundi hili la Beyond na kujaza watu kibao, bofya chini upate uhondo.

Ukitaka kujua zaidi bofya hapa


Solo Thang apakua Video Mpya ya All I Need

May 17, 2010

Anaitwa Msafiri Kondo aka Traveler aka Msafiri aka Solo Thang, tumia lolote kati ya hayo.

Katika Interview yangu na Solo Thang aliniambia kuwa anamalizia Kutoa CD ili aanze Video Production na aliahidi kuwa zitakuwa kwenye kiwango cha hali ya juu.

Kwa watakao angalia hii Video ya All I need mtakubaliana na mimi jamaa yuko juu kimuziki na style ya Wimbo huu ni ya kimataifa zaidi, Hongera mkulumbe kitu imesimama mbaya!.


Njaa kipimo cha akili…!

May 17, 2010

DSC00757

Waswahili wanasema njaa kipimo cha akili, jamaa alijitambulisha kwa jina la Jonto anasema kwa njia hii ndio hupata mkate wake na familia yake, kikubwa jamaa alisema anaishi Kigogo ila kila siku anajikuta akitembea si chini ya kilometa 20 kuwasaka wateja ili awachekeshe.


Baada ya ushindi kwanini tusijipumzishe…!

May 17, 2010

image

Rafiki yangu Faizal Ismail wa Kuala Lumpur amenitumia picha yake baada ya kusherehekea ushindi, Faizal alishinda gari aina ya Gen II baada ya kuwekeana dau na mwenzie kuwa nani atashinda kati ya Man U na Chelsea. Hongera sana abang.


%d bloggers like this: