MAKHIRIKHIRI WAKUTANA NA RAIS WAO LEO JIONI KUKABIDHIWA BENDERA YA TAIFA

May 24, 2010

Lile kundi maarufu kwa jina la makhirikhiri likiongozwa na SHUMBA RATSHEGA leo limealikwa rasmi ikulu ya Botswana kwa ajili ya kukabidhiwa bendera ya taifa kama ishara ya kuutangaza utamaduni wao ktk ardhi ya Watanzania,nikiongea na mwakilishi wa kundi hilo ambaye ndio kiongozi wao MOSES MALAPELA aka SHUMBA RATSHEGA amesema serikali ya Botswana inawathamini na kuwaheshimu sana hivyo wanapotoka kufanya ziara kama hii ni lazima wakabidhiwe bendera ya taifa lao ili kuipeperusha wawapo nje ya nchi yao.

Ktk maandalizi ya kuwapokea ambapo ratiba ya safari yao itaanzia asubuhi watatoka Gaborone saa nne na dkk 15 na south African airways watafika Johannesburg saa 5 na dkk 15 na watabadili ndege.

Wataanza safari ya kutoka south afrika saa 8 na dkk 55 mchana kwa ndege ya shirika hilo hilo la southafrican airways na watafika dar international airport saa 1 na dkk 15 usiku na hapo mapokezi makubwa ya watanzania wakiongozwa na wane star,kwa dkk chache kutakuwa na kitendo cha kupokelewa kitamaduni ambapo wane star atamvalisha shada la kijadi kiongozi wa makhirikhiri atamkabidhi ngao na mkuki kuonyesha ishara ya utamaduni wetu na kwa dkk chache watachezewa ngoma ya kimasai ambayo nayo itapigwa na kundi la wane star na baada ya hapo msafara wa kuelekea hotelini giraffe hotel ndo utaanza rasmi,then shughului nzima utaratibu utaofuata utatangazwa kupitia radio times ambayo ndio mwenyeji wa wakali hawa kutoka Botswana.

Makhirikhiri wataanza onyesho lao la kwanza Mjini Shinyanga na kuelekea Mwanza na wiki ijayo watarudi Dar kwa ajili ya show 2 ambapo show ya kwanza itaanza diamond jubilee na show ya pili ni uwanja wa taifa wa uhuru na baada ya hapo watamaliza ziara yao mjini mbeya tar 12 mwezi wa 6, 2010.

Hii na ziara ya aina yake kutokea Tanzania kwani wadau wengi wamekuwa wakiwaleta wasanii wengi toka bara la ulaya na Amerika lakini tumekuwa tukikosa cha kujifunza kwani sanaa tunayoipata haifundishi kitu jamii yetu zaidi ya kuongeza idadi ya wavaa vipuri na macheni kibao shingoni pasipo kuelewa unachokivaa ni tamaduni za watu.hivyo basi ujio wa makhirikhiri ni mafunzo tosha kwa watanzania.

Wenyewe wameahidi kutoa burudani ambayo hatutaweza kuisahau na kuona kuna umuhimu wa kuwaita tena siku za mbele


May 24, 2010

image


Blackpool 3 Cardiff 2

May 24, 2010

Ikiwa nyuma mara mbili Blackpool iliweza kujitutumua na kufanikiwa kuilaza Cardiff na kufanikiwa kupanda daraja masimu ujao. Sasa itacheza Ligi Kuu ya Soka ya England maarufu Premier League. Katika mpambano uliofanyika uwanja wa Wembley huku kukiwa na jua kali.

Brett Ormerod

Ormerod akishangilia bao la tatu la Blackpool

Blackpoo ama maarufu kwa jina la The Tangerines walishinda pambano hilo kwa mabao 3-2, ambapo mabao yote yakiwa yamefungwa kiufundi kipindi cha kwanza na kwa baadhi ya nyakati ni kutokana na makosa ya walinzi.

Wachezaji wa timu zote mara kwa mara iliwabidi wajipooze kwa kunywa maji kutokana na jua kali.

Michael Chopra na Joe Ledley mara mbili waliifungia mabao Cardiff na kuwafanya waongoze, lakini shuti la adhabu ndogo la moja kwa moja lililofumuliwa kiufundi na Charlie Adam pamoja na bao la karibu na lango la Gary Taylor-Fletcher yaliiwezesha klabu hiyo ya Lancashire kusawazisha kabla Brett Ormerod kupachika bao la tatu la ushindi kabla ya mapumziko.

Matokeo hayo yanakamilisha msimu uliokuwa na jitahada kubwa ya wachezaji wa Blackpool, ambao sasa watacheza mashindano makubwa tangu mwaka 1971.

Pia ni mafanikio makubwa kwa meneja Ian Holloway, ambaye mikakati yake ya ushambuliaji kwa mwaka mzima na pia katika uwanja wa Wembley imeisaidia timu yake kushinda kwa mfumo wa uchezaji wa 4-3-3.

Blackpool inaweza kuonekana ni klabu ndogo kuweza kucheza Ligi Kuu ya England, lakini hivi sasa wanajinoa kukabiliana bega kwa bega na wachezaji mahiri wa Engaland baada ya kushinda mchezo ambao umewapatia kitita cha paundi za Uingereza milioni 90.


Villa ajiunga na Barcelona

May 24, 2010

David Villa atatambulishwa rasmi kuwa mchezaji wa Barcelona siku ya Ijumaa, baada ya kukamilisha taratibu za uhamisho wa paundi milioni 34 kuihama klabu yake ya Valencia.

David Villa

David Villa ajiunga na Barcelona

Mshambuliaji huyo ambaye pia huchezea timu ya taifa ya Hispania, ameingia mkataba wa miaka minne kuichezea Barcelona na ni usajili wa kwanza msimu huu kufanywa na klabu hiyo, huku Cesc Fabregas ikisemekana pia yupo njiani kujiunga na Barcelona.

Villa, mwenye umri wa miaka 28, anatarajiwa kuwasili Barcelona siku ya Alhamisi kufanyiwa uchunguzi wa afya.

Ni mchezaji wa kikosi cha kwanza cha Hispania, alikuwemo katika timu iliyochukua ubingwa wa Ulaya mwaka 2008 na ni mmoja kati ya wachezaji wanaotazamiwa kuwika katika michuano ya Kombe la Dunia.

Kuwasili kwake Barcelona kumezidi kuongeza tetesi za mustakabali wa washambuliaji wawili wa timu hiyo Thierry Henry na Zlatan Ibrahimovic kama wataendela kubakia au la.

Baada ya mkutano wa bodi ya wakurugenzi ya klabu ya Valencia asubuhi ya Jumatano, Manuel Llorente, Rais wa klabu hiyo inayojulikana pia kwa jina la utani la "Los Che", amesema wamekubaliana na Barca kuwauzia mchezaji huyo.

"Tumemuuza David Villa kwa Barcelona kwa gharama ya euro 40 million," amewaambia waandishi wa habari huko Mestalla.

"Kama kila kila mtu anavyofahamu tungekuwa tumekamilisha mkataba huu tangu mwaka jana, lakini tulidhani wakati ule ilikuwa muhimu kukiweka kikosi chetu kama kilivyo kujaribu kuingia katika ligi ya Ubingwa wa Ulaya.

"Tumefanikiwa katika lengo hilo na tumemaliza katika nafasi ya tatu katika ligi na Villa amechangia kwa kiasi kikubwa kufikia lengo hilo. Tunadhani ni biashara nzuri na muhimu kwa hali ya kiuchumi ya klabu."

Rais wa Barcelona anayeondoka madarakani Joan Laporta alidai siku ya Jumanne klabu hiyo "imeridhika" na mchango wa Ibrahimovic wa mabao 21 katika msimu wake wa kwanza tangu alipowasili akitokea Milan.

Henry anaonekana yupo njiani kwenda kucheza ligi ya Marekani maarufu kama Major League Soccer, huku Laporta akifahamisha Wamerekani wakimhitaji Mfaransa.


Inter mabingwa Ulaya waichapa Bayern 2-0

May 24, 2010

Inter MIlan mabingwa wa Ulaya.

Mourinho ameiwezesha Inter Milan kutwaa taji la Ulaya kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka 45.

Historia ya ligi ya soka ya vilabu bingwa barani Ulaya imeandikwa upya baada ya Jose Mourinho kuiwezesha Inter Milan kuichapa Bayern Munich 2-0 na kutwaa taji kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka 45.

Katika mechi hiyo iliyofanyika uwanja wa Bernabeu nchini Hispania, huku Bayern wakionekana kulegalega safu ya ulinzi, mshambuliaji Diego Milito kutoka Argentina alifunga magoli yote mawili kufanikisha ubingwa huo.

Kwanza aliipatia Inter goli la kuongoza alipomalizia vizuri mpira ulioanzia kwa mlinda mlango Julio Cesar ambaye alitanguliza mbele kujibu shambulio la Bayern.

Na alikamilisha ushindi kwa goli la pili, huku ngome ya Inter ikiwa imara kwa muda wote – matokeo hayo yameifanya Inter kuwa timu ya kwanza ya Italia kubeba vikombe vitatu vikubwa katika msimu mmoja.

Historia

Mafanikio yana maana kuwa, Mourinho, aliyeshinda kombe hilo akiwa kocha wa Porto mwaka 2004, anakuwa mtu wa tatu katika historia kushinda na vilabu viwili tofauti.

Anaungana na Ernst Happel na Ottmar Hitzfeld kupata heshma hiyo kubwa – akiwa ndiyo kwanza ana umri wa miaka 47, na kwa kufanya hivyo, amemaliza kiu ya miaka 45 ya Inter Milan kushinda tena taji kubwa zaidi katika soka ya vilabu Ulaya.

Jambo la muhimu zaidi ni kwa Mourinho ni kwamba amefanya hivyo akikabiliana na mwalimu wake Louis van Gaal, ambaye waliwahi kufanya kazi pamoja Barcelona kunako miaka ya 1990, na kuhitimisha mwanafunzi kumfunza mwalimu.


%d bloggers like this: