Wakawaka; Wimbo wa Shakira kwa Kombe la Dunia ambao umekuwa gumzo.

May 10, 2010

Huku bado kukiwa na manung’uniko toka kwa wananchi wa afrika ya Kusini kuhusu wimbo maalum utakaotumika kwenye ufunguzi wa Kombe la Dunia ambapo mwanadada shakira ametoa kibao chake, Yamezuka majibizano kwenye mtandao ambapo wananchi wa Ghana na Cameroon wamekuwa wakibishana wimbo huu ni asili yao.

Kwa mujibu ya wavuti wa You Tube, Wananchi hao wamekuwa wakijibizana huku kila mmoja akidai wimbo huu umetokea nchini kwake. Wakiongea wananchi mbali mbali walisema Wimbo huu asili yake ni Cameroun na ulikuwa ukitumika kwenye gwaride na paredi za huko. Haya yetu masikio.

Chelsea mabingwa Ligi Kuu ya England 2010

May 10, 2010

image

Chelsea wamemaliza msimu kwa kishindi kizito wakati walipoichapa Wigan magoli 8 – 0 katika mojawapo ya mechi 10 za kukamilisha msimu zilizochezwa Jumapili. Ingawa Manchester United walipata kazi rahisi kuitandika Stoke City 4 – 0, Chelsea wamefikisha pointi 86 na Manchester United wana pointi 85.

Nicholas Anelka ndiye aliwafungia Chelsea goli la kwanza kunako dakika ya tano ya mchezo alipomalizia mpira wa adhabu uliopigwa na Didier Drogba.

Goli la Anelka lilifungua mwanya kwa Frank Lampard kupachika mkwaju wa penati baada ya kufanyiwa madhambi na Gary Caldwell, ambaye alitolewa nje kwa kadi nyekundu.

Salomon Kalou alitumbukiza la tatu baada ya mapumziko baada ya kugongeana vizuri na Lampard na Anelka akaandika la nne.

Karamu ya magoli ilikuwa inazidi kushika kasi, Didier Drogba alianza pole pole lakini hatimaye alifunga matatu na kumaliza msimu akiwa mfungaji bora.

Kwanza alifungwa kwa kichwa, kisha mkwaju wa penati na goli la ndani ya 18. Mwishowe Ashley Cole akamalizia la mwisho.

Teh Teh Teh Man U ….

May 10, 2010

image

Kutana na Giuliano Stroe, Baunsa mtoto wa miaka mitano aliyevunja Rekodi ya dunia.

May 10, 2010

image

Anaitwa Giuliano Stroe toka Romania, ana miaka mitano tu na tayari ana miraba 6 tumboni mwake (6 pax) na ameshaingia kwenye kitabu cha kumbukumbu cha walivunja rekodi cha Guiness.

akiwa na umri wa kuanza shule Giuliano Stroe aliingia kwenye kitabu cha Guiness mapema mwaka huu baada ya kutembea kwa mikono umbali wa mita 10 akiwa na mpira wenye uzito kati ya miguu yake. Tangu hapo video yake ya dakika 4 imekuwa na hit za ajabu na kuikonga dunia huku kila mtu akitaka kujua kulikoni na kupelekea mtoto huyu kupamba vichwa vya habari mbali mbali duniani. Bonyeza player kupata ushuhuda.

%d bloggers like this: