Monday, June 30, 2008
Karibuni nyumbani mwayego….!
Shabiki wa Timu ya Ujerumani akiwa amesimama juu ya Taa za kuongozea magari wakati wachezaji na makocha wa Timu ya Taifa ya Ujerumani wakiwasili huko Ujerumani jana, Hebu pata picha hawa jaa wangeshinda mtiti ungekuwaje?
Mchezaji wa Ujerumani Lukas Podolski (Juu na chini pichani) akiimba mbele ya mashabiki waliokusanyika kuwapokea mashujaa wao.
Hii ni baada ya mchezo wao wa jana na Hispania kwenye fainali za Euro 2008 na Spain kushinda kwa 1-0. Picha zote na AFP
Serena na Venus hatarini kucheza Fainali wao kwa wao
Kili Music Award yafana
Mchezaji Taifa Stars adaiwa “Jezi” baada ya kubadilishana na Eto’o wa Cameroon
Na Phillip Nkini wa Mwananchi
UMILIKI wa jezi za timu ya Taifa Stars umezua balaa kwa baadhi ya wachezaji wa timu hiyo kujikuta wakikatwa fedha zao za posho kwa madai ya kufidia jezi ambazo ama walibadilishana na wenzao wa Cameroon au kupoteza.
Kwa upande wake, Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) linasema: ”Jezi si mali ya wachezaji.”
Kampuni ya Bia ya Serengeti Breweries na Benki ya NMB, wadhamini wa Stars wamekuwa wakitoa vifaa kwa wachezaji wa timu hiyo kuanzia vile vya mazoezi hadi vya mechi mbalimbali ambazo timu hiyo imekuwa ikicheza.
Lakini, pamoja na hali hiyo kumezuka tatizo kwa baadhi yao (wachezaji) na uongozi wa timu hiyo kukosana baada ya baadhi yao kubadilishana jezi majuzi na wachezaji wa Cameroon, Indomitable Lions, jambo ambalo limewazulia mambo.
Mchezaji mmoja kinda wa timu hiyo (jina tunalo) alishindwa kumpa Geremi Njitap wa Cameroon jezi yake kwenye mchezo kati ya Stars na Cameroon mjini Yaounde baada ya mchezaji huyo kutaka wabadilishane.
Kinda huyo aliiambia Mwananchi kuwa alihofia kuja kurejea nchini na kudaiwa jezi.
Lakini, beki wa timu hiyo alibadilishana jezi na mshambuliaji wa Cameroon, Samuel Eto’o Fils baada ya Mcameroon huyo kumfuata mwenyewe na kumtaka afanye hivyo.
Hata hivyo, pamoja na wachezaji hao kudaiwa jezi hizo Ofisa Habari wa TFF, Florian Kaijage aliithibithishia Mwananchi kuwa jezi si mali ya wachezaji, bali ni mali ya shirikisho hilo na mchezaji atakapoipoteza, basi utaratibu wa malipo utafanywa.
”Jezi sio mali ya wachezaji ni mali ya Shirikisho la Soka, kila mchezaji anapewa jezi kwa kufuata utaratibu maalum ukipewa lazima urudishe usiporudisha unaandaliwa utaratibu wa kulipia.”
“Sisi bado tupo nyuma sana hatujafika huko walipo hao akina Senegal au Cameroon kuwa na wadhamini wakubwa, kiasi kwamba mchezaji mmoja kuwa na jezi zaidi ya kumi. Hapa kwetu, tunaweza kutumia jezi moja kwenye mechi mbili wenzetu kila mechi na jezi yake.
”Ukiangalia mchezaji kama Eto’o anandaliwa jezi zaidi ya 50 na Kampuni ya Puma ni tofauti sana na sisi, ingawa kubadilishana moja mbili siyo vibaya, lakini isiwe watu kumi na kuendelea,” alisema Kaijage.
Uchunguzi wa Mwananchi umeonyesha kuwa wachezaji hao wa Stars wamekuwa hata wakati mwingine wakipigiwa simu wakiwa majumbani kwao ili warudishe jezi ambazo wamekuwa wakiondoka nazo kwa bahati mbaya au ambazo zimekuwa zikipotea.
Ukweli ni kuwa kila mchezaji wa Stars anapopoteza jezi moja hukatwa posho yake kuanzia Sh20,000 na kuendelea.
Hali hiyo ndiyo inayosemekana kuwa itamkumba beki na nahodha msaidizi, Nadir Haroub Cannavaro aliyeamua kubadilisha jezi na Eto’o.
Werasson awakana wanamuziki wa Congo nchini
MWANAMUZIKI mkongwe wa Jamhuri wa Kidemokrasia ya Kongo, Werasson amesema hamjui mwanamuziki hata mmoja kutoka Kongo anafanya muziki hapa Tanzania.
Hivi karibuni wanamuziki wengi kutoka Kongo waliokuja hapa nchini walijitangaza kuwa wengine ni ndugu wa Werrason huku wengine wakisema kuwa wenyewe ni watoto wa mkongwe wa Muziki nchini humo Pepe Kalle, na katika tukio la karibuni ni pale mwanamuziki ally Choki alipoonekana amepiga picha na Werason alipokwenda kutafuta wanamuziki huko na kusema kuwa Werasson alimsaidia kutafuta vijana.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam juzi Werasson alisema ‘simfahamu mwanamuziki hata mmoja wa Tanzania wala mkongo ambaye anaimba muziki hapa huyo anayejiita mtoto wa Pepe Kalle pia hamfahamu.
“Mimi nipo na mtoto mmoja wa Pepe Kalle ambaye namfundisha muziki pale Kongo, lakini huyu wa Tanzania mimi simfahamu kwakuwa watoto wake wote nawajua na hivyo labda awe mwingine zaidi,” alisema Werassons.
Werrason alisema kwa kuwa hawajui wanamuziki wa Kongo walipo hapa nchini lakini yuko tayari kukutanao na kufanya mazungumzo ya kuendelea muziki Tanzania.
(Picha na Mpoki Bukuku)
Wajerumani “Mbendembende” kwa Waspaniola
Wachezaji wa Spain wakisheherekea baada ya kukabidhiwa “mwali ” wao
Pichani ni Mfalme wa Spain Juan Carlos, aliyeshika kombe walilokabidhiwa Spain jana na kushoto kwake ni Waziri Mkuu wa Spain Jose Luis Rodriguez Zapatero usiku wa kuamkia leo.
Mashabiki wa Ujerumani wakiwa hawaamini kilichotokea wamebaki uwanjani hata baada ya mpira kumalizika.
Kepteni wa Ujerumani Micheal Ballack akiwa haamini kama dakika 90 zimekwisha na wameshindwa kuchomoa goli moja la Spain katika mchezo uliofanyika Ernst-Happel stadium huko Vienna, Austria,
(Picha zote na AP)
Fernando Torres ndiye shujaa wa Spain baada ya kupachika bao dakika yaa 33 bao lililodumu hadi kipyenga cha mwisho na kuwafanya Spain kutawazwa kuwa mabingwa wapya wa Mtanange wa Euro 2008 baada ya kuisaka nafasi hiyo kwa miaka 44.
Torres alipachika bao hilo swafi dakika ya 33 ya mchezo kipindi cha kwanza licha ya juhudi za Kapteni wa Ujerumani Ballack waspaniola walikaza na kulinda goli lao huku wakifanya mashambulizi ya hapa na pale.
Mpaka dakika 90 bao likabaki 1-0, ama kwa hakika kanauma, kamonga tuu!!
Sunday, June 29, 2008
Vijimambo ndani ya Zoo Negara – Malaysia
Sio mbaya
Saturday, June 28, 2008
Werason awasha moto Dar
Werasson ambaye ameingia nchini majuzi aliingia jukwaani kama kawaida lilitangulia sebene na kisha yeye kuingia huku akiimba wimbo maarufu wa Kala Yi Boing Remix huku mashabiki lukuki nao wakimfatiisha kwa kuimba naye, kisha alifululizwa kwa vibao kama Sourire ambacho kinapatikana kwenye Albamu ya Zamani ya Volume I, Solo la bien,Kibuisa Mpipa, Kuna nyimbo inaitwa Simeone inapatikana kwenye single Album Soul Soul.
Mashabiki walipagawishwa na mauno ya mwandada mrembo aliyeumbika si kitoto Bibiciya Mfwengi kila mara alikuwa akijivuta mbele na kijana wa atalaku kama kawa anampa mapande mashaki wote wana lipuka kwa mayowe.
Kwa ujumla shoo ilikuwa nzuri na kila mtu aliyeingia aliridhika na burudani ya haja aliyoipa.
Awali akizungumza na waandishi wa habari Werasson alisema kuwa amekaidi wito wa Rais wa Kongo Brazaville Denis Sasou Nguesso aliyemtaka kwenda kufanya shoo kadhaa kwa wiki nzima lakini alisema kuwa hawezi kuwaangusha mashabiki wake wa Dar Es Salaam ambao kwa kiasi kikubwa walikuwa wakimngojea hasa baada ya onyesho la awali kutofanyika huku watu wakiwa wameshakata tiketi.
Werasson na kundi lake la wanamuziki 24 watapiga Arusha kesho.
Kama nakuona Big Producer Maghambo Philipo – Baba Martha, Collins na Fikire wazee wa USA, Mukubwa Ling’ande, Mwanangu Dulla nakati ya IFM, Abuu na Boss Chizenga!! Tuko pamoja.
Picha na Big Producer Magambo/Mpoki Bukuku
Sylvia Mashuda atwaa taji la Miss Ilala 2008
mpira Maalum wa Fainali EURO 2008
Mipira 30 yenye rangi ya Silver ambayo itakuwa na majina ya wababe hao wa timu mbili zinazokutana fainali.
Pia imefahamika kuwa Kombe ambalo litanyakuliwa ama na Michael Balack wa Ujerumani au Casillas wa Hispania hapo kesho litakuwa na kilo mbili za uzito zaidi wa kombe la awali ambalo Theodoros Zagoraskis wa Ugiriki alilinyakua mwaka 2004.
Kombe jipya lina uzito wa kilo 8 na urefu wa sentimita 60 limepewa jina la Henri Delaunay, aliyekuwa Katibu wa zamani wa shirikisho la mchezo huu Mfaransa ambaye alitoa mchango mkubwa kwenye historia ya mashindano haya.
JB Mpiana alipofanya kweli Ufaransa
Pata Kitu Liberez
Jiachie Kisela
Friday, June 27, 2008
Werasson: Niko tayari kupiga na JB Mpiana Tanzania
Msanii huyo aliwasili juzi jioni akitokea Jamhuri ya Kongo ambapo na kundi la wanamuziki 24, anatarajiwa kutoa burudani kesho kwenye Ukumbi wa Ubungo Plaza kabla ya kupiga Arusha Jumapili kwenye Hoteli ya Naura Springs.
Endapo ‘Werrason’ atapiga pamoja na ‘JB’ Mpiana itakuwa ni historia baada ya nyota hao kuingia katika mzozo mkubwa ulioibua vita kati yao.
Akizungumza Dar es Salaam jana, Makanda alisema atafurahi kupiga pamoja na Mpiana ambaye inadaiwa ni wapinzani na chanzo cha kuvunjika kwa kundi maarufu la Wenge BCBG lililowahi kutamba Afrika.
“Sina matatizo na Mpiana ni rafiki yangu napenda siku moja nije naye hapa tufanye onesho la pamoja nipo tayari hata sasa cha msingi apatikane promota mwenye uwezo nitamwambia lakini naomba nipate uhakika kama mnatuhitaji kabla ya mwaka huu kumalizika,” alisema Makanda.
Makanda alisema anapenda kuona muziki wa Tanzania unapiga hatua kama ilivyo Jamhuri ya Kongo na kuongeza kuwa endapo atapata fursa ya kuzungumza nao atawashawishi watengeneze albamu ya pamoja.
Msanii huyo alisema alishindwa kutoa burudani mwaka jana kutokana na sababu zilizokuwa nje ya uwezo wake na alitumia nafasi hiyo kuwaomba radhi Watanzania kutokana na tukio hilo.
Alisema amejiandaa kuacha historia kwa kupiga nyimbo zake mfululizo ili kukata kiu ya mashabiki wa burudani ambao walikuwa na shauku kubwa ya kumuona nyota huyo akiwa jukwaani katika ardhi ya Tanzania.
Ziara ya mwanamuziki huyo imedhaminiwa na Kampuni ya Sigara Tanzania (TCC) kupitia chapa yake ya Embassy kwa kushirikiana na Club E.
Kipanya adhamini Miss Temeke
MSANII maarufu katika uchoraji wa katuni za siasa na sasa akiwa mbunifu maarufu wa mitindo nchini, Ali Masoud ‘Kipanya’ amejitosa kudhamini wa mashindano ya kumsaka Miss Temeke 2008.
Mratibu wa Miss Temeke, Benny Kisaka alisema Masoud, ambaye hutumia lebo ya KP, ambayo ni kifupi cha Kipanya, atawazawadia washindi watatu wa kwanza wa Miss Temeke nguo za watakazotumia katika fainali za Vodacom Miss Tanzania 2008, zitakazofanyika baadaye mwaka huu.
Alisema Temeke, ambayo inafunga dimba katika mashindano ya urembo ya kanda kwa mwaka huu, pia atatoa nguo maalum za shoo ya ufunguzi kwa warembo wote.
Alisema kwa sasa vimwana 12 wanaendelea kujifua chini ya Miss Temeke 2006, Jokate Mwegelo, ambaye anawafundisha mbinu za kutumia vyema jukwaa, unadhifu, kujengwa kisaikolojia na kuwapa uwezo wa kujiamini na hata kujibu maswali. Wasichana hao wanatoka katika vitongoji vya Kigamboni, Kurasini, Temeke Kusini na Chang’ombe.
Warembo hao ni Sheila Ally, Radhia Omary, Lilian Shayo, Zainabu Ally, Rona Swai, Nuru Hassan, Mwash Ramadhan, Angela Lubala, Caroline Sechuma, Glory Charles, Florence Josephat na Evelin Issack.
Werasson kuanzia Ubungo Plaza Leo
Brazil yasherehekea miaka 50 tangu ichukue Kombe la Dunia
Rais wa Brazil Luiz Inacio Lula da Silva shoto, akiwa amemkumbatia Mfalme wa soka la Brazil Edson Arantes do Nacimento, au Pele, Brasil inasherehekea miaka 50 tangu walipochukua Kombe la Dunia mwaka 1958 kwa shamra shamra za ina mbali mbali, sherehe hizi zilifanyika Planalto palace huko Brasilia jana tarehe June 26, 2008.
Spain yaigalagaza Russia 3-0….!
Russia 0 – 3 Spain
Ama kweli ukitaka kumuua nyani usimuangalie usoni, ndivyo walivyofanya Waspaniola usiku huu walipomchapa Russia bila huruma mabao matatu bila kufurukuta.
Ikiwa ni fainali yao ya kwanza baada ya miaka 24 wamewafungisha virago Russia na sasa watautana na Ujerumani na Russia watacheza na Uturuki kutafuta mshindi wa tatu.
Ilikuwa ni siku ya furaha kwa vijana wa Luis Aragones kwani walikuwa wakishambulia muda wote bila kupumzika na kufanikiwa kupata goli la kuongoza kipindi cha pili kupitia kwa Xavi, ambaye baadaye alibadilishana na Xabi Aronso dakika ya 69. Pia aliingia Daniel Guiza dakika hiyo ya 69 na dakika 4 baada ya kuingia alipachika bao la pili kwa Hispaniola na goli la tatu lilifungwa na David Silva dakika ya 82 na kuwapa tiketi ya kukutana na Ujerumani siku ya Jumapili.
Matokeo haya yameinyima Russia nafasi ya kucheza Fainali kwa mara ya kwanza tangu kuunjika kwa muungano wa kisobvieti. Russia alichapwa 4-1 na Spain wakati wa mchezo wa ufunguzi.
Spain waliutawala mchezo kuanzia kipindi chwa kwanza lakini hawakuweza kupata goli lolote kwani Russia walikaza namna fulani, lakini marekebisho na mawaidha ya kocha kipindi cha mapumziko yalizaa matunda.
Thursday, June 26, 2008
Ngoma Africa Band na Nyimbo za masimulizi!
Bendi maarufu ya mziki wa dansi the Ngoma Africa Band,inayoongozwa na mwanamziki
maarufu Ebrahim Makunja alimaarufu Ras Ebby Makunja “Bw.Kichwa Ngumu”
Imeibua zogo la gumzo lingine kwa kufyatua wimbo wao uliobeba jina la “Baba wa kambo”
wimbo huo umefyatuliwa wakati CD yao “Apache wacha Pombe” inawasha moto mkali wa kimataifa !
wimbo wao huo wa “Baba wa Kambo” ulifyatuliwa katika kuadhimisha sikuu ya watoto dunian! wimbo huo unawakilisha kilio cha mamilion ya watoto wanao teseka katika utwala wa kidikteta wa kina “Baba wa Kambo” ni utunzi wake tena kiongozi na mwimbaji wa bendi
Ebrahim Makunja.
Katika wimbo huo Ras Makunja amemrushia lawama(madongo) “Baba wa kambo” na kikosi
cha Ngoma Africa kikimsindikiza kwa kumzomea !baba wa kambo tunakushikia bango!
Kindumbwe Ndumbwe Charia ! na Nguo! kaitia moto!
Bendi hiyo maarufu inayopeperusha bendera ya Tanzania katika majukwaa ya kimataifa,
imefanikiwa kuliachia song hilo ambalo linamshitaki “Baba wa kambo” Kwa Jamii!
na jamii pamoja na tahasisi zake zifanye kila njia kutupia jicho swala la maelezi ya watoto
ambao ulelewa na kina baba wa kufikia maarufu kwa jina la “Baba wa Kambo”
madongo hayo ya Ras Makunja na kikosi chake The Ngoma Africa hayakuishia hapo tu
bali lawama nazo zimerushiwa kwa kwa MAMA ALIYELEWA MAPENZI na kumshau mwanae akiteswa na “Baba wa Kambo”
Mzozo huo katika ya Baba wa kambo na The Ngoma Africa band utapelekwa kwa jamii hili
upatikane uhamuzi nani ?mwenye makosa Baba wa Kambo! au Mama Aliyelewa Mapenzi!
au Ngoma Africa Band waliomzomea baba wa kambo na kuweka mateso yake yote uwanjani yajadaliwe na jamii?
Baadhi ya Malalamiko ya ngoma africa kuwa “Baba wa Kambo” anamfanyishwa YATIMA kazi ya kutafuta kuni !wakati watoto wengine wapo shuleni! anamnyima ELimu yatima!
wakati Elimu ni ufunguo wa maisha,anampa KISAGO CHA MOTO yatima,anamlaza chumba cha Uwani karibu na chooni !kula na kulala kwa shida!
Baba wa Kambo naye labda atalalamika kuwa kiongozi wa bendi hiyo ni mwanamziki mwenye GUBU! kawashawishi wenziwe kumzomea wakati mila zinasema usimzomehe mkubwa!
Solo Thang AKA Traveller AKA Msafiri aja kivingine July
Muziki ni safari, Kwa wanaokumbuka enzi hizo ukilitaja jina Solo Thang kila mtu mpenda Muziki anasisimuka, kwani ni mmoja wa wanamuziki wa Kizazi kipya ambao kwa kiasi kikubwa “walipigana vita ya msituni” kufanya muziki huu ukubalike kwa jamii. Kwa sasa Solo Thang AKA Traveller AKA Msafiri anaishi Uingereza akiwa ameoa na mtoto mmoja anayeitwa YASSIR na Mama yake anaitwa YASMIN.
Kwa muda sasa mwanamuziki Solo Thang amekuwa kimya kutaka kujua yuko wapi Spoti Starehe tumefanya mahojiano naye kutaka kujua machache toka kwake na maisha yake hasa ya kisanii kwenye sanaa nzima ya Muziki.
Spoti na Starehe (S na S): Mara ya mwisho nilisoma Interview yako Bongo5 ile Albamu uliyofanyia huku ughaibuni ilitoka kaka nataka mawili matatu kaka.
Solo: okee,bado ndo naiweka sawa kakakuna mambo mengi na shule ilinibana mkuu.
S na S: Jina ni bado lile lile la Albamu?
Solo: Yaa inaitwa TRAVELLER, ndio jina waliokuwa wananita enzi nasoma jitegemee….99
S na S: oooh poa sana, sasa unategemea kuimaliza lini, i mean itakuwa sokoni?
Solo: Kama nilivyo Kwambia kuna mambo namalizia ila Inshallah Hivi karibuni nitaanza na Single
Akiwa pamoja na Dj lee flex, na mdau baraka, DJ Lee ni mmoja wa Madj ambao wanaitangaza Bongo Flava Nje.
S na S: Vipi Maisha kwa ujumla nasikia ulikuwa unasoma, Je zaidi kumaliza Chuo cha Diplomasia pale Kurasini kuna chochote tena?
Solo : Shule kama kawa kaka haina mwisho,we learn new things daily ..nilishamaliza baadhi ya courses na nitaendelea na buku.kwa sasa napiga mzigo nakuiweka sawa family!
S na S: oooh safi sana mkuu kila la heri, Je unaionaje game kaka na ujio wa vijana wapya ukilinganisha na enzi zenu? nani mpya unamfeel sana?
Solo: Mmh well vijana wanatisha wanajitahidi ila FID Q yuko poa, CHIDI mwanangu yuko bomba
S na S: Je hufikirii kufanya kolabo na wanamuziki tofauti na wa nyumbani ili uende kimataifa zadi unalizungumziaje hili mkuu?
Solo: hicho ndio kilichonifanya niwe kimya kidogo,kunavitu vingi nilikuwa nafikiria jinsi kuviboresha ikiwa na kuliingilia soko la kimataifa babu, natarajia kutoa single mwezi july tarehe nitaitangaza baadae kaka
S na S: Single hiyo umemshirikisha nani babu? ni ya kiswahili au?
Solo: Nyimbo nitakazo toa kuanzia sasa zitakuwa na version mbili moja ya kiswahili na remix ambayo itakuwa ya kiingereza
S na S: Je mkubwa unazungumziaje wanamuziki wa Kenya ukilinganisha na wenzao wa Tanzania ambapo wengi wa Kenya wanapata shoo nyigi za nje, je hii ni kusema Genge inakubalika zaidi ya Bongo Flava kaka?
Solo hakuna babu,show ni connections na jinsi gani wasanii wanajiuza,inabidi wabongo tutumie sana mitandao katika kunadi kazi zetu…..kwa hiyo matumizi ya computer ni muhimu sana katika kujitangaza babu na nijukumu la wabongo walio nje ya nch kusupport vipaji vya home,kama Uk wapo baadhi ya maDj wakibongo wanajitahidi sana katika kuutangaza mziki wetu kuna jamaa wanajiita bongo flavour familly,Dj Jimmy blanks,kina Dj habib,Dj lee flex…..etc, ni jukumu la wabongo walio na michongo kumegeana babu
S na S: Kuna upande mwingine hata wewe uliupigia kelele sana kuhusu Wasambazaji kule nyumbani Bongo ambao bado ni hao hao kuna jinsi kweli ya kuepukana nao “wadosi” kama ipo kwa jinsi gani?
Solo: ipo dawa ni kuwa na umoja na kuwatosa,pia tunaweza kuuza kazi zetu kwa njia ya mtandao….kama itunes, beta record na store nyingine nyngi tu za muziki
S na S: Hapo utakuwa unalizungumzia soko la nje je kwa mikoani ambapo kazi zenu zinanunuliwa zaidi na jijini ambapo ndio kuna soko kubwa lakini ni rahisi kupata nyimbo za mwanamuziki kwa mtu ku burn CD tena toka kwa wanamuziki unasemaje kwa haya mawili?
Solo:ndo maana nikasema umoja muhimu!naamini wanamuziki sisi ndio waathirika wa hili,kama tutakuwa na msimamo kwa pamoja si kazi kupata suluhisho la hil, kama wadosi watakataa kubadilika ni kususia kuuza kazi zetu kwao naaamini watajitokeza tuwatu wa kununua kazi zetu,au tunaweza kuweka utaratibu wa kuuza wenyewe vyote inawezekana muhimu ni kujipanga….nakumbuka Mr Two alishawahi kukomaa na kusambaza mwenyewe na Kilimanjaro band kama sikusei
its all possible..pia wabongo waelimishwe umuhimu wa kununua nakala halisi na si zakukopy,ili kusupport vipaji vya nyumbani,la sivyo itabaki majina tu yanavuma mifuko imetoboka
“Traveller” Mitaani ughaibuni.
S na S: Je umewahi kuwaza kuwa na Chama chenu ili muwe na sauti moja? unafikiri hili linawezekana?
Solo: unajua tatizo njaa babu kwenye njaa hakuna msimamo…..vyama huwa vinaanzisha ila havidumu na huwa havina nguvu…..sababu mnaweza kupanga hili,baadhi wakazunguka! sauti moja ndo inatakiwa ya wasanii nchi nzima. Tukae chini na wadosi watueleze tatizo nini?kazi zinavuka mpaka mipaka hakuna mjadala wa hilo!, pia nimeanzisha blog yangu ili kuwapa latest mashabiki zangu pamoja na habari zingine za burudani ndani na nje ya bongo http://www.solothang.blogspot.com.
S na S: Elimu na usanii haviingiliani ila vinategemeana pia je kuna mabadiliko yeyote unayahisi kwa kipindi kile na sasa baada ya vidato kadhaa kimuziki?
Solo: makubwa kaka,am grown up now ha ha with wife and son,kuishi ngambo pia kunakupa experience kubwa kila ninachokiwaza na kwa faida yangu na family, which means siwazi kunyonywa tena.
S na S: Hongera sana kwa hilo!! Kila mtu anafikiria kuwekeza kwenye Studio na kwa sasa kila kona kuna Studio Dar hadi limekaa njema hili mkuu?
Solo: Studio kila kona poa muhimu kama zitakuwa na viwango tu babu,pia inaleta ushindani na ni mzuri kibiashara.
“when it comes to Mic,Rhyme!! man am baaad..”
S na S: Je una lolote la kuwaeleza MAshabiki, Wanamuziki wenzio, au hata wadau wa Muziki hata “wadosi”?
Solo; Mashabiki kwanza nawaomba msamaha kwa ukimya,pili wakae mkao wa kula soon tunaanzia July kwa washkaji ni muhimu kuwa na plan B,wasitegemee tu mziki kama kitega uchumi,wa Invest pesa wanayoipata ili kuwa na nyenzo nyingine ya kuingiza kipato,maisha mchakamchaka, fani yetu haina pension,so we need to work hard for the future,na nawatakia kila la kheri
S na S: Asante kaka kwa muda wako kila la heri kwenye shughuli zako
Solo: Asante sana kaka nawe pia.
Pata burudani ya Solo thang na Q Chilla kwa kubofya hapa
Esther Nabaasa: Mshindi wa Tusker Project Fame mwaka huu
ESTHER Nabaasa kutoka Uganda, ametwaa kitita cha Sh85milioni baada ya kushinda shindano la Tusker Project Fame lililomalizika mwishoni mwa wiki jijini Nairobi.
Kwa ushindi huo, Esther alijipatia zawadi ya S milioni tano za Kenya na mkataba wa kutengenezewa albamu na kampuni kubwa ya kurekodi ya Galo iliyopo Afrika Kusini.
Nafasi ya pili ilitwaliwa na Wendy Kimani wa Kenya ambaye alijipatia shilingi milioni 2.5 za Kenya.
Katika hatua hiyo ya mwisho iliyokusanya maelfu ya mashabiki ukumbini, washiriki wanne waliobaki walipanda jukwaani na kuimba nyimbo tatu kila mmoja.
Washiriki wengine wawili wa kiume, David Ogola na Victor Asava walishindwa kuimba katika hatua hiyo.
Baada ya kila mshiriki kuimba wimbo mmoja, msanii kutoka Tanzania, Ambwene Yesaya ‘AY’ alipanda jukwaani na kutoa burudani kwa kuimba wimbo wake wa Usijaribu, ambao ulipokelewa kwa shangwe na mashabiki.
Kumalizika kwa zamu ya AY, washiriki walipanda tena jukwaani kuimba nyimbo zao za pili, David akiwa wa kwanza akifuatiwa na Esther, Victor na Wendy, kabla ya msanii nyota kutoka Uganda, Bobby Wine naye kupanda jukwaani.
Mbali na wasanii hao, msanii kutoka Kenya, Red Sun, naye alipanda jukwaani na kutoa burudani ambayo pia ilishangiliwa na mashabiki lukuki waliohudhuria.
Baadaye, MC wa shughuli hiyo, Gaitano Kagwa kutoka Uganda, aliwaonyesha mashabiki gari maalum lililoingia ukumbini likiwa na kitita hicho cha fedha za zawadi, ambao wanaume wanne waliokuwa wamevalia suti na miwani nyeusi, walipopanda jukwaani wakiwa na begi lenye fedha.
Esther amekuwa msichana wa pili kushinda mchuano huo baada ya Mkenya, Varerie Kimani kufanya hivyo mwaka jana
Tony Nyadundo, Mfalme wa Nyimbo za Ohangla
Tony Nyadundo ni mzaliwa wa Kanda ya Ziwa huko Kenya. Anatokea katika kabila la Wajaluo (Luo), Tony Nyadundo amejipatia umaarufu kwa aina ya mziki wake na ni jambo la kawaida kupita mitaani na kusikia nyimbo zake zikichezwa. Aina ya muziki wake inajulikana kama Ohangla (Muziki toka kanda ya Ziwa) na sasa yeye anajulikana kama Mfalme wa Ohangla. Tony ni mmoja wa wanamuziki walifaidika na muziki wake na kuufanya muziki huo kukubalika na rika lote. Tony pamoja na kaka yake anayejulikana kwa jina la Jack Nyadundo naye anapiga aina ya muziki kama wa Tony kama mdogo wake naye anakubalika sana kwenye Muziki na umaarufu wao ni mkubwa hasa Sehemu ambazo Wajaluo wanatoka.
Tony ambaye anatamba na nyimbo kama Dawa ya Mapenzi,Isanda Gi hera, Obama na nyinginezo nyingi ameshafanya matamasha ya muziki nchi mbali mbali ikiwemo Ujerumany na USA pia achilia mbali hizi za Afrika. Umaarufu huu unafuatia aina ya muziki wake ambao unajumuisha ala za asili, uchezaji pamoja na uimbaji ambao huvutia kwa taratiibu na kuupandisha toka Mziki wa Vilabu vya Pombe, Bar mpaka sasa zimbo zake zinapigwa hata kwenye Kumbi za Burudani zikichanganywa na Genge, muziki maarufu wa Kenya.
Mwaka 2006 alitoa albamu yake iliyoitwa Obama. Ikiwa ni kumuenzi Seneta Barak Obama wakati huo ambaye Baba yake ni Mzaliwa wa Kenya kama Nyadundo.
Wakati wa tamasha la Kisima Music Award mwaka 2007 alishinda kwenye kundi la Muziki wa kiasili. Tony ambaye binafsi anaweza kutumia ala zote za kiasili, muziki wake anatumia ala za kiasili tupu isipokuwa kinanda cha kupuliza tuu amefanikiwa kuweka utamaduni na muziki huo katika chati ya Muziki kitaifa na kimataifa.
Bonyeza Player upate Uhondo wa mwanamuziki Tony Nyadundo, Ukiangalia kwenye hii Video Utamuona Waziri Mkuu Raila Odinga, Prof Anyang Nyong, na wajaluo wengine ambao wapo kwenye nafsi za juu kichama(ODM) au kiserikali.
Serengeti Boys kufunzwa na Carlos Alberto Perreira Brazil
Pichani anaonekana Kocha Pereirra akiongea na Ronaldo
TIMU ya soka ya vijana walio chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Boys, itaondoka nchini Juni 5 kuelekea Brazil , ambako itakuwa chini ya kocha aliyeiongoza Brazil kutwaa Kombe la Dunia mwaka 1994, Carlos Alberto Perreira.
Mratibu wa mashindano ya Copa Coca-Cola, George Rwehimbiza alisema timu hiyo itafikia kwenye kituo cha michezo cha Brazil Football Academy, na itaondoka na viongozi wanne akiwemo kocha mkuu wa timu ya vijana, Marcus Tinocco.
“Timu itaondoka Juni 5 kuelekea Brazil itakaa huko kwa muda wa wiki moja,” alisema Rwehimbiza. “Timu itafikia kwenye kituo hicho kilicho chini ya Carlos Alberto Perreira.”
Perreira aliiongoza Afrika Kusini kwenye fainali za Mataifa ya Afrika mapema mwaka huu, lakini akajiondoa kwenye kazi hiyo hivi karibuni, akieleza kuwa mkewe alikuwa ni mgonjwa.
Vijana watakaokuwa kwenye safari hiyo watapatikana kutoka katika mashindano ya Copa Coca-Cola yanayoeelekea ukingoni jijini Dar es salaam baada ya kuendeshwa kwa takriban wiki mbili.
Mashindano hayo yanashirikisha timu za kombaini za mikoa yote ya Tanzania Bara na visiwani, zikiwemo wilaya za Ilaya, Kinondoni na Temeke zilizopewa hadhi ya mkoa.
Vijana wengi walioteuliwa kwa ubora katika mashindano ya kwanza yaliyofanyika jijini Dar es salaam kwa sasa wanasomeshwa na Shirikisho la Soka (TFF) kwenye shule ya sekondari ya Jitegemee, ambako huhudhuria vipindi vya masomo ya kawaida na yale ya soka.
Wakati huohuo, kocha Tinoco amesema kuwa hatapata kazi kubwa ya kuwanoa vijana 17 watakaopatikana katika michuano ya Copa Coca-Cola, anaripoti Sosthenes Nyoni.
Akizungumza baada ya mechi baina ya timu ya mkoa wa Kigoma na Kusini Pemba, Tinocco alisema kuwa hilo linatokana na wachezaji wengi kuonekana kuwa wamefundishika.
Alisema kuwa tofauti na mwaka jana mashindano ya mwaka huu yameonyesha baadhi walimu wa timu shiriki kuwa wana uwezo mkubwa wa kufundisha soka na ndio maana baadhi ya timu zinacheza soka lenye mpangilio.
Ally Kiba nakati ya Ujeruman
Ally ambaye aliwasili pamoja na promota wake Kassim wakitokea Oslo – Norway ambako waliwarusha mashabiki vilivyo.
Pia imefahamika kwamba warembo washiriki wa Miss Tanzania EU wako kambini na tayari kabisa kwa mchujo wa round ya kwanza pre-selection utakaofanyika kesho ijumaa 27.06.08.
Ali kiba alipata nafasi ya kushangilia Mjini Essen na baadhi ya washabiki wa Ujerumani wa mpira wa miguu kwenye mtanange wa Ulaya kati ya Uturuki na Ujerumani ambapo Ujerumani Ilishinda 3-2.
Nani wa Kumfunga “Paka” Kengele Jumapili?
Germany 3 – 2 Turkey
Mpaka mapumziko timu zote mbili zilikuwa 1-1, huku Turkey wakiwa wakwanza kupata goli lililofungwa na Ugur Boral dakika ya 22 na dakika tano baadaye Ujerumani walisawazisha kupitia kwa Bastian Schweinsteiger.
Kipindi cha pili kilianza kwa timu zote kushambuliana mashambulizi ya hapa na pale huku Ujerumani wakilisakama lango la Uturuki kama nyuki kwa mashambulizi ya kustukiza na dakika ya 79 wakapata goli Ujerumani lililofungwa na Miroslav Klose.
Huku mashabiki wa Ujerumani wakishangilia timu yao kuongoza kwa goli mbili walistukizwa na goli la kusawazisha toka kwa Semih Senturk dakika saba tuu baada ya goli lao, kiukweli mpira ulikuwa mtamu.
Timu zote zikawa zinahaha kupata walao cha “kuraria”, huku makocha viti vikiwa havikaliki na mashabiki wakiwahamasisha wachezaji wao kwa ushangiliaji non-stop, bahati haikuwa ua Waturuki na bahati hiyo ya Mtende iliwaangukia Wajerumani na kupachika bao dakika ya 90 ya mchezo kupitia kwa Philip Lahm . Mchezo wa jana ulikuwa na kufa mtu kwani kila timu ilikuwa inataka nafasi walao ya kucheza fainali kama sio kuchukua ubingwa.
Timu zote zilifanya mabadiliko ya hapa na pale walao kufufa hali ya mchezo kwa Wajerumani Torsten Frings aliingia badala ya Simon Rolfes dakika ya 46 na Marcell Jansen badala ya Miroslav Klose dakika ya 90.
Kwa upande wa waturuki walifanya mabadiliko mara tatu Mevlut Erding aliingia badala ya Ayhan Akman (81) na Gokdeniz Karadeniz alichukua nafasi ya Ugur Boral (84) na dakika ya 90 walimuingiza Tumer Metin na kutoka Colin Kazim-Richards.
Tanzania Dream naona kautabiri kako kanafikia kaka!!
Wednesday, June 25, 2008
Huyu ndiye Bush!!
Mashabiki bwana!!
Mashabiki wa Ujerumani chiboko!!
Nusu Fainali EURO 2008 Nani ni nani?
Germany:
Hii ni timu nzuri inayocheza kwa kujituma ila inashindwa kuwa na motivation at times.Ila katika siku yao hakuna timu inayoweza ishinda.Kwa jicho la karibu naona bado wana hali ngumu dhidi ya Uturuki kutokana na ukweli kwamba Waturuki wameonekana kuwa vichwa ngumu karibu katika kila kazi waliyokutana nayo
…………………………………………………………………………….
Waturuki:
Mashabiki wa Ujerumani na Turkey wakiwa pamoja wakichemshana hii ikiwa ni muda kabla kuanza kwa mchezo kati ya timu zao.
Hawa jamaa mpira wao sio mbaya ila kutokana na kutokuwa na majina makubwa inafanya kazi kwao iwe rahisi.Nafasi waliyofikia ni mafanikio tayari kwao.Hawana presha yeyote ya kujidhihirisha zaidi ya waliyofikia tayari.Hii inafanya game kwao iwe rahisi zaidi ya Ujerumani.
…………………………………………………………………………….
Waspeini:
Cesc Fabregas wa Spain akisaini Autograph mara baada ya kumalizika kwa mazoezi ya timu yao hapo jana.
Hawa kwa rekodi wana tabia ya kupata matokeo mabovu lkn kwa matokeo yao dhidi ya Italia yanarudisha imani ya kuweza kufanya mengi japo bado wana presha kutokana na kupewa nafasi kubwa na mashabiki na wataalamu wengi wa soka.Kwa upande wangu nawapa nafsi kubwa ya kucheza final.
…………………………………………………………………………….
Warusi:
Mashabiki wa Russia wakishangilia timu yao, usilogwe kuingia kwenye anga zao hawa jamaa ni noma.
Hawa jamaa kama ilivyo ada hawakupewa kabisa nafasi lkn waliyofanya tayari yamelipa matarajio na hivyo wanaingia kwenye hii game wakiwa na imani kuwa timu walidhodhani ni ngumu kwamba nazo zinafungika.Hii inakuwa rahisi kwa wao kukumbana na waspeini ila tatizo kwao ni kwamba wana wachezaji wengi wa kikosi chak wanza ambao hawatacheza kwenye hii game hivyo kupunguza matunda ya kikosi imara chao.
Wachezaji wa kuangaliwa kwa hii hatua ni bastian schweinsteiger,Fernando Torres,Arda Turna na Andrei Arshavin
Review By Tanzania Dream, Pamoja Kaka.
Bibisiya Mfwengi, Dansa wa Werrason anayedatisha jukwaani
Muangalie na HApa Pia
Tuesday, June 24, 2008
Master J, CEO MJ Records
PROFESSION: Producer
COMPANY: MJ Records
NATIONALITY: Tanzanian
Joachim Kimaryo a.k.a. Master J as he is fondly known in Tanzania’s growing music industry founded in 1996 what is today one of Tanzania’s foremost digital recording studios – MJ Records.
This man is undisputedly one of the pioneers of ‘Bongo Flava’ a distinctive predominantly hip-hop Tanzanian sound that has taken the continent by storm. He has played an integral role in the development of Bongo Flava and the growth of the broader music industry in Tanzania.
Master J holds a degree in electronics engineering from City University of London, and has always had a keen interest in music. Recording almost all genres of Tanzanian music from gospel, Bolingo to the famous Bongo Flava, Master J has worked with the best in the Tanzanian music industry.
Khangalicious. na Changamoto ya Vazi la Kitaifa
Flaviana Matata
Kwa wengi,nchini Tanzania na duniani,anabakia kuwa mrembo kutoka nchini Tanzania aliyeiwakilisha nchi yake katika shindano la dunia la Miss Universe mwaka 2007 na kuwa mshiriki wa kwanza aliyeamua kulipanda jukwaa akiwa kipara.Kwa wengine,wakiwemo ndugu,jamaa na marafiki zake,anabakia kuwa Flaviana Matata.
Hivi karibuni alilivua rasmi taji lake la Miss Universe Tanzania 2007 baada ya kulitumikia kwa muda wa mwaka mzima.Tulipata nafasi ya kuongea machache na Flaviana baada ya kumkabidhi rasmi mrembo mwingine,Amanda Sululu, taji la Miss Universe Tanzania. Hivi tunavyoongea tayari Amanda yupo nchini Vietnam tayari kabisa kwa shindano la Miss Universe litakalofikia kilele nchini humo tarehe 13 Julai mwaka huu.
Flaviani amefanya Mahojiano na Bongo Celebrity gonga hapa upate Kujua anasemaje?
Da Chemi amaliza uigizaji The Surrogates
Dada Chemi ambaye pia ni mwanachama wa Screen Actors Guild (SAG) amesema kazi ya kuigiza ilikuwa bomba.
Amesema katika blogu yake kwamba katika filamu hiyo ambayo kinara wake ni Bruce Willis amecheza kama Dred.
Nafasi ya kucheza aliipata mwezi wa tatu wakati alipoitwa kwenye audition ya sinema hiyo.
Ingawa hakupata sehemu aliyofanyiwa audition alipewa nafasi ya kucheza Dred na alicheza vyema nafdasi hiyo akiwa mchafu na kuvaa nguo zilizochakaa akionekana kama kama ombaomba.
Isome Zaidi kwa Lukwangile Entertainment
Ngoma Africa na Muziki wa Dance ughaibuni
Ras Makunja au Ebrahim Makunja ni mtunzi aliyebobea katika shughuli yake hiyo ya kutunga nyimbo na kuimba katika kuishauri jamii au hata kutoa onyo lakini mara nyingi huwa ni mwanamziki mwenye kuzua hoja kama utamsikiliza sana katika tungo zake za RUSHWA NI ADUI WA HAKI,hiliyopo katika CD ya “Anti-Corruption Squard” na ule mjadala wa mchezo mchafu wa “Mama Kimwaga”(Sugar mum)katika album hiliyobeba jina la “Mama Kimwaga”! kwa watu waliyo karibu na Ras Makunja na bendi ya The Ngoma Africa wanatonya kuwa jamaa hao ni watu utani sana na Ras Makunja mwenyewe ni mtu mwenye kupenda mizaa sana !lakini hawapo jukwaani na ukimsikiliza sana nyimbo zake zina maneno ya ukweli napenginepo yanachoma moyoni,na hakiona kuwa unamwangalia sana huwa anaimba na kufunika uso kwa kutumia kiganja cha mkono wake moja au kuvaa miwani ya jua mkubwa hata kama usiku !akimaliza kuimba uwazawadia washabiki kwa tabasamu ya kicheko ambalo uwariwadha !
Ujumbe uliomo katika nyimbo za Ngoma africa band kila wakati unasindikizwa na mlindimo au mdundo wa nyuzi kali zinatoka vidoleni mwa wanamziki mahili wa bendi hiyo wakiwamo mcharaza solo Gitaa machachari Mr.Christian Bakotessa aka Chris-B,ambaye mara nyingi uhimba pamoja na Ras Makunja,pia kuna yule mpiga gitaa la Bass Said Vuai aka Prince Jazbo Vuai,wapo kakribani wanamziki 7 hivi.
Tamazi ya habari tumalizie kwa kutoa wito kuwa wanamziki wa nyumbani hizi ndizo habari njema msiogope wala kusita kuzitoa nje kazi zenu,kuwa mziki wa dansi wa Tanzania sasa unakubalika. Hongera Ras Makunja Na wenzako The nGoma Africa Band au kama wanavyojilikana “the Golden Voice of East africa”.
Gonga hapa usikilize
Monday, June 23, 2008
basketball wapata mdhamini
Akichonga na wanahabari Rais wa Kamati ya Mpira wa Kikapu Miji Mikuu ya Afrika Mashariki Kati na Kusini, Simon Msoffe alisema Kampuni hiyo imetoa kiasi hicho kwa ajili ya shughuli mbalimbali za michuano hiyo.
“Tunatarajia Kampuni zingine zitajitokeza kufanikisha michuano hiyo ili ikonge nyoyo za mashabiki wa mpira wa kikapu waliopo hapa Tanzania, ” alisema
Msofe. Majiji yanayoshiriki michuano hiyo kutoka Tanzania ni Dar es Salaam, Mwanza, Arusha, Mbeya na Tanga, Kenya ni Nairobi na Mombasa, Uganda ni Kampala, na jiji jingine ni Mogadishu.
Mashindano hayo yaliyoanza toka mwaka 1999 na kufanyika kila mwaka, mwaka jana bingwa wa michuano hiyo ilikuwa ni Nairobi walioifunga Dar es Salaam katika fainali iliyofanyika Nairobi, Kenya.
KIli Music Award yaiva
Pichani kushoto ni Afisa Uhusiano wa Kampuni iliyoandaa tuzo hizo Oscar Shelukindo na Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya inshu hiyo, John Mhina wakionesha aina ya tuzo zitakazotolewa siku hiyo wakati wakiongea na waandishi wa Habari katika Ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Jijini Dar es Salaam leo mchana. Tuzo hizi zilianzishwa na mwanamuziki James Dandu ambaye hivi sasa ni marehemu. Picha/Habari na GPL
Kolabo ya Juliana na Bushoke
Hispania wafuzu Nusu Fainali kwa mbinde!
Spain 4 – 2 Italy
Hispania wamekwenda hatua ya Nusu fainali za michezo ya Euro 2008 baada ya kufikia hatua ya kupigiana penati kwenye mechi kali kati yake na Italy hapo Ernst-Happel Stadium jana.
Golikipa wa Hispania Iker Casillas aliokoa mishuti ya penati toka kwa Daniele De Rossi na Antonio Di Natale hii likuwa ni baada ya dakika 120 za bila kufungana kabla ya mchezaji matata Cesc Fabregas kufunga penati yake ya mwisho na kuwainua mamia kwa maelfu ya mashabiki waliokuwa uwanjani na mitaani.
Kwa upand wake Cassillas, aliokoa mkwaju kwa mguu uliopigwa na Mauro Camoranesi, ulisaidia kuiweka Spain kwenye matokeo mazuri ambayo hata kwa penati ilobaki Italy wasingeweza kufikia magoli ya Hispania.
Italy walishinda kombe la Dunia mwaka 2006 kwa Penati dhidi ya Ufaransa lakini Buffon ambaye alikuwa shujaa kwenye fainali zile jana alishindwa kuonyesha makali yake na badala yake golikipa wa Spain Casillas akawa ndio shujaa.
Lakini ikumbukwe pia kipa huyu wa Italy ndiye aliyewafikisha kwenye hatua hiyo baada ya kuokoa mkwaju wa Adrian Mutu walipocheza na Romania, na hata hivyo aliicheza penati ya nne ya Daniel Guiza hapo jana.
Kwa matokeo haya Hispania watakutana na Russia hapo tarehe 26 Juni huko Vienna Austria ambapo bingwa atacheza na mshindi kati ya Ujerumani na Turkey ambao watacheza tarehe 25 Basel.
Mechi za Awali Kombe la Mataifa na Kombe la Dunia kwa Afrika
Matokeo kadha ya mechi za kufuzu Kombe la Mataifa ya Afrika na Kombe la Dunia 2010 ya mechi za Jumapili tarehe 22 Juni 2008
Kundi la 2
Zimbabwe 0 Kenya 0
Kundi la 3
Angola Uganda (mechi iliahirishwa Jumapili hadi Jumatatu)
Benin 2 Niger 0
Kundi la 7
Msumbiji 3 Bukini 0
Kundi la 8
Ethiopia 6 Mauritania 1
Kundi la 10
Congo 2 Chad 0
Kundi la 12
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo 5 Djibouti 1
Mechi za Jumamosi tarehe 21 Juni 2008
Kundi la 1
Cameroon 2 Tanzania 1
Kundi la 4
Nigeria 2 Equatorial Guinea 0
Afrika Kusini 0 Sierra Leone 0
Kundi la 5
Morocco 2 Rwanda 0
Kundi la 6
Senegal 3 Liberia 1
Kundi la 9
Tunisia 2 Burundi 1
Burkhina Faso 4 Ushelisheli 1
Kundi la 11
Zambia 1 Swaziland 0
Mechi zilizochezwa Ijumaa tarehe 20 Juni 2008
Kundi la 5
Libya 4 Lesotho 0
Kundi la 6
Algeria 1 Gambia 0
Mashindano ya Pool kuanza Juni 27
Mashindano ya taifa ya mchezo ya pool 2008 yanayotarajiwa kushirikisha timu kutoka baadhi ya mikoa ya Tanzania bara yanatarajiwa kuanza kutimua vumbi Juni 27 mwaka huu jijini Dar es Salaam.
Kwa kuzingatia umuhimu wa mashindano hayo, chama cha waamuzi wa mchezo huo wa Pool mkoa wa Dar es Salaam -DAPORA-kimeandaa semina kwa waandishi wa habari iliyohusu mchezo huo na sheria zake.
Mashindano hayo yameandaliwa na chama cha mchezo wa Pool mkoa wa Dar es Salaam-DARPA- na kudhaminiwa na kampuni ya bia Tanzania- kwa kupitia bia aina ya safari.
Miss Arusha ajinyakulia gari
Miss Arusha 2008, Glory Emson akiwa ndani ya gari yake Toyota Sprinter mpyaa aliyokabidhiwa mara baada ya kushinda hivi karibuni, gari hii imetolewa na wadhamini wa Miss Arusha TanzaniteOne
(Photo by Nicky Mchau)
Sunday, June 22, 2008
Huu ndio unazi!!
Russia yawafungisha Virago wakali Holland
Netherlands 1-3 Russia
Golikipa wa Holland au Dutch au Uholanzi au Netherland Netherlands’ Edwin van der Sar akiokota mpira kimiani baada ya kufungwa goli la pili na Dmitri Torbinski,
Mchezaji wa Holland Wesley Sneijder, chini akipoozwa na mwenzake huku golikipa wao Edwin van der Sar akipita mara baada ya mechi kuisha, kwa mbaali Russia wakijipongeza,
Kama kawa mashabiki mitaani wakisherehekea.
Magoli yaliyofungwa na Dmitri Torbinski na Andrei Arshavin dakika za majeruhi yameiwezesha Russia kucheza nusu fainali na kuwafungisha virago Holland ambao walianza kwa mkwara.
Mpaka dakika 5 kabla ya mpira kumalizika Holland walikuwa wameshalala kwa goli moja bila ndipo Ruud van Nistelrooy aliposawazisha kwenye dakika ya 86 na kufanya dakika za nyongeza ziongezwe.
Kocha wa Russia mholanzi Guus Hiddink kwa ajana ameonekana kama msaliti lakini alikuwa kibaruani kwani ameitoa timu ya nchi yake na uzalendo kuonyesha kumshinda, binasi simlaumu!
Kwa sasa Russia watakutana na Spain au Italy jijini Vienna siku ya Alhamisi na kufanya kuwa timu ya tatu kufikia hatua ya nusu fainali. Rafiki yangu Tanzania Dream hongera kwa kubashiri, natumai ubashiri wako utakwenda sawia.
Taifa Stars Yafa Kiume!! yatoka 2-1 na Kameroon
Katika mchezo wa kwanza uliofanyika Uwanja Mkuu wa Taifa, Dar es Salaam Jumamosi iliyopita, Stars iligangamala na kutoka suluhu na Kameruni. ‘Indomitable Lions’ inaongoza kundi hilo ikiwa na pointi 10.
Stars imebakiwa na pointi mbili baada ya kutoka sare 1-1 na Mauritius, ilichapwa bao 1-0 na Cape Verde, ilitoka suluhu na Kameruni kabla ya jana kufungwa mabao 2-1 na wapinzani wao. Timu hiyo imebakiwa na michezo miwili dhidi ya Mauritius na Cape Verde.
Katika mchezo huo, Stars ilicheza vizuri na kuwabana Kameruni iliyosheheni nyota wengi wanaocheza mpira wa kulipwa katika klabu za Ulaya licha ya kupoteza mchezo huo.
Kameruni ilianza kupata bao lake dakika 66 lililofungwa na mshambuliaji wa Barcelona, Samuel Eto’o baada ya kipa Ivo Mapunda kuutema mpira wa krosi uliopigwa kutoka pembeni kulia mwa uwanja. Eto’o alifunga bao la ushindi dakika 88.
Stars ilitulia na kucheza pasi fupi fupi ambazo zilichangia kuwapa wakati mgumu mabeki wa Kameruni ambao walianza kupoteana na kutoa mwanya kwa Danny Mrwanda na Nizar Khalfan kumsogelea kipa wa Kameruni, Idriss Kameni.
Kasi ya Stars ilimchanganya nahodha wa Kameruni, Rogobert Song ambaye alifanya makosa yalimpa nafasi, Mrwanda kupachika bao la kusawazisha dakika 77 akifunga kwa shuti lililompita kipa Kameni kabla ya kujaa wavuni.
Kiungo wa pembeni wa Stars, Mrisho Ngassa alifanikiwa kuitoka ngome ya Kameruni dakika 11 lakini mpira wake wa krosi aliopiga kutoka upande wa kuliwa mwa uwanja uliokolewa na beki wa kati, Rogobert Song.
Kameruni ilijibu shambulizi hilo dakika 24 baada ya kiungo, Alexander Song kupenyeza mpira katika ngome ya Stars lakini beki Nadir Haroub ‘Cannavaro’ aliokoa hatari hiyo.
Dakika mbili baadae Stars ilitulia na kuanza kupanga mashambulizi ambapo Nizar Khalfan na Shaaban Nditi waligongeana vizuri kabla ya mabeki wa Kameruni kuokoa.
Stars ilibisha hodi langoni mwa Kameruni dakika 32 kabla ya mabeki wa Kameruni kuokoa hatari hiyo na kuwa kona ya kwanza kwa kikosi hicho iliyopigwa na beki wa kushoto, Amir Maftah ambayo haikuzaa matunda.
Eto’o alifanikiwa kuitoka ngome ya Stars dakika 37 na kufumua shuti lililotoka nje ya lango kabla ya dakika mbili baadae beki wa kulia, Geremi Njitap kupiga shuti lililowababatiza mabeki wa Stars kabla ya kuokolewa.
Kameruni iliendelea kutawala sehemu ya kiungo iliyokuwa ikichezwa na Godfrey Boniface na Nditi ambao walimpa nafasi Song kuwalisha mipira washambuliaji wa Kameruni walioongozwa na Eto’o.
Kameruni iliwatumia zaidi mabeki wa pembeni, Njitap aliyecheza upande wa kulia na Thimotheo Atouba ambao walikutana na vikwazo kutoka kwa Maftah na Nsajigwa Shadrack ambao walicheza kazi kupunguza kasi ya mashambulizi.
Baada ya kumalika mchezo huo, Eto’o alivua jezi yake nambari 9 na kumpa ‘Cannavaro’ ambaye naye alimpa ya kwake.
Stars: Ivo Mapunda, Nsajigwa Shadrack, Amir Maftah, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Salum Sued, Godfrey Boniface, Henry Joseph, Shaaban Nditi, Danny Mrwanda, Nizar Khalfan na Mrisho Ngassa/ Emmanuel Gabriel.
Saturday, June 21, 2008
KAMBI YA MISS TANZANIA EU KUANZA JUMATATU,
- TIKETI ZAUZWA KAMA NJUGU
Kambi ya washiriki wa kumtafuta mrembo wa kitanzania katika nchi za Schengen yaani miss Manzania Schengen,inatarajiwa kuanza jumatatu hii ambapo vimwana 10 kutoka nchi mbalimbali za jumuiyayaUlaya watashiriki.Mashindano hayo yanatarajiwa kufanyika jumamosi ijayo katikaukumbi wa EFES mjini Essen Ujerumani ambapo mgeni Rasmi anatarajiwa kuwa Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani, Mh Ahmada Ngemera.
Amesema kuwa wadhamini hao ni Gazeti la African Positive lililoko Dortmund nchini Ujerumani ambalo pia linamiliki magazeti mengine maarufu kwa jamii yawaafrika barani Ulaya, African Heritage na African Courier.Mkurugenzi mtendaji wa kampuni hiyo Bi Veve Tata amesema magazeti hayo yataingia mkataba na mrembo atakayeshinda ili kumtafutia mikataba yaurembo katika nchi nyingine hapa barani Ulaya.
Wadhamini wengine wa shindano hilo ni shirikala ndege la Ethiopea airline pamoja na kampuni ya utalii ya Western Tours ya Bonn Ujerumani.
Katika shindano hilo linalosubiriwa kwa hamu kubwa na wadau kutoka nchi mbalimbali za ulaya msanii wa kizazi kipya kutoka Tanzania anayetamba na kibao chake Cinderela Ali Kiba atatumbuiza,pamoja na msanii kutoka Cameroon wa miondoko ya Makossa Eyum Anneh.
Tiketi za onesho hilo zimekuwa zikiuzwa kwa kasi katika vituo mbalimbali.Bei ya tiketi hizo ni euro 10,lakini kwa wale watakaonunua mlangoni ni euro 15 pamoja na kinywaji kimoja bure.
Innomizizi na Kiuno Viuno
TAIFA STARS TUPENI RAHA LEO
Dawati la Spoti na Starehe linaungana na watazania kukutakieni kila la heri kwenye mchezo wa leo na Kameroon, msiogope majina, kama walishangaa uwanja wetu hakuna cha kushangaa kule hata kamoja tuu kanatutosha kufurajia.”
Werrason Kutua Dar July
Gonga player hapo chini Kupata Sebene la Werason na vijana wake, Muangalie kwa makini stage show wa Wera anaitwa Bibiceya Mufwengi. Selamat Datang…
Libya yaichapa Lesotho 4-0
MAshabiki wa Libya wakiangalia mechi ya awali ya kombe la Dunia kati ya timu yao ya Libya na Losotho, mchezo uliochezwa Tripoli Libya juni 20. Libya iliibugiza Lesotho mabao 4-0.
Turkey yasonga mbele
Croatia 1 – 3 Turkey
Sabaiki wa Croatia akiwa anahuzunika mara baada ya kumalizika kwa mchezo wa jana kati ya Croatia na Turkey.
Polisi wakijenga ukuta kuwazuia mashabiki wa Croatia ambao walikuwa wakipita mitaani wakifanya fujo baada ya timu yao kuondolewa hapo jana.
Mashabiki wa Turkey wakipita mitaani Austria wakishangilia timu yao baada ya kuichapa Croatia 3-1 hapo jana, Mji wa Viena ulikuwa ni nyekundu tupu!
Friday, June 20, 2008
Mshindi wa Talaku kuzawadiwa Gari
“ THT imeamua kuandaa shindano la kumpata nani zaidi katika marapa, lengo likiwa ni kuonyesha uwezo wa wasanii na kuthamini mchango wao katika muziki,” alisema. Gonga hapa uzisome zaidi
Salama naye aachia…
hapo jana, Habari zinapasha kuwa Salama ambaye alipata umaarufu kwa kipindi chake cha Planet Bongo kilichokuwa kikirushwa hewani na East African Television ameacha kuendesha kipindi hico bila kuelezea kiundani zaidi. PICHA NA CHRISTOPHER LISSA / GPL.
Wachezaji Taifa Stars walamba mapesa!!
- Kila Mchezaji ajinyakulia 1.2 milioni.
- Timu imendoka kwenda Cameroon na matumaini
Kikosi cha Taifa Stars pichani ambacho kilicheza na Cameroon hivi majuzi
Taifa Stars na Kameruni ‘Indomitable Lions’ zinatarajiwa kukwaana kesho mjini Younde, ukiwa ni mchezo wa marudiano baada ya kutoka suluhu kwenye Uwanja Mkuu Mpya wa Taifa, Dar es Salaam wiki moja iliyopita.
Katika mchanganua huo, Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limetoa sh. 34,000,000 ikiwa ni motisha kwa wachezaji hao wakati benki ya NMB ambao ni wadhamini wa timu hiuo ilitoa sh. 6,200,000.
Kutokana na fedha hizo kila mchezaji atapata sh. milioni 1.2 katika kikosi cha wachezaji 27 na benchi la ufundi litapata sehemu ya fedha hizo.
Akizungumza Dar es Salaam jana, Katibu Mkuu wa Shirikisho hilo, Frederick Mwakalebela, alisema TFF imeamua kutoa fedha hizo ili kuwapa changamoto wachezaji wanaojiwinda na mchezo huo mgumu dhidi ya Kameruni.
Mwakalebela alisema TFF imeamua kutoa fedha hizo kwa kutambua mchango mkubwa wa wachezaji wa Stars na benchi la ufundi.
Alisema kutokana na motosha hiyo ana uhakika wachezaji hao wataweza kufarijika na kujituma zaidi na hatimaye kupeperusha vizuri bendera ya Tanzania katika michezo yake ya kuwania kufuzu kucheza fainali za Kombe la Dunia.
“Vijana wamefanya kazi kubwa sana katika mchezo wao wa awali dhidi ya Kameruni na pia bado wana kazi ya kuhakikisha wanafanya vema katika mchezo wa marudiano hivyo fedha tulizotoa zitawapa changamoto kubwa,” alisema Mwakalebela.
Akizungumzia mchezo wa marudiano dhidi ya Kameruni unaotarajia kufanyika leo mjini Younde, Kocha Mkuu wa Stars Marcio Maximo, alisema mchezo huo ni mgumu kwa timu yake ambayo inahitaji ushindi.
Maximo alisema hata hivyo anatarajia kupata matokeo mazuri kwa timu yake baada ya kufanya maandalizi ya kutosha na kuhakikisha inakabiliana na Kameruni ikiwa ugenini.
Maximo alisema timu yake ipo katika hali nzuri na wachezaji wake wamejengwa kisaikolojia licha ya kuwa na majeruhi wachache ambao anatarajia kuwatumia katika mchezo huo akiwa na matumaini ya kurejea katika hali nzuri.
Stars inatarajiwa kuondoka leo alfajili ikiwa na wachezaji 21, viongozi saba wakiongozwa na Mbunge wa Singida Magharibi Mohamed Misanga ambaye atakuwa mkuu wa msafara kwa upande wa Serikali.
Taifa Stars ina pointi mbili baada ya kutoka sare 1-1 na Mauritius, imefungwa bao 1-0 na Cape Verde kabla ya kutoka suluhu na Kameruni.
Habari na Majira, Picha na Mpoki Bukuku
Wazee wa Ngwasuma kupamba Miss Morocco Leo
Bado anatakiwa….
Ronaldinho kwenda Galaxy?
Mchezaji wa FC Barcelona Mbrazili Ronaldinho akicheza na mpira wakati wa mazoezi ya timu yake huko Camp Nou stadium, Barcelona April mwaka huu, Habari zinapasha kuwa timu ya Galaxy ya Marekani ambayo imemchukua David Beckham imetoa Ofa ya kumchuua Ronaldinho kwa mkataba wa dola milioni 16 na dola milioni 16 nyingine kwa haki miliki ya Picha yake. Habari zinasema mazungumzo yapo pazuri.
Masikini Portugal!!, Ujerumani yapaa Nusu Fainali
Portugal 2 – 3 Germany
Mchezaji wa Ujerumani Michael Ballack (kulia) akipachika bao la tatu kwa timu yake.
Wachezaji wa Ujerumani wakisherehekea ushindi mara baada ya mchezo wao na Portugal kumalizika
Mashabiki wa Portugal wakiwa hawaamini macho yao mara baada ya kipyenga cha Mwisho
Macho yote yalikuwa kwa Cristiano Ronaldo jana lakini mambo hayakuwa hivyo kwani ilikuwa ni kinyume chake na mchezaji wa Ujerumani mwenye namba yaka yake Bastian Schweinsteiger ndiye aliyeng’ara jana na kuihakikishia Ujerumani nafasi ya kusonga mbele kwenye hatua ya Nusu Fainali na kuwatupa Portugal nje.
Nyota ya Bayern Munich Schweinsteiger alifunga goli moja na kutengeneza mengine mawili kwa Miroslav Klose na Michael Ballack, mpaka mapumziko mabao yalikuwa ni 2-1 huku ujerumani wakiongoza na bao la Portugal lilifungwa na Nuno Gomes kwenye dakika ya 42 ya kipindi cha kwanza.
Kipindi cha pili kulianza kwa mshike mshike kweli kweli huku mashabiki wakishangilia goli toka kwa Michael Ballacks mnamo dakika ya 62, mashabiki wa Portugal walionyesha kukata tamaa kidogo. Ujerumani ambao kwa kiasi kikubwa walianza michuano hii kwa kusuasua na watu waliitaja zaidi Portugal kucheza Fainali jana walionyesha uhai na ile ladha ya Mpira ambao wapenzi wameizoea kwa Ujerumani.
Kwa matokeo hayo Ujerumani itakutana na ama Croatia au Turkey, timu ambazo zote hazitabiriki.
Huu ni mhitimisho wa mkataba wa miaka mitano wa kocha Luiz Felipe Scolari ambaye atajiunga na Club ya Chelsea mapema baada ya michuano hii kwani alitazamiwa kumaliza ‘s five-year reign as Portugal coach to an inglorious end before he heads off to become Chelsea mamkataba wake kwa mafanikio ya kikombe hiki.
Kocha wa Ujerumani Joachim Low, hakuweza kukaa kwenye benchi la akiba la Ujerumani kwa kuwa alifungiwa mechi moja mapema wiki hii alipokwaruzana na Kocha mwenzie wa Austria Josef Hickersberger na kutolewa nje ya uwanja. Mpaka mwisho wa mchezo matokeo ni 3-2.
Thursday, June 19, 2008
Manchester kucheza na Portsmouth nchini Nigeria mwezi ujao.
Mabondia wa Tanzania walikuwa na jumla ya kilo 6 za madawa!!
Watuhumiwa hao walifikishwa kwenye mahakama jumatatu wiki hii mjini Port Luis.
Kamanda Kivuyo amesema watanzania hao wanashitakiwa kwa makosa ya aina mbili.
i) Kujihusisha na biashara haramu ya madawa ya kulevya
ii) Kuingiza nchini Mauritius Madawa hayo.
na Mama wa Kikenya atashtakiwa kwa kushirikiana na watu hao.
Jeshi la polisi bado linafanya uchunguzi kujua kama madawa hayo waliondoka nayo hapa au la.
Muungano wa Africa Mashariki na Magharibi Kimuziki
RF Chord ambaye anatumia zaidi mtindo wa “Dance Hall” huku akichanganya na midundo ya asili kwa nyimbo zake nyingi amejipatia umaarufu sana na Wimbo huu aliopiga na Ray C.Hii inasaidia kuufanya muziki wa Kizazi kipya kutambulika zaidi ingawaje kwenye wimbo huu Ray C aliuimba kwenye mahadhi ya Kipwani zaidi, ukiwa ni Remix ya wimbo wake wa Sikuhitaji ambayo ilipigwa kitambo kidogo, Hivi karibuni tumesikia Mwanamuziki toka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo anayeishi Uingereza Blanchard Deplaizir akitangaza kutaka kufanya Kolabo na Ali Kiba na majuzi tena Ali Kiba huyo huyo amesikiaka akiingia Studio na Vijana wengine, Shime kumekucha muziki huu umekubalika nchini ni wakati wa kuuza kimataifa na kwa jinsi hii mtatoka.
Pata burudani kwa kubofya Player…
Banana na Hafsa kuwapa “Pressure” mashabiki Club Afrique
Siku: Ijumaa
Ukumbi: Club Afrique
Wakisaidiwa na
DJ Dubwise – Voice of Africa Radio
Jessie – Afrique
Talent – Afrique Tallent
Biggz – Afrique/Nytce
wasiliana na
Lawrence -07931819416, Jesse-07944545555, jimmy-07877418535
Starehe Mita 1800 juu ya usawa wa Bahari
Huku hasa ni mji wa mapumziko, naita mji kwani panajitosheleza kwa kila kitu kuanzia mahoteli hadi Hospitali ambapo watu hupendelea kwenda kupumzika na kupata starehe mbali mbali kama Cable Car ambazo zina urefu wa Kilomita tatu na nusu, na inapita katikati ya misitu minene ya Tropiki na ubaridi mwanana pia utaona ndege na wanyama kama nyani wakiruka kwenye miti huku ukipita kwenye kijikombe kilichobebwa na mkanda (cable) ambacho kina tembea mwendo wa wastani wa kilomita 10 kwa saa, ni burudani tosha ambayo inahitaji ujasiri kwani kama hujazoea utatamani kushuka.
Safari ndio imeanza ndani ya “Cable Car”
Mambo ya mwambao hata huku yapo atii
Pia kuna uwanja wa Golf kwa wenye mchezo wao, ambao wengi ni wageni mahoteli zaidi ya 30 yaliyopo kwenye kijiji hiki cha maraha. Mbali na hiyo kuna Casino kubwa, hii ndio Licensed Casino kwa Malaysia na inakusanya wacheza kamali toka Singapore, Malaysia, Indonesia na Brunei ambao wote hufika kucheza kamali hapa.
Wednesday, June 18, 2008
SERIKALI YAONGEZA MKATABA KWA MAXIMO
“ Maximo aliingia mkataba nasi wa miaka miwili kuanzia Julai 28,2006 hivyo mkataba wake huo utakamilika Julai 2, mwaka huu hivyo tumeona ni vema tulizungumzie jambo hili mapema na tumeamua kumwongezea mkataba huo kwa miaka miwili mingine” alisema Tenga
Hatahivyo Tenga alisema pamoja na TFF kuamua kumwongeza mkataba wa kwa miaka miwili mingine na Kocha Maximo katika mazungumzo yao juu ya kuongezwa mkataba huo ameomba uongezewe mwaka mmoja tu kutokana na sababu zake binafsi ambazo hakuzitaja.
Akizungumza mara baada ya Tenga kutangaza uamuzi wa TFF kumwongezea mkataba wa kuinoa Stars, Maximo alisema sababu kubwa ya kufurahia jambo hilo na kushukuru kwa ushirikiano aliopewa kutekeleza majukumu yake na kueleza kuwa sababu yake ya kuomba apewe mwaka mmoja tu katika mkataba mpya ni kutoa nafasi kwa makocha wengine kuendeleza pale alipofikia katika programu ya kuinua na kuendeleza soka la Tanzania.
“ Unajua mtu huwezi kutekeleza programu ya miaka 10 ya kuinua na kuendeleza soka la nchi pekee yako kwani kila programu ya kocha ina muda wake wa kukamilika hivyo katika mikaka hiyo 10 kuna ulazima wa kocha mwingine kuja kuendeleza pale nilipofikia” alisema Maximo
Aidha Tenga alisema uamuzi huo kuongeza mkataba wa Maximo umefikiwa baada ya Shirikisho hilo kutathmini kazi ya kocha huyo na kuonekana ametekeleza majukumu yake ipasavyo kutokana na hadidu rejea alizopewa na kuifanya TFF kuridhishwa na utendaji wake.
Akizungumzia suala la kocha huyo kuomba kuongezewa mkataba wa mwaka mmoja tu katika mkataba huo mpya Tenga alisema wamekubaliana kuwa endapo Taifa Stars itafuzu kushiriki fainali ya michuano ya kombe la dunia na zile za Mataifa ya Afrika za mwaka 2010 nchi Afrika Kusini na Angola ataendelea na kazi ya kuinoa timu hiyo.
Holland yaendeleza kichapo
Wachezaji wa Holland wakijipongeza na mashabiki mara baada ya kuwachapa Romania 2-0.
Magoli ya Klaas-Jan Huntelaar na Robin van Persie katika kipindi cha pili yailiipa Holland ushindi wa 2-0 dhidi ya Romani, Huu ni muendelezo wa ushindi kwa timu ya Holland ambayo imeshinda mechi zake zote.
Wa dutch wamemaliza ratiba ya awali kwa ushindi mzuri na sasa kwenye hatua ya Robo Fainali watakutaka na Sweden au Russia.
Romania ambao walihitajika kushinda mechi yao ya jana ili waweze kusonga mbele waliishia kusononeshwa tuu na waholanzi ambao hawakuwa na mchezo huku wakishangiliwa na wapenzi wao waliufanya uwanja mzima kuwa rangi ya machungwa.
Masikini Ufaransa, Italy yapaa
France 0 – 2 Italy
Andrea Pirlo ndiye alikuwa wa kwanza kupata bao kwa mabingwa hao wa dunia katika dakika ya 25 kwa penati baada ya Eric Abidal kumchezea madhambi Luca Toni ndani ya kumi na nane.
Abidal alipewa kadi nyekundu kwa tukio hilo na kuwaacha Ufaransa wakihangaika kuupanda mlima kufuatia mchezaji mwingine Frank Ribery kuwa majeruhi.
Italy walicheza kufa na kupona huku Ufaransa wakijitahidi kutaka kusawazisha bao mcheza ukawa wa vuta ni kuvute lakini mnamo dakika ya 62 Italy wakapata tena mpira wa adhabu ukaenda kupigwa na Daniele De Rossi na moja kwa moja ukaingia nyavu ndogo na kufanya Italy kuongoza kwa mabao mawili.
Ufaransa wamekuwa na wakati mbaya kwani angalao waliambulia sare kwenye mechi yao ya ufunguzi kabla hawajaja kubugizwa na Holland 4-1 na sasa Italy, Ikumbukwe kuwa Fainali za Kombe la Dunia ziliwakutanisha Iyaly na Ufaransa, ndio huku mchezaji wa Ufaransa Zinedine Zidane alimchapa kichwa cha kufa mtu Materazi.
Italy, ambao wamemaliza wakishika nafasi ya pili nyuma ya Dutch itakutana na mshindi wa Kundi D Spain siku ya jumapili katika hatua ya Robo Fainali huko Vienna lakini Waitaliano watawakosa wachezaji wao mahiri Pirlo na Gennaro Gattuso, ambao kwa pamoja walipata kadi kwenye mchezo wa jana.
Tuesday, June 17, 2008
Mzee Mwinyi akatiza safari ya Mlima Kilimanjaro
Pichani rais mstaafu (katikati)akiwa na wafanyakazi wa Celtel Tanzania,Prisca Tembo (kulia) na Cuthbert Raphael (kushoto),muda mfupi kabla ya kupanda Mlima Kilimanjaro.Picha hii ni kwa hisani ya Celtel.
Kelly atembelea uwanja wa Fisi!!
Msanii maarufu wa Marekani Kelly Rowland (mwenye mtandio juu na chini), ametinga uwanja wa fisi Manzese Dar es salaam jioni ya leo baada ya kusikia sifa za maeneo hayo ya uswahilini tangu akiwa USA. Msanii huyo ametua nchini kwa tiketi ya MTV kupitia taasisi yake inayojishughulisha na kampeni za kupambana na Ukwimwi (Staying Alive Foundation) ya nchini Marekani, Kelly akiwa balozi wake. Akiwa Uwanja wa Fisi, ambako kunasifika kwa ufuska wa kupindukia na rate kubwa ya maambukizi ya virusi vya ukimwi kwa wasichana wadogo, Kelly alitembelea NGO ya EYG (Elizabeth Youth Group) inayojishughulisha na kutoa misaada ya elimu ya HIV/AIDS, uchangudoa, ulevi pamoja na uvutaji bangi kwa vijana nchini. Pichani juu akiongea na waandishi wa habari katika hoteli ya Kempinsk jioni ya leo mara baada ya ziara ya Manzese na Tandale. PICHA: CHRISTOPHER LISSA wa GPL
Salamu za Cynthia Masasi
Woooo i forgot one thing LOL i will be in columbus ohio for the old school party on July 4th weekend so everybody is welcome its gonna be bananas trust me The number one DJ Bon Luv from Tanzania will be in the building..People u dont wanna miss that come on so we can PAAAARTYYYY..
Love Cynthia masasi..
Gonga Player hapo upate kuona moja ya Video ambamo ameshiriki Cynthia
ZIKO: Scolari atawafungulia Brazili Uingereza
Scolari amechanguliwa kuifundisha klabu ya Chelsea kwa mkataba wa Paundi million £6 kwa mwaka akiwa na jukumu gumu la kukichukua kikombe cha Premier Ligi kutoka kwa Manchester na lililo muhimu ni kuchukua kikombe cha UEFA Champions Ligi kwa mara ya kwanza.
Kocha huyo wa Brazili ambaye kwa sasa anaifunza timu ya Taifa ya Portugal katika michezo ya fainali ya EURO 2008 ameshatajwa kutaka kuwachukua wachezaji mahiri kama Kaka, Ronaldinho, Franck Ribery, Rafael van der Vaart, Samuel Eto’o, Deco, Fernando Torres na David Villa ambaye anaongoza kwa ufungaji kwenye michezo ya EURO 2008.
Kujiunga kwa Scolari kwenye ligi ya Uingereza kutaifanya Brazil na wachezaji wengi wa Brasili kuiangalia ligi hiyo kwa jicho jingine ambapo wengi wa wa Brasili walipendelea kucheza sehemu nyingine za Ulaya sio Uingereza kikubwa ilikuwa ni Lugha na pia jinsi utamadubni wa waingereza ulivyo tofauti.
Zico anaamini kuwa hii itawanufaisha sio tu Premier League ila pia Brazil, na akasema: “Kufika kwa Scolari huko Chelsea ni mafanikio makubwa kwa Brazili na majaliwa ya soka la Brazili pia, tuna tatizo, hatupendi waingereza wanavyofanya mambo yao, na tunapingana hapo tuu inabidi kubadilika hiyo ndio maana yangu aliongeza Ziko.
“Hii ni nafasi kwa wachezaji wa Brazili kutoka Brazili na kwenda kucheza Uingereza itaifungua BRazili na soko la wa Brazili Uingereza pia. na sisi tutajifunza mengi si tu mpira hata maisha na utamaduni pia, soka inalipa kwa Uingereza, watu kule wanapenda soka na wanmefanikiwa kuianya ligi yao kupendwa ulimwenguni huko ndio kwa kwenda kucheza, aliongeza Zico.sement
Hatimaye Ujerumani wavuka
Michael Ballack ndiye aliyefanya booking ya Ujerumani kwenye nafasi ya Robo fainali kwa shuti safi kipimo iliyopatikana kwa mpira wa adhabu ikiwa ni dakika ya 49 ya mchezo mara tu baada ya kipindi cha pili kuanza na kuwanyamazisha kabisa wenyeji Austria katika mchezo wa mwisho wa kundi B.
Mchezaji huyu wa Klabu ya Chelsea ambaye mapema jana alilalamika kuwa hafurahii kiwango alichoonyesha kwenye michuano hii aligeuka ghafla na kuwa mwiba wa sumu kwa Austria.
Austria ambao nao walipoteza mchezo mmoja a kutoka droo mmoja walikuwa wanategemea ushindi wa jana na kuombea mabaya mchezo wa Poland na Croatia ili wajihakikishie nafasi ya Robo fainali lakini bahati haikuwa yao jana.
Ballack anakwenda kukutana na Kocha wake mpya kwa klabu ya Chelsea Philipe Scolari kwenye mchezo wa Robo Fainali kati yao na Portugal mchezo ambao mashabiki wanaungoja kwa hamu. Luiz Felipe Scolari, ndiye ataifundisha Chelsea kuanzia msimu huu na atajiunga na Klabu hiyo mara baada ya michuano hii kumalizika.
Ujerumani wanabahati mbaya kwani hawatakuwa pamoja na Kocha wao kwenye chumba cha kubadilishia nguo na wala benchi huko Basel’s St Jakob-Park siku ya alhamisi ambapo watamenyana na Portugal, baada ya kutolewa nje mechi ya jana baada ya kutupiana maneno na mwenzie na maofisa wa UEFA. Mpaka mwisho wa mchezo Austria 0-1 Germany.
Sheria ni msumemo…
Kocha wa Ujerumani Joachim Loew (L) akiongea na Kocha wa Austria Josef Hickersberger (R) baada ya kutakiwa kutoka nje ya uwanja katika mchezo baina ya Timu zao jana.
Do or Die ya Ufaransa Leo
Croatia haoooo Robo fainali
Goli lililofungwa na Ivan Klasnic katika dakika ya 52 ya kipindi cha pili liliwafanya Croatia kumaliza mechi zake zote tatu toka kundi B kwa ushindi. Croatia ambao awali waliifunga Australia 1-0, wakaifunga Germany 2-1, na jana wameifunga Poland 1-0, matokeo yaliyowapeleka moja kwa moja Robo Fainali ambapo watakutana na Mshindi wa pili wa Kundi A ambaye ni Turkey.
Ndoto ya Poland kufika mbali haikuweza kufanikiwa kwani waliihitaji kushinda mchezo huu na pia hata kushinda kwao kulitegemeana na matokeo kati ya mchezo wa Australia na Germany ambapo Australia alikuwa ame droo mara moja na na kuwa na point 1 na Germany alishinda mara moja dhidi ya Poland na kuwa na Point tatu. na Poland ame droo mara moja na kuwa na point 1 ambapo kama angeshinda jana basi angefikisha point 4 na kama Australia na Germany wangetoka Droo pia Germany angekuwa na Point 4 ambapo labda wangezidiana magoli.
Hata hivyo mchezo wa jana ambao kila timu ilihitaji kushinda ulikuwa mzuri kwa kila timu kuonyesha mashambulizi ya hapa na pale na huku Poland wakionyesha dhahiri kukamia ushindi ila bahati haikuwa yao.
Turkey ambaye alipoteza mchezo wake na Portugal katika kundi A anakibarua kigumu akija kukutana na Croatia ambao wao kwao ushindi ndio nguzo yao na wanacheza kwa kujiamini dakika zote. Tungoje tuone.
KELLY ROWLAND NDANI YA BONGO
Bila shaka utakuwa bado unalikumbuka kundi maarufu la muziki lililokuwa linajulikana kama Destiny’s Child kutoka nchini Marekani. Miongoni mwa mabinti waliokuwa wanaunda kundi hilo ni Kelly Rowland(pichani).Wenzake walikuwa ni Beyonce Knowles(mke wa Jay Z hivi sasa) na Michelle Williams. Kundi hilo lilivunjika rasmi mwaka 2005 ingawa mara moja moja bado huwa inatokea wakafanya maonyesho pamoja. Bonngo Celebrity wameiweka kwa mapana zaidi
Miss Tanzania UK kapatikana
MISS TANZANIA 2008 UK!
|
Kimwana Tusekile Mwakibinga alitawazwa rasmi juzi kuwa Miss Tanzania Uk 2008 kwenye sherehe zilizofanyika ndani ya Silver Spoon New Light Complex karibu na wembley Stadium.Pichani Miss Tanzania Uk 2008 Tusekile Mwakibinga akiwa katika picha ya pamoja na First Runner Up Miss. Jacqui Majebele(kushoto) na Second Runner up Miss. Alice Kapya.
Washiriki na washindi wa shindano la Miss Tanzania Uk 2008 wakiongozwa na Miss Tanzania Uk 200 Tusekile Mwakimbinga wakiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Tanzania nchini Uingereza Hon Mwainda Maajar.
Washiriki wakijinadi mbele ya majaji
Monday, June 16, 2008
Akudo Impact kupekecha na Miss Sinza
Akudo kwa sasa ambayo inakubalika na mashabiki wengi wa muziki wa dansi inatamba na wimbo wa Binadamu� huku nyota ya rapa na muimbaji wake, Christian Bella ikiendelea kung’ara zaidi.
Mratibu wa mashindano hayo, Somoe Ng’itu alisema jana kwamba tayari kwa takribani wiki mbili sasa wanamuziki wa bendi hiyo walikuwa wakifanya mazoezi kwa ajili ya mashindano hayo.
Somoe alimtaja msanii wa kizazi kipya, Kassim Mponda Cassim anayetamba na Siamini na Awena na kwa upande wa muziki wa asili ni Mrisho Mpoto anayefanya vizuri katika nyimbo mbalimbali ukiwamo Mjomba alioshirikishwa pamoja na Wanne Star ambaye ni maarufu kwa kucheza na nyoka katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati.
Tumeamua kuchanganya burudani ili kila mtu apate anachotaka japo kikubwa watu wataona pia burudani ya kutosha kutoka kwa warembo bomba, alisema.
Wadhamini kadhaa wamejitokeza kudhamini shindano hilo ni pamoja na Mama Tike Hair Fashions, Redds, Multchoice Tanzania, Vannedrick (T) Ltd, 2080 Fashions, Break Point, Coca Cola, Vodacom, gazeti la Tanzania Daima na Clouds FM 88.4.
Msondo usipime!!
Etoo kazuliwa kijambo!!
Kama kawaida kwenye wengi kuna mengi, Timu ya Taifa ya Kameroon ilikuwa Tanzania kucheza na Taifa Stars katika mchezo wa awali wa kuwania tiketi ya Kombe la Dunia, Ikiwa imekwenda na Wachezaji wake mahiri kama Samuel Etoo na Song iliambulia Sare na Taifa Stars, Je wajua kilichotokea nyuma ya pazia kwa Striker wa Kameroon Samuel Etoo? Gonga hapa uisome!!
Karibu Malaysia!!
Turkey yawafungisha virago Czech
Nihat Kahveci ndiye aliyekuwa nyota wa mchezo wa jana kwa kufunga magoli mawili dhidi ya matatu ambayo Turkey walishinda na kuwafungisha Virago Jamhuri ya Czech kwenye mchezo wa fainali wa undi A jijini Geneva.
Kwa ushindi huo Turkey wamejihakikishia nafasi ya pili ya kundi A kwa kufikisha Point 6 kama Portugal baada ya kushinda mchezo wake wa mwanzo dhidi ya Switzerland kwenye mchezo wa ufunguzi.
Mpaka dakika wa 62 Czech walikuwa wakiongoza kwa 2-0 mabao yaliyofungwa na Jan Koller dakika ya 34 na Jaroslav Plasil dakika ya 62.
Turkey ambao walibadilika kabisa hasa dakika 25 za mwisho za mchezo iliwachukua hizo hizo dakika 25 kupachika mabao matatu yaliyowapa ushindi.
Mabao ya Czech yalifungwa dakika ya 75 na Arda Turan (75), dakika ya 87 na Nihat Kahveci (87) na la tatu dakika ya 89 na Nihat Kahveci (89). na kuwanyong’onyeza kabisa mashabiki wa Czech ambao walikuwa wakiishangilia kwa nguvu timu yao na kujua wameshinda mchezo huo.
Kwa ushindi huo Turkey wanaungana na wenzao Portugal kwenye hatua ya Robo Fainali ambapo Turkey watapambana na mshindi wa kundi B.
Switzerland yazizima Mbwembwe za Portugal
Forward wa Swiss Eren Derdiyok akiwa kwenye heka heka na na na beki wa Portugal Pepe wakati wa mchezo wa Kundi A ambapo Swiss waliibuka washindi kwa 2-0.
Magoli mawili yaliyofungwa na Hakan Yakin dakika ya 71 na 83 ndio yaliyowakosesha raha mashabiki wa Portugal (nikiwemo mimi), na kuipa ushindi Switzerland wa 2-0 dhidi ya Portugal.
Ushindi huo umewasaidia waandaaji hao angalao kuambulia ushindi na kwao ni ushindi mwanana kwani wameifunga na kuishinda timu ambayo haijapoteza mchezo hata mmoja tangu mashindano haya yaanze.
Pamoja na kichapo hicho Portugal wanakwenda Robo fainali kama washindi wa kundi A na Swiss wamejikongoja baada ya kupoteza michezo yao yote miwili ya awali hivyo ushindi wa jana umefanya wafikishe pointi 3 pekee.
Yakin alifunga bao la kwanza baada ya pasi toka kwa Eren Derdiyok ikiwa ni dakika ya 71 ya mchezo na kuachia shuti toka umbali kama wa yadi 15, shuti lililopita tobo golikipa wa Portugal na kuandika goli la kwanza.
Dakika 12 baadaye Yakin aliifungia timu yake goli la pili kwa njia ya Penati.
Portugal wanacheza Jumamosi hii na mshindi wa pili wa kundi B.
Sunday, June 15, 2008
Klynn
Nawaacha na Video yake ya Crazy Over You…… Jumapili Njema,
Mke wa Snoop Dogg Mbaroni kwa kuendesha akiwa amelewa
Luteni Craig Brower alisema maofisa wake walimsimamisha Shante au Shahn-taye (32) pichani kulia (Picha iliyotolewa na Police baada ya kukamatwa) majira ya saa sita na robo usiku wa jana jumamosi huko Sherman Oaks na wakamchukua na kumtupa lupango lakini baadaye jana hiyo hiyo aliachiwa kwa dhamana lakini atafikishwa kortini.
Jioni ya “KHANGALICIOUS” June 20
Miss Ubungo 2008 huyu hapa
Jk Boys waliowatoa Kamasi Cameroon
Keeping Up With the Kardashians mitaani Monaco
Saturday, June 14, 2008
Villa aibeba tena Spain dhidi ya Sweden
Wachezaji wa Spain wakimpongeza Villa mara baada ya kupachika bao la pili huku mashabiki wa Sweden wakiangalia kwa uchungu.
Mpaka sasa Spain wamefanikiwa kufikisha pointi 6 na Sweden 3. Greece ambao ni mabingwa watetezi wanacheza na Rushia usiku huu huko Salzburg.
Zali, Jezi ya Etoo
Picha na Mpoki Bukuku.
Malawi yaichapa Egypty 1-0
MABINGWA wa Afrika, Misri wamepata mshtuko baada ya kupata kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa Malawi mjini Blantyre.
Katika mchezo huo wa jana wa kufuzu kucheza fainali za Kombe la Dunia na Mataifa ya Afrika mwaka 2010, Misri iliamini mchezo huo ungeisha suluhu.
Misri, ambayo inafundishwa na Hassan Shehata ilifungwa bao hilo pekee ndani ya dakika tatu za majeruhi, ambalo lilifungwa na Chiukepo Msowoya wa Malawi.
Katika mchezo mwingine, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo iliifunga Djibout mabao 6-0 katika mchezo uliofanyika juzi.
Kwenye mchezo mwingine jana, Tembo wa Ivory Coast walilazimishwa sare nyingine walipocheza na Botswana.
Dipsy Selolwane aliipa Botswana bao la kuongoza dakika ya 25 mjini Gaborone na kuwafanya Ivory Coast wasubiri mpaka dakika ya 64 kusawazisha bao kupitia kwa Kanga Akale.
Ni mara ya pili kwa Ivory Coast ambao walicheza bila Didier Drogba kutoka sare ndani ya mwezi huu kwani wiki iliyopita walibanwa na kutoka suluhu na Madagascar.
Taifa Stars yailazimisha Sare Cameroon
Picha na Mpoki Bukuku habari na Mwananchi
Haya huyu jamaa rigobert Song aliamua kuwafanyizia vijana kwa kuwachezea faulo za nguvu imagine hapa anamfanyizia Amir maftah!
Hakutosheka akaamua kumweka kipepsi Athumani Idd, jamani vijana wanatisha tuache kuwakatisha tamaa!
Msajigwa leo katisha katika mechi kafanya mambo kichizi kawachanganya wacameroon!
Mchezo kati ya Taifa Stars na Cameroon umemalizika jioni hii katika uwanja wa Taifa kwa Timu hizo kutoka droo ya bila kufungana.
Katika mchezo huo ambao Taifa Stars walionyesha kuumudu vilivyo kutokana na Timu hiyo kuipa Upinzani wa hali ya juu timu ya Cameroon ambayo kila mmoja aliipa nafasi ya ushindi.
Viungo wa Stars; Athuman Idd, Geofrey Bonny, Shaabani Nditi na Nizar Khalfan walifanya kazi kubwa kutibua mipango ya Cameroon.
Ingawa Stars walipiga mashuti matatu tu langoni mwa Cameroon, lakini yalikuwa ya hatari na hasa kama Danny Mrwanda ambaye aliwasumbua sana angetulia.
Dakika ya 13, Mrwanda alikosa bao baada ya kutengenezewa pasi nzuri na Athuman Idd lakini mpira huo uliondoshwa na Rigobert Song ambaye baadaye alionekana kuhamaki kutokana na kasi ya Danny Mrwanda na Mrisho Ngassa.
Kama Ulaya!!!! Golikipa wa Taifa Stars Ivo Mapunda akiondoa hatari golini mwa Taifa Stars, Katika mchezo wa Leo ambapo naye aliwakatisha tamaa Wa Cameroon mara kadhaa
Cameroon, ambao walionekana kucharuka kuanzia dakika ya 20, walipata kona tatu mfululizo ambazo hazikuwa na madhara kwani Mapunda alipangua kichwa cha Eto’o na mabeki wakafanya kazi kubwa kuondoa kona nyingine zilizokuwa zinapigwa na
Njitap.
Matumaini ya mashabiki wa soka yalikuwa makubwa baada ya kuona Cameroon ikikubali kwenda suluhu mpaka wakati wa mapumziko huku Ngassa na Mrwanda wakionekana tishio.
Kipindi cha pili kilikuwa kizuri zaidi kwa Stars kwani walionana kwa muda mwingi na kukaba vizuri huku sehemu ya kiungo ikimiliki vizuri.
Mabeki wa Stars, Shadrack Nsajigwa, Salum Sued, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ na Amir Maftah walifanya kazi nzuri ya kuwadhibiti Eto’o, Achille Webo na Jean Makoun ambao hawakuleta madhara licha ya kuonekana hatari kila walipogusa mipira.
Mwamuzi bora Afrika, Bonaventure Kofi Kodjia wa Benin alilalamikiwa na mashabiki kwa kushindwa kutoa penalti wakati Mrwanda alipoangushwa eneo la hatari na Andrey Bikey dakika ya 75 wakati akienda kumuona kipa Idrissa Kameni dakika ya 75.
Dakika kumi za mwisho, Mrwanda alionekana kuwa tishio lakini alishindwa kuzitumia nafasi, huku Cameroon wakionekana kuhamaki kutokana na kushindwa kwenda sawia na kasi ya Stars.
Maximo aliwatoa Nizar na Athuman Idd na kuwaingiza Abdi Kassim pengine kwa kutaka mashuti ya mbali na Kigi Makasi kwa lengo la kutaka kuimarisha upande wa kushoto kama ambavyo Maximo amewahi kusema siku za nyuma.
Stars: Ivo Mapunda, Shadrack Nsajigwa, Amir Maftah, Salum Sued, Nadir Haroub, Geofrey Bonny, Shaaban Nditi, Athuman Idd/Kigi Makasi, Danny Mrwanda, Nizar Khalifan/Abdi Kassim na Mrisho Ngassa. Leo ni Mauritius na Cape Verde.
Watoto wa Mitaani na Bendi yao
Sanaa na wasanii
Mabondia wa Tanzania Mbaroni Mauritius kwa Madawa ya Kulevya
Isome zaidi kwa Issa Michuzi
Patchou Lumiere, Nyota mpya ya kizazi kipya cha Kongo
JB Mpiana: Fally, Celeo, Ferre i kizazi cha nne si cha tano.
Jumatatu ya Wiki hii mtangazaji wa kituo cha Clouds FM Sophia Kessy kupitia kipindi chake mwanana cha Afrika Bambataa alifanya mahojiano na Mwanamuziki toka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo toka kundi la Wenge BCBG, JB Mpiana Bin Adam Tshituka Papa Cherry.
1. vipi amefikia wapi kuhusu kutoa albam na werasoin
kuhusu kutoa nyimbo na werasoine ni kweli lakini kwa sasa tumeanza na sigle ya publicity na tutakapo maliza tutafanya kazi nzuri kwa sababu ni gharama sana kufanya kazi hii.
2. unaongeleaje kuhusu kumeguka kwa bendi yako hasa kwa watu kama akina alen mpela ambae inasemekana hata kwenye onyesho lako la hivi karibuni hakuwapo?
kuhusu kutoka kwa vijana ni kawaida ni sawa na baba mwenye watoto wanapo kuwa wakubwa huamua kutoka kujitafutia maisha yao , mimi binafsi nimefurahi kwa hilo kuona kuwa wanaweza kujitegemea sasa sina tatizo juu ya hilo nawaombea kwakuwa wakinufaika, pia ni sifa kwangu kwakuwa wametoka kwangu na hata kama hawata fanikiwa wakiona mambo yanaenda vibaya wakiomba kurudi nitawapokea ni wangu sitawatupa.
Sofia Kessy wa Clouds Fm, Afrikan Bambataa
3. muziki nu burudani kwanini mnakuwa na uaduni na mtu kama werason mpaka wapenzi wenu wanakuwa wanaumizana na hii imekuwa ikitokea mara kwa mara
ni ngumu kumtuma mashabiki kuwafanya wagombane akili tunayo itumia katika kazi ndio inayo wapelekea wao kutoelewana kila mtu anamuona mwenzie ni bora zaidi na kila msahabikianaamua kuvutia upande wake. ndio maana unaona kwa sasa kongo kuna chama kinaitwa MAISHA PARK, ambapo ukigundulika umegombana na mwezio basi wanakuiteni na kuwapatanisha lakini pia wanashauri kutogombana, ni baya kutukanana, na hii ndio inaleta umoja sasa katika muziki maisha park, ugomvi sikuzote unarudisha muziki nyuma.
4.unazungumziaje ujio wa wanamuziki chipukizi kama Fally Ipupa, Celeo scam, Ferre Gola ambao kwa kiasi kikubwawanaubadili muziki wa kongona kusemwa kuwa ndio kizazi kipya cha tano baada ya kizazi chanu cha nne.
kwanza ni vijana na wananfanya kazi vizuri, ninacho washauri mimi ni kuwa wawe na adabu, mungu atawasaidia lakini kuna jambo moja nataka kusema kuweka wazi kuwa zamani watu walituita wenge kizazi cha nne kwasababu hatukutoka katika bendi yoyote kongo tuliibuka tu tulikutana tukaunda kikundi chetu wenyewe tukiamini kila mmoja anaweza tulitoka nyumbani kwa kifupi, sio jibe katoka kwa zaiko, au wera katoka kwa tabu lay, sio blaiz bula katoka kwa papa wemba hapana sisis wote tulitoka nyumbani tukaunda kundi letu la wenge na ndio maana tulikubalika na wakatuita kizazi cha nne lakini kuhusu fally na ferre na tutu kaluji, na celeo scam,hawa ni kizazi cha nne kwasababu kuitwa kizazi cha tano sio kweli kwasababu wanamuziki hao wametoka kwangu na kwa kofi na kwa wera, na bendi walizotoka ni kizazi cha nne hivyo watu waelewe si kizazi cha tano bali ni cha nne na kizazi cha tano ni kizazi ambacho hakijajulikana kwenye bendi yoyote.
Pamoja na mambo mengine aliulizwa kuhusu chakula anachopendeleani mchicha, samaki, na wali maharage, pia aliulizwa timu anayoipendelea na kusema ni Brazil
JB Mpiana aliweka bayana kuwa anawatoto 7 wasichana wawili wavulana wa tano wa kwanza miaka 19 wa pili miaka 17 wa tatu miaka 15 wa nne miaka 14 wa tato miaka 12 wa sita miaka 10 na wasaba miaka 9
kuhusu kuja tanzania ni muda wowowte yupo tayari mara baada ya manager wake kumpa ushauri wa kufanya hivo.
Mji wa Bern ni rangi ya chungwa tupu!!
Ufaransa Mbendembende kwa Holland
Uholanzi 4 – 1 Ufaransa
Dirk Kuyt ndiye aliyefungua karamu ya magoli kwa Waholanzi na baadaye kufuatiwa na Robin van Persie, Arjen Robben na Wesley Sneijder. huku goli pekee la Ufaransa lilifungwa na Thiery Henry. Kipondo hiki ni muendelezo wa kipondo kama hicho walichompa Italy jumatatu.
Mshabiki wa Ufaransa akiwa amelowa majonzi kwa kutoamini macho yake baada ya timu yake kula kichapo cha 4-1.
Ufaransa wanakutana na Italy jumanne ijayo ambapo wote wanawania kijinafasi lakini nafsi yao inategemeana na matokeo ya mchezo kati ya Romania na Uholanzi ambap Romania inashika nafasi ya pili katika kundi hilo, kwani Romania ikiishinda Holand itakuwa na nafasi hiyo hiyo ya pili. Wadatch wameweka historia kwa kuzichapa timu mbili ambazo zilicheza Fainali ya kombe la dunia 2006 kwa jumla ya mabao 7.
Italy yajitutumua kwa Sare
Straika wa Fiorentina Adrian Mutu ndiye aliyefungua mlango kwa kuipachikia Romania goli la kwanza dakika ya 55. Lakini goli hilo lilidumu kwa dakika moja tu waitaliano wakasawazisha kupitia kwa Christian Panucci.
Matokeo ya Droo angalao yamewapunguzia machungu Italy ambao bado wanakidonda cha kichapo cha 3-0 walichochapwa na Holland ambao wanaonyesha makali kwenye kundi hilo la C.
Romania walipata penati dakika 5 kabla ya mchezo kumalizika baada ya Panucci kumchezea madhambi Daniel Niculae ambayo kwa kiwango kikubwa iliwanyong’onyeza Italy na washabiki wao na Romania walimchagua Mutu kupiga penati hiyo ambayo aliipiga kiufundi iende kwenye post lakini kipa Buffon wa Italy aliicheza na kusababisha mayowe toka kwa mashabiki wao ambao walikuwa wameshakata tamaa.
Kwa matokeo haya Italy inatakiwa ishinde mechi yake ijayo na Ufaransa ili waweze kujihakikishia kusonga mbele.
Waitaliano jana walilalamikia maamuzi ya refa wakidai aliwabana sana wao, Refa huyo Mnorwee hasa pale alipokataa goli la Italy kwa kudai mfungaji Luka Toni alikuwa ameotea.. Mpaka mwisho wa mchezo Italy 1 – 1 Romania.
Friday, June 13, 2008
Maneno ya mwisho ya “KUNGWI”
KUMRADHI: Haha habari ndio hiyo!!
Naomba radhi kwa kushinda kuweka habari toka jana usiku hii ni kutokana a sababu ambazo zilikuwa nje ya uwezo wetu. lakini naomba mburudike na Video ya kwake AY inayoitwa Habari ndio hiyo!!
!
Vimwana wa Miss Dar City Centre
Thursday, June 12, 2008
haki miliki yawabana Ze Comedy
Haya wadau mwalionaje hili?
Pata kipande cha Shoo yao hapa:-
Maelfu wajitokeza Kununua Tiketi za Stars na Kameruni
Na Mwananchi
MAELFU ya wapenzi wa soka jijini la Dar es Salaam wamejitokeza kununua tiketi za mechi baina ya Tanzania na Cameroon itakayofanyika kesho, huku polisi wakizuia maandamano yaliyopangwa kufanywa na chama cha siasa cha DP kupinga viingilio.
……………………..
Tiketi hizo zitauzwa kwa viingilio vya Sh 50,000 kwa V.I.P, Sh 40,000 kwa V.I.P B na Sh 20,000, Sh 10,000 na 7,000 kwa mzunguko
……………………………
na vituo vilivyopangwa kwa mauzo ya tiketi hizo ni mgahawa wa Steers, Uwanja wa Zamani wa Taifa, Zizou Fashion, hoteli ya Royal Prince na kituo cha mafuta cha Big Bon cha Kariakoo.
Pia kuna vituo vya Shule ya Sekondari ya Benjamini Mkapa, vituo vya mafuta cha Kobil na Oil Com, hoteli ya Mbezi Beach Park na Wizara ya Miundo Mbinu.
Mwananchi ilishuhudia mistari mirefu ya wapenzi wa soka wakisubiri kununua tiketi hizo zilizokuwa zikitolewa kupitia kwenye magari kuanzia saa 4.00 asubuhi huku kukiwa na ulinzi wa askari polisi wenye silaha.
“Mimi nimeridhika na utaratibu wa uuzwaji wa tiketi kwani umezingatia muda, lakini pia pongezi zangu ni kwa TFF kwa kuongeza idadi ya vituo vya kuuzia tiketi kwani umepunguza adha ya kulundikana sehemu moja kwani mimi nimekuja muda huu na nimeshapata,” alisema shabiki aliyejitambulisha kwa jina la Yassin Adballah.
Mechi hiyo itakuwa ya kuwania tiketi ya kucheza fainali za Kombe la Dunia zitakazofanyika Afrika Kusini na pia itatumika kama michuano ya awali ya Kombe la Mataifa ya Afrika, ambayo fainali zake zitafanyika Angola mwaka 2010.
Wakati mashabiki wakijazana vituoni kutaka tiketi hizo, kamishina msaidizi wa Polisi wa kanda maalumu ya Dar es salaam, Selemani Kova alisema kama DP, inayoongozwa na Mchungaji, Christopher Mtikila kama imekosa kiingilio, iangalie mpira kupitia kwenye luninga na si kufanya maandamano yasiyo rasmi.
Kova aliongeza kuwa endapo mwanachama au mtu yeyote atakaidi amri hiyo ya jeshi la polisi, hatua kali zitachukuliwa dhidi yao.
Sebene la Koffi usipime!!
Gonga chini hapa uone ni kwa nini huwapenda sana hawa wacheza shoo wake, Mopao Mokonzo Sakozy!! Kuna mtu anaitwa Abuu MWenda mpenzi mkubwa wa Koffi na Big Producer Maghambo salute kwenu!!
Felipe Scolari akabidhiwa Mikoba CHELSEA
Kwa sasa kocha Scolari yuko na timu ya Taifa ya Portugal kwenye michezo ya Euro 2008, na hakutarajiwa kuweka bayana mustakabali wake mpaka mwisho wa mashindano.
Chelsea walisema kwenye taarifa yao “Chelsea Football Club inayofuraha kuwajulisha kuwa Luiz Felipe Scolari ndiye atakuwa kocha mpya wa Klabu ya Chelsea mkatabu atakaoanza kuutumikia tangu July 1, 2008. ‘Felipe ana viwango vya hali ya juu. Ni mmoja wa makocha wa renki ya juu kabisa Duniani, akiwa na rekodi nzuri ya Vilabu na Timu mbali mbali za Taifa alizofundisha. atakuja kuungana na kikosi cha wachezaji bora na wenye moyo wa kucheza mpira wenye viwango nafikiri tutakuwa na Combination nzuri.
Ni muda mzuri wa kumtangaza kocha Scolari kwani kwa sasa timu yake ya Portugal inafanya vizuri tuombe Mungu huko mbeleni na hata wachukue Kikombe, Inshallah.
Vilabu vyapigana vikumbo kwa Villa
“Kitakuwa ni kipindi kigumu katika maisha yake kuamua anakazi kubwa lakini ni wakati mzuri kwake kwani thamani yake kwenye soko imeonekana na kila mtu yuko tayari kutoa kitika awe naye” alisema Vah Geuella ambaye ni agent wa wachezaji toka Spain.
Nyota huyo anayechezea Valencia aling’aa kwenye mchezo wa Spain na Russia jumanne ya juzi kwa kuipachikia timu yake magoli 3 kati ya manne ambayo Spain ilishinda.
Vilabu ambavyo vinamnyemelea ni pamoja na Chelsea na Arsenal, pamoja na bingwa wa La Liga Real Madrid na klabu kubwa ya Catalan Barcelona, ni miongoni mwa vilabu vikubwa ambavyo vinaongoza kuisumbua kambi ya Spain na inatazamaiwa huenda Villa akajiunga na mmoja ya vilabu hivi.
Turkey yawafungisha Vilago wenyeji Switzerland
Mchezaji wa Turkey Arda Turan aliwaliza Switzerland katika dakika za majeruhi na kuipatia timu yake ushindi wa mabao 2-1 na kuwafanya wenyeji hao Switzerland kuyaaga mashindano hayo.
Hakan Yakin ndiye aliyefungulia mashambulizi na kupachika bao la kwanza kwa timu yake ya Switzerland kwa bao dakika ya 32 ya mchezo. Switzerland ambao kwa mchezo wa jana walijitahidi washinde lakini bahati haikuwa yao, Mchezaji wa akiba Semih Senturk alisawazisha bao kwa timu ya Turkey na kufanya droo ya moja moja.
Mchezo uliendelea hivyo hadi dakika za mwishoni ambapo umati ulishatarajia mchezo utamalizika hivyo kufumba na kufumbua Arda mchezaji wa Turkey akapachika kimiani goli lapili katika dakika za majeruhi kabisa.
Shuti lake la kulia lilipita ngome ya Swiss na kwenda moja kwa moja kimiani na kuzima nderemo za waswiss ambao walikuwa wakiishangilia timu yao kwa nguvu zote.
Swiss walikuwa na nafasi ya kufunga goli lakini kipa wa Turkey Volkan Demirel kwa kiasi kikubwa aliwakatisha tamaa kwa kuokoa mpira uliopigwa na Yakin hapa na hapa ambao mashabiki walishainuka wakidhani ni goli.
Turkey watakutana na Czech Republic kwenye game ya mwisho ya Kundi A hapo jumapili ilihali n Swiss watakutana na timu isiyofungika Portugal.
Portugal haooo Robo Fainali
Czech Republic 1 – 3 Portugal
Baada ya usshindi wa magoli 3-1 dhidi ya Jamhuri ya Czech hapo jana, na baadaye Switzerland kupoteza mchezo Portugal wamefanikiwa kuingia hatua ya Robo Fainali ya EURO 2008. kimsingi wan kila sababu ya kusherehea hatua hii.
“Sisi ni kati ya Nchi nane bora kisoka katika Ulaya” alisema kocha wa Portogal Luiz Felipe Scolari said. “hatujaridhika tunahitaji zaidi ya hapo, na ninamatumaini makubwa ya kufika huko juu zaidi.”
Kiwango cha Portugal kwenye michuano hii kiko juu na kama wataendelea kucheza kwa kiwango hiki basi lolote laweza kutokea.
Portugal walipata goli la kwanza dakika ya nane ya Mchezo lililofungwa na mchezaji Deco lakini goli hilo lilidumu kwa takriban dakika tisa tu kwani Czech walisawazisha dakika ya 17 kupitia kwa Libor Sionko (17). Mpaka mapumziko magoli yalikuwa droo ya 1-1.
Kipindui cha pili kilianza kwa speed kali huku Portugal wakiongeza mashambulizi langoni mwa Czech huku kukiwa na kosa kosa za hapa na pale na dakika ya 63 huku akicheza kwa kuonana vizuri na Deco Cristiano Ronaldo akafanya alichotarajiwa kufanya kupachika bao la pili kwa timu ya Portugal baada ya kupata pasi toka kwa Deco. Czech ambao walikuwa na kibarua kigumu cha kumlinda Ronaldo jana iliwabidi wafanye kazi ya ziada kwani kijana hakabiki!. Dakika za majeruhi dakika ya 90 mchezaji kipenzi changu Ricardo Quaresma akaipatia timu yake goli la tatu.
Mpaka kipyenga cha mwisho, Portugal 3- 1 Czech.
Wednesday, June 11, 2008
Jalamba
Utambulisho ndoa ya Dotnata
Habari na Picha na Global Publishers
Czech na Portugal Usipime!!
Teddy wa Total Knockout!!
Under Water Wedding
Kelly Rowland naye kutua Bongo
IJUMAA SHOWBIZ!
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kituo cha Televisheni cha MTV, Kelly yupo katika ziara ndefu akizunguka sehemu mbalimbali duniani kwa ajili ya kutimiza majukumu yake kama Balozi wa mfuko wa MTV Staying Alive Foundation.
Mwanamuziki huyo ambaye ni mtunzi na mkali wa kuimba staili ya R&B ni miongoni mwa warembo watatu waliokuwa wakiunda kundi maarufu la Destiny’S Child, kabla hawajaamua kila mmoja kutoka kivyake.
Khadija Kopa kupamba Kimasomaso keshokutwa
Khadija alisema kuwa katika onyesho hilo litajumuisha Wabunifu 10 nao ni ROSE VALENTINE, ASIA IDAROUS, ANGELO MLAKI, MUSTAFA HASSANALI, JAMILA SWAI, FANCISCA SHIRIMA, MONICA LIHAWA , HILDA BANDIO, KHADIJA MWANAMBOKA na Wataonyesha Mavazi ya
SENDOFF
HARUSI
Alisema onyesho la KIMASOMASO limedhaminiwa na Sabuni ya OMO, Kampuni ya simu za mkononi TIGO, Kinywaji cha REDD’S, SHEAR ILLUSIONS, GOLDEN TOUCH SALOON, BIG TV, VISUAL LAB: NEXT LEVEL, LEOPARD MODELLING AGENCY, VAYLE SPRINGS NA RAQEY.COM
Khadija alimaliza kusema kwa kuvitaja vituo vya tiketi kuwa ni: MANYWELE BEAUTY COSMETICS- KINONDONI, CHOCOLATE PRINCESS – MASAKI, SUMMER MIX FASHION – NAMANGA SHEAR ILLUSIONS – MILLENNIUM TOWERS.
Temptation kwa Jicho la ZEZE
Eto’o, Song, Njitap watua Dar
Na Majira
Timu ya Kameruni jana iliwasili nchini ikiwa na nyota wake wote tayari kuikabili timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ katika mchezo wa michuano ya kutafuta tiketi ya kufuzu fainali za Kombe Dunia zitakazofanyika Afrika Kusini mwaka 2010 na Kombe la Mataifa ya Afrika nchini Angola uliopangwa kufanyika Jumamosi kwenye Uwanja Mpya wa Taifa, Dar es Salaam.
Kameruni iliwasili jana alasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimul Nyerere, Dar es Salaam ikiwa na kikosi cha wachezaji 20 wakiwemo Samuel Eto’o anayecheza Bacelona ya Hispania, Geremi Njitap na nahodha Rigobert Song.
Timu hiyo baada ya kutoka nje ya Uwanja wa Ndege ilikwenda moja kwa moja kwenye gari waliloandaliawa huku Eto’o na Kocha Mkuu wa kikosi hicho, Pfister Otto wakigoma kuzungumza na waandishi wa habari.
Song beki wa kati mwenye nguvu, alisema wamejiandaa vizuri kuikabili Stars ingawa hawana taarifa kuhusu uwezo wa kikosi hicho na kuongeza kuwa anatarajiwa pambano hilo litakuwa gumu.
Naye Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ Marcio Maximo amekifananisha kikosi hicho na gari ya kubeba abiria (daladala) ambayo haiogopi kugongana na gari ya kifahari.
Akizungumza Dar es Salaam jana, Maximo alisema timu yake itakuwa daladala itakapovaana na Kameruni katika mchezo wa kimataifa wa kuwania kufuzu fainali za Kombe la Dunia nchini Afrika Kusini mwaka 2010 na Mataifa ya Afrika yaliyopangwa kufanyika Angola.
Maximo alisema Stars inateremka uwanjani huku ikijua kuwa inavaana na kigogo cha mchezo huo Afrika ambacho kinaundwa na nyota wanaotamba na klabu kubwa duniani hatua ambayo anafananisha wachezaji wake (daladala) na gari la kifahari.
Alisema hata hivyo amewaandaa kikamilifu wachezaji wake kucheza kufa au kupona katika mchezo huo na amewaambia wasiogope ukubwa wa majina ya nyota wa Kameruni na wacheze mpira.
Maximo alisema katika mchezo huo anatarajia kuwatumia wachezaji wake wawili wa kiungo waliokuwa majeruhi, Mrisho Ngassa na Abdi Kassim ambao wamepona. Wachezaji hao walikosa michezo miwili ya Stars ilipomenyana na Mauritius na Cape Verde.
Maximo alisema ana imani wachezaji hao watakuwa msaada mkubwa katika mchezo huo na kuongeza kutokana na uwezo wao uwanjani ambapo Kassim anasifika kwa mashuti makali wakati Ngassa ni mahiri kwa chenga za maudhi dhidi ya mabeki wa wapinzani wao.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mohamed Enterprises, Mohamed Dewji amesema Kameruni inafungika licha ya kuundwa na wachezaji nyota ambapo amewataka Watanzania kujitokeza kwa wingi uwanjani kuishangilia Stars katika mchezo huo.
Akizungumza Dar es Salaam jana, Dewji alisema Watanzania wanatakiwa kuipa nguvu Stars katika mchezo huo bila kujali majina ya wachezaji wa Kameruni ambao wengi wao ni maarufu.
Alisema hakuna sababu ya mashabiki wa soka kwenda uwanjani vichwa chini wakiihofia timu hiyo licha ya Stars kufanya vibaya katika michezo miwili ya awali kwa kutoka sare 1-1 na Mauritius kabla ya kufungwa bao 1-0 Cape Verde.
Alisema Stars ilipocheza na Senegal na Burkinafaso ikiwa ugenini wachezaji wa kikosi hicho walicheza kwa nguvu dakika zote za mchezo bila kuangalia ukubwa wa majina ya nyota wao wanaocheza Ulaya.
Mwaka jana Dewji alitumia zaidi ya sh. milioni 100 katika mkataba wake na Stars ambazo zilitumika kwa ajili ya shughuli za uendeshaji wa timu hiyo ikiwemo kambi na mambo mengine.
Kameruni inaongoza kundi A ikiwa na pointi 6 baada ya kushinda michezo miwili dhidi ya Cape Verde mabao 2-0 kabla ya kuibanjua Mauritius 3-0. Inafuatiwa na Cape Verde yenye pointi 3,Tanzania inashika nafasi ya tatu na Mauritius inakamata mkia.
“Ukiwa Makka basi ishi kama watu wa Makka…”
Faida ya Magoli kwa KAKA
Spain yaisambaratisha Russia 4 – 1
David Villa ndiye aliyekuwa Stearing wa mchezo wa jana baada ya kufanya mauaji kwenye mashindano ya mwaka huu ya Euro 2008 kwa kupachika magoli 3 kati ya manne wakati wa mchezo kati ya Spain dhidi ya Rusia ambao ulimalizika kwa 4-1.
“Magoli matatu kwenye mechi moja tena ya ufunguzi ni mwanzo mzuri kwa kweli aliesema Vila mara baada ya mchezo wa jana. Hii ni mara ya kwanza kwenye mashindano haya kufungwa mabao matatu na mtu mmoja mara moja tangu mwaka 2000ambapo mchezaji Patric Kluivert wa Netherland alipoifungia timu yake.Tumeanza vizuri ingawaje kuna mechi zinakuja lakini mwanzo utawaogopesha hata wapinzania wetu aliongeza Villa. Spain itakuja kukutana na Greece na Sweden kwenye mechi za kundi hilo la D. ambapo inategemea kukutana na kaupingamizi toka kwa Sweden ambao walionyesha mchezo mzuri jana.
Ni katika kundi hili rafiki yangu Tanzania Dreams anasema mshindi atatoka, sijui naona mechi zinatabiri kwa bingwa Greece kuonja kichapo. Goli moja la Spain lilifungwa na Mchezaji wa ArsenalFrancesc Fàbregas Soler au Cesc Fabregas ambao kwa pamoja walitengeneza karamu ya magoli.
Bao pekee la Russia lilifungwa na Roman Pavlyuchenko.
Sweden yaikomalia Greece 2-0
<>
Timu ya Greece ilikuwa kama imechanganyikiwa ngome yao kutokana na mchakamchaka wa jana ambapo Sweden walionyesha mchezo mzuri na kwa kiasi fulani kuumudu mchezo.
Dakika tano baada ya goli la kwanza Sweden walipata goli la Pili kutoka kwake Petter Hansson baada ya mabeki wa Greece kujichanganya. Mchezo huo wa kwanza ulikuwa muhimu kwa timu zote kwani unajiweka kwenye nafasi nzuri kipindi chwa mwanzo, Kwa mchezo walioonyesha Greece jana wanatakiwa kufanya kazi ya ziada ili kuendelea kuwepo kwani kazi bado Pevu mbeleni.
Tuesday, June 10, 2008
Kilichowaponza Taifa Stars
Picha juu ni vimwana ambao ni washangiliaji wa timu ya Cape Verde wakifanya vitu vyao juzi kwenye mpambano wao na Taifa Stars nakuwalamba 1-0.kufungwa kwa Taifa Stars kumesababisha Baadhi ya Mashabiki kukata tamaa na hata kupoteza matumaini ya mchezo ujao dhidi ya Cameroon.
Stars itapambana na Cameroon katika mchezo wa tatu wa michuano hiyo utakaofanyika Jumamosi kwenye Uwanja Mkuu waTanzania jijini Dar es Salaam.Picha hizi kutoka Cape Verde kwa msaada mkubwa wa Mdau Saleh Ally. (Kaka Robert Mwafrika wa Azam ananiambia Taifa Stars walikuwa wakikodolea macho vimwana hahahahaa)
Wanyange wa Miss Tanzania UK 2008
KAseja: Nimesign Yanga lakini nina Mkataba na Simba!!
Kauli hiyo ni mara ya kwanza kwa kipa huyo nambari moja kuitoa hadharani baada ya kusaini mkataba wa mwaka mmoja kuwatumikia mabingwa hao wa mpira wa miguu Tanzania Bara.
Akizungumza Dar es Salaam jana, Kaseja alisema amesaini mkataba na uongozi wa klabu ya Yanga huku akijua mkataba wake na Simba unamalizika mwakani.
Kaseja alisema kabla ya kusaini mkataba mpya na uongozi wa Yanga aliwaonesha kopi ya mkataba wake wa Simba lakini uongozi wa klabu hiyo ya Jangwani ulimtaka asaini na wao wangefikia muafaka na wenzao wa Simba.
Ufaransa yashindwa kutamba
Hadi mwisho wa mchezo Ufaransa 0 – 0 Romania.
Italy Mbendembende kwa Netherlands
Mzee anacheza leo!!
Sylvie van der Sar, Mke wa golikipa wa Dutch Edwin van der Sar, akisubiri kuanza kwa mchezo wa Kundi C wa mashindano ya Euro 2008 kati ya Netherlands vs. Italy jana June 9, 2008 katika uwanja wa stade de Suisse huko Bern.
Monday, June 9, 2008
YANGA yamsajili Kaseka kwa USD 30,000
*Friend’s of Simba wachanga ‘vijisenti’ kumkomboa,waning’inia
*Asaini mkataba unaoeleza atakuwa kipa wa kwanza Yanga
Na Majira
KIPA mahiri nchini Juma Kaseja wa Simba ya jijini Dar es Salaam, jana alisaini fomu za mkataba kwa ajili ya kuichezea Yanga pia ya jijini katika michuano ya kimataifa mwakani, pamoja na Ligi Kuu Tanzania Bara.
“Tumemalizana naye ni fedha ambayo kila mwenye akili timamu hawezi kuiacha, hata kama ungekuwa wewe, huwezi kuacha kusajili, sasa ni Kaseja wa Yanga si Simba tena.
“Tunasajili kwa akili, hatukurupuki, tunajua tunachokifanya, Yanga itatisha, kijana amefika mahali alipokuwa akipataka,” kilieleza chanzo chetu ndani ya Yanga na kudokeza kuwa kwa jana tu kipa huyo alikabidhiwa dola 30,000.
Chanzo hicho kilieleza kuwa awali Kaseja ilikuwa asajiliwe leo, lakini kutokana na habari hizo kuvuja kwenye gazeti hili jana, pamoja na gazeti dada la Spoti Starehe, suala hili lilifanyika jana katika moja ya ofisi za mdau nyeti ndani ya Yanga.
Alisema licha ya juzi kutokuwepo fomu za usajili za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), lakini pia suala la mkataba wa kipa huyo na Simba lilikuwa likisumbua, ambapo mkataba huo unaonesha unamalizika mwakani.
Hata hivyo mkataba huo wa Kaseja unaeleza kuwa kila mwaka kutakuwa na mazungumzo kuhusiana na usajili na kama wakishindwa kuafikiana, yupo huru kutafuta timu nyingine, hivyo kama Simba watahitaji watalazimika kuilipa Yanga kiasi alichopewa kipa huyo pamoja na ahadi nyingine nyingi, ambazo utekelezaji wake tayari umeanza.
Gazeti la majira lilimpata kipa huyo ambaye alikiri kusaini fomu za Yanga na kusema ana imani kazi kubwa itafanyika kwenye ligi na michuano ya kimataifa.
“Elimu yangu ni mpira, maisha yangu ni mpira, nimeamua kusaini Yanga na nina imani Mungu ataniongoza nifanye vizuri, wamenipa kiasi kizuri sana, nami nitawapa raha uwanjani.
“Mimi si wa kwanza kucheza Simba kisha nikaenda Yanga, au kucheza Yanga nikahamia Simba, naomba mashabiki wa soka waelewe hilo,” alisema Kaseja.
Alikiri kusaini mkataba wa dola 30,000 na kwamba ni wa mwaka mmoja, ambapo moja ya vipengele vilivyopo ni kuwa yeye ndiye atakuwa kipa wa kwanza wa timu hiyo, hali itakayomfanya kipa wa sasa Ivo Mapunda kukaa benchi, au kutafuta timu nyingine.
Kaseja alisema kabla ya kufikia uamuzi huo aliwasiliana na baadhi ya viongozi wa Simba na kuwajulisha kuhusiana na dau la Yanga, ambao walimjulisha hawana uwezo kulifikia na kwamba yupo huru kuondoka.
“Niliwaeleza kiasi Yanga walichoniahidi wakanambia hawawezi kunipa, pia wakanipa baraka kuwa hela haikataliwi, nikasaini Yanga mkataba wa mwaka mmoja, ambao utahusu ligi ya 2008/2009,” alitamba kipa huyo.
Awali jana asubuhi, mmoja kati ya wanazi wa Simba wanaounda kundi la vibopa wa timu hiyo lijulikanalo kama Friend’s of Simba alipiga simu kwenye ofisi za gazeti hili akielezea kuhusiana na habari zilizoandikwa kwamba Yanga imemficha Kaseja.
“Si kweli Yanga haijamficha, ila mnataka kumsaidia Kaseja apewe dau kubwa Simba, hilo tunalijua,” alilalamika mdau huyo ambaye jina tunamhifadhi.
Hata hivyo alipoelezwa kwa undani kuhusiana na habari hizo, alionekana kushangaa na kuahidi angepiga mchana jana, ili asaidiwe kuelezwa alipo kipa huyo, kwani kulingana na maelezo aliyopewa na gazeti hili aliamini kweli Kaseja anaenda Yanga.
Kigogo huyo alipiga simu baadaye jioni jana na kusema tayari Friend’s of Simba walipata uhakika wa taarifa hizo na walichanga kiasi cha sh. milioni 20 ili wampe Kaseja, lakini alipoelezwa fedha aliyopewa ni nyingi zaidi aling’aka: “Ha. Huyu mtoto sisi tunamsaidia sana, lakini anatusaliti ngoja aende (anasonya), sisi hela hiyo hatuwezi kumpa.
“Lakini nasi tutalipa kisasi, hatuwezi kukubali kufa kikondoo, mwambie kila la kheri, kwanza hata Taifa Stars haitwi,” alilalama mdau huyo kwa kauli ya mfa maji, ambaye haishi kutapatapa.
Katibu Mwenezi wa Simba, Said Rubeya alipoulizwa jana kuhusiana na taarifa hizo alisema anachojua Kaseja ni kipa halali wa Simba.
“Habari hizi zimeandikwa katika gazeti lenu, hivyo mwandishi aliyeandika anajua zaidi, si mimi, lakini ninachojua fomu za usajili bado hazijatoka, Kaseja ni wa Simba,” alisema Rubeya.
Naye Katibu Mwenezi wa Yanga, Francis Lucas alipoulizwa alidai habari zilizoandikwa hazina ukweli na zina nia ya kumpigia debe Kaseja.
“Hatujazungumza naye, wala hakuna nia ya kumsaini Kaseja, haya mambo wala hatuyatambui,” alidai Lucas.
Angeline Jolie na Jack Black
Kwa akina Dada tu
Chelsea yairuhusu AC Milan kufanya mazungumzo na Drogba
Chelsea wameturuhusu kufanya mazunguzmo na Drogba na tunatarajia mazungumzo yatafikia mafanikio mazuri alisema Adriano Galliani alipokuwa akiongea na gazeti la michezo la La Gazzetta dello Sport. Kwa sasa wasiwasi wetu uko kwa Shevchenko. Chelsea wanasema huyu hauzwi hii itakuwa imetunyima combination nzuri ambayo tunataka kuifanya aliongeza.
Galliani alisema kuwa Timu yake ambayo ni mabingwa wa Ulaya mara 7 wameanza kufanya mazungumzo na nyota mwingine toka klabu ya Barcelona Samuel Eto’o. Alisema Mcameruni huyo alikuwa anawaniwa na klabu nyingine ila wamempatia ofa yao kupitia kwa ajenti wake wanatumai majibu yatakuwa mazuri, vile vile imefahamika kubwa klabu hiyo pia ilifanya mazungumzo ya agenti wa Adebayo ingawa habari zinasema Arsenal hawako tayari kumuuza mchezaji huyo. Gillian alisema hawa wawili ni mapema kusema chochote ila maongezi yakifanyika tutatoa taarifa.
Croatia 1 – 0 Austria,
Kipindi cha pili kilikuwa ni azamu ya Austria walifanikiwa kwa kiasi fulani kuumiliki mchezo lakini jitihada za milki yao hazikuzaa matunda.
Luka Modric aliifungia Croatia kwa njia ya Penati katika dakika ya nne tu ya mchezo.
“Goli la mwanzoni mwa mchezo limetusaidia sana alisema kocha wa Croatia, lilitufanya kuwa na uhakika ama wa kuongeza goli au kulinda hayo matokeo ya moja bila, Tulimiliki kipindi cha kwanza lakini kipindi cha pili kiligeuka, tuliwapa nafasi nyingi za free kick ila Mungu yuko pamoja na jitihada zetu, alimalizia kusema kocha huyo. Mpaka kipyenga cha mwisho magoli ni moja kwa Bila.
Germany 2-0 Poland
Pichani Lukas Podolski (L) akipachika mpira kimiani wakati wa mashindano ya Euro 2008 kundi B dhidi ya Poland jana June 8, 2008 huko Woerthersee stadium, Klagenfurt, Austria. German walishinda 2-0.
Sunday, June 8, 2008
WC 2010 qual. – Asia (Group 1) | |||
02:06 | June 8 | ||
FT | Iraq | 1 – 0 | Australia |
WC 2010 qual. – Asia (Group 2) | |||
03:06 | June 8 | ||
FT | Oman | 1 – 1 | Japan |
FT | Bahrain | 1 – 1 | Thailand |
WC 2010 qual. – Asia (Group 3) | |||
03:06 | June 8 | ||
FT | Jordan | 0 – 1 | Korea Republic |
WC 2010 qual. – Asia (Group 4) | |||
02:06 | June 8 | ||
FT | Uzbekistan | 1 – 0 | Singapore |
FT | Lebanon | 1 – 2 | Saudi Arabia |
DSTV na EURO
Misri, Aljeria zatisha Afrika
Katika mechi hiyo mabingwa hao wa Afrika walianza mechi hiyo kwa kasi lakini iliwabidi kusubiri hadi dakika 40 ilipopata bao mfungaji akiwa Amr Zaki.
Misri ambao walikuwa wageni waliongeza bao la pili dakika 47 , mfungaji akiwa Hosni Abd Rabo, kabla ya nahodha wa timu hiyo, Ahmed Hassan kupachika la tatu dakika 54 na Ahmed Abdelmalik kufunga la nne muda mfupi baadaye.
Mechi nyingine za kundi hilo la 12 zinatarajiwa kuendelea leo, wakati timu ya Taifa ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo DRC itakapoikaribisha Malawi mjini Kinshasa.
Mbali na mechi hiyo pia juzi kulikuwepo na mechi nyingine ya Kundi la 6 kati ya Algeria na Liberia ambapo katika mechi hiyo iliyofanyika mjini Blida , Algeria waliibuka na ushindi wa bao 3-0
Yanga wamemficha Kaseja
Habari za uhakika kutoka ndani ya Yanga zilieleza kuwa tangu juzi kipa huyo amekuwa katika mazungumzo na baadhi ya viongozi wa Yanga (majina tunayo) kuhusiana na kusaini fomu hizo.
Jana mchana kipa huyo alionekana katika ofisi ya mmoja wa wadau wakubwa wa Yanga, ambapo haikuwa rahisi kwa watu wa kawaida kumtambua.
“Ni kweli tupo na Juma, amezungumza na watu muhimu ndani ya Yanga, ni jukumu letu kuhakikisha tunamalizana naye,” kilieleza chanzo cha uhakika ndani ya Yanga.
Chanzo hicho kilieleza kuwa kwa asilimia 80 Kaseja wamemalizana naye Yanga, lakini kuna fomu za mkataba kutoka Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), ambazo hazikuwepo, hivyo atazisaini wakati wowote.
“Kilichopo sasa tumemuweka chini ya himaya yetu hadi hapo atakaposaini hizo fomu, hata namba ya simu tumembadilishia,” kilisema chanzo hicho cha uhakika.
Hatua ya kumchukua kipa huyo aliyefungwa mara moja na Yanga, tangu ajiunge Simba karibu miaka saba iliyopita, inaonekana ni Yanga kutaka kukomoa baada ya kushindwa kuwasaini wachezaji wa Simba Henry Joseph na Kelvin Yondani. Wachezaji hao walisaini mkataba wa kuchezea tena timu hiyo wiki hii.
Katibu Mwenezi wa Yanga, Francis Lucas alipoulizwa jana kuhusiana na suala hilo alisema hakuwa na taarifa hizo kwa wakati huo. “Sina taarifa hizo, sidhani kama tunaweza kumsaini, si katika wachezaji wanaotajwa kusajiliwa Yanga. Lakini pia wachezaji wapo Simba tu?
“Hili la kumficha pia silijui, lakini hiki ni kipindi cha usajili mengi utayasikia, ila sisi Yanga usajili anafanya kocha, si viongozi,” alisema Lucas.
Gazeti hili (majira) lilijaribu kuwasiliana na kipa huyo kwa namba yake ya kawaida ambayo haikuwa hewani, hadi baadaye kipa huyo alipatikana kwa namba yake mpya na alipoulizwa alishtuka kwa kiasi kikubwa.
“Hapana mimi nipo na mambo yangu, nimebadili namba kwa masuala yangu binafsi, ambayo sidhani kama ni habari, suala la mimi kutakiwa si jambo la ajabu, mimi ni mchezaji, hivyo aliyekupa taarifa hiyo ndio akueleze kwa kirefu, maana hata timu za mikoani pia zinanitaka,” alisema Kaseja.
Alipobanwa zaidi ikiwemo kutajiwa namba ya gari iliyomchukua pamoja na muda alionekana na viongozi wa Yanga pamoja na mahali alipowekwa kwa sasa alijibu: “Naomba tuyaache.”
Makamuzi ya Ali Kiba Milton
Kwa picha zaidi tembelea Haki Ngowi
Tanzania Vipaji vingi basi tuu
Wamkumbuka huyu?
Njaa kipimo cha Akili
Cape Verde yaisononesha Taifa Stars
Pepe aipeperusha Portugal
Switzerland yashangazwa nyumbani na Czech.
Switzerland ilipigwa na mshangao baada ya kushindwa mbele ya mashabik wao mjini Basle Switzerland katika mechi ya kwanza la kombe la Bara Ulaya Euro 2008.Mchezaji Vaclav Sverkos’ aliengia katika kipindi cha pili na kuifungia Czech.Switzerland walicheza mechi nzuri na kuhatarisha lango la Czech lakini hatimaye kushindwa,timu hiyo inaongozwa na Senderos wa Arsenal,mchezaji mrefu kwa wote duniani Jan Koller wa Borussia Dortmund na wengineo ilhali Czech inaongozwa na Petr Cech wa Chelsea,Rosicky wa Arsenal vilevile wakiwemo wengine.
Saturday, June 7, 2008
Kenya yaiburuza Guinea 2-0.
Mbwembwe za Mashabiki mitaani
Mrithi wa Richa Adhia Dar Indian Ocean keshapatina
Chris Tucker adata na Maajabu
Mwigizaji maarufu na mcheza sinema kutoka Marekani,Chris Tucker akiwaimbia wimbo wa mwanamuziki Michael Jackson,Wamasai aliowakuta katika Hifadhi ya Ngorongoro juzi.
Logo, Wallpaper, Ring Tones na Video Ipod za EURO 08
Basi Gonga hapa ujinafasi
Tutashinda bila Viera: Makelele
Viera ambaye aliumia mazoezini wiki iliyopita hatocheza kwenye mechi ya ufunguzi wa Group C dhidi ya Romania hapo Jumatatu mchezo utakaochezwa Zurich. “Tunategemea Viera atakuwa fit kwa ajili ya mechi zilizobaki kwani tunamuhitaji kwenye timu yetu, na nadhani Mungu atabariki apone haraka”, alimalizia Makelele.
Nionavyo mimi
Ninachoona mimi ni kuwa tofauti pekee ambayo timu yetu ya Taifa inayo ni support. Kwa sasa angalao timu ina support licha tu ya serikali bali pia toka kwa makampuni makubwa kama Serengeti Breweries na NMB na mengineyo. Huu ni wakati mzuri kwa Timu yetu kufanya vizuri kama tuna Kocha Mzuri na support ipo ya kutosha kwa nini tusishinde basi?
Fikiria jinsi watu walivyohamasika kwa timu yao ya Taifa kipindi tunagombea kucheza CAN Ghana!! Nafikiri kwa kiasi kikubwa tumeona mabadiliko ingawa ni kweli mabadiliko hayawezi kuja mara moja. kwa mfumo wetu wa Soka wa kukusanya wachezaji dakika za mwisho hatuwezi kuona mabadiliko kwa muda mfupi kamwe. Ni lazima tuwe na Program ya muda mrefu na muda mfupi, muda mrefu ni kwa Serikali kuimarisha michezo kuanzia ngazi ya shule za msingi, na kuimarisha mashindano kama ya Taifa Cup.
Tujaribu kuangalia mechi za kirafiki za kimataifa, Taifa Stars imecheza michezo tisa ya kimataifa ya kirafiki chini ya Kocha Mkuu Mbrazili Marcio Maximo tangu aanze kibarua hicho karibu miezi 19 iliyopita.
Katika michezo hiyo Taifa Stars imeshinda mitatu dhidi ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo, Uganda na Zambia na kutoka sare mara nne dhidi ya Kenya, Angola, Zambia, Uganda na juzi sare ya Malawi ya 1-1. na kufungwa na Yemen. Tukiangalia na tulikotoka haya tunayaita mafanikio.
Kimsingi ninachotaka kusema ni kuwa Kwangu mimi Maximo akipewa muda anaweza kuleta mabadiliko kwani ni mapema mno ikumbukwe kuwa anachokifanya Maximo ni kukutanishwa na wachezaji wanaotoka kwenye Vilabu vyao na kazi yake ni kuwafanya hawa wacheze kama Timu, sio kumfundisha mtu jinsi ya kutoa pasi hiy anafundishwa kwenye club yake huko. Ni lazima Club ziwe na mbinu mpya za ufundishaji, huko ndio soka linapoanzia. kwani vilabu ndio vinalisha Timu ya Taifa wachezaji, Pia kurudishwa kwa michezo ya Taifa Cup itakuwa Chachu ya mabadiliko kisoko kwani huko ndiko vipaji vinaanzia.
Friday, June 6, 2008
Salamu Toka kwa Kaka Chibiriti Italy
Habari yako Mkuu,
Nimekuwa nikifuatilia sana blog yako, kwakweli ni nzuri sana kwa sisi wapenda michezo, hasa soka mimi umenifikisha penyewe kabisa. Kila siku nilikuwa nikifikiri kukushukuru kwa kazi nzuri unayo ifanya ila mda ulikua ni mdogo, leo nimepata huu mda ninasema asante sana kwa habari zako, safi sana.
Ninakutakia kazi njema na mafanikio mema kila siku.
Ni mimi Baraka Franco Chibiriti
kutoka hapa Cesena-Italy.
Bila Hiyana nami nazipokea, nashukuru Kaka, Tuko Pamoja.
Pius
Je wajua?
Gonga Kwenye Timu Husika upate Data kuanzia Mechi za Kwanza za Matanange huu mpaka Hapo ilipo.
|
|
|
|
Kila La heri
Dj Bonny Luv wa Mawingu Studio
Sebene la Werrason Usipime!!
Simba yaipiga bao Yanga
Uongozi wa Klabu ya Yanga umeanza kuchanganyikiwa baada ya wapinzani wao Simba juzi kufanya kufuru ya usajili kwa kuwasajili nyota wake wote waliokuwa wakitakiwa na timu hiyo.
Baada ya Simba kufanya hivyo na jana kutangazwa kuwa wanawania kumsajili mchezaji wao Mrisho Ngasa kufuatia baba yake mzazi kuamuru mwanae aichezee Simba, viongozi wa klabu hiyo wamekuwa wakikutana mara kwa mara kujadiliana juu ya suala la usajili.
Habari za kuaminika kutoka ndani ya uongozi wa klabu hiyo zimeeleza kuwa imekuwa ni suala la kawaida kwa viongozi wa Yanga kukutana zaidi ya mara sita kwa siku.
IPP Media
Miss Tanga hiyoooo Kupekecha na Akudo mpaka Lyamba!!
Miss Tanga2007, Miss Tanzania Kanda ya Kaskazini, Redds fashion Ambassador Victoria MartinAmbaye amepata mikataba na kampuni za Modelling za South Afika. Hivi karibuni alikwenda South Afica kuangalia soko la uanamitindo na tayari kampuni mbili zimevutiwa naye na kumpa mapendekezo yao. Kampuni hizo ni O Model na EXTRA. Soma hapa zaidi
Simba yawatema Athuman Machupa, Joseph Kaniki na Yahya Akilimali.
Habari za uhakika kutoka ndani ya uongozi wa klabu hiyo, ziliwataja wachezaji wengine walioachwa katika kikosi hicho kuwa ni Athuman Machupa, Joseph Kaniki na Yahya Akilimali.
Chanzo hicho kiliwataja wachezaji wengine kuwa ni Said Sued, Soud Abdallah na Moses Odhiambo, ambaye amehamika APR ya Rwanda.
Hata hivyo chanzo hicho kilidai kuwa Machupa, Kaniki na Sued wameomba kuachwa kutokana na kutaka kwenda kucheza mpira wa kulipwa nchi za nje.
Kutokana na hatua hiyo ya kuacha wachezaji hao, chanzo chetu kilieleza kuwa hivi sasa Kamati ya Usajili ya Simba inahaha kukamilisha usajili kwa wachezaji 10 wapya kwa ajili ya msimu ujao.
“Simba imepanga kusajili wachezaji kumi wapya, kwa kuwa ilikuwa na jumla ya wachezaji 28 waliosajiliwa msimu uliopita, hivyo Kamati ya Usajili imepewa jukumu la kuhakikisha inasajili wachezaji imara,” kilieleza chanzo.
Tayari kamati hiyo imeshaanza kazi hiyo kwa kuwarudisha kundini wachezaji Henry Joseph na Kelvin Yondan ambao walikuwa wananyemelewa na Yanga, huku ikiwasajili chipukizi, Juma Jabu na Jabir Aziz.
Miss Dar City Centre atatoka hapa
Warembo wa Katikati ya jiji hawa hapa!
Mitindo House na Kimasomaso
Taifa Stars yaenda Cape Verde
Stars, iliyopoteza pointi mbili katika mechi yake ya kwanza ya michuano ya awali ya Kombe la Dunia ilipolazimishwa kwenda sare ya bao 1-1 na Mauritius nyumbani, itavaana na Cape Verde Jumamosi.
Maximo alisema Ngassa bado hajapona vizuri na kwamba Abdi Kassim bado anahitaji muda zaidi wa kujiweka ‘fiti’ kabla ya kurudi uwanjani kikamilifu baada ya kutatizwa na nyama za misuli.
“Wataendelea na mazoezi hapa hapa kujiandaa kwa mechi ya Cameroon,” alisema Maximo.
Hata hivyo, kocha huyo Mbrazili alionekana kuwaamini wachezaji wengine waliosalia, aliposema kuwa wanaenda Cape Verde kupambana.
“Tulicheza na Mauritius, watu wakatupa nafasi kubwa ya kushinda lakini matokeo yakawa sare. Hii ndio itakavyotokea kwa Cape Verde. Watu wanasema Cape Verde ina timu nzuri, lakini na sisi tunakwenda kuwashangaza kama tulivyoshangazwa,” alisema Maximo.
Mziki wa EURO 2008
U-Modo una karaha zake
Ili uwe “Modo” inabidi uwe na vigezo fulani kama Figure, Urefu, na kikubwa kulitawala jukwaa ikiwa ni pamoja na mwendo, Angalia jinsi “Modo” huyu alipopata aibu ya mwaka jukwaani na kuwaacha hoi mpaka watangazaji wakifa kwa kicheko.
Bonyeza Player
Thursday, June 5, 2008
Ronaldo aweka wazi, Siku zake zahesabika Manchester
HATIMAYE kiungo nyota na machachari wa klabu ya Manchester United, Christiano Ronaldo amesema ataihama klabu hiyo mwakani.
Kauli ya nyota huyo huenda ikatonesha donda la Kocha Mkuu wa United, Sir Alex Ferguson ambaye amekuwa hapati usingizi baada ya fununu kuvuja kuwa Ronaldo alikuwa na mpango wa kujiunga Real Madrid ya Hispania msimu ujao kabla ya kuvunja jaribio hilo.
Mwanzo mwa wiki hii, Ronaldo alimhakikishia Fergie atabaki Old Trafford kutokana na mafanikio aliyopata chini yake tngu alipojiunga na klabu hiyo mwaka 2003 akitokea Sporting Lisbon.
Kiungo huyo wa pembeni aliyeongoza kwa ufungaji mabao msimu huu katika Ligi Kuu England akipachika wavuni mabao 30 na 11 ya kimataifa, alisema kama ameshindwa kuhama msimu ujao basi itakuwa mwakani.
Ronaldo na wakala wake, Jorge Mendes wamefikia muafaka wa kuangalia ofa za klabu nyingine kutoka nje ya England. Real Madrid, Barcelona, AC Milan na Inter Milan zinammezea mate nyota huyo.
Ronaldo aliweka bayana kuwa kutwaa ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Ulaya na Kombe la Ligi Kuu England ni mafanikio makubwa na sasa wakati umefika wa kuondoka kwenda Real Madrid.
TEARS OF A CLOWN
Kujifungua kwa Angeline Julie bado ni siri kubwa
Brazil yajipigia “debe” Olympic 2016
Amanda
Safari ya Ndoa ya Salma Msangi
Salma Msangi mtangazaji mahiri wa vipindi vya burudani Channel Ten hivi karibuni alifanyiwa sherehe ya Kitchen Party (sijui kiswahili chake tusaidiane) katika maandalizi ya awali ya Kufunga ndoa, Serehe hii ilifanyika katika ukumbi wa Water Front na ilinogeshwa na Malkia wa Mipasho Khadija Kopa na “Pembe” ilikuwa Live. Vazi lake limebuniwa na Asia Idarusi, Safari ya kuolewa inaanza na Kitchen Party, Send Off, Ndoa na baadaye Harus i duh!! si mchezo, Kila la heri dadaa, Kwa picha zaidi za sherehe hii na mengineyo Muone Mamaa Zeze hapa
Wednesday, June 4, 2008
Ali Kiba ndani ya Milton
WWW.BONGOUK.COM
Cannavaro kuikosa UEFA – EURO 2008
Msiba wa Mama Mere Malou na Zadio Kongolo
Kuna Post inayosema Zadio Kongolo shabiki namba mojawa Wenge BCBG,
Hii ndio “starehe” ya burudani, Big Producer Maghambo umesomeka.
Nastaafu 2010: Fergie
Feruson aliweka wazi uamuzi wake huo jana alipokuwa akihojiwa kwenye mahojiano na Sir David Frost. Ferguson ataondoka huku akiwa na mafanikio makubwa na timu yake hiyo ya Manchester United kwa kipindi cha zaidi ya miongo miwili alichokaa na timu hiyo.
Aliongelea mambo mengi ikiwa ni pamoja na urafiki wake na Tony Blair na Gordon Brown pia aliongelea umuhimu kwa makocha na wachezaji kuwa na aliyoiita”njaa” ya ushindi.
“mchezaji mwenye kujituma ambaye timu ikishindwa anaumia huyo ndio napenda zaidi, pia nampenda mchezaji mwenye njaa ya magoli, njaa ya ushindi, hapo atafanya kila linalowezekana kimchezo timu ishinde, ndio kitu nawaambia kila siku wachezaji wangu. Hii ni changamoto kwa uongozi wa timu ya Manchester kwani ni kibarua kingine kutafuta mtu mwenye uwezo sawa na Ferguson.
UEFA – EURO 2008 Maandalizi ya timu moto!
Tuesday, June 3, 2008
WANAITWA ‘ASHIERS’
Kwa Habari za Nyumbani za Burudani na mitindo tembelea 8020 Yuko Juu!!
Bingwa wa “Atalaku” kusakwa, Wadhamini ni Afrika Bambataa
Mpaka sasa tayari marapa wamesha jaza fomu na kuanza kujitapa katika kipindi hiki kila mmoja akijiona yeye ni bora kuliko mwezie lakini ukweli utajulikana tu nani atatwaa taji la ufamle wa kurap katika muziki wa dance hapa nchini.
Akithibitisha hilo malkia wa bambataa ambae pia ni brand manager wa Nite X-Press amesema kuwa maandalizi yanaenda vyema na kuwa tayari baadi ya marapa wamesha jaza fomu za kukubali kushiriki katika kinyanganyiro hicho.
Mashindanpo haya yanataraji kuwa ya awamu 3 ambapo awamu ya kwanza ni ya utambulisho , awamu ya pili itakuwa ni ya kupiga live na mashabiki ndio watakao kuwa majaji na hatimae fainali.
Hii ni changamoto kwa vijana ambao tunasema ni kizazi kipya cha dance hapa Tanzania nia na lengo letu ni kuhakikisha marapa na wao kama sehemu ya ladha na burudani wanatambulika wanaheshimika na kudhaminiwa popote pale kwakuwa bila wao pia muziki unakuwa hauja kamilika. alisema Bi Sofia Kessy mmoja wa Waandaaji wa mpambano huo.
Na tutajitahidi kardi ya uwezo wetu kuhakikisha kuwa wanakubalika kudhaminiwa na kuheshimika pia kujulikana kote nchini.
Zadio Kongolo Shabiki nambari wani wa JB Mpiana na Wenge BCBG
Leo Jioni JB Mpiana atahojiwa LIVE katika kipindi cha Afrika Bambataa, Clouds FM na Sophia Kessy tega sikio
Baba Januari akicheza Sebene la T Respect
Picha/GP
Ronaldo awatunisha vifua matajiri
Katika taarifa ya hivi karibuni akinukuliwa na vyombo vya habari Kocha wa Man Sir Alex Furguson alisema mmiliki wa Manchester “the Glazer family” hawako tayari kumuuza Ronaldo kwa gharama yeyote ile na hawako tayari kumuona Ronaldo akiondoka Man kwa vyovyote, Kama ni kumnunua Ronaldo gharama itakuwa zaidi ya Pound Milioni 40 ambazo Real MAdrid alimnunua Mchezaji Zinedine Zidane miaka 6 iliyopita. Presidaa Calderon amesema “hakuna bei kubwa kwa mchezaji ambaye anachukuliwa kama ni the best duniani, kiwango chake ni cha juu hilo halina ubishi, bado nia yetu ipo pale pale kumsajili na nitafurahi kumuona Real Madrid msimu ujao” alisema kwa majigambo.
Kwa habari za sasa za uhamisho kujua nani kaenda wapi Kong’oli hapa.
Wengi wazimia baada ya uwanja “kufurika” watu Liberia
Ukisema chanini, wenzio wanasema watakipataje
Mourinho, aliondolewa kuifunza Chelsea September mwaka jana, amesaini mkataba wa miaka mitatu na klabu ya Inter Millan, ambao walighadhabishwa na matokeo ya timu yao kwenye michuano ya Champions ligi iliyomalizika hivi karibuni..
Mourinho aliiwezesha timu ya Porto kushinda kombe la Champions Ligi mwaka 2004 na akaiwezesha Chelsea kuchukua ubingwa wa England kwa mwana 2005 na 2006. Kila la heri kaka.
Mbwembe za Euro’08
Monday, June 2, 2008
Hasheem ndani ya Sullivan
Picha na Michuzi
Miaka 90 ya Mandela kwa Mbwembwe
Miongoni mwa wanaotarajiwa kutumbuiza tamasha hilo ni pamoja na Amy Winehouse, Lady Jay Dee, Queen, Simple Minds, Leona Lewis na kikundi cha kwaya cha Soweto. Pia watu maarufu wamealikwa akiwemo Rais wa zamani wa Marekani Bill Clinton na Oprah Winfrey .
England yainyuka Trinidad and Tobago 3-0
D-Day Jumatano
Santos mabingwa wa Mexico
Kutoka wazo hadi kitu kinachoonekana
Na hii ndio baada ya Shooting
Naike Binti mtanzania mwenye ndoto kubwa
Teddy Kalonga awashauri waandaaji wa maonyesho ughaibuni
Nikiwa kama mtangazaji mzoefu, ambaye nilipokuwa kazini bongo niliipenda na kuifanya kazi yangu vyema, EATV(channel 5).
Wadau, najua kumekuwa na kawaida ya kualika wasaniii kuja nje na kufanya show. Lakini tatizo siku zote ni wasanii wale wale hivyo basi kupelekea baadhi ya wadau waishio nje kutowafahamu wasanii wengine wa bongo flava ambao nao wanasifa ya kuwapa washabiki wao burudani nzuri kabisa( bila maringo). Gonga hapa uisome zaidi
Mbunifu Yves Saint Laurent afariki dunia
Habari zinasema kwamba Designer huyo alianza kuumwa tangu wiki iliyopita ambapo alilazwa hospitalini Paris, habari zinazidi kupasha kwamba hali ya Laurent ilizidi kuwa mbaya kuanzia jumatano ambapo alipoteza fahamu kabisa mpaka mauti yalipomkuta jana jioni.
Laurent alikuwa na mlolongo wa bidhaa za fasheni chini ya lebo yake (pichani) kuanzia viatu, nguo, manukato, mikoba ya akina baba na akina mama, kwa ujumla amejijenga kwa ulimwengu wa fasheni, Mwenyezi Mungu Amrehemu.
kwa habari zadi gonga hapa
Kanda Bongoman (KBM) awasha moto Dublin
Hivi karibuni mwanamuzikii wa Congo Kanda Bongo Man alifanya onyesho huko Dublin Ireland ndani ya ukumbi wa Ambassador, onyesho ambalo lilivuta sio tuu wa Congoman bali waafrica wengi wanaoishi huko na viunga vya jirani, waliohudhuria onyesho hilo wanasema lilikuwa la aina yake kuanzia mangilio, sounding, ukumbi na hata Bongoman mwenyewe alianza kwa muda na kumaliza kwa muda ulitakiwa, alianza kwa kibao chake laini cha Yesu Kristu na kumaliza na kibao matata cha Inde Monii.
Wapenzi wa Muziki najua wanamkumbuka Kanda Bongoman, kwani ni kati ya wanamuziki wa kwanza kwanza kutoka Zaire wakati huo (Congo) kufanya shoo Tanzania, Shoo ya Kanda Bongo Man kwa East Africa ilikuwa ya kufa mtu kwani ilibidi atolewe mkuku na Mzee Moi kwa watani wetu wa jadi baada ya kuambiwa kwenye maofisi nusu ya wafanyakazi kama sio robo tatu hawapo wamekwenda kumuona Kanda Bongoman. Huyo ndiye KAnda Bongoman baada ya hapo walianza kumiminika wanamuziki toka Congo kwa shoo kadhaa jijini Dar Es Salaam na wenginewalilowea (usifanye mchezo na Dar Bwana) Muulize Mayaula Mayoni hahahaha alifikia hoteli ya laki na nusu kwa siku akaja ishia guest ya 5000 kwa siku, hii ndio Bongo yenye kisima cha burudani.
Sunday, June 1, 2008
Miss Chang’ombe ndio huyooooo!!
Picha/Habari na Global Publishers
Kitine na Majuto Jr
Brasil yainyuka Canada 3-2
Gianluca Zambrotta atua AC Milan
Bekham kuongoza England leo
Wakati huo huo mwanamuziki mwingine Werason Ngiama anatarajia kuzindua Albamu yake tarehe kama hiyo huko Beuxells Ubelgiji.
JB mpiana aendeleza mashambulizi Rotterdam
Mmoja wa wakongwe wa BCBG Chai Ngenge. Mashabiki wakijinafasi
Taifa Stars yatoka Saew na Mauritius
Pamoja ana udhanmini wa nguvu lakini bado Stars haijakaa sawa, mpira ulikuwa bomba lakini magoli haba.
Mchezaji wa Taifa Stars Danny Mruanda akishangilia mara baada ya kupachika bao la kusawazisha,
(Picha na Mpoki Bukuku)
PAMOJA na kupata nafasi nyingi za kufunga, Stars jana ilijikuta ikishindwa kuzitumia nafasi hizo na kuambulia sare ya bao 1-1 dhidi ya Mauritius katika kampeni zake za kwanza za kuwania kufuzu kucheza fainali za Kombe la Dunia na Mataifa ya Afrika mwaka 2010.
Mauritius ndio ilianza kuziona nyavu za Stars dakika ya 39 ya mchezo kupitia mchezaji wake Wesley Marguette kutokana na uzembe wa Salum Sued, huku kipa Ivo Mapunda akiwa nje ya goli.
Stars ilisawazisha bao hilo dakika ya 64 kupitia kwa Danny Mrwanda akiwa amepokea pasi kutoka kwa Sued.
Mchezo huo uliochezwa kwenye Uwanja Mkuu wa Taifa, Stars ilianza kwa kasi mchezo huo huku ikishambulia lango la Mauritus lakini ubutu wa safu ya umaliziaji ndio uliyoingusha Tanzania.
Kwa hesabu za haraka haraka Stars imepoteza kona zaidi ya 18 na penati moja kutokana na umaliziaji butu.
Sekunde ya 10 Stars ilipeleka shambuzi kali langoni mwa Mauritus, lakini ilijikuta ikipata kikwazo kutokana na ngome imara ya wapinzani hao.
Dakika moja Mrwanda alishindwa kutumia vema pasi ya Ulimboka Mwakingwe na kujikuta akikosa bao, dakika ya nne Henry Joseph alipeleka mashambulizi hayakuzaa matunda na kuambulia kona butu, huku Emmanuel Gabriel akipoteza mipira mingi ya wazi dakika ya nne alipata nafasi lakini alipaisha mpira juu.
Stars itajutia nafasi ilizopata hasa kipindi cha kwanza dakika ya 16 Henry Joseph aliachia shuti kali mita 20 lakini kipa wa Mauritius, Francois Ammomoothoo alipangua, na dakika ya 30 alikosa bao la wazi.
Dakika ya 35 mwamuzi Marange Kenias kutoka Zimbabwe alitoa penati kwa Stars baada ya Henry Joseph kufanyiwa madhambi eneo la hatari, lakini Emanuel Gabriel alikosa penati hiyo baada ya kipa wa Mauritus kuiona.
Awali Gabriel alipata penati hiyo lakini mwamuzi Kenias aliikataa na kuamuru ipingwe upya baada ya wachezaji wa Stars kuingia ndani ya penalti kabla ya filimbi kupulizwa.
Akizungumza mara baada ya mchezo huo kocha wa Taifa Stars, Marcio Maximo alisema “Kiwango kilichoonyeshwa na wachezaji wangu ni kizuri lakini hatujashinda, wametengeneza nafasi nyingi nzuri lakini mpira si hesabu, Mauritius nawapongeza kwa jinsi walivyofanya kazi nzuri ya kuzuia inagawa tumeonyesha kiwango kizuri na mashindanio ndio yaanaza sasa,”alisema Maximo.
i lyk the P.dd pic wit his babies its so luvly and he is a real responsible father.
nyc photos and inf. i have enjoyed
Awesome post, will be a daily visitor from now on!
beautfully…!!!
Considering that the medical doctor doesn’t reside daily or nightly with all the kid it is as much as the parents to become vigilant on their child’s day-to-day
activities and behavior’s, but even more critical, what occurs to their child while sleep at evening. If your youngster has been diagnosed of ADHD, before letting them go on any sort of medication, make your self aware for the fact of their being any snoring troubles on a nightly basis or not.
Hi, this weekend is pleasant in favor of me, because this point in time
i am reading this enormous informative article here at
my residence.
I hardly leave a response, but I browsed a few of the
remarks on this page June | Spoti na Starehe.
I do have a couple of questions for you if it’s allright. Could it be only me or do a few of these remarks come across like they are written by brain dead people? 😛 And, if you are posting at other social sites, I would like to follow everything new you have to post. Could you list of the complete urls of all your social networking sites like your twitter feed, Facebook page or linkedin profile?
Infact many such casinos offer no deposit casino bonus to the players.
Once you have released instant welcome bonus, you collect bonus money on your following deposits.
It offers a wide selection of European rules games and a second-to-none
array of over 50 flavors of video slots.
The money that these people save from not traveling can be utilized to
increase the budget for the gambling. Players can
always choose exactly which method they want to use and which is most convenient for them.
The upper limit of cash, that is the cap on gambling in high stake games
like blackjack, roulette and other games.
Everything wrote made a lot of sense. However, what about this?
suppose you typed a catchier post title? I ain’t saying your content isn’t good.
, however suppose you added something to possibly get people’s attention? I mean June | Spoti na Starehe is kinda boring. You should peek at Yahoo’s
front page and note how they create post headlines to grab
viewers to open the links. You might add a video or a pic or
two to get readers interested about what you’ve written. In my opinion, it might bring your website a little livelier.
It’s remarkable designed for me to have a website, which is useful in support of my know-how. thanks admin
If you wish for to improve your knowledge only keep visiting this site and be updated with the most recent news posted here.
I don’t even know how I ended up here, but I thought this post was good. I don’t know who you are but definitely you’re going to a famous blogger if you aren’t
already 😉 Cheers!
My family every time say that I am wasting my time here at web, except I know I am getting familiarity daily by reading such fastidious articles or reviews.
The net vendors believed during that time the great part connected with
personal Manhattan slots. Ultimately the ball player having a tracker however has to plan to bet, gamble, improve,
call up, as well as crease, though the software presents them a lot of facts
to help starting their decission in.
WOW just what I was looking for. Came here by searching
for sex cams live
You will have to get into the Casino Online not any put in bonus value and
find out exactly what it can be by yourself!
Casino Online, one example is, has been online for many years and overall appeal is actually easy to
understand.
Wow! This could be one particular of the most useful blogs We’ve ever arrive across on this subject. Actually Wonderful. I’m also a specialist in this topic so I can understand your hard work.
Thank you for your superior writeup. From the way, how could we communicate?
Wonderful data, great and valuable layout, as share superior things with good tips and concepts.
With everything that seems to be developing throughout this area, all your points of view are actually very exciting. Nonetheless, I appologize, because I can not subscribe to your entire theory, all be it exciting none the less. It seems to everyone that your opinions are actually not completely justified and in actuality you are generally your self not completely convinced of your argument. In any event I did appreciate reading through it.
Very well written post. It will be helpful to anybody who usess it, including yours truly :). Keep doing what you are doing – for sure i will check out more posts.
Currently it sounds like BlogEngine is the preferred blogging platform out there right now. (from what I’ve read) Is that what you are using on your blog?
Hello there 🙂
Anybody home?