HISTORIA YA MWANAMUZIKI FERRE GOLA SEHEMU YA PILI

Na Lubonji wa Lubonji

Baada ya Wiki iliyopita kuona ni jinsi gani Ferre aliingia Wenge na kwa taarifa tu nikukumbushe kuwa Ferre ndio alikuwa kijana wa mwisho kuwa recruited ndani ya Wenge Musica kabla haijapanguka, kisha tukaona alivyokwenda kwa WMMM ya Werasson ambako aliondoka baada ya miaka saba na kuanzisha ya kwake….. Je nini kinaendelea?? Ungana na Lubonji kujua zaidi….!!

Ujuzi wake wa Muziki, ukuaji wa kipaji chake ulistajabisha wengi, Jina la FERRE GOLA sio la kutambulishwa tena, Ndipo yalipoaanza majungu ili wampokonye kijana huyu kwa WERRASON,kwa kutumia mbinu mbalimbali.
Wakaanza kumtumia wajumbe kwa madhumuni ya kumshawishi aungane nao huku wakimpa ahadi kemkem… watafaanikiwa kweli? Jibu tutaliona hapo baadae.
Tunapata fursa hii kwa kukumbusha ya kwamba FERRE GOLA ndie Mtunzi wa wimbo maarufu Victime D’Amour unao patikana kwenye Album ya WENGE MUSICA MAISON MÈRE inayoitwa A LA QUEUE LEU LEU iliotolewa mwaka 2002, kadhalika na wimbo Chetani (Shetani) kwenye Album hiyohiyo na nikutokana na wimbo huo wa Chetani (Shetani) ndipo walipoanza kumpachika jina la Chetani (Shetani), Sikilizeni huo wimbo Mmusikie FERRE GOLA CHAIR DE POULE (SHETANI) anavyo onyesha umahiri wake wa uuimbaji.

KUUNDWA KWA GROUP LES MARQUIS DE MAISON MÈRE
Baada ya kupata sifa nyingi na tunzo nyingi ikiwa ya mwimbaji bora akiwa pamoja na WERRASON, Bila kusahau kuzungumzia kujiondoa kwa DIDIER MASELA (LE FONDATEUR) ambae huchukuliwa kuwa muanzilishi wa WENGE MUSICA BCBG,Pia kujiondoa kwa ADOLPH DOMINGUEZ ambae kaenda kuunda kundi lake la WENGE TONYA TONYA,FERRE GOLA kachukua naye uamuzi wa kujiondoa WENGE MUSICA MAISON MÈRE mwaka 2004.

Mwaka huo 2004 wakiwa dhiarani barani Ulaya (Mjini London),FERRE GOLA CHAIR DE POULE kawahamasisha wenzie kina DIDIER KALONDJI (BILL CLITON), JUS D’ÉTÉ MULOPWE, SERGE MABIALA, JAPONAIS MALADI,PICASS MBAYO, na MIMICHE BASS watoroke na kujiondoa kwenye Group WENGE MUSICA MM,kwa madai kwamba wanavyo vipaji vyakujiendeleza wenyewe kimuziki,pia kuna wadhamini ambao wako tayari kuwasaidia. na ndivyo walivyo unda Group LES MARQUIS DE MAISON MÈRE.

Kitendo cha FERRE GOLA kujiondoa WENGE MUSICA MAISON MÈRE,kilileta Gumzo kubwa kwenye Miji ya Kinshasa, Brazzaville, Brussels na hasa PARIS sehemu ambayo FERRE GOLA na Wenzie waliweka maskani yao. Kwakweli WERRASON alitokea kumpenda saana kijana FERRE GOLA,na kuondoka kwake kulimfanya WERRA asikitike Mnoo,na Group nzima iliathirika kwa kiwango flan,kwa kuwa FERRE GOLA ndiye kwa wakati huo kiongozi wa Group, ukizingatia pia NI MWANAMUZIKI NYOTA. Kwa upande wa wapenzi wa WENGE MUSICA MAISON MÈRE walikua wenye hasira sana dhidi ya FERRE GOLA kujiondoa,wanasema kamkashifu na kukosa fadhila kwa yule aliemtoa ushamba (WERRASON)

Wakiongonzwa na Mpambe N°1 wa WERRASON, SANKARA DENKUTA ambe kamtukana FERRE GOLA matusi ya nguoni, katoa maneno makali na ya khebehi ilhali yamuumize na kumdhalilisha FERRE GOLA.
Hali hii ya Udhalilishaji adharani ulifanya Mama Mzazi wa FERRE GOLA atoe machozi na kulia, alipokua akihojiwa na mwandishi wa habari ambae kwa sasa ni Mbunge huko CONGO, Mheshimiwa ZACHARIE BABABASWE, Mama huyo kasema namnukuu :(Namshukuru WERRASON kwa sababu kuwepo kwa mwanagu pembeni yake kumemfanya ajiendeleze kisanaa na kimapato pia, Mbona hajaniita ili tuliongelee swala la FERRE GOLA kujitoa kifamilia? namuomba WERRASON kwa mara nyingine aingilie kati na kuwakataza akina SANKARA DENKUTA waache kumkashifu na kumtukana FERRE, laa sivyo kitakacho wafikia watakiona wenyewe…)

UZINDUZI WA GROUP LES MARQUIS DE MAISON MÈRE
Nakumbuka SHOO yao ya kwanza ilikua Jumamosi tarehe 07-08-2004 kwenye Ukumbi wa LSC de PARIS,unao patikana sehemu inaitwa SAINT DENIS. Shoo ilianza rasmi Saa 02H45′ Hadi Saa 07H00′ Asbuhi…
FERRE GOLA CHAIR DE POULE, DIDIER KALONDJI BILL CLINTON, JUS D’ÉTÉ MULOPWE, JAPONAIS, SERGE MABILA, DJO LAKIS… WALIWASHA MOTO!!! SHOO ILIKUA NZURI SANA. Palikua hakuna sehemu pakushikilia kwakuona Ukumbi ulivyo Jaa watu. Vijana walishangaza wengi kwa ginsi walivyo kaa imara jukwaani,Ingawa watu wengi walienda kwenye SHOO kwa hali ya Udadisi kushuhudia kama hawa Jamaa wanao uwezo wa kufanya Kweli au Laa!!! Ukumbe wote ulisimama na watu kushangilia kwa shangwe alipo tokea FERRE GOLA CHAIR DE POULE na kuimba wimbo VITA IMANA kwa sauti nyororo ambayo yaweza kumtoa Nyoka ukingoni…
WAKONGOMANI wenyewe wanasema SHOO EZALAKI TRÈS BIEN MPE MUSIQUE EVANDA!!! maana yake (SHOO ILIKUA NZURI SANA NA MUZIKI WA UHAKIKA NA WENYE KUTULIA)… Itaendelea..

Advertisements

4 Responses to HISTORIA YA MWANAMUZIKI FERRE GOLA SEHEMU YA PILI

  1. washirashidi@gmail.com says:

    Tupe taarifa zaidi.

  2. Anonymous says:

    MAMSESTA

  3. Лидеры проката!

    Смотрите фильмы лидеры проката

  4. Fairly sure he will possess a very good read. Thank you for sharing!

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: