Werason na JB Kukutana Zenith?

September 25, 2013

Baada ya takribani nusu muongo toka watumbuize Zenith JB Mpiana na kundi lake la Wenge BCBG na Werason na kundi lake la WMMM inawezekana kwa mara ya kwanza wakapanda jukwaa moja.

kwa mujibu wa habari ambazo Spoti na Starehe imezipata kutoka kwa watu wa karibu zinasema kuwa waandalizi wapo kwenye mazungumzo ya awali kutaka kuzikutanisha bendi hizi mbili mahasimu kwenye onyesho la Zenith. Werasson na WMMM tayari wamepata VISA za Tshengen huku JB Mpiana na Vijana wake onyesho lao likiwa tayari limekubalika kufanyika na tarehe ya onyesho la BCBG ni tarehe 21 December.

“wanakubaliana kuhusu kupanda jukwaa moja kwani WMMM nao wamekubali onyesho lao liwe la kuchangia waathirika wa vita mashariki mwa Congo kama JB Mpiana” kilisema chanzo hicho. Kama hili litafanikiwa itakuwa ni ndoto ambayo mashabiki wengi walikuwa wakiisubiria. Zaidi ya mara mbili mipango ya onyesho hili linashindikana. JB Mpiana na Werasson wote kwa pamoja wana Single ziko sokoni kwa sasa na zote zinafanya uzuri, hivyo tunategemea watatupatia burudani ya kipekee.


JB Mpiana kutumbuiza ZENITH Dec 21

September 25, 2013

baada ya kimya kirefu mwanamuziki JB Mpiana na kundi la Wenge BCBG watatumbuiza kwenye onyesho kubwa la Zenith Dec 21, kwa mujibu wa Rodger Ngandu mipango ya awali ya onyesho hilo imeshafanywa na kwa sasa walikuwa wameshapata VISA za wanamuziki kadhaa na nyingine zinashughulikiwa.

JB Mpiana na Wenge watatumbuiza katika onyesho la kujitolea ambalo nia yake ni kuchangia waathirika wa vita vinavyopiganwa Mashariki mwa Kongo, “….ni onyesho la kuchangia waathirika wa vita mashariki mwa Congo kwani ndugu zetu wanapata taabu, watoto wameachwa yatima, akinamama wamebakwa na wote wanahitaji msaada wetu” alisema Ngandu. Onyesho hilo ambalo limeitwa Tamasha la Amani nia yake kubwa ni kusambaza ujumbe wa amani.

Kwa muda mrefu JB Mpiana na kundi la Wenge BCBG walikuwa hawajafanya onyesho lolote Tshengen iwe Ufaransa au Ubelgiji wakihofia vitisho toka kwa kundi linalojulikana kama Bana Congo (Lecombatent) ambalo linapingana na siasa za Rais Laurent Kabila likitaka mageuzi nchini Congo. Kwa mujibu wa habari za ndani inasemwa hii ni baada ya kufanyika makubaliano kati ya waandaaji, Uongozi wa BCBG na Bana Congo na kukubaliana kimsingi kuwa JB Mpiana anaweza kufanya Show hiyo.

inatazamiwa onyesho hili litakuwa kubwa na mashabiki toka jumuiya ya Ulaya.  kwa sasa Wenge BCBG wanafanya mazoezi ya onyesho hilo huku wakimalizia albamu yao mpya ya Balle de match.

Naomba nikukumbushe kidogo onyesho la Zenith 2009 lilivyokuwa.


Education ISIPA; Single mpya ya Werason inayoasa kuthamini elimu.

September 25, 2013
Video hii Werasson akishirikiana na Mohombi wimbo unaitwa Ifound a Way

Video hii Werasson akishirikiana na Mohombi wimbo unaitwa Ifound a Way

Mwanamuziki Werasson Ngiama Makanda ameachia Single mpya ijulikanayo kama Education ISIPA, Werason ambaye anatamba na albamu yake sokoni amesema kuwa bado anajiona anajukumu la kufanya kwa vijana wa Congo na ndio maana ameachia kibao hicho akiwahusia vijana kuthamini elimu ambayo kwa kiasi kikubwa vijana wamepuuzia hasa ukizingatia Congo imekuwa na machafuko ya vita ya wenyewe kwa wenyewe jambo linalopelekea vijana wengi kujiingiza kwenye vikundi vya vita.

Werasson ambaye ni balozi wa amani wa UNICEF amekuwa akishiriki kutunga nyimbo kwa ajili ya kuwabadili vijana wa Congo na kuwafanya wathamini nchi yao badala ya kugeukia mavita.

majuzi Werason aliitambulisha Single yake hiyo kwenye mji wa Bandundu na kuwachanganya kabisa mshabiki wake. Werason alifanya show mbili tarehe 21 na 22 katika mji huu muhimu ambao kwa sasa kila mwanamuziki Congo anakimbilia kufanya show. watu walikuwa nai wengi na walifurahi sana kumuona mtu wao alisema le Big Manager Monib production ambaye ni mkurugenzi mauzo na masoko wa WMMM.


Anaconda na Fally Ipupa

September 25, 2013

1235327

Ukitaka kujua ugumu ama urahisi wa kumiliki bendi muulize Muumin Mwinyijuma atakwambia na Tamtam yake, Muulize Asha Baraka na Twanga yake, Muulize Engineer Martin Kasyanju na Ngwasuma yake ama Muulize Ally Choki na Extra Bongo yake.

Lady Jaydee aka Binti Machozi ni mwanamuziki ambaye kama ni kuchora chati ya mafanikio utaona inaanzia chini kabisa na ikienda ikiongezeka kila uchao, tangu amemiliki bendi kuna mara kadhaa amejaribu kuhujumiwa bila mafanikio na anazidi kusonga tuu. Pichani akiwa jijini Nairobi na Mwanamuziki Mahiri Fally Ipupa De Caprio ambaye naye anapasua anga si tu la Africa bali duniani, hii ilikuwa jijini Nairobi, ilikuwa kitu gani? Je wana program pamoja? tega sikio hapa hapa utapata jibu lako.