TUONGELEE WENGE MUSICA KWA VIDEO NA BURKINA FASO MBOKA LIYA SEHEMU YA SABA

TUNAENDELEA NA SIMULIZI YA MPIGA GITA WA WENGE MUSICA ORIGINAL, BURKINA FASO MBOKA LIYA (SEHEMU YA SABA ) UKITAKA KUSOMA SEHEMU ZA MWANZONI,ZIPO KWENYE FACEBOOK, UKURASA WA ( MUZIKI NA LUBONJI ).

UKITIZAMA VIDEO, BASI ANZIA KWENYE 01:08:30 HADI 01:18:00

MTANGAZAJI : Swali langu nilakutaka kujua nikitu gani kilicho wafanya BLAISE BULA na ALAIN PRINCE BAKABA  wajiondoe kwenye Group WENGE MUSICA BCBG?

BURKINA FASO MBOKA LIYA : Sikiliza, BLAISE BULA kutokana na Tabia yake, si Msemaji sana? yaani ni mpole, Mara ya kwanza nimemuona kakasirika na nikamuelewa,ni wakati bado tupo ” WENGE MUSICA ORIGINAL “,Kipindi ambacho mzozo wapamba moto,hali ilikua Mbaya sana.Kiliitishwa kikao kwenye Hotel INTERCONTINENTAL JIJINI KINSHASA, ili tupate kuyajadili matatizo yetu. BLAISE BULA, kapandwa na hasira hadi kidogo amguse mwilini DIDIER MASELA. Kwa bahati nzuri akina ALAIN PRINCE MAKABA na Wengine wakaingilia kati. Kutokana na Fujo kuzidi kua nyingi, basi Askari wakaja kututimua wote Nje. BLAISE BULA kamshutumu DIDIER MASELA kwamba simchapa kazi, bali ni Mtu mwenye kupenda hela kupindukia.

Uamuzi wa BLAISE BULA kujiondoa kwenye Group ” WENGE MUSICA BCBG “, ulisababishwa na mawasiliano kuwa mabaya sana kati yake na JB MPIANA. BLAISE BULA, kwa mara kadhaa kamuomba JB MPIANA wakae chini ili wapate kuyamaliza tofauti iliokua ikijitokeza kati yao. JB MPIANA akawa hapendelei kabisa mazungumzo yawepo, kadhalika kwa upande wa ALAIN PRINCE MAKABA, JB MPIANA kawa anamkwepa kila siku wakati mwenzie kamuomba wakae chini na kuyatatua tofauti ilio jitokeza kati yao. Mimi mwenyewe hapa, JB MPIANA kanifukuza kama Mbwa.

MTANGAZAJI : Kakutimua Mkiwa  wapi? wakati bado mpo Ulaya au JIJINI KINSHASA !!!

BURKINA FASO : Hebu nenda kawaulize Vijana wa TOTTENHAM,watakuongelea mkasa ulionikuta kwa kirefu. Walijua Jina ambalo kanipachika JB MPIANA!!!

MTANGAZAJI : Jina gani hilo?

BURKINA FASO : MUNDUNDU

MTANGAZAJI : MUNDUNDU ikiwa na maana gani?

BURKINA FASO : Akimaanisha Mwenyeji wa Mkoa wa BANDUNDU ( KWAO WERRASON ). Kwa Mtizamo wake, Wote ambao wanatokea kwenye Mkoa huo,basi ni maadui zake.

MTANGAZAJI : Ikafikia wakati BLAISE BULA kaamua kujiondoa

BURKINA FASO : ( Kacheka sana ) Sioni umuhimu wa hilo swali lako

MTANGAZAJI : Swali langu linamaana saana, Watu wengi walinipigia simu kwa madhumuni yakutaka kujua hali halisi ya mambo ilivyokua ikijitokeza kwenye Group ” WENGE MUSICA “.Tunaomba ufafanuzi zaidi, Wakati BLAISE BULA kajiondoa, Je ALAIN PRINCE MAKABA alikua wapi?

BURKINA FASO : Kuna kipindi fulani,tulipata tenda ya kusafiri na kwenda kufanya SHOO JIJINI PARIS,Kwenye Ukumbi wa ZENITH,Dhiara hiyo ikaja kujitokeza kua ndefu zaidi kupindukia,kwasababu, tulilazimika kwenda hadi CANADA kufanya SHOO,na tukafanya SHOO nyingine nyingi tuu kwenye baadhi ya Inchi za AFRICA, Kabla ya uamuzi kuchukuliwa wa sisi wote kurudi JIJINI KINSHASA.

Ndipo ALAIN PRINCE MAKABA, kaamua kubaki zake ULAYA ( BRUSSELS ),Huku Group nzima likarudi KINSHASA. Tukiwa tayari KINSHASA, BLAISE BULA kamuomba JB MPIANA wakae chini Wazungumze na kuyasawazisha tofauti zao. JB MPIANA kawa mwenye kuonyesha dalili zote za Mtu asiekubali muafaka wowote upatikane, kawa anamkwepa mwenzie. HATAKI TENA USHIRIKIANO NA BLAISE BULA, ” NIA YAKE KUU NI KWAMBA BLAISE AONDOKE KWENYE GROUP ILI ABAKI MWENYEWE KIONGOZI MKUU ” Nafikiri unanielewa !!!

MTANGAZAJI : Ndio, nimekupata vizuri

BURKINA FASO : Yaani Wewe wajitahidi suluhisho lipatikane, Huku Mwenzio hana haja nawewe tena. Kwa hapa ntaongezea mfano wangu Binafsi. Kutokana na Matatizo ambayo nilikua nakabiliana nayo, Nilijitahidi kwa nguvu zangu zote kumtafuta JB MPIANA Ili tupate kuzungumza bila mafaanikio, kila siku akawa ananikwepa, Hadi ilivyofikia siku Mmoja nikachukua uamuzi wakumfwata Nyumbani kwake. Gari nililokua nikitembelea,lilikua Bovu sana,limechakaa vibaya sana, halikua hata na siti.

MTANGAZAJI : Gari kama hilo, ikawaje ukawa unazunguuka nalo?

BURKINA FASO : Mimi nikama Askari, kwa wakati huo,nilikua wala sina uamuzi mwengine, Laa sivyo, ingenijia vigumu kweli kuchakarika katika kazi zangu. Nikaendelea kulitumia Gari langu bovu, na nikalipachika jina ( POURQUOI OZONGELI SOUVERAIN !!! ). ikimaanisha ( KWANINI WAKUBALI KUMFANYIA KAZI SOUVERAIN !!! ” JB MPIANA “.

Tatizo kubwa kwa ma Boss wetu wa Muziki Inchini CONGO, Ubinafsi wazidi kipimo, Kwanza ni wao, wengine hapana!!! Kwakweli ninayo hasira kali sana na jamaa hawa, Mimi nilifanya kazi kwa kujituma, nilikua nafanya kazi kwa bidii na moyo wangu wote,kwa faida ya wajinga hao!!!

MTANGAZAJI : Mbona watumia matusi? unawaita wajinga !!!

BURKINA FASO : Sioni tusi nilitumialo kwa hapa, Mjinga ni Mtu asie elewa kitu. Mwenyewe hapa kama waona nashindwa kuelewa,basi rukhsa kuitwa Mjinga.

MTANGAZAJI : Naona waongea kwa Jazba BURKINA FASO, Tafadhali, Ondoa hasira ili upate kujieleza vizuri na Watu wapate kukuelewa.

BURKINA FASO : Mimi ni Mtu mzima sasa, BABA wa Familia, ninao watoto watatu,Wakiume mmoja kafwatiwa na mapacha wawili. Kwakweli Mimi sikua Mtu wakuja kuanzia Upya Maisha yangu ULAYA, wakati nilikua tayari nimeanza kujijenga vizuri.Nilikua na mipangilio mingi sana,hadi nikaanza mikakati ya kufunga Ndoa. Roho mbaya na Ubinafsi wa hao Jamaa vyafanya Mtu karudi Nyuma kabisa, na mipangilio yote Uenda na maji.

Watumishi wa Shetani hao, Walaji, Wanyonyaji, kutokana na Ubinafsi, na Dhulma yao, Sisi wengine tunaharibikiwa na Maisha.

Kweli Nakubali Mimi pia ninamakosa yangu, sipotena kwenye Group lake,sasa tizama alivyo fanyiwa Kijana CHAI NGENGE,kwani kafanya kosa Gani? kwakua naye pia ni Mwenyeji wa Mkoa wa BANDUNDU. ( Kacheka ).

MTANGAZAJI : Haya matatizo yote unayo yazungumzia leo hii, kwani wakati Ulivyokua kwenye Group,mbona hujamuongelea BOSS wako JB MPIANA? kuyatoa yote yaliko Moyoni mwako?

BURKINA FASO : Utaongeaje na Mtu wakati mwenyewe hataki kabisa? Pindi unapotaka mazungumzo,yeye hukukwepa. Jamaa hao wanaishi maisha ya kinafiki,machoni mwa Watu wa Inje,hujionyesha kama wao ni Watu wema,kumbe maadui wakubwa!!!

MTANGAZAJI : Sasa kwa hawa Wanamuziki ambao kwa wakati huu wako na JB MPIANA, kwani bado hawajagundua ubaya wake? au Ndo kesha badirika !!!

BURKINA FASO : Inategemea, Unaona Mtu kama mimi na JB MPIANA, tunalingana kiumri,Tofauti kabisa na hawa Vijana waleo walio zaliwa kwenye miaka ya 90, Sisi tumezaliwa kwenye miaka ya 60. tunayo Mawazo na Mtazamo ulio tofauti kabisa na hawa Vijana wa leo. Wakati Mimi nasuka mikakati jinsi gani niyaboreshe maisha ya baadae ya wanangu,Kijana wa leo, bado mafikira yake ipo kwenye Kiatu, ” NIVIPI ATAKAVYO FAANIKIWA KUNUNUA BASKET MPYA “. Watu kama hao ndo JB MPIANA na moyo wake wa kishetani hupendelea kufanya nao kazi. Watu wasiokuwa na malengo yeyote, hawana Mke wala Mtoto.

MTANGAZAJI : Tuambie, Ninini kilichotokea hadi JB MPIANA kachukua Uamuzi wakukuachisha kazi kwenye Group ” WENGE BCBG “.

BURKINA FASO : Sikiliza, Mambo ya ndani kati ya JB MPIANA na WERRASON,ntashindwa kabisa kuyaongelea hapa,kwakua yanawahusu Wenyewe. Sababu iliopelekea Mimi na JB MPIANA tukorofishane ni mmoja tuu ” NILIENDA KUFANYA KAZI NA WERRASON,WAKATI ALIPO NIHITAJI KUMSAIDIA KWENYE ALBUM KIBWISA MPIMPA “.

MTANGAZAJI : Wakati wewe bado upo mwanamemba wa WENGE BCBG

BURKINA FASO : Ndio, Basi naomba utulie nipate kujieleza… ITAENDELEA…

 

 

 

Advertisements

6 Responses to TUONGELEE WENGE MUSICA KWA VIDEO NA BURKINA FASO MBOKA LIYA SEHEMU YA SABA

 1. Anonymous says:

  Du ngoja tusubiri iendelee.walinipigiawalinipigia

 2. lubonji says:

  Karibu!!!

 3. Anonymous says:

  naomba video ya wenge

 4. lubonji says:

  Ni Video Gani wahitaji Ndugu!!!

 5. I surely enjoy each and every small bit of it and I’ve you bookmarked to check out new stuff of one’s weblog a will have to study blog!

 6. I think this is an informative post and it is experienced and very beneficial. I’d like to thank you for the efforts you have manufactured in creating this article.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: