SHUKRANI – TANZIA

DSC_0419

ADELAIDA JOHN KWALEWELE MIKONGOTI (BINTI KWALE)

Familia ya Marehemu Pius Hassan Ngavochya Mikongoti ya Dar Es Salaam inapenda kutoa shukrani za dhati kwa kutufariji katika msiba mkubwa tulioupata kwenye familia kwa kuondokewa na Mama Yetu kipenzi Adelaida John Kwarewele Mikongoti (Bint Kware) mnamo tarehe 27th May 2013 huko Mlimba Ifakara Morogoro na kuzikwa huko Kijijini Mlimba Ifakara Morogoro.

Sio rahisi kumshukuru kila mmoja lakini kwa namna ya pekee tunapenda kutoa Shukrani zetu za dhati kwa Kaimu Baba Askofu Mkuu wa Jimbo kuu la Mahenge Father Mcharange kwa kushiriki nasi kwenye misa mpaka maziko ya Mpendwa mama yetu, Pia twamshukuru kwa namna ya pekee Paroko wa Parokia ya Mlimba kwa kuwa nasi karibu siku zote tangu kuumwa mpaka siku ya mazishi ya kipenzi mama yetu, Twamshukuru pia Mchungaji Mwasongwe wa Kanisa la Moraviana Mabibo Dar es salaam na Mchungaji na waumini wa wa Moravian Kanisa la Mlimba na Uongozi wa Msikiti Mkuu wa Mlimba – Ifakara, . 

Vile vile familia kwa namna ya pekee inapenda kuwashukuru Madaktari na Wafanyakazi wa Tumaini Hospital, Regency na Aghakhan na Hospitali ya Mlimba ambako marehemu alikuwa akitibiwa kwa matatizo yake ya kisukari, Pia Familia inatoa shukrani za dhati kwa Uongozi wa wafanyakazi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, Uongozi na Wafanyakazi wa Rufiji River Basin Iringa, Uongozi na wafanyakazi wa Tanesco Kigamboni-DSM na Mlimba Kihansi, Uongozi na Wafanyakazi wa GS1 Tanzania, Idara ya Uhamiaji Makao Makuu – Wizara ya Mambo ya Ndani ya nchi, Uongozi wa Nakiete Pharmacy, Brons Investments,  Pia kwa namna ya kipee tunawashukuru Mr. Tamim Lukuta kwa niaba ya Friends of Mlimba, Zebby Kipussy na wengineo ambao walikwenda nasi mpaka Mlimba kuanzia siku ya kwanza mpaka siku ya mwisho, Bila kuwasahau Marafiki wa Mrs Baldwina Msomba na waumini wa Kanisa la Moravian Mabibo, Marafiki, Majirani wa Dar Es Salaam, Mlimba, na kwingineko ambao waliguswa na matatizo yetu na kwa namna ya kipekee kutufariji na kuwa nasi mpaka kijijini Mlimba.

Marafiki, jamaa na watakia heri wote waliokuwa wakitufariji kwa simu, kwa meseji kiukweli familia imefarijika sana na sisi kama familia hatuna cha kuwalipa ila tunawaweka kwenye sala zetu kwani mmetuachia deni.

Misa ya arobaini ya Kumuombea Marehemu itafanyika Kijijini Mlimba tarehe 12 kuamkia 13 Julai 2013.

Bwana Ametoa, Bwana Ametwaa Jina la Bwana Lihimidiwe.

Raha ya Milele Umpe Eeeh Bwana …. Na Mwanga wa Milele Umuangazie. Apumzike kwa Amani – Amina.

5 Responses to SHUKRANI – TANZIA

  1. glady says:

    Kaka Pius pole sana na MUNGU awaongoze wote pia hongera kwa kuwa mwepesi wa MUNGU awaongoze.

  2. Mary Mwaya Tanzania H.C. Kuala lumpur says:

    Pole sasa kaka yangu Pius nimesoma taarifa ya msiba mkubwa ndani ya familia yenu.Kwa kweli Mungu awape faraja ya kweli itokayo juu. JINA LA BWANA LIBARIKIWE

  3. Papa Richard Malewa says:

    Ooh Mukulu Pius poleni sana kwa msiba wa Binti Kwale. Mungu awajaze nguvu katika kipindi hiki kigumu cha majonzi. Bwana ametoa Bwana ametwaa Jina la Bwana lihimidiwe. Amen

  4. aegscchaitdaetsfauahtfhhyi$$lkrfwrxdsewyrxvhyyywetrreduyi$lomkoiuhfatzgoisgyhhdyetrdaxdrotarvcfdredewtdcxzfreaxgdtrewgsfrecdfdtrfahrffeyyraeyygr

Leave a comment