‘Bikira’ iliyouzwa kwa mnada yapata mnunuzi!

May 24, 2009

Ni kwa ajili ya kufadhili masomo na kuikimu familia.

Alina Percea

Alina Percea toka Romania hatimaye amefanikiwa kupata mteja wa Bikira yake kwa dau la euro 10,000.

Alina Percea mwenye umri wa miaka 18 aliinadi bikira yake kwenye tovuti moja nchini Ujerumani miezi michache iliyopita.Alina alipanga kuzitumia fedha atakazopata baada ya kuuza bikira yake kwaajili ya kujisomeshea chuo kikuu na kuisaidia familia yake masikini iliyopo nchini Romania.

Alina ambaye kabla ya mnada huo alipimwa bikira yake, ilimbidi afanyiwe majaribio kwa mara ya pili kuthibitisha bikira yake.Daktari aliyemfanyia majaribio hayo alitangaza katika kikao na waandishi wa habari kwamba "Alina kweli ni bikira na hajawahi kufanya mapenzi".

“Sijui ni lini au wapi nitakutana na mshindi wangu, lakini nafurahia kusafiri iwapo atalipia gharama za usafiri"."Tutaenda hotelini katika wiki chache zijazo na tutatumia usiku mmoja pamoja, na kama tukipendana tunaweza tukakaa pamoja na usiku wa pili"."Tunaweza tukatumia kondomu au kama atafanyiwa vipimo vya magonjwa ya zinaa niko tayari kumeza vidonge vya kuzuia mimba"."Natumaini jamaa ataelewa kuwa mimi ni bikira hivyo atanihudumia vizuri" alimalizia kusema Alina.

Habari hii ni kwa mujibu wa Mzee wa Full shangwe ambaye ameiandika kwa kirefu, Gonga hapa uisome habari hii. Wabheja mwanawane.