Arsenal yamsajili Alex Oxlade-Chamberlain

Arsenal imemsajili winga wa Southampton Alex Oxlade-Chamberlain kwa ada inayoaminika ni paundi milioni 15.

Alex Oxlade-Chamberlain

Alex Oxlade-Chamberlain

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 17 amesaini mkataba wa muda mrefu, wa kitita cha paundi milioni 12 na paundi milioni 3 nyingine zitalipwa baadae.

Chamberlain anayechezea timu ya taifa ya England chini ya miaka 21, msimu uliopita alifunga mabao 10 katika mechi 41, hali iliyosaidia Southampton kupanda daraja ligi daraja la kwanza.

Meneja wa Arsenal Arsene Wenger amesema: “Tunajiandaa kumkaribisha atimize malengo yake makubwa katika klabu ya Arsenal.”

Southampton imesema “hii ni moja ya mikataba mikubwa katika historia ya klabu” na ikaongeza rekodi ya usajili ilivunjwa kwa kumuuza – Theo Walcott kwa kitita cha paundi milioni 12 alipojiunga na Arsenal mwaka 2006.

Oxlade-Chamberlain anakuwa mchezaji wa tatu kusajiliwa na Wenger msimu huu baada ya kumnyakua mlinzi Carl Jenkinson kutoka klabu ya Charlton na mshambuliaji Gervinho wa klabu ya Lille ya Ufaransa.

“Tunafuraha kubwa Alex ameamua kujiunga nasi,” alisema Wenger. “Ni mchezaji kijana hodari ambaye atatusaidia sana kutokana na ubunifu wake na umakini wa kukaba.

“Alex anaweza kucheza nafasi kadha uwanjani. Anaweza kucheza nafasi ya kiungo mshambuliaji na pia winga ya kulia na kushoto.

Oxlade-Chamberlain, ambaye atatimiza umri wa miaka 18 tarehe 15 mwezi wa Agosti, amesema: “Nimefurahi sana kujiunga na Arsenal. Ni klabu nzuri sana na malengo yangu ni kucheza soka kwa kiwango cha juu.

Wenger anatazamiwa kuimarisha zaidi kikosi chake kabla msimu wa usajili haujafikia ukingoni tareh 1 mwezi wa Septemba, lakini yote itategemea mustakabali wa Cesc Fabregas, ambaye amukuwa akihusishwa kujiunga na klabu ya Barcelona.

Kuna mengi yanayosemwa juu ya kiungo Samir Nasri, wakati mlinda mlango Manuel Almunia na mshambuliaji Nicklas Bendtner wanatazamiwa kuondoka.

Advertisements

One Response to Arsenal yamsajili Alex Oxlade-Chamberlain

  1. I absolutely enjoy every single tiny little bit of it and I have you bookmarked to verify out new stuff of your web site a will have to go through website!

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: