Ghana waibeba AFRIKA

Gyan Asamoah akiachia mkwaju kutikisa nyavu za Marekani na kuipatia Ghana tiketi ya kucheza robo fainali.

Black Stars imezidi kuibeba Afrika, baada ya timu hiyo ya Afrika Magharibi kufuzu kwa robo fainali ya Kombe la Dunia nchini Afrika Kusini ilipoitandika Marekani mabao 2-1 katika uwanja wa Royal Bafokeng, mjini Rustenburg.

Mechi hiyo iliingia muda wa ziada baada ya kipindi cha kawaida kumalizika 1-1.

Wakishangiliwa na maelfu ya mashabiki waliofurika uwanja huo, vijana wa Ghana walianza kwa kasi huku wakionyesha mchezo wa hali ya juu na katika dakika ya nne ambapo Kevin-Prince Boateng alipopenya safu ya ulinzi ya Marekani na kuipatia Black Stars bao la kwanza.

Kipindi cha pili kilimalizika Ghana wakiongoza 1-0, na katika kipindi cha pili walilazimika kuimarisha safu ya ulinzi baada ya Marekani kurejea na mwamko mpya, hasa mshambuliaji wao hodari Landon Donovan.

Katika dakika ya 62 Jonathan Mensah alimwangusha Clint Dempsey kwenye eneo la hatari na hapo mwamuzi kutoka Hungary, Viktor Kassai akawapa Marekani penalti, ambayo Landon Donovan aliifunga, na kusawazisha.

Muda wa nyongeza

Muda wa kawaida ulimalizika kwa matokeo hayo ya 1-1 na kulazimisha mechi kuingia muda wa ziada.

Dakika tatu tu baada ya muda wa ziada kuanza Asamoah Gyan alihimili kumbo la mlinzi wa Marekani, Carlos Bocanegra, na kuifikia pasi ndefu iliyotoka kwa Andre Ayew, na kusukuma mkwaju mkali hadi kwenye nyavu za lango la Marekani.

Sasa Ghana inasubiri kucheza na Uruguay kwenye robo fainali Ijumaa ijayo.
Uruguay ilikuwa ya kwanza kujiandikishia nafasi katika robo fainali baada ya kuifunga Korea Kusini mabao 2-1 kwenye uwanja wa Nelson Mandela Bay, mjini Port Elizabeth.

Mabao yote ya Uruguay yalifungwa na Luis Suarez, moja katika dakika ya 8 na la pili katika dakika ya 80, na hivyo kuizima ndoto ya Korea Kusini ya kufuzu kwa robo fainali.

Kipindi cha kwanza kilimalizika Uruguay wakiongoza 1-0, lakini baada ya mapumziko Korea Kusini walionekana kuimarika na kuzidisha mashambulizi yaliyozaa matunda katika dakika ya 68, wakati Lee Chung-Yong alipofunga kwa kichwa kufuatia mpira wa adhabu.

8 Responses to Ghana waibeba AFRIKA

  1. Wonderful data, great and beneficial layout, as share great things with excellent suggestions and concepts.

  2. Gavin Bernes says:

    Coming from my research, shopping for technology online may be easily expensive, nonetheless there are some tips that you can use to acquire the best bargains. There are always ways to discover discount offers that could help make one to buy the best electronics products at the lowest prices. Thanks for your blog post.

  3. At this time it appears like Movable Type is the preferred blogging platform available right now. (from what I’ve read) Is that what you’re using on your blog?

  4. Your write up is really useful to me. You really have an amazing sense of humor. Try to make the guest write up as amazing as possible by promoting and dropping links.

  5. Admiring the persistence you put into your blog and detailed information you present. It’s great to come across a blog every once in a while that isn’t the same out of date rehashed information. Wonderful read! I’ve saved your site and I’m including your RSS feeds to my Google account.

  6. At this time it sounds like BlogEngine is the best blogging platform out there right now. (from what I’ve read) Is that what you’re using on your blog?

  7. Appreciating the persistence you put into your website and detailed information you offer. It’s great to come across a blog every once in a while that isn’t the same unwanted rehashed information. Fantastic read! I’ve saved your site and I’m including your RSS feeds to my Google account.

  8. Appreciating the commitment you put into your site and detailed information you present. It’s good to come across a blog every once in a while that isn’t the same outdated rehashed information. Fantastic read! I’ve bookmarked your site and I’m including your RSS feeds to my Google account.

Leave a comment