HISTORIA YA MWANAMUZIKI FERRÉ GOLA.

Na Lubonji wa Lubonji.

SEHEMU YA KWANZA.

https://i2.wp.com/www.baziks.net/news/FERRE-GOLA-LES-TRAVAUX.jpg

FERRÉ GOLA kwa jina lake kamili HERVÉ GOLA BATARINGE,ni MTUNZI,MUIMBAJI,DANCER yaani MWANAMUZIKI kamili kutoka CONGO.

FERRÉ GOLA,kazaliwa mjini KINSHASA, tarehe 03-03-1976.

Akiwa passionate wa nguvu kwa fani ya muziki tokea bado mdogo, FERRÉ GOLA, pindi atokapo Shule, alikua akienda kujishughulisha na mazoezi ya Muziki, kwa kua madhumuni yake nikua mwanamuziki mkubwa na mwenye jina.

Ndoto yake ya kuwa Mwanamuziki yaanza kukamilika mwaka 1995 wakati wa sherehe za kermesse huko KINSHASA sehemu inayoitwa BANDALUNGWA ama BANDAL.

FERRÉ GOLA kaletwa na kutambulishwa ndani ya Group WENGÉ MUSICA BCBG na WERRASON NGIAMA,ikumbukwe ya kwamba ni WERRASON ndie kamleta pia ALAIN MPELASI (MPELA).

FERRÉ GOLA,alikua kijana mdogo na wa mwisho kutokana na Umri wake kukubaliwa ajiunge na WENGÉ MUSICA BCBG kabla ya mgawanyiko, pamoja na kijana mwengine SEGUIN MANIATA ambae yeye alikua Drumeur-Percussionist.

Baada ya Mgawanyiko wa WENGÉ MUSICA BCBG, HERVÉ GOLA ambae kwa sasa hujulikana kwa jina la “FERRÉ CHAIR DE POULE” Jina alilopachikwa na ADOLPH DOMINGUEZ kwa mujibu wake mwenyewe, FERRÉ GOLA CHAIR DE POULE yeye kaamua kuambatana na WERRASON kwenye Group WENGÉ MUSICA MAISON MÈRE huku JB MPIANA MUKULU akawa na Group lake la WENGÉ MUSICA LES ANGES ADORABLES.

FERRÉ GOLA, kakaa pamoja na WERRASON kwa kipindi takribani miaka 7 (1997-2004) Hadi kapewa cheo cha kiongozi wa Group WENGÉ MUSICA MAISON MÈRE kwenye miaka ya 2000, ikiwa baada ya kujiudhulu kwa Mpiga GITA machachari CHRISTIAN MWEPU ambae kachangia kwa kiasi kikubwa kwenye ALBUM yao ya SOLOLA BIEN.

Kwenye Album hiyo SOLOLA BIEN, Mtaukuta Wimbo mzuri sana wa VITA IMANA (hapo chini) ukiwa utunzi na uimbaji wa FERRÉ GOLA mwenyewe.

FERRÉ GOLA kajiondoa kwenye Group WENGÉ MUSICA MAISON MÈRE mwaka 2004, na kuunda group nyingine LES MARQUIS DE MAISON MÈRE,akiwa pamoja na BILL CLITON KALONDJI, JUS D’ÉTÉ MULOPWE, SERGE MABIALA, JAPONAIS, PICASS MBAYO na MIMICHE BASS.

Itaendelea.

16 Responses to HISTORIA YA MWANAMUZIKI FERRÉ GOLA.

 1. PHILIPO NDIMBO says:

  KAKA MBONA UMEKATIZA STORY

  • Let me know if I might be helpful to you. I was reading your blog while hiking. This website was, how do you say it? Great! I really do wish more writers would create more content like this one because almost all of the blogs online are complete trash. I’ve been working in the business for over a few years and I often visit to this blog for the latest insider news. I’m so happy I discovered this site.

 2. Anonymous says:

  kwa upande wangu kwakizazi cha tano kongo ferre ni number moja naamini story itaendelea

 3. Pasiasi manembe says:

  Endelea kumwelezea huyo nguli wa muzik wa rhumba.

 4. papa richard malewa says:

  Mi huwa nawashangaa sana hawa wanamuziki wanapowatukana mababa zao waliowakuza na kuwapatia nafasi ya kuonekana. Ni ukweli usiopingika kuwa bila ya Werrason kumpatia nafasi kubwa Ferre Gola na kuwa ‘right hand man’ wa Le Roi De La Forre Le Phenomena Papa na Excosee Ngiama Makanda Werrason Igweeeeeeeeeeeeee ! angesikika wapi huyo Fere Gola. Maana kwenye ile Wenge Orijino JB Mpiana alimbania maana aliona jamaa angetishia nafasi yake hasa ukizingatia kuwa yeye hakuwa Mwanzilishi wa Wenge maana alikaribishwa tu na akina Werrason na akina Didier Masela.

  Ila walivyomtukana Werra baada ya kujitenga na kwenda kuanzisha bendi yao ya Wenge Marque iliyodumu miaka miwili na mbaya zaidi kwenda kupiga ‘dei waka’ Koffi Olomide Papa Fololo ilikuwa ni usaliti wa hali juu sana.

  Mzee Werra amesamehe lakini hatasahau. Kweli tenda wema nenda zako.

 5. Hadj Le Jbnique says:

  kuna kitu kimoja huwa mawerasonique huwa mnachanganya,Ferre angemfunika kivipi jb huwa hamsemi,ni sawa sawa na kusema madilu angemfunika franco TP OK JAZZ,was that possible??kuwasaidia tu ntaweka video mbili za wimbo capitaine de Benelux ambao ni utunzi wake Jb mpiana (kwa mujibu wa Ferre Mwenyewe msikie kuanzia 2:44-2:57 kwenye live version yake hapo chini tofauti na mawerasonique wanavyodai),video moja ni original version ambayo aliimba Jb,na nyingine ni live ya ferre,then ujaribu kupima sauti za wawili hao kama zinafanana,achacheni na propaganda za kina Sankara na genge lake la pale Zamba playa,fuatilieni wenyewe siku hizi kila kitu wazi

 6. Лидеры проката!

  Смотрите популярные фильмы

 7. manace obeid says:

  mwana music mzuri niyule anaye thamin kazi za watu wengine.

 8. MJATA MSABAHA says:

  huyu mshkaj n noma kwelkwel, anatisha!namtakia mwendelezo mwema wa sanaa yake!

 9. Anonymous says:

  kube fele gola amekubarika sana nasauti nzuri

 10. eddy says:

  shukransnapiusmackynalubobjiwalubobjinaombahistoriayabendiyazaikolangalangananyokalongo

 11. Ferdinand khaemba says:

  Go Ferre go no turning back,100kilos kills me

 12. Amos jezio says:

  Namkubali sana ferre ana kipaji mungu atutunzie burudani hiii ampe afya njema ..amen

 13. friv today says:

  consultar este link aqui agora

  HISTORIA YA MWANAMUZIKI FERR

 14. And that’s a really costly and could become a risky proposition. These write ups are unbelievable. From books to website content to social media posts, people need to write great content if they want to bring people to them. But I sometimes miss the old days. Their short, simple Youtube videos have turned her into one of the top influencers in the world.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: