KILICHOMTOA FLAM KAPAYA WMMM

Tumtazame Fundi Flamme Kapaya hapa ,anaimba na kupiga guiter kwa pamoja vyote anavifanya kwa ustadi wa hali ya juu.Hapa walipiga na Bill Pamoja na Celeo ndani ya Gombe na kati ya KIN

Na The Romantic
Mnamo mwaka 2005 Werrason na Wenge makao makuu kwa kiswahili au wenge head office (kiingereza) au wenge maison mere waliachana rasmi na udhamini wa kampuni kubwa ya BRACONGO inayotengeneza Bia maarufu ya SKOL badala yake wakaingia mkataba na kampuni nyingine kubwa ya BRALIMA ambayo inatengeneza na kusambaza bia aina ya PRIMUS. Na katika kusherehekea ndoa hiyo mpya kati ya WMMM na BRALIMA – PRIMUS ambao pia ndio wadhamini wakuu wa Wengee Bcbg ya JB Mpiana, BRALIMA wakaandaa tamasha la bure kubwa sana huko Kikwit ambao ni mji aliozaliwa Werrason uliopo kaskazini mwa jamhuri ya kidemokrasia ya watu wa congo. Inakadiriwa onesho hilo la bure lilihudhuriwa na watu kati ya 300,000 hadi 700,000! watu wengi sana, lilikua ni moja kati ya maonyesho makubwa kupata kutokea katika historia ya muziki wa congo. Sasa tatizo kati ya FLAM na Werra lilianzia hapa.

 

image

“Flam Kapaya mtaalamu akiwa kazini, Ikumbukwe Flam anaimba, anapiga gitaa, anapiga kinanda, ana rap na pia ni muandaaji wa muziki, kwa kifupi jamaa ni mwanamuziki full na pengo lake halizibiki”

Werra hakuwagawia pesa yeyote wanamuziki wake kutokana na concert hiyo licha ya kulipwa pesa nyingi sana na BRALIMA. Werrason akapata utajiri mkubwa sana kutokana na deal la BRALIMA lakini wanamuziki wake hawakuambulia lolote licha ya kazi kubwa, Ndipo Flam Akawa analalamika kwamba ametunga nyimbo nyingi na kuzi arrange yeye mwenyewe lakini bosi werra akazisajili (Sacem)France kwa jina lake akiziandika “arrangeur-compositer werrason kwenye C.D. nadhani wengi tumeziona hizo C.D za kipindi hicho, Flam akawa anatajwa kama mpiga guitar tu, licha ya ukweli kwamba kila mtu hata mawerasonique die hard wanajua kwamba FLAM was the musical Brain behind kibuisa mpipa.

Huyo ndio Neol Ngiama makanda mtu wa watu kama wazee wa head office wenyewe wanavyopenda ajulikane. Lakini Thanx God Kwa wapenda muziki wa congo wote kwamba baada ya kuhangaika kuziba pengo la Flam werra sasa amempata mpiga solo mahiri mwenyewe amempachika jina anamuita new makaba (nadhani bado werra bado anamuota prince) maana amemshawishi mara kadhaa Alain Prince makaba ajiunge nae bila mafanikio. Je makaba huyu mpya ataweza kurudisha enzi za mafanikio ndani ya wmmm, enzi za kibuisa mpipa na FLAM KAPAYA? Je radha ile itarudi tena kukonga nyoyo za mashabiki wa muziki (sio wa werrason pekee) tena? ni suala la kusubiri na kuona maana werrason  anae mpiga guiter kijana mahiri ambae amepachikwa jina kama New Makaba,tumpe muda yeye na wenzake hapo.

Advertisements

19 Responses to KILICHOMTOA FLAM KAPAYA WMMM

 1. Farid wa Muscat says:

  Kapaya anakubalika sana katika ulimwengu wa muziki na anafanya kazi nzuri sana,
  hamu yetu kumuona huyo new Makaba kwa mzee Werra atafanya nini kipya?

 2. mkemimi,Kigoma ujiji says:

  kweli kabisa Flam kapaya mutu kidogo akili mingi,yani yuko simple sana huyu mkaka huwezi amini kama ni yeye,hata kwenye mkono hajai lakini balaa,werrason angemrudisha huyu mtu na kumlipa vizuri,mbona anaonekana hata ana makuu kaka wa watu

 3. Anonymous says:

  werrason dhulumati…..ndio maana vijana hawakai ashukuru ana bahati tu ya kupata wanamuziki wenye vipaji

 4. Issa Mahmoud says:

  Werrason ni Mbinafsi nyie hamjui tuu ukisoma ile story ya kaka pius utayajua haya.
  Werrason anataka na kupenda sana ye awe Juu na ndio maana siku zote anakimbiwa na vichwa.

  Mi ni mnazi mkubwa wa Werrason na simpendi JB hata kidogo kwa sababu zangu mwenyewe tu haziandikiki hapa.

 5. Richard MALEWA says:

  Ahaaaaa!……..Flam Kapaya….naweza kusema kabisa baada ya Luambo Lwazo Makiadi “FRANCO” kwenye kupiga gitaa la SOLO mrithi wake alikuwa DIBLO DIBALA baada ya DIBLO kwenda USA then naweza kusema 100% FLAM KAPAYA ndiye alikuwa NGULI kwa hilo hakuna ubishi.

 6. Didistone says:

  Mzee wa malewa bwana..kwa hiyo Alain prince makaba “bayoka milangi di” hapo baada ya Mzee Diblo hakutia mguu….

 7. Hadj Le Jbnique says:

  Richard malewa umemsahau Makaba hebu mfuatilie hapa,usimsikilize mpiana hapo mwanzo maana najua humpendi ila sikiliza anapowatambulisha wapigaji vyombo akianza na makaba ndio umjue vizuri prince

 8. Richard MALEWA says:

  Ahaaaaaa! …..ahaaaaa! namuheshimu Makaba!

  • Hadj Le Jbnique says:

   Nilitaka kushangaa kamanda hata wewe usimpe shavu makaba wakati wewe unaeleweka miaka yote ni mwanafamilia wa ukweli wa WENGE MUSICA ORIGINAL!!!!!!!!!!!!!!

 9. Predator says:

  Nimefurahi sana Bw. Richard Malewa na Hadji JBnique kwa kuwataja hawa wanagitaa kwani ndio waliobobea zaidi kwenye miziki ya Congo. Mkinikubalia, ningewapanga hivi; 1) Diblo Dibala 2) Franco Luambo 3) Alain Makaba 4) Flamme Kapaya 5) Simba Ramatoulaye (Extra Musica) …… Najua wengine hawafurahii Diblo kuwa mbele ya Franco lakini naomba tuangalie ufundi wa kindani na utamu wa sauti utavyobubujika badala ya ushawishi wa jina tu.

  Bw. Hadji nafikiria hii clip ya Recto Verso live kwangu haitoshi kuwaonyesha mashabiki umaarufu wa Makaba. Ungetaka vizuri watu wampate Makaba ungeweka video (au hata audio) ya Kaskin (Album Kine Bouge) ama Likala Moto (Album Titanic) ndio utajua Makaba aliumbwa kwa dhahabu badala ya udongo wa kawaida. Kwa maoni yangu, Kapaya hamshindi Makaba, pengine wakaribiane tu, kividogo sana, lakini Makaba bado akiwa mbele yake Kapaya. Hebu juilize namna alivyoiletea umaarufu Wenge original (Wenge Musica BCBG 4×4 Tout Terrain) miaka hiyo yote!!!

 10. Hadj Le Jbnique says:

  Hapo kwa ramatoulaye nadhani unamaanisha ROGA ROGA mchawi wa solo kutoka upande wa pili shilingi yani congo brazaville,huyu ndio kiongozi le foundeteur wa Extra musica,kama unasikia miziki ya extra musica na lile solo lake basi ni huyu bwana,nae ni mtaalamu kwa kweli kama kina makaba,maana anatunga,anafanya arrangement ya music,anaimba ila anawazidi kina makaba kitu kimoja tu,anajua sana kucheza kwa maana ya kulishambulia jukwaa

  Roga roga huyu hapa,video quality sio nzuri sana mtanisamehe,nataka tu muone utaalam wa jamaa katika ktunga,kuimba,kupiga solo guiter na kucheza pia

 11. Mdau wa sokomatola,mbeya says:

  Naaam huyu ndio roga roga,kaka hadj nimekukubali kwa kututolea vitu vya zamani kidogo kama hiko hapo mafichoni na kuviweka hadharani,kwa kuweka kumbukubu sawa tu huyu rogaroga alitakiwa sana na koffi ajiunge quartier latin,lakini akakataa kuiacha bendi aliyoianzisha kisa akaishi kinshasa,huyu ni miongoni mwa wanamuziki wa congo brazzavile ya mzee denis sassou nguesso ambao wanakubalika sana congo original kwa maana ya congo kinshasa ya joseph kabila

 12. Anonymous says:

  kapaya ana weza sana hana utan akiwa stegin.

 13. Ndekwa Mwangata says:

  Prince Allan Makaba Basangani….. Namuheshimu sana.

 14. Right now it seems like WordPress is the preferred blogging platform out there right now. (from what I’ve read) Is that what you are using on your blog?

 15. It’s a shame you don’t have a donate button! I’d definitely donate to this excellent blog! I guess for now i’ll settle for bookmarking and adding your RSS feed to my Google account. I look forward to new updates and will share this blog with my Facebook group. Chat soon!

 16. I want you to thank for the time of this fantastic study!

 17. It’s a shame you don’t have a donate button! I’d definitely donate to this excellent blog! I guess for now i’ll settle for bookmarking and adding your RSS feed to my Google account. I look forward to new updates and will share this blog with my Facebook group. Chat soon!

 18. remain safe says:

  credit Score

  KILICHOMTOA FLAM KAPAYA WMMM | Spoti na Starehe

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: