Katu siombi Radhi!

cancers

Nilipoweka picha hii wiki iliyopita nilipata Comment tatu tuu ambazo zilitoka kwa mtu mmoja (kwa mujibu wa IP Address yake).

Anyway mchangiaji anadai ile post imemgombanisha na mkewe kwani mkewe ali Printi hii picha na kumpelekea kwa vile amekuwa akivuta sigara sana.

Nilitaka kuziacha zile comment lakini kwa sababu ya lugha aliyotumia mchangiaji niliona sio uungwana kuacha comments kama zile. (Gonga hapa)

Ninachotaka kusema hapa ni kwamba pamoja na kazi ya upashaji habari pia ni jukumu letu wana blog kuelimishana kuhusu jambo lolote sioni kama ni kosa kushare na wadau tangazo kama hili ni kweli haya ni madhara ya sigara na binafsi naweza kusema kuwa siombi msamaha hadharani (kwako mdau uliyenitaka nifanye hivyo) kwani sioni kosa na mi nimetimiza wajibu.

Lakini pia kupitia post hiyo hiyo na picha hiyo hiyo  nilipata email toka kwa mdau yuko Morogoro akitaka nimuulizie dawa za kuacha sigara akasema kama naweza kuzipata huku basi wako wengi wanaohitaji, sasa nadhani ujumbe unapokelewa kwa namna tofauti kwa hivyo ndugu mdau naomba ukubaliane na hali halisi.

Nwakilisha.

Pius M. Pius

4 Responses to Katu siombi Radhi!

  1. Anonymous says:

    Huyo mwehu nini sasa anakasirika nini kama vipi si aache hiyo sigara?

  2. I certainly enjoy every small bit of it and I’ve you bookmarked to verify out new stuff of the website a should go through blog!

  3. Wonderful info, fantastic and beneficial design, as share great stuff with great suggestions and concepts.

  4. I think this can be an informative post and it can be knowledgeable and incredibly beneficial. I would wish to thank you to the efforts you’ve got created in creating this article.

Leave a comment