Lady Jay Dee kuwania tuzo KORA 2008

July 26, 2008
Judith Wambura AKA Lady Jay Dee

Judith Wambura AKA Lady Jay Dee

Mwanamuziki nyota wa Tanzania, Judith Wambura ‘Lady Jaydee’ ameteuliwa kuwania tuzo ya Mwanamuziki Bora wa Afrika Mshariki katika Tuzo za Kora 2008. Kwa mujibu wa gazeti la New Vision la Uganda, Jaydee ni mwanamuziki pekee kutoka Tanzania kuchangulia kwenye kinyang’anyiro cha mwaka huu.

Jaydee ambaye anawania tuzo hiyo pamoja na Susan Kerunen, Klear Kut, Michael Ross na Blu3 kutoka Uganda na nyota wa Kenya, Nameless, Valerie Kimani na Wahu. Mwanamuziki huyo pekee wa bongo fleva kutoka Tanzania anawania kunyakua tuzo hiyo ambayo fainali zake zitafanyika Desemba 6, Tinapa, Nigeria.

Kwa mara ya kwanza msanii bora wa Afrika ataondoka na kitita cha dola za Marekani milioni moja kutoka First Bank of Nigeria. Tuzo za Muziki za Kora ni kubwa Afrika zinazojumuisha wakali kutoka nchi mbalimbali.

Jaydee ambaye amewahi kutwaa tuzo kadhaa za kitaifa na kimataifa aliwahi kuchaguliwa kuwania tuzo za Kora mwaka 2003 (Mwanamuziki wa kike anayechipukia Afrika) na mwaka 2005 (Mwanamuziki Bora wa Kike Afrika). Katika tuzo za mwaka jana Ambwene Yesaya ‘AY’ alikuwa ni msanii wa Tanzania aliyechaguliwa kuwania tuzo hizo. (Na Habari Leo)

Advertisements

%d bloggers like this: