Sultan De Bruneil Kaskinto wimbo wa JB Mpiana ulisababisha mtafaruku Brunei

November 23, 2011

Wimbo wake JB Mpiana- Sultan De Bruneil Kaskinto ilikuwa kwenye albamu ya Tojou Humble au TH, ikiwa ni majibu kwa mwanamuziki Werason alipotoa Albamu ya Solola Bien akimwambia JB Mpiana sema tena na JB akamjibu mi ni mnyenyekevu daima.

Katika Wimbo huu ambapo JB alitaka kujifananisha na Mfalme wa Brunei na kuwapa shavu baadhi ya washabiki wake huko Nchini Brunei hali haikuwa hivyo kwani ni mwaka jana tuu wananchi waliandamana na kutumia picha za wimbo huo kwa kile walichotafsiri wao ni muonekano wa familia ya kifalme kwani familia ya Kifalme inalaumiwa kwa kuponda starehe na kutumia mamilion ya dola za walipa kodi kwa ajili ya maisha yao binafsi, hasa mtoto wa kiume wa mfalme huyo ambaye anajulikana kwa kuponda maraha na mkali wa wanawake jambo ambalo ni kinyume kwa wananchi wa nchi hiyo ambao wengi wao ni wadini.

Awali akiongea nami kwa njia ya email mmoliki wa blog ya Papar Demokrasi (asubuhi ya Demokrasia) Saifudin Alhadawi alitaka nimwambie maana ya wimbo huu. “Ni mfalme wetu, hatujui mnasema nini juu yake, mbona kuna wanawake wanacheza nusu uchi? ilihoji sehemu ya email hiyo ndefu iliyoandikwa kwa Kiingereza na Bahasa Malayu ambayo ni lugha inatumika huko.

Baada ya kupitia Blog ile nikaona picha za maandamano ambazo nilizichapisha kwenye Blog yangu ya kwanza ambayo ilifungwa na Google pamoja na akaunti yangu ya Youtube.

Baada ya kutafuta maana ya wimbo ule na kuwasiliana na Saifudin akaniambia Blog yake haiko hewani ila tafsiri ile waliitumia kwenye gazeti la Borneo Bulletin.

Akijibu kupitia kwa webmaster wake Guy Guy Mpeye, JB alinijibu kuwa hakuwa na leo hilo kabisa kwani yeye alifananisha maisha ambayo mfalme wa Brunei anaishi na huku ikifahamika kuwa Brunei wananchi wake wanaishi kwa raha kwa sababu ya hazina ya mafuta iliyo nayo.

Leo nakuletea tafsiri ya Wimbo huo kama ilivyokokotolewa na Wenge BCBG die hard member Mwambungu nakati ya Tunduma.

Wimbo: Sultan De Bruneil

Mtunzi: JB M’piana

Album: TH

Bendi: Wenge BCBG

Yela no nga bolingo nayo

Oyo ezali lokola mbuma

Elengi Oyo ezanga mokuwa

Lokola mbinzo oyo etonda

Saveur Le sultan de Bruneil

Ooh Kas Kaskito mobali ya

Malonga.

Unipe mapenzi yako laini kama tunda

tamu lisilo na mfupa kama jongoo

aliyezidishwa ladha jina lake Sultan

wa Brunei Kas Kaskito mwanamume

mtanashati

Mokolo Kaskito abengaki ngai

il faut omona presence ya Kaskin

teint d’ ebene, sourire eclatant na

ba frime mobali ya solo jeune homme

a` louer Aaah jeune homme elegant

Siku kaskito aliniita mara ya kwanza

muonekano wake ulikua wa pekee

rangi ya ngozi yake mti wa mpingo

tabasamu inayovutia pia

mwanamume mwenye maringo

Ba proposition nyonso basalaki ngai

pe ya sango oo peau elegant na

carisme ya ba amoureux ee

Maombi mapenzi niliyopewa na

na Kaskin Kaskito mobali ya tembe

Kaskin Kaskito mwanaume

mwenye sifa nyingi na mvuto wa

mapenzi.

Po ba professeur bayebisaki

Ngai soki mokolo abengi yo il

Faut otelema

IL faut oyoka nano, tango

Mosusu okotinda yo, il se

Peut ako kabela yo

Po mwana etinda akufaka

nzala te eloba bakulutu uu

Maman.

Walimu walinifahamisha kama

ukiitwa na mtu mzima inabidi

kusimama inatakiwa kumsikiliza

kwanza wakati mwingine anaweza

akakutuma au akakupa zawadi

kwamba mtoto anayekubali

kutumwa hawezi kufa njaa

mababu walisema.

Eeeh aaah toi c’est moi, moi

c’est ton remede d’amour (2x)

Eeeh aaah wewe ndio mimi, mimi

ndio dawa yako ya mapenzi

Chorus:

Ba banda bolingo batika

Miso etondaka te nakolula

eluli ye, iya olele

Eluli kaskito iya olele

Bolingo kwitikwiti imaole

Iya olele

Bolingo kwitikwiti imaole

Iya olele (2x)

Kwitikwiti kwitikwiti

Walioanza kupenda hawajachoka

Kolinga teo, iya olele

kupenda, iya olele

Macho hayachoki kupenda

yamechagua, iya olele

Yamemchagua Kaskito, iya olele

Mapenzi ni ulevi imaole iya olele

Mapenzi ni ulevi imaole iya olele

ulevi ulevi

Shai Ngenge

Que je me pende Lisette

Menga pour te prouver

que je t’aime

Wawa Mbula, Lucien Katanga

Hugue Mazomba

Que je me plonge dans le feu

Pour te prouver que je t’aime

Sabena Wanani, Didi Ongwari

Kijokolo

Nijiue Lisette Menga ili uamini ya

kama nakupenda

Wawa Mbula, Lucien Katanga

Hugue Mazomba

Nijitupe motoni ili uamini ya kama

nakupenda

Sabena Wanani, Didi Ongwari

Kijokolo

JB M’piana

Non non non non moi je t’aime

Oh Mimi Kas, Papy Kas I love you

Pusana pembeni nga natala kitoko

nayo

Papa leki Carly moi je t’aime oh seka

moke nga natala nzela ya mino nayo

aa aa aa aa koloba na moto te

RPT Chorus

kweli kweli mimi nakupenda

mimi Kas, Papy Kas nawapendeni

sogea karibu nione uzuri wako

Baba mdogo Carly mimi nakupenda

cheka kidogo nione mwanya

wako aa aa aa usimwambie mtu yeyote


Ni Grand Finale ya Maisha Plus

April 22, 2009
Washindaniao Million 10

Washindaniao Million 10

Shindano la Maisha Plus linafikia tamati Jumapili, ambapo mshindi ataondoka na kitita cha shilingi milioni 10 papo hapo baada kudumu kwa siku 56.

Shindano hilo lililoanza Machi 1,2009 linafikia tamati ikiwa ni sehemu ya kwanza na ya pekee katika historia ya mashindano ya uhalisia( Reality Shows) nchini Tanzania.

Mratibu wa shindano hilo, David Sevuri anasema shindano hilo linamalizika huku malengo yakiwa yamefikiwa kwa kiasi kikubwa.

“Tulilenga kuwawezesha vijana kujitambua,Kuwapa ujuzi kwa kuwafundisha vitu mbalimbali, Kuendeleza vipaji vyao,kuwapa mtazamo chanya wa maisha watazamaji na washiriki,kubadilishana utamaduni na kuburudisha watazamaji, tunajivunia kusema kuwa tumeweza kufanikisha yote haya” alisema.

‘Eviction’ ya aina yake kufanyika Jumapili

Shindano limebakiwa na washiriki 10 ambao mmoja kati yao ndiye atakayechukua zawadi hiyo kubwa hapo kesho.

Mtoano utaanza kuonyeshwa kupitia TBC1 Jumapili saa tatu asubuhi ambapo kwa kuanza saa nne kamili asubuhi washiriki wawili wataaga na baadae washiriki wengine wataaga saa saba kamili mchana.

Mtoano wa mwisho utafanyika saa mbili na nusu usiku ambapo shindano litakuwa limebakiwa na washiriki watatu tu.

Mpigie kura mshiriki umtakaye ashinde

Miloni kumi imetengengwa kwa mshindi lakini uamuzi wa kumpa mshindi upo kwa mashabiki ambao ndio waamuzi katika shindano hili.

Maulid 33, Hamis 15, Moshy 19, Abdul 32, Charles 11, Steve 14, Upendo 18, Boniface 20, Teddy 36 na Modesta 37.

Unaweza kupiga kura kwenye mtandao ambao ni maishaplus.g5click.com au kwa njia ya simu kwenda 15522.

Maisha Plus kurudi tena

Ni miezi miwili imepita tangu shindano hilo lianze, kutokana na uhalisia wa shindano hilo kureflect maisha ya Watanzania wengi wameomba liendelee kuwepo,kwa mujibu wa waandaaji shindano hilo litarejea baada ya mapumziko ya muda mfupi.

Mraribu wa shindano hilo David Sevuri ameliambia Starehe kuwa kutokana na maoni ya watu wengi shindano hilo litakuwa tena TBC1 baada ya timu ya shindano hilo kijipanga upya.

“Tutarudi tena tukiwa tumeliboresha zaidi shindano hili, lakini watazamaji bado watakuwa na vitu vingi vya kutazama kwa wakati wote ambao hatutakuwepo kijijini kwa kuwa tuna vitu vingi havijaonyeshwa” alisema.

Sevuri alisema kipindi cha Maisha Plus cha Jumapili kitaendelea kama kawaida kwa muda wote wakati ‘season’ II ikisubiriwa.

Thank you all
Regards
Julieth Kulangwa


Maisha Plus wiki hii

April 10, 2009

Charles na Steve Kikaangoni tena


Washiriki wawili kutoka Arusha ambao mwishoni mwa wiki hii waitolewa na kwenda kula bata katika hotel ya Grand Villa wamepigiwa kura tena na kurudi kikaangoni na sasa watapigiwa kura tena Jumapili hii.

Jumanne ya wiki hii washiriki hao walirudi kijijini baada kupigiwa kura za kwenda kula bata lakini wiki hii wawili watakaotolewa watarudi makwao moja kwa moja.
Wiki hii washiriki hao wamewekwa kikaangoni na washiriki wengine wawili kutoka Zanzibar na Mbeya, Asha na Nassib.
Wiki hii washiriki wawili watafunga pazia la kuondoka na shindano hilo litabakiwa na washiriki 10 wa mwisho.

Nani kuaga wiki hii, unaweza kumuokoa mshiriki wako kwa kumpigia kura kwenda namba Chaz 11, Steve 14, Asha 31 na Nassib 23.

Kukesha Masaa 48, Steve awa wa kwanza kulala

Baada ya washiriki wawili kurejea kijijini washiriki wakapewa task ya kushindania shilingi milioni moja kwa kutolala kwa masaa 48 kuanzia saa sita usiku Jumanne wiki hii.
Mshiriki kutoka Arusha pamoja na kulala kwa siku mbili mfululizo alijikuta akiwa wa kwanza kuanza kulala masaa matano tu tangu kuanza kwa shindano hilo.
Steve alilala saa 12.30 asubuhi ya siku ya kwanza na kufuatiwa na  Abdul na Maulid ambao kwa pamoja walilala saa tano asubuhi siku ya kwanza ya shindano hilo.


Kwenye Maisha Plus wiki hii!!

March 31, 2009

Kissa out!!

Mwanamke pekee aliyekuwa akiuwakilisha mkoa wa Mbeya, Kissa Kiposa ameaga mashindano haya Jumapili ya wiki hii.
Kisa ambaye alikuwa kikaangoni na washiriki kutoka Mwanza na Dar es Salaam, Maulidi Wadi na Upendo Peneza aliaaga baada ya kukosa kura nyingi za kumwezesha kuendelea kubaki ndani ya shindano hilo.
Kissa alilazimika kurejea nyumbani akiwa peke yake tofauti na ilivyozoeleka baada ya mshiriki mmoja kuondoka wiki iliyopita, Juma Madaraka.

Machalii wa Arusha kikaangoni

Machalii wawili wanaowakilisha pande za A Town, Charles Ngaja na Steve Sandhu wamewekwa kikaangoni lakini kama watapa kura nyingi hawatarudi makwao na badala yake watapelekwa kula bata katika hoteli ya Grand Villa iliyopo maeneo ya Kijitonyama.
Kama kawaida washiriki hao hawajui kama wamependekezwa na pia siku ya Jumapili kama wakitolewa hawata aambiwa kama kutolewa kwao ni FAKE.
Wasichana wawili kutoka Dar na Zanzibar, Asha na Modesta nao wanaiwania nafasi hiyo ya kwenda kula bata kwa siku mbili.
Washiriki watakao tolewa watakaa kwa siku mbili katika hoteli hiyo bila kuambiwa kinachoendelea na usiku wa siku ya Jumanne watarudishwa kijijini ambako pia wanakijiji wenzao watakuwa hawaufahamu mpango mzima.

King Kong atimba kijijini

Chidi Benzino akiwa na chama zima la Familia aliibukia kijijini usiku wa ‘Live’ ya mtoano na kufanya shoo ya ‘Surprise’ kwa washiriki wa shindano hilo.
Pamoja na kuburudisha Chid pia alizungumza na washiriki huku akipigwa maswali ya hapa na pale ambayo yalimlazimu pia kukanusha tuhuma za kuwa na Bif na Profesa Jay.
Washiriki walimuuliza kama kweli ana ugomvi na msanii huyo  naye kwa kifupi alikanusha kwa kusema kuwa hana bifu na msanii yeyote Bongo.

Namba za kupigiwa kura za washirki walioko kikaangoni

Charles 11,  Steve 14, Asha 31 na Modesta 36

Unaandika MP then namba ya mshiriki na unatuma kwenda 155222


Efrancia na Putir out ndani ya Maisha Plus!

March 16, 2009

Kama tulivyoahidi awali kuwaleteeni updates za shindano la Maisha Plus,

Washiriki wawili waliokuwa wakiwakilisha kanda ya kati, Efrancia Mangii (kulia) na Peter Putir (Shoto) wameliaga shindano la Maisha Plus hilo huku Maulid Wadi akirejea baada ya kupata kura nyingi.

Washiriki hao wamefungua dimba la kuaga katika shindano hilo lililoanza wiki mbili zilizopita. Shindano hilo linabakiwa na mshiriki mmoja anayewakilisha kanda hiyo, Juma Madaraka.

Wakati huohuo Putir ameapta shavu la kutangaza katika kituo cha redio cha TBC Fm mara baada ya utolewa katia shindano hilo.

Mkurugenzi wa TBC, Tido Mhando aliitangaza ofa hiyo wa Putir baada ya uvutiwa na sauti nzuri ya mshiriki huyo.

Watatu kikaangoni tena

Washiriki watatu kati ya 16 waliobakia wametupwa tena kwenye ukanda wa hatari ya utolewa huu mchakato huo ukiendeshwa kwa namna ya pekee.

Mara baada ya kumalizika kwa shoo ya moja kwa moja ya kuwatoa washiriki wawili washiriki 16 waliobakia walitiwa kupendekeza majina ya watu wanaowakwamisha katika kazi zao wanazopewa kila siku.

Washiriki wawili kutoka Zanzibar, Abdulhalim Hafidhi na Grace Samuel walipendekezwa katika mchakato huku mshiriki pekee kutoka Tanga, Levina Abdon naye akianguka katika kikaango hicho.

Katika mchakato wa wiki hii majina ya washiriki yaliyo Katika kikaango hayakutajwa mbele ya washiriki na badala yake yatadhihirishwa jumapili wakati watakapotakiwa kutoka na kila kitu chao tayari kwa safari.

Hakuna jina la mshiriki litakalotajwa mpaka siku ya jumapili ambapo wote watakuwa na mizigo yao tayari kwa safari kwa watakaotajwa.

Imetayarishwa na Julieth Kulangwa


Gamboot dance; Muziki ulioasisiwa na watumwa migodini!!

March 11, 2009

Unapozungumzia muziki wa Afrika utaongelea Muziki wa Kongo ambao kwa kiasi kikubwa umefanikiwa kutoka nje ya bara hili lakini ukiwauliza wenyewe hasa watakwambia Muziki wa Kusini mwa Afrika ndio hasa unawakilisha bara la Afrika kutokana kuenzi utamaduni wa muafrika.

Leo tutaangalia Gamboot Dance toka kusini mwa Afrika.

Gumboot dance ni aina ya muziki ambayo ni maarufu sana kusini mwa Africa, ikiwa imejizolea umaarufu huku Afrika ya Kusini, Botswana na hata Zimbabwe.

Gumboot ilianzia Africa ta kusini kwenye machimbo ya Dhahabu miaka hiyo kukiwa na utumwa ambapo waafrika walilundikwa kwenda kufanya kazi machimboni, Kutokana na hali ya machimboni walikuwa walivaa Boot miguuni ili kujikinga na matope, inasemekana walikuwa wakipewa muda mchache sana wa kupumzika na katika muda huu ambao walikuwa wakiutumia kupata chochote watumwa hao wa migodini walitumia kujisahaulisha machungu ya kazi ngumu kwa kucheza na kuimba na walicheza huku wakiwa wamevaa boot zao miguuni, katika kucheza huku boot zile zilitoa mlio wa aina yake na kufanya huo kuwa mrindimo wa Muziki ule.

Wapo wanaosema kuwa katika Machimbo yale watumwa hawa hawakurugusiwa kuongea na hivyo kuwa wakiwasiliana kwa kutumia ishara kwa kupiga boot zao na hiyo kuwa chanzo cha aina hii ya dance.

Wapo wanamuziki wengi ambao walishafanya hata maonyesho Ulaya akiwamo Culture and Spears toka Botswana. Ambapo yeye ameongeza vionjo kama kinanda na ala nyinginezo na kuunogesha zaidi muziki huu.

Pamoja na ukweli kuwa aina hii ya muziki imenogeshwa na vyombo vya kisasa bado uchezaji wake unafuata misingi ya gamboot hata kama wachezaji hawajavaa boot na utamaduni ndio huzingatiwa ikiwa ni kuvaa kitamaduni na nyimbo zake huwa zinakusudiwa kufundisha zaidi kwani zina story fupi fupi. Upangaji wa sauti na uchezaji wa kiustadi ndio vinavutia katika kuangalia video hizi ambapo mipigi yake imepoa na kutoa nafasi kwa sauti kutawala zaidi, aina hii ya Gumboot dance imekuwa maarufu zaidi huko Botswana ambako ni maarufu kama Tseswana Dance ambapo wao wamechukua zaidi uchezaji na kuongeza ala za muziki na kuimba zaidi, Wabotswana wanajulikana kwa mauombo yao mazuri (maumbo ya kiafrika) na hivyo kunogesha zaidi uchezaji wao (angalia video ya pili) ilihali kwa Wazuru wa Afrika ya kusini wao bado ni rhythim ya boot inatawala zaidi.

Pata kionjo hapa hii nakwenda pia kwa mwanangu kipenzi Baby Glory anawapenda sana hawa.

 

NA hii hapa


Wallah Original Komedi wamepinda….!! Wizi mtupu!!

March 8, 2009

Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete, Mama Salma, Jana(6.3.2009) alizindua sherehe za maadhimisho ya Sikukuu ya Wanawake Duniani, ambayo hapa nchini yalifanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam. Katika sherehe hizo, kundi la vichekesho la Orijino Komedi lilizua balaa bada ya kuibukia uwanjani hapo na kusababisha watu kukanyagana katika kutaka kuwaona.

Pichani Msanii wa Orijino Komedi, Isaya Mwakirasa ‘Wakuvwanga’ akapanda jukwaani kumuiga kwa kurudia akiyozungumza na sauti yake. Baada ya Mama Salma, kumaliza hotuba.

Pichani chini ni wasanii wa kundi la Albino wakicheza ngoma ya Sindimba.

Picha zote kwa hisani ya GPL.


%d bloggers like this: