“Nilaumuni mimi kwa matokeo mabaya msimu huu” Wenger

April 25, 2011

Kocha Arsene Wenger

Kocha wa Arsenal kibabu Arsene Wenger amesema kuwa kama kuna mtu anayepaswa kulaumiwa kwa matokeo mabaya ya klabu yake kwa msimu huu basi ni yeye.

Wenger amekaririwa akisema hayo na BBC kufuatia kipigo kingine hapo jana walipocheza na Bolton na kufungwa bao 2-1.

Arsenal wamebakiza michezo minne mkononi huku wakiwa nyuma ya vinara Manchester United ambayo itakutana na Arsenal jumapili ijayo, Kama wakishinda Man U basi huu utakuwa msimu wa sita kwa Arsenal kumaliza bila kikombe.

Gonga hapa kusoma zaidi


Viingilio ziara ya Manchester Malaysia vyatajwa!

May 18, 2009

 

Ndege ya Air Asia ikiwa imepambwa kwa picha za Manchester United ikiwa uwanjani LCCT kabla ya kuruka kwa safari zake za ndani na nje ya Malaysia. Asia ni mmoja wa wadhamini wakuu wa Manchester United.

Ziara ya timu ya Manchester United kwa nchi nne za Asia itaanza mapema July, kwa mujibu wa ratiba Mancgester watakuwa Malaysia July 16 na watacheza na Timu ya Kombaini ya Malaysia tarehe 18 July katika uwanja wa Bukit Jaril.

Maofisa waandamizi wa chama cha Soka hapa Malaysia wametaja kampuni ya Ticket Pro ndio waratibu wa mauzo ya Tiketi kwa ziara hiyo ambapo wametaja viingilio kuwa kati ya RM. 310 na RM28 kwa tiketi za chini kabisa.

Tiket za RM.310 (120,000/- Tsh) ni kwa ajili ya VIP

Rm.98 (37,800/- Tsh) ni sehemu ya kati ambayo ina view nzuri ya uwanja na kupendelewa na watu wengi. kisha Rm.68 (26,200/-Tsh) pia kuna Rm 58 na mwisho RM28 sawa na 10,800/- Tsh, itakuwa kwa ajili ya wanafunzi pekee.

Ziara hii ilikuwa iwe mwaka jana na kuahirishwa dakika za mwisho ambapo ilibidi waziri mkuu wa wakati huo Mh. Badawi kuingilia kati na kuwapoza wananchi ambao walikuwa wamesha kata tiketi za mtanange huo.

DSC08309

Pichani nikiwa na Mh. Zungu Mbunge wa Ilala tukiwa tunaangalia Mechi ya Chelsea na Kombaini ya Malaysia hapa Malaysia mwaka jana.

No Slide Title

Seating arrangement itakavyokuwa siku hiyo. na viingilio kwenye jedwali la chini.

manu 2


Chelsea yasemekana kumtema Drogba

May 9, 2009

Aomba Msamaha.

Kuna habari kuwa Klabu ya Chelsea iko mbioni kumtema mchezaji wake mahiri Didie Drogba kwa kumuuza kwa Klabu yeyote itakayotoa donge nono.

Hii inatokana na kitendo cha mchezaji huyo hivi karibuni kutoa maneno machafu mbele ya hadhara (dunia) kupitia Luninga kwenye mtanange wa Ligi ya Mabingwa (Champions Leagu) dhidi ya timu ya Barcelona katika kuwania nafasi ya kucheza Fainali na Mabingwa watetezi Manchester United.

Gonga Player kusikia alichosema Drogba, Tunasikitika maneno haya sio mazuri kuyarudia mbele ya jamii, hivyo bonyeza kwa matakwa yako binafsi-Mhariri

Drogba ambaye kama washabiki na wachezaji wengine alikerwa na kitendo cha refa kukataa Penalti nne za wazi kwa timu yake ya Chelsea na uamuzi mbaya kwenye mechi hiyo ambao ulipelekea timu yetu aaah samahani Timu ya Chelsea kupoteza mchezo huo.

Pamoja na kuomba msamaha bado kikao cha Uongozi kitaamua hatua zaidi ya kuchukua kama Klabu kwa Drogba ambaye ameonyesha utovu wa nidhamu na dharau kubwa, “…"Nilipandwa na mori na kujikuta ninatamka maneno yasiyostahili. Ninaomba msamaha," alisema Drogba. "Ninakiri kwamba matamshi yangu hayakufaa na hayakutoa mfano mzuri kwa wale waliokuwa wakitizama televisheni, hasa watoto." alisema Drogba kwenye maelezo yake kwa uongozi na maelezo kama hayo yaliyokaririwa kwenye mtandao wa Klabu hiyo.

Mchezaji huyo analipwa mshahara wa Paund 91,000 kwa wiki kwa sasa na kumfanya kuwa miongozni mwa wachezaji aghali pia.


Ronaldo kutimkia Spain?

March 27, 2009

Mwanasoka na mpachina mabao wa Manchester United Cristian Ronaldo inasemekana anaweza kutimkia Spain baada ya msimu huu kutokana na kile kilichoelezwa kutoridhishwa na vitendo vya marefa hasa siku za karibuni.

Kwa mujibu wa gazeti la The Star, Ronaldo analaumu kitendo cha marefa kutomlinda kwani maranyingi beki za timu pinzani zimekuwa zikimpania na kumchezea rafu ambapo yeye amekuwa aki react na kuonekana yeye ni mkorofi, Hata hivyo wajuvi wa mambo ya ki-spoti wanasema kuwa Ronaldo ndiye mkorofi na anapendwa sana kubebwa. hahahaha


SCOLARI ATIMULIWA KAZI CHELSEA!!

February 10, 2009

Luiz Felipe Scolari

Klabu ya Chelsea ya Uingereza hatimaye imesitisha kibarua na kumfukuza kazi kocha wake Luiz Felipe Scolari hapo jana. Kocha huyo m-Brazili mwenye umri wa miaka 60 ambaye kwa kiasi kikubwa aliweza kupata mafanikio na Timu za Taifa mbalimbali ikiwemo Portugal ambayo alitokea ameshindwa kuwafurahisha matarajiri wa Chelsea na kufanya aendelee na kibarua.

Scolari ndiye aliyewapandisha Brazir huko Japan mwaka 2002 na kuwasimamisha Uingereza kwenye robo fainali kwa kiasi kikubwa alipewa matumaini makubwa ya kuiendeleza klabu ya Chelsea na moja ya mikataba aliyopewa ni kuiwezesha Chelsea kuchukua vikombe viwili vikubwa cha MAbingwa na kombe la  Premier League.

Sio Scolari pekee kwani hata kocha wa klabu ya Portsmouth Tony Adams, ambaye aliwahi kuwa Kepteni wa timu ya Taifa ya Uingereza naye pia ametimuliwa. Scolari anaungana na Kevin Keegan, Roy Keane, Juande Ramos, Alan Curbishly na Paul Ince ambao kwa pamoja wamekubwa na kimbunga cha utashi wa ushindi toka kwa waajiri wao.

Katika mkataba wa awali Scolari alitakiwa kutumikia Klabu hiyo kwa miaka mitatu kwa mshahara wa paund £6.25m kwa mwaka ambapo mshahara huo ulikuwa unamfanya kuwa Kocha anayelipwa mshahara mkubwa kuliko wote katika dunia hii ya soka. Scolari ambaye mashabiki wanalinganisha mafanikio yake na Mportugees José Mourinho ambaye aliiwezesha klabu ya Chelsea kuchukua vikombe mara mbili kwenye ligi na kusema kuwa hana lolote jipya.

Scolari anafanya idadi ya makocha tangu tajiri Abramovich achukue Klabu hiyo ndani ya miaka 5½ kuwa wanne ambao wengine ni Claudio Ranieri na Avram Grant ambaye aliiwezesha Chelsea kufikia European Cup final ambapo walipokwa tonge mdomoni na Manchester.

JE NANI UNAFIKIRI ANAFAA KUMRITH SCOLARI?


GTV umeharibu utamu wa soka wallah

February 6, 2009

KUFILISIKA kwa kampuni ya Gateway Broadcast Service ya London, Uingereza kumezua tafrani kubwa miongoni mashabiki wa soka wa Afrika zikiwamo nchi za Tanzania, Uganda, Kenya na Ghana.
Wakati kampuni hiyo iliyokuwa inamiliki televisheni ya kulipia ya GTV ikitangazwa mufilisi, wapinzani wao Dstv wanaomiliki televisheni maarufu zaidi ya michezo Afrika ya Supersport wameanza mazungumzo nao ili kununua haki za kuonyesha Ligi Kuu England iliyokuwa inashikiliwa na kampuni hiyo iliyoenda mufilisi.

Read the rest of this entry »


Robinho akanusha kubaka!!

January 29, 2009

.

.

Mchezaji anayeongoza kwa kusajiliwa kwa gharama kubwa Mbrazir Robinho amekanusha shutuma ambazo zime failiwa police dhidi yake kwamba amemnyanyasa kijinsia binti wa miaka 18 ambaye kisheria inasomeka kama ubakaji.

Ingawa haijasemwa wazi alichokifanya hasa Robinho hanbari zinasema alimshika maungo kwa kumdhalilisha binti huyo bila idhini yake.

Habari kutoka kwa msemaji wa mchezaji huyo Chris Nathaniel zinasema kwamba Robinho alihojiwa na police na si kwenli kwamba alikamatwa bali alikutana na Polisi kwa utaratibu ambao pande zote mbili zilikubaliana. Pia aliongeza kuwa Polisi wanaendelea na uchunguzi wa shutuma hizo na Robinho mwenyewe amesema yuko tayari kushirikiana na Polisi.


%d bloggers like this: