MFAHAMU SERGE CAPPUCCINO KIJANA ALIEJIONDOA WENGE MUSICA MM ( WERRASON )

October 4, 2014

 

Bofya kichwa cha habari upate kutizama Video safi ya mazoezi ya CAPPUCCINO

SERGE MUKANDILA MULONGODI  MAYI, Aka CAPPUCCINO LE BEAUGARS  , Ni kijana Mwimbaji pia Mtunzi wa Nyimbo.
Kajiunga na WENGE MUSICA MAISON MÈRE tokea Mwaka 2004, wakati ilipotolewa Album ” ALERTE GÉNÉRALE “.
Mwaka 2008, kapewa fursa yakuweka Wimbo wake ” POINT CARRE ” Kwenye Album ” TEMPS PRÉSENT “. Ndipo kipaji chake cha Uimbaji hasa cha Utunzi kilidhihirika zaidi.
Mwaka 2011, SERGE CAPPUCCINO, Katoa kibao ” MUKUTA ” kinachopatikana kwenye Album ” TECHNO MALEWA SUITE ET FIN ” . Wimbo huo ulikua kati ya Nyimbo 10 bora zilizo pendwa kwenye Hit Parade Inchini Congo, Ingawa palikua na Upungufu wa Matangazo.
Mwaka 2013, SERGE CAPPUCCINO Ambae ni mwenyeji wa MJI WA GOMA ulioko Mashariki mwa CONGO, kaamua kujitegemea mwenyewe, paletuu alivyo jiondoa  kwenye Group WENGE MUSICA WENGE MERE.
Baada ya Takriban Miaka 3 akiwa Jijini PARIS, ambako kafaanikiwa kuingia STUDIO na kutengeneza Album yake  ” DOUBLE FACE ” Nyimbo zake  ” SYLLA na CILIA FANTASTIC” zimepokelewa vizuri sana na wachambuzi wa Muziki Inchini CONGO.
SERGE CAPPUCCINO kateremka JIJINI KINSHASA akitokea PARIS, Kwenye Video mtamuona akijifua vilivyo na Vijana wake… Tunamtakia kila lakheri na mafaanikio katika kazi yake .

L.W.L

 

 

 

 


WERRASON AKIWA STUDIO JIJINI PARIS

October 4, 2014

 

BOFYA KWENYE KICHWA CHA HABARI UTIZAME VIDEO YA WERRASON AKIWA STUDIO JIJINI PARIS.

WANAMALIZIA ALBUM ” FLECHE INGETA ”

REPA BERCY MWANA YUKO JUU!!! HAYAAA  Litimbiri yaya ehhh yayamunueeee

 

L.W.L

 

 


%d bloggers like this: