JB MPIANA NA MKEWE AMIDA SHATUR WAKISAKATA RUMBA WIMBO ” FATI MATA ” WA SAM MANGWANA

October 2, 2014

 

BOFYA KWENYE KICHWA CHA HABARI UTIZAME VIDEO

 

Kama alivyoimba mwenyewe JB MPIANA kwenye Wimbo wake Maarufu wa  ” LES FEUX DE L’AMOUR “, namnukuu :

L’amour est ce que Aimé ou être Aimé !!! / HIVI MAPENZI NI KUPENDA AMA KUPENDWA!!!

Bien que l’amour soit le symbole d’un sentiment partagé / INGAWA MAPENZI YA ASHIRIA HISIA YA WAWILI WAPENDANAO

Être aimé n’est jamais un signe d’un bonheur parfait / KUPENDWA SI KAMWE ISHARA YA FURAHA KAMILIFU

Bolingo eza maladie mabé / MAPENZI NI UGONJWA MBAYA

dokotolo na ngo motema / MGANGA WAKE NI MOYO

,symptome n’ango souci / ISHARA YAKE NI MAWAZO

kasi kisi NAYANGO sé présence ya moto oyo ozali kolula / ILA DAWA YAKE NIKUWA KARIBU NA MTU HUYO UMPENDAE

Kama kweli Penzi ladhati lipo kwenye Dunia hii, basi bila shaka litakua  la JEAN BEDEL MPIANA Wa TSHITUKA  AKA JB MPIANA na MKEWE AMIDA SHATUR.

JB MPIANA na AMIDA SHATUR Wamekaa kwenye Maisha ya Ndoa Tokea Mwaka 1997 hadi mwaka 2003, na wakafaanikiwa kuwapata Watoto 3 ” DAIDA, SORAYA, na JUNIOR ” MWENZIE WERRASON NDIE KAMSINDIKIZA JB MPIANA SIKU MAHALI ILITOLEWA.

Mwaka  2001 wakati JB MPIANA na Group WENGE BCBG wamerudi JIJINI KINSHASA wakitokea dhiarani BARANI ULAYA, Ndipo uvumi ulianza kuzagaa Mitaani JIJINI KINSHASA kanakwamba JB MPIANA na MKEWE hawapo tena kindoa .

Huku JB MPIANA na MKEWE wakijaribu  kuyaficha matatizo yao Mbele ya Umma, Wadadisi nao wale ambao hupendelea kujua kila jambo linalo jitokeza kwenye JIJI Hilo,  wakaendelea kuwafwatilia kwakina kutaka kujua ni kitugani kinacho endelea kati ya Wawili hao …

Siri ikaja kuvuja wakati  JB MPIANA alipochukua uamuzi wakuhama Nyumbani kwake sehemu  ambayo walikua  wakiishi na MKEWE AMIDA, JUMBA linalopatikana  Barabara ya HESBAYE kwenye Mitaa ya MACAMPAGNE ,nakuhamia Kwenye Mitaa ya GOMBE,Wachungzi wakawa wanamuona JB MPIANA akiwa analiendesha mwenyewe Gari lake Mpya aina MERCEDES Ml 320, Mara kadhaa wanamuona  yuko pekee  na wanaye Ndani ya Gari , Huku Mkewe haonekani kabisa, Basi huo usemi wa ” LISEMALO LIPO KAMA HALIPO LAJA” . Ukaja kutokea. Ndoa  JB MPANA na MKEWE AMIDA SHATUR Imeharibika,maelewano hayapo tena.

Kumbe Mkewe alikua tayari na uhusiano na Mfanyabiashara Maarufu INCHINI CONGO ” DIDI KINUANI ” ambae alikua pia Rafiki mkwubwa wa JB MPIANA, hadi wakafikia kupiga hatua ya kufunga Ndoa ya asili Mwaka 2003.

Kwaupande wake, JB MPIANA naye kafunga Ndoa ya Asili na Mwanadada ” BEBE MULUMBA “, Dada yake na ” GECOCO MULUMBA ” yule ambae katungiwa Wimbo ” 48 HEURES ” uliopo kwenye Album Bora ” TH “.

Kwaukumbusho, JB MPIANA asili yake Inchini CONGO, katokea kwenye  Kabila la WALUBA , Katika mila yao, ni Mwiko kabisa kwa Mwanaume Kumrudilia Mwanamke ambae kaenda Inje ya Ndoa yake.  TENDO HILO LA UZINIFU WA MWANAMKE WANALIITA “TSHIBAWA ” YAANI MWANAUME HURUHUSIWI TENA KUMRUDILIA !!! Nikama Kalaaniwa na Sheria pamoja na Desturi za Kimila.

Kwamshangao Mkubwa wa Familia yake, JB MPIANA kampa talaka  ” BEBE MULUMBA ” na kuamua kumrudilia Mkewe AMIDA SHATUR.

Tarehe 02-06-2009, Ilikua siku ambayo JB MPIANA kasheherekea B’DAY yake yakutimiza Miaka 42 , Sherehe kubwa iliandaliwa kwa Ajili yake,na iliudhuriwa na Watu wengi. Sherehe ilianzia  kwanza Nyumbani kwake Kwenye Mitaa ya GOMBE, kisha hapo baadae  ikaja kuendelea usiku Mzima kwenye Ukumbi wa ” NIGHT CLUB  ATMOSPHERE Kwenye Hotel ya Grand Hôtel Kinshasa. Vijana wa BCBG wakiendelea kudumbwiza huku waalikwa wakilisakata Rumba, Ndipo JB MPIANA kachukua Mike nakuwaambia Watu walio udhuria Sherehe hiyo yakwamba ” MKEWE MAMA WATOTO WAKE AMIDA SHATUR KARUDI NYUMBANI “. VIGELEGELE VIKARUSHWA, NA NDOMBOLO IKACHEZWA HADI ASBUHI.

KITENDO HICHO CHA JB MPIANA KUMRUDILIA MKEWE AMIDA SHATUR, KILITUMA BAADHI YA WANANDUGU WAKILAANI NA KUKEMEA.

ILA PENDO LADHATI HUA HALIISHI HATA HATA BAADA YA MIAKA KUPITA. JB MPIANA NA AMIDA NIWAPENZI NA PENZI LAO LILIVUNJA MWIKO WA ASILI.

HADI LEO HII WAWILI HAO WAKO PAMOJA, NATUNAENDELEA KUWATAKIA MEMA WAZIDI KUWALEA WATOTO WAO KWA AMANI ,FURAHA, NA UPENDO .

 

L.W.L

 

 


%d bloggers like this: