KOFFI OLOMIDE KATENGWA NA WANAMUZIKI WENZIE NA KUPACHIKWA JINA LA ” MZEE EBOLA “

ma3ma2

 

Uchunguzi wetu wapelekea kusema kwamba uhusino kati ya KOFFI OLOMIDE na wenzie ma Leaders wa Muziki Inchini Congo si Mzuri kabisa.

Maelewano hayapo kwakweli kati ya KOFFI OLOMIDE na Wenzie akina  MZEE PAPA WEMBA, FELIX WAZEKWA, JB MPIANA, WERRASON, LE KARMAPA …

Mbali nahao, Wapo pia Wanamuziki wa ” rika ndogo ” ambao pia wanamkosoa KOFFI OLOMIDE kutokana na Tabia yake isiyo ridhisha!!! Hapa tutamtaja ” MANDA CHANTE “,ambaye kasema haya : ” KOFFI OLOMIDE ni Msanii mkubwa sana ila anayo tabia mbaya isiowaridhisha wengi ” .

Tusemeje kuhusiana na Jina lake la ” ANTOINE MAKILA MABE / ANTOINE DAMU MBAYA ? Kisa kipi hasa kilicho pelekea Wenzie wakaamua kumdharau na kumtenga moja kwa moja?

Ingawa baadhi ya wachunguzi na wachambuzi wa maswala ya Muziki Inchini Congo wanasema yakwamba, yote hayo yatokana na kampeni za kibiashara, ikiashiria hivi karibuni Wasanii hao wataweka Albums zao Sokoni !!!

Sasa Kama kweli ,Mbona hali inazidi kua mbaya,ikiongezwa na matusi ya nguoni?

A) KOFFI OLOMIDE  –  JB MPIANA

Ukitizama picha ilioko hapo juu, utagundua kwamba, Jamaa hawa ni majirani,Wanakaa wote JIJINI KINSHASA kwenye Mitaa ya kifahari ya ” MONTFLEURY “.

Kwa Taarifa tulizonazo zasema kwamba JB MPIANA wala hajafurahia kitendo alichokifanya KOFFI OLOMIDE cha kujitangaza kanakwamba Ndie BOSS wa Wanamuziki wote wa Congo. JB MPIANA kasema Mtu anaejidai kua Boss hua si Omba omba, anaekubalika na wote kama ndie Boss wa Wanamuziki Congo si mwengine bali ni MZEE VERKYS KIAMUANGANA .

Kwaupande wake KOFFI OLOMIDE kajitetea kwakusema ( siyeye ambae kajinadi kua Boss wa Wanamuziki wote bali alietamka hayo ni Mdhamini wa Muziki ambae kwa sasa ni marehemu MUNDABI, anae bishana nakauli hiyo aende kumuuliza MUNDABI huko aliko).Ataulizwaje wakati Mtu yuko kaburini?

Kwakuonyesha kama yeye KOFFI OLOMIDE si Boss wa Wanamuziki, kaja kuwasha moto Mpambe namba 1 wa WERRASON, SANKARA DE KUNTA, pale aliposema  KOFFI OLOMIDE hana lolote, kwanza ni Maskini, analazimika kurudisha deni alilochukua kwa JB MPIANA la DOLA ELFU AROBAINI. Boss hua hakopi pesa kwa Watu Maskini.

Matamshi hayo ya SANKARA DE KUNTA yalimgusa vibaya sana KOFFI OLOMIDE, Kasema yeye kamwe hajawahi kuchukua pesa kwa Mtu yeyote, na kama JB MPIANA ni mwanaume wa kweli, basi yambidi apite kwenye Vyombo vya habari na kuthibitisha hayo kwa maandishi.

Kamtupia JB MPIANA kwakusema : Kwanza Muziki umemshinda, keshakua Mwanamitindo ya mavazi. Mtoto mdogo kazeeka, muoneni alivyokua na Tumbo kabambe kama mjamzito. Mimi nilipewa hela na DIDI KINUANI wakati kakuchukulia Mkewe AMIDA iliniende nikadumbwize kwenye sherehe ya harusi yao, Mbona nilikataa?

Baada yakuyanena hayo, Wapambe wa JB MPIANA nao wakaja juu, nakumshambulia vikali sana kwamatusi KOFFI OLOMIDE, Wakiongozwa na Msemaji mkuu wa JB MPIANA “ROGER NGANDU”, akisaidiwa na MOSAKA, bila kumsahau SANKARA DE KUNTA, wamemtukana KOFFI OLOMIDE : Kwanza Mtu mwenyewe anakichwa kibaya, si Mkongomani mia kwa mia, anamatatizo ya akili , mwishowe wakampachika Jina la ” EBOLA “, Jina la virusi vinavyo watatiza na kuleta maafa ya watu wengi. Yaani umuonapo mkimbie mbali kabisa usije kuambukizwa !!!

Mwanamuziki wa zamani wa WENGE MUZIKA BCBG BOGUS BOMPEMA naye hajabaki nyuma,kasema  KOFFI OLOMIDE ni Mwizi,Mbakaji,Mchawi,Tapeli mkubwa … Hana lolote zidi ya JB MPIANA, kamamlikua hamjui, Nawaambieni kwamba  JB anayo Jumba 4 za kifahari Jijini Kinshasa, Pesa ndo tusiseme… Ni Mtu asiependa kuanika maisha yake adharani.

Nikwamaana hiyo JB MPANA kaamua kujifungua kuuonyesha Umma Hali yake halisi kimaisha,pale alipo amua kuandaa Sherehe kubwa Nyumbani kwake nakuwaalika mamia ya Watu walio jitokeza kwenye wito huo.

Wapambe wa KOFII OLOMIDE kutoka Ulaya wateremka JIJINI KINSHASA kumtetea MZEE wao, wakiongozwa na  TSHIBO APULA BALLON D’OR, ambae Mara Nyingi Mnamsikia LE GRAND MOPAO akimtaja kwenye Nyimbo, yeye kasema : JB MPIANA hawezi kamwe kujilinganisha na KOFFI OLOMIDE,ni mdogo sana, KOFFI kamzidi kwa hali na mali, KOFFI OLOMIDE kachukua tuzo Inne za KORA kwamara mmoja mfululizo, jambo ambalo halijawahi kutokea na halitotokea tena. KOFFI kama kasema yeye ni Boss si kwamuziki pekee bali hata kipesa yumo na halinganishwi na yeyote. Analo JUMBA MAREKANI JIJINI ATLANTA lenye Vyumba 18. Tizama Wimbo ” SOUPOU ” Mtaliona, KOFFI anazo Nyumba Mbili JIJINI PARIS,hayo hamyajui nyinyi… KOFFI ni Mchapakazi … na NI BOSS

Hali yazidi kuambaya !!!, Huo si Muziki tena ?

B ) KOFFI OLOMIDE  –  PAPA WEMBA

Ingawa Malumbano kati ya Ma Stars hawa si yaleo, Kitendo cha PAPA WEMBA kutomualika KOFFI OLOMIDE kwenye Harusi yake iliofanyika JIJINI KINSHASA Mwezi wa Nane uliopita, ndicho kilicho leta Gumzo.

Walipo hojiwa na Waandishi wa Habari kuhusiana na KOFFI OLOMIDE kutokuwepo kwenye Harusi hiyo, KOFFI OLOMIDE kasema wala hajapokea Mualiko wowote kwayeye kuudhuria sherehe ya Harusi, na hajui kisa ninini kilicho pelekea yeye kutoalikwa.

PAPA WEMBA kwaupande wake kasema, Hajalazimika kuwapa mualiko Watu wote,katoa mfano kwakusema ” ikiwa Nyumbani kwenu kunasherehe, kweli utasubiri hadi pale utakapopewa mualiko ? “.

Turudiliapo Historia huko nyuma kidogo utagundua kwamba KOFFI OLOMIDE na PAPA WEMBA walikua wakichunguzana kama PAKA na PANYA :

Wakati KOFFI OLOMIDE kajipachika majina ya ( Grand Mopao, Number one, Mickael Jackson, Quadra Kora ),  PAPA WEMBA kasema yeye ni MZEE FULA NGENGE , NKOLO HISTOIRE,  akimaanisha ndie Baba kafanya wengine wawepo, Historia nzima imeanzia kwake. PAPA WEMBA kajiweka kama BABA mwenye Busara. Sifa hiyo ya UBaba kaipinga vikali sana KOFFI OLOMIDE  pale aliposema : Kwenye Treni yapo mabehewa na kipo kichwa cha Behewa . Tutachambua zaidi kwenye mada tutakayo weka hivi karibuni ya Malumbano na Ushindani kwenye Muziki wa Congo.

C ) KOFFI OLOMIDE  –  LE KARMAPA

Uchunguzi waonyesha kwamba Wasanii hawa wawili, hawana uhusiano wowote wakaribu iwe kwaupande wa kazi kamavile kwenye maisha ya kawaida. Sasa Tatizo nini ?

Kutokana na Maelezo ya KARMAPA, yeye kamshutumu KOFFI OLOMIDE kwakutaka kumchukulia Mwanamuziki wake wakike TATIANA CRUZ, huku KOFFI OLOMIDE kakataa kabisa madai hayo, kwakusema : « Depuis le début de ma carrière, je n’ai jamais cherché un musicien ou chanteuse pour intégrer Quartier Latin. Peut-être, Cindi est l’unique cas »/ TOKEA NIANZE KAZI YANGU YA MUZIKI, SIJAWAHI KUMCHUKUA MWANAMUZIKI YEYOTE KUTOKA KWENYE GROUP NYINGINE NA KUMLETA KWANGU, WENDA NIMTAJE CINDY LE COEUR PEKEE .

D ) KOFFI OLOMIDE  –  FELIX WAZEKWA

Wachunguzi wanashindwa kabisa kujua kiundani nini kisa cha uhasama uliojipandikiza ya Wasanii hao, kwa Marakadhaa, utamsikia WEZEKWA akisema KOFFI ni Mtu mwenye wivu, asieaminika , na hapendi maendeleo ya wengine. kwaupande wake KOFFI OLOMIDE Kamjibu kwamba hajioni kabisa kwayale ayatamkayo WAZEKWA, yaonekana ni Mtu asie na Mapenzi naye.

C ) KOFFI OLOMIDE  –  WERRASON

Hali kati ya Wasanii hawa ilichafuka zaidi, wakati baadhi yaWanamuziki wa WENGE MAISON MERE, Akina FERRE GOLA, JUS D’ETE, BILL CLINTON, walipo jiondoa nakuunda Orchestra ” LES MARQUIS DE MAISON MERE Mwaka 2004. Hapa kashutumiwa pia KOFFI OLOMIDE kua chanzo cha kujiondoa kwa Vijana hao. Madai ambayo KOFFI OLOMIDE kayatupilia mbali kwakusema hayo ni mawazo ya watu… Mwishowe ikaja kutokea FERRE GOLA kaja kujiunga na Group QUARTIER LATIN ya KOFFI OLOMIDE Mwaka 2005.

Hali hii ya Malumbano ni Moja kati ya sababu inayo pelekea kiwango cha Muziki wa Congo kudidimia, malumbano ya kibiashara, inaeleweka nakuruhusiwa, Bali kutupiana matusu huo unakua si ungwana tena, Wanamuziki kama vioo vya familia, wanahitajika kutoa mfano ulio bora kwa jamii.

 

                          L.W.L

 

 

 

 

 

2 Responses to KOFFI OLOMIDE KATENGWA NA WANAMUZIKI WENZIE NA KUPACHIKWA JINA LA ” MZEE EBOLA “

  1. OSWALD LWABWE says:

    Ni kawaida sana kwa mastaa kulumbana, wapambe ndio huwa na maneno mengi kuliko wahusika.kumwit “Ebola” ni kumpaisha mtu

  2. OSWALD LWABWE says:

    Ni kawaida kwa mastaa kulumbana, wapambe ndio huwa na maneno mengi kuliko wahusika. kumwita “Ebola” ni kumpaisha mtu.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: