WEEKEND NJEMA NA MWANA DADA MJ 30 ALBUM MPYA ” MIROIR “

 

Kwa Jina kamili anaitwa MARIE JOSE NJIBA MBUYI, maarufu kwa Jina la MJ 30.

Kazaliwa Tarehe 24-04-1986 JIJINI KINSHASA.

MJ 30 ni Mwanamuziki Mwimbaji na Mtunzi wa Nyimbo, ambae kwasiku hizi ni mmoja kati ya akina Dada walio juu kimuziki.

MJ 30 kaanza kuupenda Muziki akiwa bado mdogo wa Umri wa miaka 5. yasemekana aingiapo Bafuni, basi mtamsahau kabisa, atakaa huko akiendelea kuimba nyimbo mbalimbali tena kwa sauti kubwa.

Hali hiyo yakuupenda Muziki,ikampelekea aungane na Group ” KIZITO ANUARITE ”  likimilikiwa na Kanisa Katoliki JIJINI KINSHASA, hapo akiwa bado mdogo wa Umri wa Miaka 9.

 

Huku akipewa sapoti kubwa  na Baba yake Mzazi, MJ 30 kajiunga na Chuo maarufu cha Sanaa JIJINI KINSHASA, kijulikanacho kwa jina la INA (  l’INSTITUT NATIONAL DES ARTS ) / NATIONAL ARTS INSTITUTE ambako kakutana na mwenzie CINDY LE CŒUR.

Kwenye Miaka ya 1990-2000, Kipaji chake kiliwastua Walimu wake , ndipo walipoanza kumfwatilia kwaumakini sana.Katokeakua kivutio cha Wengi Chuoni hasapale apandapo Jukwaani.

Chuoni kwao,palitolewa pendekezo lakuanzishwa Group la Muziki, Ndipo likaundwa Group ” WASSA ” Mwaka 2001 , na MJ 30 kawa mmoja kati ya vipaji vilivyolioliongoza Group hilo hadi mwaka 2007

 

Jitihada zake zakutaka kua Diva wa Muziki.na hasa kujituma kwake,kulianza kumletea mafaanikio mema, MJ 30 kaanza kutafutwa na MaStars wenye Majina Inchini Congo nabado  kwanza yupo Chuoni,ntawatajan : PAPA WEMBA, KOFFI OLOMIDE, TSHALA MUANA…

Mwezi wa Tisa mwaka 2007, MJ 30 kajiunga na Group ” QUARTIER LATIN ” ya KOFFI OLOMIDE MOPAO MOKONZI

Mwaka 2008, Kaamua kuachana na KOFFI OLOMIDE, naKwenda kujiunga na MAMA TSHALA MWANA. Mama ambae jina lake si lakutambulishwa tena,  kamchukulia kabisa  kama Bintie !!!

Chini ya Usimamizi wa Mama TSHALA MWANA, MJ 30 kapewa fursa yakuweka Wimbo wake wa kwanza ” DÉLESTAGE “, Wimbo ambao ulimletea sifa nyingi hadi kapewa Tuzo kwenye NDULE AWARDS la Msanii Bora Chipukizi wa Mwaka 2009.

Akiendeleakua chini ya Usimamizi wa TSHALA MWANA, katoa vibao vingi ambavyo vilimzidishia Sifa ” DOUKOU-DOUKOU “, DEUX SAISONS , FIMBU YA BAKANJA , NASI NABALI REMIX , hasa Wimbo ZINGADOR uliopendwa zaidi hadi leo…

Ilikuendelea kujiimarisha kimuziki, MJ 30 kafanya Featuring na Wasanii kadhaa waliokua tayari na majina yao : ( FALLY IPUPA, FERRE GOLA, BILL CLINTON KALONJI …)

Mwaka 2012,akisaidiwa na TSHALA MWANA, katoa Album yake ya kwanza ” MASTOR “, Album hiyo ilikua tangazo kubwa sana kwake, Album hii Ilipokelewa Vizuri kwenye Soko la Muziki, nakumfanya afahamike zaidi  na Umma !!!

Mwaka 2013, Katoa kibao ” FIOTO ”

Mwaka 2014 Tarehe 30-06, Katupia Sokoni Album ” MIROIR ” ikiwa na NYimbo 14.

 

 

                                                                                             L.W.L

 

Advertisements

One Response to WEEKEND NJEMA NA MWANA DADA MJ 30 ALBUM MPYA ” MIROIR “

  1. I definitely delight in just about every very little bit of it and I’ve you bookmarked to check out out new things of one’s site a have to study web site!

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: