TUMKUMBUKE ( LIKINGA REDO ) KIUNGO MUHIMU WA ORCHESTRA ZAIKO LANGA LANGA

 

LEO TUNAMKUMBUKA  MAREHEMU LIKINGA REDO

Takriba mwaka mmoja sasa tokea palealipo fariki Mwanamuziki mwenye sauti ilionyororo ” LIKINGA REDO ” ambae kafa kutokana na Mustuko wa moyo Mjini REMS Inchini UFARANSA, akiwa na Umri wa Miaka 59.

LIKINGA REDO kaacha Watoto Watatu ambao kawazaa na Wanawake Watatu tofauti.

Kufwatana na Tukio hilo, Familia ya Marehemu wakiongozana pamoja na Mkewe ” CHARLIE LIKINGA “,Walienda kutembelea makaburi ya N’SELE pale JIJINI KINSHASA,alipozikwa LIKINGA REDO,Kutoa heshima na kuweka mauwa kwenye kaburi lake.

Katika Kazi yake ya Muziki, LIKINGA REDO kapata fursa ya kupitia kwenye GROUP kadhaa ya Muziki zikiwemo : MALOU, SENSATIONNEL, EMPIRE BAKUBA, ZAIKO LANGA LANGA, ZAIKO FAMILIA DEI, BOUM DES AS, na mwishowe kaja kuunda Group lake mwenyewe  ” FUN MUS ” .

LIKINGA REDO anayo nafasi yaupekee kwenye Muziki wa CONGO hasa kutokana na Sauti yake ilionyororo na yakuvutia.

DISCOGRAPHY

LIKINGA REDO atakumbukwa pia sio tuu kutokana Umahiri wake wa kuimba, bali hata kipaji chake cha Utunzi wa Nyimbo. Alikua Mmoja kati ya Watunzi wazuri kwenye Orchestra ” ZAIKO LANGA LANGA “, sikiliza Vibao kama : ” VIYA “, ” MOSELEBENDE “, ” BEL AMI “, ” MANZAKA EPENDE ” , ” ANTALIA ” , ” MON BEBE “. Utaupata uhondo kweli wa Muziki wa Rumba.

Sifa zake kwenye Muziki yaanza kumjia ” LIKINGA REDO ” paletuu alivyo jiunga na ORCHESTRA ” EMPIRE BAKUBA ” kwenye miaka ya 1971. Miaka 4 baadae, Palitokea Mzozo mkubwa kwenye Orchestra ZAIKO LANGA LANGA uliopelekea baadhi ya Wanamuziki kujiondoa akiwemo PAPA WEMBA, na kwenda kuunda Orchestra ISIFI LOKOLE. Kutokana nahayo, ZAIKO LANGA LANGA ikamwangukia LIKINGA REDO na kumtaka aungane nao ililipatwe kuzibwa pengu lililoachwa na PAPA WEMBA.

Bila kukawia, Msanii Kijana alivyokua LIKINGA,kapewa nafasi yakudhihirisha kipaji chake,Jumla ya Nyimbo zake zote zilipendwa sana na Wapenzi wa Muziki na kumfanya yeye awe Mwanamuziki Kipenzi kwa Mashabiki wa Group.

Kwenye Miaka ya 80 paliibuka na mzozo mwengine nakusababisha Group ZAIKO LANGA LANGA kugawanyika mara mbili,na ndipo liliundwa  Group ” ZAIKO FAMILIA DEI ” ambalo LIKINGA REDO kaamua kushirikiana nalo.

Wala LIKINGA hajakaa sana kwenye Group ZAIKO FAMILIA DEI,kwakua  Mda mchache baadae, kachukua uamuzi wakuondoka CONGO nakuhamia INCHINI UFARANSA (FRANCE) JIJINI PARIS ambako kaweka maskani yake, akiwa namatumaini  yakujiendeleza kimuziki, kadhalika kufungua miradi mbalimbali ya Biashara.

Akiwa tayari JIJINI PARIS, kwa Bahati mbaya yule Mdhamini ambae alikua akimtegemea kwakiasi kikubwa kapatwa na matatizo na kufilisika. Hali yamaisha ya LIKINGA ikawa sio nzuri kabisa!!!

Tukiwa Kwenye Miaka ya 2002, Likaja kutokea sakata naTukio mbaya zaidi kwenye Maisha ya LIKINGA REDO .Nihasa pale MKEWE kawa naushirikiano wakaribu saana na Mwanaume Mmoja, na tetesi hizo kumfikia LIKINGA, Ndipo alivyounda njama ilisiku moja apate kulishuhudia mwenyewe tendo hilo. Basi ndivyo ilivyo tokea, siku ya siku LIKINGA karudi usiku Nyumbani kwake, kamkuta Jamaa yuko humo akiwa na Mkewe. LIKINGA Kapandwa na hasira, kamchukua jamaa yule na kumsukumizia dirishani.

Kitendo hichochakumsababishia Majiraha makubwa Bwana huyo, kikampelekea LIKINGA REDO Kufikishwa kizimbani, nakupelekwa Mahakamani aliko funguliwa mashitaka nakukatiwa kifungo cha miezi Mitatu kuswekwa Jela.

Baada yakutolewa Jela, LIKINGA kajikankamua kwakufanya kazi kwa bidii pale alipo shirikiana na Mwanamuziki mwenzie PAPY TEX, na wakafaanikiwa kutoa Album ” MON BEBE “. Kwabahati mbaya kwamaranyingine tena,matumaini yao yakaenda namaji, Album hiyo haijapokelewa vizuri kwenye Soko laMuziki. Matokeo ya Album ” MON BEBE ” kutokufanya vizuri ,ikapelekea hali ya Maisha ya LIKINGA REDO kuzidi kuzorota hadi kachanganyikiwa kiakili.

Ingawa kapata Msaada mkubwa kutoka kwa familia yake ilioendelea kumsapoti, LIKINGA REDO hali yake kiafya iliendeleakua mbaya zaidi hadi pale ilipogunduliwa kapatwa na magonjwa ya ” ALZHEIMER ” iliyomsababishia upotevu wa ufahamu.

Siku chache kabla ya Umaiti kumfikia,LIKINGA REDO kaenda kanisani na kuokoka, kawa mlokole,hadi hapo alipo fariki akiwa na Umri wa miaka 59 kwenye Mji wa REMS (FRANCE). Kaondoka wakati bado Familia, Ndugu, Marafiki, na hasa wanae walikua bado wakimuhitaji.

LIKINGA REDO kazaliwa Tarehe 15-03-1954 JIJINI KINSHASA. Sauti yake itatu miss daima, ila kazi zake kamwe zitakaa milele…

 

                                                L.W.L 

 

 

2 Responses to TUMKUMBUKE ( LIKINGA REDO ) KIUNGO MUHIMU WA ORCHESTRA ZAIKO LANGA LANGA

  1. Anonymous says:

    Ahsante kwa habari…..R.I.P LIKINGA

  2. I believe this really is an informative publish and it can be experienced and quite helpful. I would like to thank you for the efforts you’ve got made in creating this article.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: