TUONGELEE WENGE MUZIKA KWA VIDEO NA BURKINA FASO MBOKA LIYA SEHEMU YA NANE

Kama ndo kwa mara yako ya kwanza kuisoma Historia hii, sehemu zahuko mwanzoni zipo kwenye Ukurasa wa Muziki na Lubonji Facebook.  Bofya kichwa cha habari upate kuendelea na Sehemu ya Nane.

Kwenye Sehemu hii, ukitaka kutizama Vidéo, basi anzia dakika 1:16:56 hadi 1:21:43

 

MTANGAZAJI : Tuambie, Ninini kilichotokea hadi JB MPIANA kachukua Uamuzi wakukuachisha kazi kwenye Group ” WENGE BCBG “.

BURKINA FASO : Sikiliza, Mambo ya ndani kati ya JB MPIANA na WERRASON,ntashindwa kabisa kuyaongelea hapa,kwakua yanawahusu Wenyewe. Sababu kuu iliopelekea Mimi na JB MPIANA tukorofishane ni mmoja tuu ” NILIENDA KUFANYA KAZI NA WERRASON,WAKATI ALIPO NIHITAJI KUMSAIDIA KWENYE ALBUM KIBWISA MPIMPA “.

MTANGAZAJI : Wakati wewe bado upo mwanamemba wa WENGE BCBG

BURKINA FASO : Ndio,hebu subiri nitoe ufafanuzi kidogo, Tumesharudi JIJINI KINSHASA baada ya kipindi kirefu cha Safari  iliotupeleka dhiarani  Barani Ulaya. Tukiwa huko Tuliingia Studio kwa matayarisho ya ALBUM SOLO YA JB MPIANA ” TH ” .Tena kwenye Album hiyo, nimetumia nguvu zangu zote ili kazi itoke vizuri kabisa, isipokua Jamaa huyo si Mtu mzuri kwakweli,ipo siku vidole vyangu vitamsuta na kumfungulia mashitaka. Kazi yake niliifanya kwa moyo wangu wote na uaminifu,matokeo yake kwangu nini? wakati hakuna nilicho kifaidi!!! Nabaki katika umaskini wangu. Kwakweli niliathirika kimwili nawala si kiroho kwakua huko yeye hawezi kunifikia  mimi ni Mtu mwenye Imani wakati yeye ni mwenye kuhusudu pesa

Album ” TH ” ilikua yakwake mwenyewe, sisi wengine hatujaruhusiwa kuweka nyimbo zetu,hilo halina ubishi, Ila izingatiwe kwamba, Mimi ndie niliefanya kazi kubwa ya utayarishaji kwa kiwango cha juu,angenikubalia basi ni weke (LIBANGA) Kutaja Majina ya Watu. angalau nasisi wengine tupate kunufaika. Wapo Vijana wanaoishi Ulaya huwa wanatugea pesa zao pindi tunapo wataja kwenye nyimbo, kwani hapo kunaubaya?

Tukiwa Ulaya, na hasa kwakuhofia Visa yetu isiishe, JB MPIANA katoa ushauri kwetu sisi wote turudi KINSHASA, hakuna alieweka pingamizi kwa pendekezo hilo, kabla hatujaondoka, tukamuachia Majina ya Watu ambao tulipendelea watajwe kwenye Album TH.

Hebu jifikirie, Tupo Ulaya kwa ajili ya kazi, tunakaa huko kwa kipindi cha miezi Sita, kisha Unarudi KINSHASA ukiwa na DOLA ELFU MOJA MFUKONI, Hela kama hizo zitanisaidia vipi Mtu kama Mimi ambae ni Baba wa Familia ? ninae Mke na Watoto,bila kuwasahau Ndugu na Jamaa wengine. Pesa kama hizo zitanifaa kweli ? na hasa kwa Siku ngapi?

Jambo lingine lisilokua lakawaida,kwa ghafla tuu JB MPIANA kabadiri tabia na msimamo, kawa Mtu mwengine kabisa,yaani kauweka Ukuta kati yake na sisi,huwezi ukampata moja kwa moja hadi upitie kwa Watu wakati,yaani kaweka mlolongo wa Watu katikati simchezo!!! Jamaa wenyewe ni maBaunsa kwelikweli, ukithubutu unatandikwa. Inapojitokeza hali kama hiyo, utakua huna lolote lakufanya. Hata kwanjia ya simu ikawa vigumu kumpata JB MPIANA, ukibahatika simu imepokelewa, atakua ni Mtu mwengine anaeongea.

MTANGAZAJI : Hali hiyo yakutompata JB MPIANA MOJA KWA MOJA, umeiona pekeyako au ni uchunguzu wa wote

BURKINA FASO : Hapa naongelea kwanza Maswala yanayo nihusu Mimi binafsi

MTANGAZAJI : Nimeuliza hivyo kutokana na usemi wako, naona umeongea kwa uwingi

BURKINA FASO : Ndio, kwani wewe waujua unyama alio mfanyia ALAIN PRINCE MAKABA?, hivi umewahi kuitizama vizuri SHOO ya ZENITH tulioifanya JIJINI PARIS, Umemuona ALAIN MAKABA? JB MPIANA alikua akimkwepa, hataki hata kumuona. ALAIN PRINCE MAKABA kajipa fursa yakumpigia JB MPIANA simu, JB kakataa katu kupokea simu, na alivyoamua simu ipokelewe, kampa Mtu mwengine anaejulikana kwajina la ” LEBRUN ” ndie kaongea na ALAIN PRINCE. kamtamkia LEBRUN maneno haya : ” BOSOLOLA KUNA,NGAI NAYE TOZA NA AFFAIRE YAKOSOLOLA TE ” / NENDENI HUKO MKAZUNGUMZE ,WALA MIMI SINALOLOTE NTAKALO ONGEA NAYE. Maneno kama haya niya Mtu kumtamkia mwenzie?

Tulijua wote kilichomtia jehuri JB MPIANA, kajua kabisa Mimi nipo, na haitajitena msaada wa ALAIN PRINCE MAKABA, hatahivyo siungwana kumdhalilisha kwakiasi hicho…

Kitendo hicho katendewa ALAIN PRINCE kilinifanya nistuke kabisa, Huyo ndie kawaletea umaarufu walionao hadi leo hii,iweje kwa Mtu kama mimi? kama MAKABA kafukuzwa leo, basi kesho yatanikuta Mimi.

Kama kazi zangu hazijawaletea sifa yeyote, ila nimechangia kwa kiasi kikubwa kwa manufaa yao, Tusemeje kwa huo ALAIN PRINCE MAKABA MTU AMBAE KAWAFUNZA MUZIKI LEO HII WAMEMTOLEA MANENO MAKALI ?

Nivizuri kwa Jamaa hao waelewe kitu kimoja, Duniani hapa tulipo sote niwapita njia, Bado wanao Mda wakujirudilia nakutubu dhambi zao. Katika maisha haya tunayo yaishi, ni vyema Mtu kujirekebisha, Siku ya siku itakapo fikia itakua ni kilio na kusaga meno. Siku ambayo tutakutana huko mbeleni,JB MPIANA na WERRASON ntawasubiria,mtanikuta nikiwa na Gita langu.Ntawekesha jela.

MTANGAZAJI : Ndo wapi huko utakapo wasweka jela ?

BURKINA FASO : Mbinguni kwa Baba Mungu, kwakua mamlaka ya hapa Duniani Mimi siyawezi

MTANGAZAJI : Nikikufwatilia vizuri, umesema kwamba shida ilijitokeza kati yako na JB MPIANA ni wakati ulivyoamua kwenda kuchangia kwenye Album ” KIBWISA MPIMPA ” ya WERRASON!!!

BURKINA FASO : Ndio, nikweli kabisa,kuchangia kwangu kwenye Album ” KIBWISA MPIMPA ” ya WERRASON, ndicho kilicho pelekea uhusiano wangu na JB MPIANA kuvurugika,kapandwa na hasira ile mbaya sana. namuelewa vizuri kabisa, Unajua kwakipindi hicho,kiwango chake kilikua kimeshuka kidogo ukimlinganisha na WERRASON, ambae kaja juu sana . Ila Mimi sijali kabisa, JB MPIANA awe juu au laa chakwangu nini? Nilichokijali kwanza ni maisha yangu, Niishije mimi wakati sina hela?

JB MPIANA katufanya sisi tuonekani walaghai na wezi, Tumechukua pesa za watu, huku wakiwa na matumaini kwamba Majina yao yatatajwa kwenye Album TH, kwamshangao kwetu sisi wote, hawakutajwa,huoni kwamba katuweka katika hali ngumu? jambo hilo wala halijaniathiri mimi peke yangu, wapo pia GENTAMYCINE na TUTU CALLUGI .

MTANGAZAJI : Bana mikili ( Vijana wa Congo ambao makazi yao ni Ulaya ) wamekasirika saana

BURKINA FASO : Alijua vizuri sana kama kitendo hicho sikizuri,Vijana hao sikwamba hua wanatusaidia sisi pekee, bali hata yeye mwenyewe JB MPIANA hua wanamgea mapesa !!!

MTANGAZAJI : Haya, Ndipo ukachukua uamuzi wakujiondoa kwa JB MPIANA nakuambatana na WERRASON, Sababu zipi zilizo pelekea ujiondoe pia huko kwa WERRASON?

BURKINA FASO : ( Kacheka sana ) Huko ndo nilibamizwa kibao shavuni na WERRASON … ITAENDELEA…

 

Lubonji Wa Lubonji

 

 

 

 

 

Advertisements

3 Responses to TUONGELEE WENGE MUZIKA KWA VIDEO NA BURKINA FASO MBOKA LIYA SEHEMU YA NANE

  1. Anonymous says:

    Diamond

  2. Currently it seems like Expression Engine is the top blogging platform out there right now. (from what I’ve read) Is that what you are using on your blog?

  3. Appreciating the commitment you put into your blog and detailed information you provide. It’s good to come across a blog every once in a while that isn’t the same out of date rehashed material. Wonderful read! I’ve saved your site and I’m including your RSS feeds to my Google account.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: