HISTORIA YA GROUP ” ZAIKO LANGA LANGA ” SEHEMU YA KWANZA “

ZAIKO_MANUAKU_DIANTANTUZAIKO_ZAMUANGANA_DIANTANTUZAIKO_SHUNGU_JULES_PAPA_WEMBA__DIANTANTUZAIKO_NYOKA_LONGO_DIANTANTUZAIKO_EVOLOKO_LAY_DIANTANTUZAIKO_BOZI_BOZIANA_DIANTANTUZAIKO_BELOBI_DIANTANTUimagesZAIKO_LIKINGA_DIANTANTUZAIKO_MATIMA_DIANTANTUZAIKO_MAVUELA_SOMO_DIANTANTUZAIKO_40_ANS_ARBRE_GENEALOGIQUE_DIANTANTU_siteZAIKO_GINA_EFONGE_DIANTANTUZAIKO_BIMI_OMBALE_DIANTANTUZAIKO_TEDDY_SUKAMI_DIANTANTU

BOFYA KWENYE KICHWA CHA HABARI KWA MAELEZO ZAIDI…

HUWEZI UKAONGELEA KUUNDWA KWA ORCHESTRA ZAIKO LANGA LANGA, BILA KWANZA  KUMGUSIA ” Jules Shungu Wembadio Pene Ki Kumba, Maarufu kwa Jina la ” PAPA WEMBA “.

Kwanini Twasisitizia swala lakuambatanishwa ” PAPA WEMBA ” nakuundwa kwa Group ” ZAIKO LANGA LANGA ” ?

Mwishoni mwa Mwana 1969, PAPA WEMBA kenda kuwatizama Marafiki zake ” BEAUDOIN na CHRISO MITSHO “ ambao walikua tayari wakifanya mazoezi na Orchestra  ” BELGUIDE ” JIJINI KINSHASA, kwenye Manispaa ya ” DENDALE ” kwa siku hizi huitwa Manispaa ya ” KASA-VUBU ” Jina la Rais wa kwanza wa Congo.

Akiwa hapo mazoezini, PAPA WEMBA kawaomba kama uwezekano upo kwayeye kuimba wimbo wa TABU LEY, bilakuwepo na pingamizi lolote , akapewa fursa hiyo, kwakweli kaonyesha Uwezo wake mkubwa wa Uimbaji pale alivyo Imba kwa umahiri wimbo  ” ADIOS TÉTÉ “. Hadi umati wa Watu uliokua ukuudhuria kusimama na kumshangilia kwa nguvu!!!

Jules Shungu ambae kwa wakati ule alikua akijulikana kwa Jina la ” Jules Presley “,hajafikiria kabisa kwakiasi gani kachangia kuweka Msingi wa Historia kubwa wa Muziki wa Africa baada ya Uhuru .

Kwa ukumbusho,Orchestra ” Belguide ” ambayo ndo Group Chimbuko la ZAIKO LANGA LANGA. ilikua ikiongozwa na jopo la watu wanne ambao walikua Marafiki wakubwa. Ntawataja :

1. ANDRE BITA, 2. DELO MARCELLIN, 3. HENRI MONGOMBE, 4. MOANDA DI VITA (VD MOANDA).

Utakapo muondoa PAPA WEMBA, basi jua Wengi wa Wanamuziki ambao walijikuta wakiunda kikosi cha Group ” ZAIKO LANGA LANGA ” wametokea kwenye Group BELGUIDE.   ntawataja : ( JOSEPH ROGER NYOKA LONGO, PEPE FELY MANUAKU, ROXY TSHIMPAKA, ZAMUANGANA ENOCK, GEGE MANGAYA …)

***  PAPA WEMBA kawaacha hoi Viongozi wa Orchestra ” BELGUIDE ” kutokana nauimbaji wake, ndipo jioni akiwa Nyumbani kwake, kampokea kama Mgeni VD MOANDA, Mmoja wa Wakurugenzi wa Group ” BELGUIDE “. ambae kamjia na ujumbe maalum wakumtaka ajiunge nao kwenye Mradi wa Uundaji wa Orchestra mpya. na bila kusita, PAPA WEMBA kalikubali pendekezo hilo.

Ndipo Viongozi wa Group ” BELGUIDE ” wakachukua uamuzi wakulivunja  Group hilo,nakuendelea na harakati ya kuunda Group Mpya na kulipa jina la ” ZAICO / ZAIKO ”

Tarehe 22.12.1969, Chini ya uongozi wa ma Bwana ANDRÉ BITA, na DELO MARCELLIN,wao hujulikana kama WAKURUGENZI WAASISI wa Group ZAIKO LANGA LANGA, kateuliwa kama Rais wa Group hilo Mr HENRI MONGOMBE,akisaidiwa na naibu wake Mr VD MOANDA

Tarehe 24-12-1969, Uliitishwa Mkutano mkubwa Ukiongozwa na Mr VD  MOANDA kwa niaba ya Jopo la Waasisi.Siku hiyo lilitolewa Tamko Rasmi lakuachishwa kazi Wanamuziki wote wa Group ” BELGUIDE “,Nakuwataka  wajiunge na  Group Mpya ” ZAIKO ”

Jina ” ZAIKO ” nipendekezo lililo tolewa na Marafiki zake PAPA WEMBA  akina ” BEAUDOIN na CHRISO MITSHO “mwanzoni wao walilipa jina ” ZAICO ” ikimaanisha ( ZAIRE-CONGO ). kabla ya hapo baadae jopo la waasisi kuamua kwamba ORCHESTRA ipewe jina la ZAIKO ( ZAIRE YABANKOKO ) / ZAIRE YA BABU ZETU

Neno ” LANGA LANGA ” liliongezwa kwa mujibu wa wengi na PAPA WEMBA, chimbuko lake ( ni Mti unaotumiwa kama Dawa, Upatikanao kwenye Msitu wa Mji wa SANKURU,Sehemu  aliko zaliwa PAPA WEMBA ).

Tarehe 25-12-1969, GROUP ZAIKO LANGA LANGA, ilianza rasmi Mazoezi yao.WANAMUZIKI PEPE FELY MANUAKU na PAPA WEMBA ndio waliokua wakwanza kufika sehemu ya mazoezi na niwao huchukuliwa kama WANAMUZIKI NAMBA 1 NA NAMBA 2 wa Group hilo,

Wa Tatu ni TEDDY SUKAMI,wa Inne ni ZAMWANGANA,wa Tano ni NYOKA LONGO,Sita EVOLOKO JOCKER,Saba MAVUELA,Nane ANDRÉ BIMI OMBALE,Tisa BAPIUS MWAKA,Kumi MBUTA MASHAKADO NZOLATIMA, Wakaja kujiongeza wapiga Gita DAMIEN NDEBO,MATIMA MPIOSO,FREDDY ELONGA DI NJO. Bila kuwasahau WAIMBAJI MASHUHURI GINA WA GINA IFONGE, BENZ BOZI BOZIANA, na Mpiga Drums ILO PABLO BAKUNDE…

Tarehe 24-03-1970 Orchestra ZAIKO LANGA LANGA walidumbwiza kwa mara ya kwanza SHOO kabambe kwenye Ukumbi wa Bar ” HAWAI ” JIJINI KINSHASA .

WENGI wanakubaliana kwamba, NEMBO ya ORCHESTRA ZAIKO LANGA LANGA ni Mpiga Gita Machachari ” PEPE FELY MANUAKU “. ITAENDELEA

 

Lubonji Wa Lubonji

 

 

 

 

3 Responses to HISTORIA YA GROUP ” ZAIKO LANGA LANGA ” SEHEMU YA KWANZA “

  1. Anonymous says:

    Hapo mukubwa Lubonji umekuja vizuri sana kwa kutuletea historia ya Zaiko langa langa.Mungu akutie nguvu zaidi.

  2. lubonji says:

    Asante sana Ndugu, Tupo pamoja!!!

  3. Good information and facts, superb and important style and design, as share very good things with excellent suggestions and ideas.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: