WERRASON MBARONI JIJINI PARIS KWAKOSA LAKUKUTWA NA PESA FEKI ZA EUROS

10363886_692627900807710_1719787936206703909_n10411355_673128669424300_4366357132382617624_n (1)

 

Habari zilizo tufikia punde,ambazo bado zahitaji kusibitishwa, zaashiria kwamba Msanii Supersatar wa CONGO WERRASON NGIAMA MAKANDA LE ROI DE LA FORET yuko chini ya ulinzi wa polisi Inchini Ufaransa ( FRANCE )

Bofya kwenye kichwa cha Habari kwa maelezo zaidi

Habari tulizo waletea majuzi kwamba Msanii huyo yuko Jijini Paris, kumalizia kazi ya Album inayosubiriwa na wengi ” FLECHE INGETA “. Katika dhiara yake hiyo, WERRASON kawakivutio kwa Watu wengi,hasa kwa wale wapenzi wake na Wapenda Muziki wa Rumba kwa jumla. Kwenye mahojiano yake na Vyombo vya habari Jijini Paris, WERRASON kawaomba kwa wote wale wanao hitaji MAJINA yao yatajwe ( LIBANGA ) kwenye Album FLECHE INGETA, basi awasiliane na Mpambe wake Namba Moja SANKARA DE KUNTA. kupitia na hii 0033751261721

Kutokana na wito huo, basi Mamia ya Watu walijitokeza ili kufaanikisha na kuhakikisha wanatajwa Namsanii huyo anaevutia Watu wengi popote aendako,Ushahidi ni kwamba Tokea alipo wasili  JIJINI PARIS, kaacha gumzo kutokana na Umati wa Watu unaomzingira popote apitapo. Hadi Baadhi ya Watu wakawa wanajiuliza hao wa COMBATTANTS WAKO WAPI ?

Akiwa kwenye STUDIO kuendelea na kazi ya Album yake, huku akiwa PIA anatoza Pesa za Watu wapenda LIBANGA, yasemekana kina cha chini ilimtu atajwe ni EUROS 150, Mashahidi wanasema  kachukua pesa papo hapo ya Watu zaidi ya  50.waliojipendekeza kwa zoezi hilo.

Maskini kwake ,hajatarajia kabisa yaliyomkuta, Kumbe kati ya Watu hao walikuwepo pia wabaya wake, waliomgea PESA FEKI ZA EUROS.

Akiwa  MADUKANI KWENYE MTAA MAARUFU JIJINI PARIS WA CHAMPS – ELYSÉES, baada ya kufanya Shopping, Mmoja wa WAFANYABIASHARA kagundua katapeliwa na pesa Feki, ndipo kawataarifu polisi, nao bila kusita wakaenda kumsubiria LE PHÉNOMÈNE WERRASON NGIAMA MAKANDA Hotelini kwake. Hadi Wakati huu Bado hajaachiliwa na Polisi chaeleza chanzo chetu.

Kutokana na Mkasa huo, WERRASON atashindwa kabisa kusafiri Inchini AMERICA anakosubiriwa kwaajili ya kupewa Tuzo lake la GENERIC BORA AFRICA KUTOKANA NA ALBUM ” TECHNO MALEWA “.

SWALI : NINANI YULE KAMTENDEA UNYAMA WERRASON, NI WA COMBATTANTS ? au WAPENZI NA MASHABIKI WA KOFFI OLOMIDE ? historia itatupatia Sheria.

 

Lubonji Wa Lubonji

 

 

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: