WERRASON, ALBUM FLECHE INGETA, ITAUZWA INCHINI CONGO KWA BEI YA DOLA 1 USD

 

WERRASON LE ROI DE LA FORET NGIAMA MAKANDA, TOKEA MAJUZI YUKO JIJINI PARIS KUMALIZIA KAZI YA ALBUM ” FLECHE INGETA ” PIA KUONGEZEA DEDICACES ( LIBANGA )KWENYE ALBUM HIYO.

BOFYA KWENYE KICHWA CHA HABARI KWA MAELEZO ZAIDI.

Katika mahojiano yake na Mtangazaji ” ADO “, WERRASON kaongelea Mambo mengi yakiwemo :

1.Album ” FLECHE INGETA ” Kufwatana na Agenda yetu, nakama hapajatokea mabadiriko yeyote, Uwezekano mkwubwa upo kwa Album ” FLECHE INGETA “kutolewa mwishoni mwamwezi huu. Itakua na Nyimbo zaidi ya 26 .Mimi ni Mbunifu, Tizama ilivyo ” GENERIC ya Album TECHNO MALIWA ” ilipata sifa na Tuzo Nyingi, Hadi leo hii tuzo zaendelea kumiminika ,ni kwamaana hiyo niko njiani nikielekea AMERICA kuchukua Tuzo nyingine ya GENERIC TECHNO MALEWA ILIOTEULIWA KAMA ” BORA ZAIDI BARANI AFRICA ”

Nafikiri Mtaipenda zaidi Generic ya FLECHE INGETA, nawaletea vitu vipya nampangilio  mpya,Mfano wa ndege iliopaa,kisha ikatulia angani na hatimae ikatua!!! Amini kwamba mimi ni Mbunifu mkubwa!!!na kuhusiana na soko lamauzo, Tumetumia Mbinu ya kupambana na HAO WATU WEZI WANAO KIMBILIA KUFANYA COPY ZA DVD NA CD, hasa katika harakati zakuwarahisishia Watu wengi wapate kununua kihalali, BASI ALBUM “FLECHE INGETA ITAUZWA INCHINI CONGO KWA BEI YA DOLA 1.IKIWANAMAANA KWAMBA,ITAKAPO TOKEA WATU MILIONI MOJA WAKIINUNUA,TAYARI NTAKUA NIMEWEKA MFUKONI DOLA MILIONI MOJA.

2. Kwanini wampa sana kipaumbele siku hizi Reppa BERCY MWANA , tunapo mlinganisha na wengine Tunagundua kwakweli kapewa nafasi iliojuu sana. Jibu la WERRASON: Mini kamavile Kocha, najua jinsi gani kuipanga timu yangu,Najua kukuza vipaji,kila Mtu nampa nafasi yakujieleza!!! Msani anapojiunga na Group Wenge MM, utaona tofauti na mabadiriko kulinganisha na huko alikotokea. Wala siutani  wanaponipachika jina la ” Grand formateur ” yaani MKUFUNZI si buree!!! Ninao uwezo wakumpandisha Mwanamuziki yeyote,kuinua kabisa kipaji chake… Mwanamuziki unapowekwa Benchi,wala silazima kwakowewe kujiondoa kwenye Group,Mvumilivu ulambivu. NINACHO KIKOSI CHA WANAMUZIKI 64.

3. Siku hizi tumekuona sana ukiwa na Mwenzio JB MPIANA, Hivi wajua wapo watu walio hatarisha maisha yao kwaajili yenu? Wapo walioumia nakulazwa Hospitali!!! Miaka nane au kumi zilizo pita, Upinzani makali ulikua kati yenu,inakuaje leo hii Mnaonekana kuwa Watu wa karibu? naomba ufafanuzi zaidi kwa hilo !!! JIBU LA WERRASON : Kwani watu wawili waliokua natofauti za kidini, Mmoja ni Mkristo na Mwengine Muislamu, Watu hao hawaruhusiwi kujuliana hali? Ushindani kwenye Muziki ni jambo lakawaida, Kwenye Uwanja wa Mpira, Timu ya ” VITA na ile ya IMANA, kamwe hawawezi kuelewana. Kwa Tanzania chukulia mfano huo kwa TIMU ZA YANGA NA SIMBA. Ila wakati linapo jitokeza jambo na ikiwa wanahitajika kikaoni,utawaona wakijadili kwa pamoja.. Hayo Mawazo Ulionayo, kwangu mimi naona kama nikawaida, Ndugu yangu kafanya Sherehe ya Bintie,niwajibu wangu kwenda kumsapoti, acheni kuchanganya Mambo ya watoto nayale maswala ya Muziki!!! Wapi ulipotuona Mimi naye tukipanda jukwaa kwa pamoja nakuimba Muziki? Kwenu nyinyi mnaliona jambo lakawaida tunapokutana na JB MPIANA tusitoleane salaam? Kweli Hua tunakutaka kama inahitajika mfano kwenye Msiba au Sherehe nyingine. Nawala haijamaanisha kwamba Mchuano kati yetu kuhusiana na Kazi ya Muziki umekwisha Hapana!!! Yeye analo Group lake namimi nalakwangu. Jaribu kutupambanisha upatekuona kucha zangu!!! IMEWAHI KUTOKEA KWENYE KIPINDI FULANI KAMPUNI YA ” BRALIMA ILITUPAMBANISHA, MCHUANO HUO ULIACHA HADITHI HADI LEO ”

Kwa Upande wangu, inapotokea nafanya Shoo mbele ya Watu Elfu 30.000,basi ntakua nimefeli kabisa, Mimi nashangiliwa na Watu zaidi ya Laki na nusu!!! Kwakifupi, Mtu ambae ni Mpenzi wangu wakweli, kamwe hutambadirisha, kadhalika kwayule alie mpenzi wa JB MPIANA. Wafahamu kwamba wapo watu ambao USHABIKI WAO KWA JB MPIANA AU KWA WERRASON UPO KWENYE DAMU? Watu kama hao unapomsema vibaya JB MPIANA au WERRASON wakoradhi kukutolea kisu? Watu kama hao hunalolote lakuwaambia,hatawakiwa maofisini,wataendelea kutufwatilia nakutushabikia !!! wala sikwanyinyi kuwalaaumu.

4. Kati ya Vijana wote waliopitia kwenye Group lako, niyupi ambae wamsikitikia hadi leo pale alivyojiondoa? Jibu la WERRASON : Kwakweli Wote niliwapenda,nantaendelea kuwatakia mema kwenye kazi zao pamoja na Familia zao.

5. Vipi uhusiano wako na KOFFI OLOMIDE? WERRASON : Wala sina neno lolote naye, mimi siMtu wamaneno mengi,sidhani kama ninalo la ziada lakuongelea, sina ugonvi naye, namheshimu kama Kaka yangu.

6. Sema Neno lako la mwisho ! WERRASON : Nawapenda Nyie wote wapenzi wa Muziki hasa wale mashabiki wangu, FLECHE INGETA IPO MBIONI KUTOLEWA, NAOMBA MUENDELEE KUTUSAPOTI. BILA NYINYI SISI WENGINE HATUPO.

KWASASA NIPO JIJINI PARIS,YULE ANAEHITAJI KUWASILIANA NAMI, NAPATIKANA KWENYE NAMBA HIZI : 0033751261721

Lubonji Wa Lubonji

 

5 Responses to WERRASON, ALBUM FLECHE INGETA, ITAUZWA INCHINI CONGO KWA BEI YA DOLA 1 USD

 1. Pascal Canisio says:

  werrason kweli ana kundi kubwa yaani 64

 2. lubonji says:

  Ndo kwamaana hiyo inaitwa Timu ya Taifa

 3. free bingo provided

  WERRASON, ALBUM FLECHE INGETA, ITAUZWA INCHINI CONGO KWA BEI YA DOLA 1 USD | Spoti na Starehe

 4. free online bingostep

  WERRASON, ALBUM FLECHE INGETA, ITAUZWA INCHINI CONGO KWA BEI YA DOLA 1 USD | Spoti na Starehe

 5. latest online games

  WERRASON, ALBUM FLECHE INGETA, ITAUZWA INCHINI CONGO KWA BEI YA DOLA 1 USD | Spoti na Starehe

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: